CHADEMA yapinga tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Mwanasheria wa CHADEMA kamanda Lissu amesema kuwa si halali waziri kuunda tume maana hana mammlaka hiyo hasa kwenye matukio ya kifo zaidi ya raisi wa jamuhuri ya muungano. Amesema CHADEMA inashauri iundwe tume itakayokuwa na wajumbe ambao ni majaji wa mahakama kuu na si vinginevyo.

source:ITV
 
Yasema Nchimbi hana uwezo wa kuunda tume za uchunguzi isipokuwa Rais tu.
Ni kauli ya Tundu Lissu akiongea na media leo
 
Kumbe "Bwanyenye" alikuwa anatwanga maji kwenye kinu pamoja na mbwembwe zote ni mbumbumbu wa Sheria! Duh, hawa ndio mawaziri wetu. Hawajui hata wajibu na mipaka yao wanaingilia mpaka kazi za dhaifu! Kweli kule juu kuna guo guo!
 
mwanasheria mkuu yuko wapi?wizara ya mambo ya ndani haiwezi kujitenga na polisi tuache ujinga.
 
Waziri kivuli wa sheria na katiba wa chama pendwa CHADEMA mh.TUNDU LISU amesema tume iliyoundwa na mh. EMANUEL NCHIMBI ni batili kutokana na katiba ya jamhur ya muungano wa Tanzania kwan mwenye uwezo huo n Mh. Rais na ndie anayetoa hadidu za rejea za tume husika pia mh waziri mhusika hvyo hapasw kuunda tume ya uchunguz kwn wizara yake ni watuhumiwa pia
 
Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwanasheria wa chama hicho Mhe. Tundu Lissu kimesema, tume ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ni batili.

Lissu amesema, kwa mujibu katiba Nchimbi hana mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza mauaji, na mwenye mamlaka hayo kwa mujibu wa katiba hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee. Hivyo chama hicho kimemtaka Rais kuunda tume huru ya uchunguzi wa mauaji hayo.
 
Source:ITV
Kamanda amefunguka ya kuwa Waziri hana mamlaka kisheria ya kuunda tume ya uchunguzi....mwenye mamlaka hayo ni rais wa jamhuri.
Hii imekaaje wakuu, je kukurupuka na kupoteza mwelekeo kwa magamba sugu kunaendelea
 
mwanasheria mkuu yuko wapi?wizara ya mambo ya ndani haiwezi kujitenga na polisi tuache ujinga.

Hizi habari si ngeni Tanzania.

Tushaona Basil Mramba akipewa kazi ya kumchunguza mwanawe kwa Anna Mkapa kwenye issue ya Simu 2000.

Na Mkapa.

Mtu unachunguzwa, baba wa kambo rais, anayekuchunguza baba yako Waziri. Na hana hata aibu ya ku- declare "conflict of interest".

Some guys have all the luck.
 
Waziri kivuli wa sheria na katiba wa chama pendwa CHADEMA mh.TUNDU LISU amesema tume iliyoundwa na mh. EMANUEL NCHIMBI ni batili kutokana na katiba ya jamhur ya muungano wa Tanzania kwan mwenye uwezo huo n Mh. Rais na ndie anayetoa hadidu za rejea za tume husika pia mh waziri mhusika hvyo hapasw kuunda tume ya uchunguz kwn wizara yake ni watuhumiwa pia

Mh.Lisu yuko sahihi kabisa, wizara ya mambo ya ndani ni watuhumiwa pia katika mauaji ya mwandishi Daud Mwangosi. Waziri Nchimbi anaendeleza itikadi zile zile za ulevi wa madaraka.
 
Back
Top Bottom