Mwananchi: Wabunge 15 wa UKAWA watajwa kuhamia CCM. Yumo Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Taarifa ya James Millya kujivua ubunge wa Simanjiro kwa tiketi ya Chadema na kujiunga CCM, haiwezi kuwa habari kubwa katika kipindi ambacho takriban wabunge sita wameshafanya uamuzi kama huo.

Millya alitangaza uamuzi huo juzi, akisema anarejea CCM kuungana mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli na hivyo kuwa mbunge wa saba kuachia nafasi hiyo tangu uchaguzi wa mwaka 2015, ikiwa ni rekodi ya pekee tangu siasa za vyama vingi zirejeshwe nchini takribani miaka 25 iliyopita.

Alitangaza uamuzi huo saa chache baada ya katibu wa uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kutangaza kuwa chama hicho, ambacho kimekuwa kikiwapokea na kuwapa fursa ya kutetea nafasi zao wabunge wote wanaohamia CCM, kitawafungia mlango watakaoshindwa kutangaza kujiunga ndani ya miezi miwili.

Millya hakuwa na sababu inayotofautiana na waliomtangulia kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM; kuunga mkono jitihada za Rais, kurudi nyumbani na wengine wamekuwa wakitoa sababu za matatizo ya uongozi katika vyama vyao na kushindwa kutekeleza majukumu yao wakiwa upinzani.

Pengine “nani anayefuata” ndilo laweza kuwa swali kubwa kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa, na Mwananchi imekusanya taarifa, uchambuzi na mwenendo unaoweza kutoa picha ya kifuatacho katika sakata la hamahama linalohusisha wabunge na madiwani wa kuchaguliwa.

Millya, aliyeihama CCM 2013, alimshinda Christopher Ole Sendeka katika uchaguzi wa mwaka 2015. Sendeka sasa ni mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Arusha anaingia katika orodha ya wabunge na madiwani walioamua kurejea chama chao cha zamani baada ya kukaa upinzani, wengi kwa kipindi kifupi.

Baadhi walilazimika kuihama CCM kutokana na ama kukatwa katika mchakato wa kura za maoni za ndani wakati wa uchaguzi na kwenda kutafuta fursa upinzani, wengine kutokana na migogoro ya kiuongozi, tofauti na aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyejivua ubunge kwa maelezo kuwa CCM imeacha misingi yake na kutozingatia haki za binadamu.

Wabunge waliotimkia CCM mpaka sasa kutoka Chadema ni Mwita Waitara (Ukonga), Godwin Ole Mollel (Siha), Julius Kalanga (Monduli), Marwa Chacha (Serengeti) na James Millya (Simanjiro).

Wengine ni kutoka chama cha CUF ambao ni Zuberi Kuchauka (Liwale) na Maulid Mtulya (Kinondoni).

Waitara alitokea UVCCM baada ya kutokea mgogoro wa uongozi katika jumuiya hiyo, wakati Kalanga, Mollel, Kuchauka na Millya walitimkia upinzani kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo ya kuachwa katika kura za maoni.

Uchunguzi wa Mwananchi unaonyesha kuwa wabunge wenye historia na sifa kama hizo (waliojiunga upinzani miaka michache iliyopita) wapo takriban 15 na baadhi yao na wengine wasio na sifa kama hizo wamekuwa wakitajwa kuwa wataondoka, ingawa wamekuwa wakikanusha vikali.

Mmoja wao ni Saed Kubenea (Ubungo) ambaye mara kadhaa amehusishwa na mpango huo, lakini amekuwa akijibu kuwa hawezi kuhamia CCM na kwamba anaamini kuna watu ndani ya Chadema wanampiga majungu.

Kubenea alienda mbali zaidi na kudai kuwa ametibiwa nje ya nchi mara kadhaa bila gharama za Serikali na kwamba ameomba kutibiwa macho nje ya nchi, lakini amekataliwa kwa hiyo hawezi kuhamia chama hicho.

Mwingine ni mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu aliyetajwa na Waitara kuwa mmoja wa wabunge watano walio njiani, lakini amekanusha tuhuma hizo, akisema hawezi kuondoka Chadema na hajawahi kufanya mazungumzo na mbunge huyo wa Ukonga, akijinasibu kuwa yeye ni mmoja wa waasisi wa upinzani nchini na anajivunia historia hiyo.

Katika kundi hilo la watuhumiwa, yupo meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ambaye pia amekanusha vikali taarifa hizo, akisema amesikitishwa, kupata mshtuko na simanzi baada ya kusambaa taarifa alizoziita za kizushi na kuomba zipuuzwe kwa kuwa zina mpango wa kumchafua.

Mtuhumiwa mwingine mwenye ‘asili’ ya CCM ni Cecil Mwambe (Ndanda), ambaye alikatwa jina dakika za mwisho za kura za maoni kabla ya kujiunga na Chadema.

Pia yumo Esther Bulaya, ambaye alitangaza kujiondoa CCM muda mfupi baada ya Bunge la Kumi kuvunjwa na kuhamia Chadema ambako aliamua kushindana jimboni na kushinda.

Pengine tuhuma zinazovuka mipaka ya sifa za historia za waliojivua ubunge ni zile zinazoelekezwa kwa naibu katibu mkuu wa Chadema (Bara) na ambaye pia ni mbunge wa Kibamba, John Mnyika, ambaye hana historia ya kuwa au kuwania uongozi ndani ya CCM.

Kama ilivyo kwa wengine, Mnyika, ambaye ni mbunge kwa kipindi cha pili mfululizo baada ya awali kuongoza Ubungo, amesema taarifa hizo ni za uzushi na hana mpango wa kuhama Chadema.

Wengine kama Mnyika ni pamoja na Joshua Nassari, ambaye ni mbunge wa Arumeru Mashariki, Joseph Mkundi (Ukerewe), Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) na Jafary Michael (Moshi Mjini).

Katika idadi hiyo pia wapo wabunge wa CUF ambao ni Magdalena Sakaya (Kaliua), Abdallah Mtolea (Temeke), Maftaha Nachuma (Mtwara Mjini) na Musa Mbarouk (Tanga Mjini) ambao wamekuwa katika mgogoro na chama chao kwa muda mrefu.

Katika andiko lake la jana, mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amezungumzia hamahama hiyo akisema ni kitu kizuri kukijadili lakini akataka kuwepo na tahadhari kubwa.

Katika andiko hilo kwenye mtandao wa kijamii, Lissu anahoji: “Hivi inakuwaje wanaounga mkono jitihada za Rais Magufuli (na kuhama chama) ni wana Chadema pekee?

“Vipi akina (mwenyekiti wa TLP, Augustine) Lyatonga Mrema au Profesa (Ibrahim) Lipumba, (mwenyekiti wa UPDP, Fahmy) Dovutwa na wengineo wa vyama vingine. Au ndio kusema hawa hawana madhara yoyote kwa CCM hata wakibaki kwenye vyama vyao?”

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • IMG20181009044404.jpg
    IMG20181009044404.jpg
    68 KB · Views: 120
IMG_9153.JPG

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, John Mnyika.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, ni mmoja wa Wabunge 15 ambao wamekuwa wanatajwa tajwa kuhamia CCM muda wowote.
Wabunge hao sasa watakuwa kwenye sintofahamu ya kuhamia CCM hasa baada ya Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole kueleza kuwa, wanaotaka kuhamia CCM, wafanye hivyo kabla ya mwaka huu wa 2018 kuisha.

IMG_9150.JPG
IMG_9151.JPG
 
Parapanda litalia parapanda!Kwanini Stamina(kingunge) haukumpa ujumbe huu Roma(Nyerere)?
Ungemwambia kuna sayansi ya siasa imetamalaki,sasa ni kuunga mkono juhudi kwa gharama za walipa kodi!
 
Wahamie wote, hadi Mbowe halafu mimi niwe mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA nipange safu yangu ya wagombea ndani ya CHADEMA, halafu uitishwe uchanguzi uwe wa huru na haki kama sijaingia IKULU na wabunge wangu wakutosha, nisipo ingia Ikulu nipigwe risasi mbele ya vyombo vya habari local and international media

CCM siyo chama, ni genge la walaguzi, na mafisadi
 
Back
Top Bottom