PreGE2025 CHADEMA yamvua Uongozi Lemburus Mchome

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Madikteta uchwara wa Chadema na majizi ya Ccm tofauti yao ni mmoja hana madaraka tu ila wakishika madaraka ukiwa na wazo tofauti jiandae kufukuzwa hata nchi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini kimemvua uongozi mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Lemburus Mchome leo Jumamosi, Mei 17, 2025.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Ndonde Tottinan amethibitisha kuvuliwa uongozi wa Mchome katika kikao cha mashauriano Mkoa wa Kilimanjaro, kilichoketi leo Mei 17, 2025 mjini Moshi.

Mwananchi limemtafuta Mchome kuhusu taarifa hizo ambapo amedai hana taarifa lakini huenda suala hilo likawa kweli kwa kuwa dalili zilianza kuonekana siku nne zilizopita alipoondolewa kwenye makundi sogozi ya WhatsApp kuanzia la Kanda ya Kaskazini, mkoa hadi wilaya.

Mchome amekutana na kadhia hiyo kipindi ambacho amekuwa na migogoro na chama chake hasa baada ya barua ya malalamiko dhidi ya baadhi ya viongozi wa sekretarieti na kamati kuu akidai walipitiswa na Baraza Kuu Januari 22, 2025 likiwa halina akidi.

Malalamiko hayo ambayo aliyawasilisha ndani ya chama chake na nakala kwa msajili, yamefanyiwa kazi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo ameitaka Chadema kuitisha Baraza Kuu jipya ili kufanyia kazi upungufu huo.

Chanzo: Mwananchi

Msajili mjinga mjinga unaenda kuwalipia kodi watu kama hawa🤦🏾‍♂️🤦🏾‍♂️
 
wamemvua uanachama the terminator? :pedroP:

wamefuata taratibu za katiba ya chama kweli au wanataka kufurahishwa zaidi?:pedroP:
Wewe kila siku nakuambia ni mtoto wa vilabuni maana hauna akili!! Yule aliyepinga Samia kujiteua vipi nae kufukuzwa kwake ndani ya CCM taratibu zilifuatwa.
 
Jikite kwenye hoja bila mihemko wala makasiriko 🐒
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini kimemvua uongozi mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Lemburus Mchome leo Jumamosi, Mei 17, 2025.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Ndonde Tottinan amethibitisha kuvuliwa uongozi wa Mchome katika kikao cha mashauriano Mkoa wa Kilimanjaro, kilichoketi leo Mei 17, 2025 mjini Moshi.

Mwananchi limemtafuta Mchome kuhusu taarifa hizo ambapo amedai hana taarifa lakini huenda suala hilo likawa kweli kwa kuwa dalili zilianza kuonekana siku nne zilizopita alipoondolewa kwenye makundi sogozi ya WhatsApp kuanzia la Kanda ya Kaskazini, mkoa hadi wilaya.

Mchome amekutana na kadhia hiyo kipindi ambacho amekuwa na migogoro na chama chake hasa baada ya barua ya malalamiko dhidi ya baadhi ya viongozi wa sekretarieti na kamati kuu akidai walipitiswa na Baraza Kuu Januari 22, 2025 likiwa halina akidi.

Malalamiko hayo ambayo aliyawasilisha ndani ya chama chake na nakala kwa msajili, yamefanyiwa kazi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo ameitaka Chadema kuitisha Baraza Kuu jipya ili kufanyia kazi upungufu huo.

Chanzo: Mwananchi

lipilau hilo, limewekwa kiunyumba na msajili kule masaki
 
Back
Top Bottom