DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,152
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kibamba, mkoani Dar es Salaam, kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Edward Kinabo, Septemba 2, 2025, akiwa katika Kata ya Saranga, ameahidi kuboresha maslahi ya waendesha bodaboda endapo atapewa nafasi ya kuwakilisha wananchi wa jimbo hilo bungeni.
Akizungumza na wananchi wakati wa kujitambulisha kwa wapiga kura, Kinabo alisema kuwa waendesha bodaboda wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo unyanyasaji unaotokana na mifumo ya usafirishaji kwa njia ya mtandao.
Ameeleza kuwa bodaboda ni kundi kubwa linalochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa vijana na familia zao, lakini mara nyingi wamekuwa wakikosa utetezi wa kweli, hivyo ameahidi kuwa akipewa ridhaa ya kuwa Mbunge, atahakikisha maslahi yao yanaboreshwa kwa kuweka mifumo rafiki zaidi ya kisheria na kiutendaji.