CHADEMA yashindwa vibaya Arusha


kwa hiyo unataka kusemaje???
kwamba ccm ndio imeshinda arusha?
hongereni ccm kwa ushindi mnono
hahahaha
daaaah hapa duniani kuna watu wa ajabu sana.!?
 
Ulitaka tujitokeze kwa maelfu ili mtulipue tena kama mlivyofanya kwa kusaidiwa na mapolisi wenu ile siku ya kuhitimisha zile kampeni?
Kwa taarifa zako wengi waliojitokeza walikuwa wafuasi wa CCM waliochoshwa na jinsi chama chao cha kijangiri na kigaidi hicho kinavyowahujumu wakazi wa mkoa huu.
Hivi hamna hata mshipa wa aibu kuleta tena nyuso zenu huku wauaji na wabakaji wa demokrasia wakubwa nyie?
Down with CCM.
 
Kwa mawazo yako unataka kutuambia kuwa hao watu 60,000 wangejitokeza kupiga kura sisiem ndo wangeshinda? Kwa taarifa yako ingekula kwao fulmazinonda. Sisiem si kitu kwa CDM Arusha. Ila mfa maji haachi kutapatapa.
 

Ngoja nijaribu kusaidia kukuelewesha. Naishi Arusha. Wananchi wametishwa sana kuhusu huu uchaguzi, na waliokuwa wanatisha watu ni polisi na uongozi wa serikali wa mkoa na wilaya. Jumamosi jioni kuna watu wamepita nyumba kwa nyumba kuwakumbusha kuhusu bomu la Soweto. Watu wametangaziwa wakae majumbani kwa kuwa kuna tishio la mabomu. Wakati huohuo CCM walikuwa wanatuma ujumbe wa simu kukumbusha watu kwenda kuwapigia kura (mimi pia nilitumiwa sms na balozi wa mtaa wetu ambaye nina uhakika hauelewi mrengo wangu maana huwa sijadili hizi siasa mtaani kwangu). Jana jumapili mitaani kulikuwa na polisi tele, wamevaa kivita (bullet proof) na silaha nzitonzito, na katika vituo vya kura walizungushia utepe na kuuzingira. Nimeshuhudia watu wakikamatwa na kusweka kwenye magari yanayodaiwa ni ya polisi (hayakuwa na namba za polisi, lakini tunafahamu silaha zile hakuna raia anazo). Hii yote ilikuwa kutishia CHADEMA wasiende kupiga kura. Na kweli wengi hawakwenda. Hao wachache ambao ilidhaniwa kuwa ni CCM, walipoingia chumba cha kura wakachagua kilicho moyoni: CHADEMA. Ndipo watu wa Arusha walipofikishwa.
 

Kama unajua umuhimu wa kupiga kura halafu huendi kupiga kura, je wasiojua umuhimu wa kupiga kura na wakauza shahada zao wanafanya makosa? Na je, usipopiga kura (hali ukijua umuhimu wake) na ikatokea waliochaguliwa huwapendi/huwataki utakuwa na haki ya kulalamika?
 
Kilio cha samaki machozi kwenda na maji, mbona hao wanaoimba KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI hawakujitokeza kukidumisha chama chane? Nenda ukamhoji nchimbi akueleze ni kwanini aliamuru kutawanywa mtaani askari wengi kiasi kile ili kuwatisha wananchi?
 
Last edited by a moderator:
Ndio sasa nasema msitumie kauli mbiu ya people's power kirejareja kwa maana hamuiwezi kinadharia people's power ni kama ile pale Tahrir square Misri na ni kwamba ije mvua, yaje mabomu, zije risasi watu wanatoka tuuu na wala hawastuki mshipa wa fahamu; mpoooo? people'sssssssssss
 

na siyo kwamba hayoa yote siyajui.
myself sitegemei mwanasiasa aniletee mabadiliko kamwe........... manake nimekuwa nikakuta hakuna walichokifanya na wala hakuna kinachofanywa nao zaid ya kula na kujineemesha wao.
sasa kuliko nimpe mtu kura ya kwenda kuninyonya heri nisimpe kabisa nijue ananinyonya kwasababu karuhusiwa na wengine ile sio mimi niliyemruhusu.
 

Mungu ana taabu sana na nyie viumbe wake, alikuumba na ufahamu kamili lakini kwa sababu unazozijua wewe umeamua kujitoa ufahamu. Kazi ipo...!
 

Mwanzoni nami nilikuwa nafikiria kama wewe. Baadaye nikagundua kwamba wanasiasa wanapenda watu wanaozira mambo ya siasa (ndiyo maana wakaleta slogan kama siasa ni mchezo mchafu n.k) ili watu weledi wasitamani kuingia huko. Ndiyo maana mwanafalsafa mmoja wa Urusi akasema 'politics is too important to be left to politicians'.

Lakini ukweli unabaki kwamba politics rules the world, and if you dont want to play politics then cast only the vote otherwise some funny people will continue deciding your fate.

Go voting now, not only to your own good, but to the better life of many others.
 
Mungu ana taabu sana na nyie viumbe wake, alikuumba na ufahamu kamili lakini kwa sababu unazozijua wewe umeamua kujitoa ufahamu. Kazi ipo...!

Haya ni maneno ya kwenye khanga sio jibu la hoja sasa sijajua kama ufahamu hapo upo au ndio walewale
 
kwa hiyo unataka kusemaje???
kwamba ccm ndio imeshinda arusha?
hongereni ccm kwa ushindi mnono!
Duniani kuna watu wa ajabu sana!

Kweli mkuu CCM kazi yao ni kusema "this is white" while kila mtu anaona ni nyeusi.
 
Kwa ufahamu wako mdogo tukufahamishe wenye akili walishahama ccm zile kura ulizoziona za ccm ndio wanachama waliobaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…