Ki ukweli CCM ikiendelea kurudia makosa kama yanayofanyika kwenye jimbo la Kibamba na Ubungo, haya majimbo hatutayakomboa kirahisi. Toka tumenza kupoteza jimbo la Ubungo huko nyuma tatizo lilianzia kwenye kura za maoni kwani wanashinda watu kwa nguvu ya pesa na ambao si chaguo la wananchi. Viongozi wa Chama (W) wanakumbatia wagombea wasio na sifa kisa wana pesa. Kwa kuwa wananchi hawawapendi wanakula pesa zao ila kura hawawapi. Wananchi wa sasa wameelimika, ukija na pesa yako wanakula tu na kura hawakupi.....mnalutea watu amabo si wakazi wa huku na wasio na historia yoyote ya uongozi wa Chama au kusaidia jambo lolote katika jimbo letu, badala yake mnaleta watu wanaowahonga ninyi amabo huku hawajulikani. Msipobadilika CCM tutaendelea kupigwa tu katika majimbo ya Ubungo na Kibamba. CCM makao makuu badilisheni haraka uongozi wa CCM wilaya, makatibu wa majimbo n.k. kwani wameshindwa kabisa zaidi ya kujali matumbo yao. HII NI AIBUUUU. Haijawahi kutokea.