PreGE2025 CHADEMA yamvua Uongozi Lemburus Mchome

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kiuhalisi chadema ikiingia ikulu itakuwa mbaya hata kuliko CCM kama wasemavyo chadomo kuwa ccm ni wabaya.ebu angalie ,leo ukiikosoa chadema utaambulia matusi au kuvuliwa uanachama ni kwamba tu hawana uwezo wa kukuteka na kukupoteza .wakiwa na jeshi na mamlaka kamili they will do worse kwa sababu watakuwa hawaambiliki.

Zitto Kabwe avuliwa rasmi uanachama Chadema​

Jumanne, Machi 10, 2015 — updated on Machi 09, 2021

Tanzania: Wanachama 19 wa Chadema wavuliwa uanachama​


Pre GE2025 John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA​


Aliyekuwa Naibu Meya Chadema avuliwa uanachama​

Jumamosi, Aprili 28, 2018 — updated on Februari 21, 2021

LIST INAENDELEA


THIS IS UNSTABLE POLITICAL PARTY
 
Kwani amevuliwa uanachama kwa kukosoa chama?
 
Amesema Jtatu anakwenda kusema kwa babake Mtungi - chama chenu kifutwe.
 
Wafuasi wa ccm hao hawaamini jinsi walivyonyanganywa ugali wao.
 
CHADEMA inaongozwa na madikteta
 
Lissu haya akiwa peke yake ccm yote inajifungia chumbani huku ikipiga yowe la kuombq msaada polisi. Ccm bila vyombo vya Dola haijiwezi.
Kwani Lissu anapambana na CCM au anapambana na Vyombo vya Dola? Au huelewi unaongea nini dogo?
 


Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Lembrus Mchome leo Jumamosi, Mei 17, 2025 amevuliwa nafasi yake ya uongozi ndani ya chama hicho.

Soma pia Mchome alimwa barua
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Ndonde Tottinan amethibitisha kuvuliwa uongozi wa Mchome katika kikao cha mashauriano Mkoa wa Kilimanjaro, kilichoketi leo Mei 17, 2025 mjini Moshi.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo, kuhusu taarifa hizo Mchome amedai kuwa hana taarifa lakini huenda suala hilo likawa kweli kwa kuwa dalili zilianza kuonekana siku nne zilizopita alipoondolewa kwenye makundi sogozi ya WhatsApp kuanzia la Kanda ya Kaskazini, mkoa hadi wilaya.

Mchome amekutana na kadhia hiyo kipindi ambacho amekuwa na migogoro na chama chake hasa baada ya barua ya malalamiko dhidi ya baadhi ya viongozi wa sekretarieti na kamati kuu akidai walipitiswa na Baraza Kuu Januari 22, 2025 likiwa halina akidi.

Malalamiko hayo ambayo aliyawasilisha ndani ya chama chake na nakala kwa msajili, yamefanyiwa kazi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo Msajili ameitaka Chadema kuitisha Baraza Kuu jipya ili kufanyia kazi upungufu huo.

Waliopitishwa na kikao hicho chini ya uenyekiti wa Tundu Lissu wako wanane akiwemo Katibu Mkuu, John Mnyika, naibu makatibu wakuu, Amani Golugwa (Bara), Ally Ibrahim Juma (Zanzibar) na wajumbe wa kamati kuu, Godbless Lema, Rose Mayemba, Salma Kasanzu, Hafidh Ally Saleh na Dk Rugemeleza Nshala ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
 

Attachments

  • Screenshot_20250517_211857_Google.jpg
    214.2 KB · Views: 24
  • Screenshot_20250517_211857_Google.jpg
    214.2 KB · Views: 21
  • Screenshot_20250517_211857_Google.jpg
    81.3 KB · Views: 23
Ataenda mahakani na kurejeshwa uanachama wake...CCM wamefanya mihimili mingine ime-paralyse
 
Mbowe ni mtu mbinafsi sana. Yaan haya yote yanatokea yeye kakaa kimya
 
#HABARI Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Lembrus Mchome leo Jumamosi, Mei 17, 2025 amevuliwa nafasi yake ya Uongozi ndani ya Chama hicho Kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Ndonde Tottinan amethibitisha kuvuliwa uongozi wa Mchome katika kikao cha mashauriano Mkoa wa Kilimanjaro, kilichoketi leo Mei 17, 2025 mjini Moshi.

Mchome amekutana na kadhia hiyo kipindi ambacho amekuwa na migogoro na chama chake hasa baada ya barua ya malalamiko dhidi ya baadhi ya viongozi wa sekretarieti na kamati kuu akidai walipitiswa na Baraza Kuu Januari 22, 2025 likiwa halina akidi. #EastAfricaRadio
 
Chadema kwa sasa ni dictatorship of the majority
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…