CHADEMA yamrudisha Kagasheki Bukoba

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Baada ya mkutano mkubwa uliohutubiwa na Makada wa CHADEMA, Kunti Yusuph, Josephat Isango, Mh. Anthony Komu na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Mzee Silvesta Masinde, Waziri wa Maliasili na utalii, Hamisi KAGASHEKI amerudi Jimboni ghfla na kesho anatarajiwa kujibu hoja zilizoibuliwa na CHADEMA, ikiwemo ya kutaka kuvunja soko la Bukoba mjini.

CCM wataondoka bungeni Kama mikutano ya CHADEMA ikiendelea.
 
yaani chadema wanawapelekesha ccm, mpaka wanachanganyikiwa, chadema sasa ndio imekuwa chama tawala, maana ccm wanahangaika nao kweli kweli, big up chadema.
 
Shokonyuuude!!? Walizoea wakishachaguliwa wanaishia Dar. M4C ni moto wa hatari!
 
ha ha ha hab!! Matumbo moto kwelikweli!! Sidhani kama watalala usingizi hawa jamaa wa nyinyiem! Kwa huu moto wa CDM, lazima watawajibika tu!! Blalifaken!!
 
Natamani CDM waendelezi mikutano yao ya M4C kipindi cha vikao vya bunge,na hapa ndiyo watajua faida ya Dr Slaa na Lema kuwa nje ya Bunge.Lazima watatoroka na kukimbilia kujibu hoja za CDM.
 
inabidi watanzania tutafute menejment ya kiendesha nchi kwa sababu sasa ccm hawahangaiki na kutekeleza sera bali wamepaki basi golini kuzuia mashambulizi.
hongereni makamanda kazeni uzi.
 
Hata hapa JF walikuja kwa kaasi sasa sijui wamevuaga magamba yao, watujuze basi kama tuko nao safari moja
 
Comrade na umesahau kwamba wanacheza pungufu maana wachezaji wao watatu wametolewa kwa kadi nyekundu "Lowasa,Maide,mkulo," tehe tehe tehe wamekwisha hawa wehu

Mechi ikiongezwa dk 6 cdm watapata penati hapo ndo mshangiliaji wao maaruf NAPPE atajambamaputo.
 
Hivi CHADEMA wanatumia hii mikutano kuandikisha wanachama wapya na kuwapa kadi?? pia wanakumbuka kuwaambia wananchi umuhimu wa kujiandikisha kwenye dafatari la kupiga kura na muhimu zaidi kwenda kupiga kura uchaguzi mwingine ukifika? Ni muhimu kuanza uhamashishaji huu sasa badala ya kusubiri mpaka June 2015
 
Natamani CDM waendelezi mikutano yao ya M4C kipindi cha vikao vya bunge,na hapa ndiyo watajua faida ya Dr Slaa na Lema kuwa nje ya Bunge.Lazima watatoroka na kukimbilia kujibu hoja za CDM.
hivi kwa nini huna hata tone la hurumma dhidi ya hiki chama huu mpango wangelipanga hivyo sidhani kama bajeti za chai zingepita maana wapitishaji wote wangekuwa kujibu mapigo ya M4C
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom