CHADEMA yapinga tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

1. By bagamoyo Mh. Emmanuel Nchimbi inabidi sasa ajiuzulu, kwani tunaona mlolongo wa kushindwa kutoa maamuzi sahihi kusimamia Jeshi la POLISI kufanya kazi kwa kufuata sheria na yeye pia kukurupuka kuunda TUME iichunguze wizara yake kufuatia mauwaji ya wananchi

Madaraka Nyerere anatukumbusha juu ya uungwana wa kuwajibika waziri husika kama kunatokea mlolongo wa mauwaji ya wananchi kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mzee Ali Hassan Mwinyi alivyojiuzulu:

2. By kudi shauri mwaka 2006 kulitokea mauaji ya wachimba madini kutoka mahenge nje kidogo ya dar es salaam baada ya hao jamaa kukamatwa na polisi. Rais kikwete aliunda tume huru iliyo ongozwa na jaji wa mahakama kuu kuchunguza vifo hivi. Tume ilitoa ripoti yake na kulaumu polisi kwa mauaji ya hao wachimba madini wa mahenge. Kutoka hapo askari polisi kadhaa walikamatwa na kushtakiwa kwa ya mauaji hayo akiwepo aliye kuwa regional crimes officer wa dar wa wakati huo bwana zombe. Sioni tofauti ya kesi hiyo ya wachimba madini wa mahenge na hii ya ndugu mwangosi. Tindu lisu na cdm are right - waziri nchimbi na ag werema wacheni usanii kwenye mambo ya sheria!

3. By Kudi Shauri ---The issue hapa sio kilichotokea kwenye kesi ya akina Zombe Mahakama kuu. The issue ni uchunguzi wa mauaji ya hao jamaa wa Mahenge ambao mwanzoni walisingiziwa kuwa walikuwa majambazi waliouwawa na Polisi. Tume Huru ikiongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu ilidhibitisha hao jamaa hawakuwa majambazi bali ni raia wema waliouliwa kinyama na Polisi wa Tanzania wakiongozwa na Zombe. Tume ikapendekeza kina Zombe washitakiwe kwa kosa la mauaji. Kesi ilifunguliwa na DPP na Serikali ilishindwa kisanii katika mahakama kuu. Tuliambiwa kuwa Serikali/DPP walikuwa wamedhamiria kukata rufaa katika kesi hii - mpaka leo hatujasikia lolote juu ya rufaa hiyo - usanii mwingine katika ofisi ya AG.

Ndo maana naipenda Jamiiforums kwa kuweka hoja na data kukumbushia historia ya utendaji wa serikali ya CCM na vyombo vyake vya dola.

Nafikiri safari hii serikali na chama 'tawala' CCM wamebana hatoki mtu hapa bila kufikishwa kwa Pilato na wengine kadhaa kuachia ngazi/bodi
 
JK anapiga deal tu ikulu watu wake wanaisha kwa kupiga mabomu tu yeye kimya kama hayupo!!alipokimbilia kuchukua fomu na kutumia mipesa yote ile alidhani ni rahisi hivyo?awajibike sasa si alitaka hata kuhama chama sababu ya urais mwaka 1995??mbona hawajibiki kwa watanzania wenye kinyongo na serikali na watendaji wake?anamtengenezea mazingira mabaya sana mgombea ajaye!
 
Mhhh KUMBEEE, Mbona huko nyuma tume nyingi za uchunguzi zimeundwa na mawaziri???? Au sheria hii ni kwa ajili ya suala la Mauaji Pekee???
 
Chadema mbona amueleweki huyo Tundu Lissu anasema Tanzania hakuna majaji, sasa hiyo tume ya nini, halafu mbona Chadema hawapingi sensa.
 
kWELI KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA NONGWA, SASA WEWE INAKUUMA NINI? NA AKISEMA NAPE? NADHANI MAMBO YA KISHERIA SIKU ZOTE ANAONGEA LISSU, SASA LEO INAKUUMA NINI KUONGELA HILOOOOO?

kauli ya lissu imekuwa ya chadema? kweli mweshimiwa 6 hakukosea!
 
Huo ndio uwazimu sasa, alisema baadhi ya majaji uteuzi wao unawalakini, na kawataja majaji wasiozidi 20, lakini kwa sasa tuna majaji zaidi ya 60, maana yake waliobaki 40 ndio makini.......kuhusu sensa unadhani cdm ni mapunguani kama hao wanapinga kwa kivuri cha dini?

chadema mbona amueleweki huyo tundu lissu anasema tanzania hakuna majaji, sasa hiyo tume ya nini, halafu mbona chadema hawapingi sensa.
 
Umeambiwa tuma ya kuchunguza mauaji! Mbua mzee mwinyi alijiuzuri kwa watu kuteswa tu, sembuza hapa mtu anauwawa, waziri mwenye dhaman anaunda tu? Maigizo hayoooo...... Kumbuka wafanya biashara wa morogoro ilivyokuwa, watuhumiwa ni polisi, rais ndio aliunda tume! ..........msiwe na kili za samaki!
mhhh kumbeee, mbona huko nyuma tume nyingi za uchunguzi zimeundwa na mawaziri???? Au sheria hii ni kwa ajili ya suala la mauaji pekee???
 
Waziri kivuli wa sheria na katiba wa chama pendwa CHADEMA mh.TUNDU LISU amesema tume iliyoundwa na mh. EMANUEL NCHIMBI ni batili kutokana na katiba ya jamhur ya muungano wa Tanzania kwan mwenye uwezo huo n Mh. Rais na ndie anayetoa hadidu za rejea za tume husika pia mh waziri mhusika hvyo hapasw kuunda tume ya uchunguz kwn wizara yake ni watuhumiwa pia




lissu ameanza kuchangikiwa sasa. Tume ya kiuchunguzi iko hata ndani ya wizara na mawaziri wana madaraka hayo kwani wanafanya kazi kwa niaba ya Rais, lissu arudi kwenye katiba . Na lissu yeye ni mtaalam wa sheria za mazingira na si sheria za katiba , na hili lajulikana, una uhakika cdm ndio chama pendwa? hebu tuonyeshe tafiti juu ya hoja yako hiyo na ilifanyikaje? , no research no right to speak.
 
Chadema anzisheni uchunguzi wenu halafu toaeni majibu.
 
Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwanasheria wa chama hicho Mhe. Tundu Lissu kimesema, tume ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ni batili.

Lissu amesema, kwa mujibu katiba Nchimbi hana mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza mauaji, na mwenye mamlaka hayo kwa mujibu wa katiba hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee. Hivyo chama hicho kimemtaka Rais kuunda tume huru ya uchunguzi wa mauaji hayo.

Hivi Rais wa nchi yupo? ndiye aliye apa kulinda katiba na watu wake sasa analinda walio kufa na kukaa kimya!
 
Mkuu Ritz,
Siasa ngumu Tundu si ndiye anayelalamikia elimu za majaji wa mahakama kuu anadai wengi wao ni voda fasta sasa leo hii ameona wana elimu ya kutosha kuwemo kwenye tume ya mauaji? Chadema bana hujui nani mlevi na teja kama wamechanganyikiwa hivi!

Chama
Gongo la mboto DSM-safarini Brussels

Kwani aliwatuhumu wote?!! Acha siasa nyepesi wewe!
 
Mkuu Ritz,
Siasa ngumu Tundu si ndiye anayelalamikia elimu za majaji wa mahakama kuu anadai wengi wao ni voda fasta sasa leo hii ameona wana elimu ya kutosha kuwemo kwenye tume ya mauaji? Chadema bana hujui nani mlevi na teja kama wamechanganyikiwa hivi!

Chama
Gongo la mboto DSM-safarini Brussels

Mkuu chama,
Chadema kila mtu anafyatuka na lake madude hayo kila mtu anatoa tamko na wote wanalikubali ukiona watu wanakubaliana kila jambo hujue ni mateja.
 
Last edited by a moderator:
Kumbe "Bwanyenye" alikuwa anatwanga maji kwenye kinu pamoja na mbwembwe zote ni mbumbumbu wa Sheria! Duh, hawa ndio mawaziri wetu. Hawajui hata wajibu na mipaka yao wanaingilia mpaka kazi za dhaifu! Kweli kule juu kuna guo guo!

mtampata wapi waziri kama nchimbi?
 
Hata kama waziri nchimbi angekuwa na mamlaka ya kuunda tume hiyo, bado watu walioteuliwa kuunda tume hiyo nao wana walakini hasa mwenyekiti wake jaji mstaafu Ihema-huyu ni jaji asiyejua kuandika hukumu kama ilivyoelezwa na Tundu Lisu katika utetezi wake katika kamati ya bunge, kwahiyo kwa vigezo vya aina yoyote hana sifa ya kuongoza tume ya kuchunguza kifo cha Mwangosi.

Pili naibu kamishna wa polisi Isaya Mngulu naye hastahili kuwemo katika tume hiyo kwakuwa mtuhumiwa namba moja katika sakata hili ni jeshi la polisi ambalo yeye ni mtumishi wake, na tukienda mbele kidogo katika sakata hili IGP Mwema na Waziri Nchimbi wanatakiwa kuhojiwa ushiriki wao katika kutoa amri na maelekezo ya kutekeleza mauaji hayo, na naibu kamishna Mngulu hana uwezo kwa kumhoji bossi wake Mwema.
 
Acha ujuha tayari ki itifaki inakuwa kauli ya chama maana kaitolea akiwa ofisi makao makuu ya chama akiwa ndani ya Gwanda tena alitoa kauli kwa kutambulishwa kuwa ni mwanasheria wa chama na mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Jibu swali, kwa hiyo kauli ya mwanachama/kiongozi wa cdm ndio kauli ya chama? Rejea kauli za Nassary
 
Back
Top Bottom