CHADEMA Yampitisha Mshimbe Mgombea Zanzibar; Yatoa Taarifa kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Yampitisha Mshimbe Mgombea Zanzibar; Yatoa Taarifa kuhusu maamuzi ya Kamati Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Jan 24, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]
  TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAAMUZI YA KAMATI KUU
  [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Taarifa ifuatayo inatolewa kwa umma kuhusu Maamuzi ya Mkutano wa Kawaida wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), uliofanyika kwa siku mbili tarehe 20 na 22 Januari 2012 katika Hoteli ya New Africa Jijini Dar es salaam.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Mkutano huo wa kawaida wa Kamati Kuu ulikuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo Uteuzi wa mgombea wa uwakilishi wa Jimbo la Uzini na kupitisha mkakati na bajeti ya uchaguzi husika; Taarifa ya Kamati Maalum ya Kamati kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na Taarifa ya Fedha (Mapato na Matumizi ya chama) kwa mwaka 2011.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Kuhusu Uchaguzi wa Uwakilishi katika Jimbo la Uzini:[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Katika kikao chake cha tarehe 20 Januari 2012, Kamati Kuu ilimteua Ali Mbarouk Mshimba kuwa mgombea wa uwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Jimbo la Uzini kwa tiketi ya CHADEMA. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Aidha, katika kikao chake cha tarehe 22 Januari 2012 Kamati Kuu ya chama imepokea na kujadili mkakati na bajeti ya uchaguzi wa Jimbo la Uzini.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Kamati Kuu imeridhika na maandalizi ya awali ambayo chama kimeyafanya katika Jimbo husika na kuagiza sekretariati ya chama kufanya maandalizi zaidi kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi husika. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Pia, kamati kuu imefanya mapitio ya bajeti na kuweka kikomo cha matumizi ya fedha katika uchaguzi tajwa ili kuhakikisha kwamba kampeni zinafanyika kwa ufanisi na kuendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa mikakati husika kwa kuzingatia mahitaji.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kuhusu Taarifa ya Kamati Maalum kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba:[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kamati Kuu imepokea na kujadili taarifa ya Kamati Maalum kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 iliyoundwa na kamati kuu tarehe 20 Novemba 2011. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Pamoja na masuala mengine, Kamati Kuu ilitaarifiwa juu ya yaliyojiri katika mikutano kati ya Kamati Maalum ya CHADEMA na Rais Jakaya Kikwete na serikali tarehe 27 na 28 Novemba 2011 na tarehe 21 Januari 2012.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Aidha kamati kuu ilijulishwa hatua ambazo serikali imefikia katika maandalizi ya kuifanyia marekebisho sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 katika Mkutano wa Sita wa Bunge unaotarajia kuanza tarehe 31 Januari 2012.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Kamati Kuu imeamua kwamba Kamati Maalum iendelee kufanya mawasiliano na mashauriano na Rais Kikwete na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 inafanyiwa marekebisho ya msingi kabla ya mchakato wa kukusanya maoni kwa mujibu wa sheria husika haujaanza.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Kamati Kuu imeendelea kusisitiza Azimio lake la kikao cha Novemba 20, 2011 kwamba “Ushiriki wa CHADEMA katika mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya uliowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba utategemea utayari wa Serikali ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sheria hiyo kwa lengo la kujenga muafaka wa kitaifa juu ya mchakato huo”.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Aidha, Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu hatua ambayo imefikiwa na chama katika kufanya mikutano ya ndani katika maeneo mbalimbali ya kuelimisha viongozi, wanachama na wananchi kuhusu upungufu wa sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 pamoja na kupokea maoni kwa ajili ya kuboresha sheria husika.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT] [FONT=&quot]Kamati Kuu ya chama imeamua kwamba CHADEMA kiendelee kutekeleza azimio la kikao cha Kamati Kuu cha Novemba 20, 2011 la kutoa “kutoa elimu kwa wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na juu ya haja ya kuwa na sheria itakayoweka utaratibu bora zaidi wa kuunda Tume Shirikishi ya Katiba kwa lengo la kukusanya maoni ya wananchi, kuandaa ripoti na Rasimu ya Katiba Mpya, Bunge Maalum la Katiba na usimamizi wa kura ya maoni itakayowezesha wananchi kufanya maamuzi kwa uhuru na kwa haki”.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Kamati Kuu inaendelea kuwaagiza viongozi wote wa chama kama ilivyoelekezwa na Waraka wa Katibu Mkuu Namba 3 wa mwaka 2011, katika ngazi zote kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na madhara yake kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya na bora kwa nchi yetu kwa lengo la kuunganisha umma wa watanzania kuweza kufanya mabadiliko ya msingi.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]
  Kuhusu Taarifa ya Fedha (Mapato na Matumizi ya chama) kwa mwaka 2011:[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Kamati kuu imetaarifiwa kuhusu vyanzo mbalimbali vya mapato ya chama kwa mwaka 2011. Aidha Kamati Kuu imetaarifiwa kuhusu matumizi ambayo yamefanywa na chama katika mwaka 2011 kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa chama 2011-2016 na Mpango Kazi wa mwaka 2011.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  Kamati Kuu imejulishwa matumizi yaliyofanywa katika utekelezaji wa mipango kwenye vipaumbele mbalimbali ikiwemo upelekaji wa ruzuku majimboni/wilayani/mkoani; ulipaji wa madeni ya uchaguzi mkuu wa 2010 na uwekezaji; uendeshaji wa makao makuu ya chama; utekelezaji wa operesheni za chama na mfuko wa uchaguzi mkuu 2015.[/FONT][FONT=&quot]

  Kamati Kuu imepokea taarifa ya fedha kwa mwaka 2011 na kuagiza sekretariati ya chama kuandaa mkutano maalum kwa ajili ya kuendelea kujadili taarifa husika sanjari na Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2012; taarifa zaidi kuhusu fedha na mipango itaelezwa baada ya mkutano huo.[/FONT] [FONT=&quot][/FONT][FONT=&quot]
  Imetolewa tarehe 23 Januari 2012 na:[/FONT]

  [FONT=&quot]John Mnyika (Mb)[/FONT] [FONT=&quot]Mkurugenzi wa Habari na Uenezi[/FONT]
   
 2. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Naona hapa bado makamanda wanaendeleza kauli ya Kamanda Slaa kuwa tutajulishwa wanayoyajadili huko magogoni mda muafaka ukifika. Usiri huu mwishowe tutapigwa bao la kete.

   
 3. t

  true JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Chama makini na viongozi wake makini, ni lazima siku zote mambo yake yako wazi na mipango iko wazi. Heko CHADEMA kwa mikakati ya kutukomboa Watanganyika ktk huu ukoloni mambo ss wa hawa Magamba!!
   
 4. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  kuendelea kufanya siri kilichozungumzwa ikulu ndicho kilichowafanya hata mwanzo kikwete kuwaumbua....ngoja tuone. au mkienda huko hamna mnalokubaliana sasa huwa mnafanya nn
   
 5. Ibrahim K. Chiki

  Ibrahim K. Chiki Verified User

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ishara tosha ya utawala bora....! Big up chadema.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,521
  Trophy Points: 280
  Asante JJ Mnyika, uenezi Chadema imepata mtu!.
   
 7. L

  Luiz JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera sana kwa taarifa hii tunaomba sana mfanye zaidi ya hapa ili tuonekane kuwa chama chetu ni makini kama kauli mbiu ya chama ilivyo.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nimefurahishwa na taarifa hii kwa umma ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. Ni hatua nzuri kuujulisha umma yale yanayoendelea na yanayopangwa kuendelea.

  Kasoro moja niliyoiona, isipokuwa kama itakuwa ni "SIIRI ZA NDANI ZA CHAMA", ni vile kukosekana kwa takwimu juu ya bajeti zote mbili, ile ya matayarisho ya uchaguzi Uzini na ile ya mwaka ambayo pia kulitajwa vyanzo mbali mbali vya mapato kwa chama. Nahisi ingekuwa ni uwazi zaidi kuufahamisha umma juu ya hili. Lakni hili ni angalizo langu kwani sielewi taratibu za chama.

  Asanteni Makamanda kuwa kuwa karibu na wananchi.
  Demokrasia na maendeleo ni haki na wajibu kwa Watanzania.
   
 9. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #9
  Jan 24, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii................ulipaji madeni ya uchaguzi mkuu 2010...........................hapa ningepeda udadavuzi zaidi (Nani alikikopesha Chama, shs ngapi, kwa nini, kulikua na maridhiano ya chama kukopeshwa, yatalipwaje, ruzuku ya chama je? Vipi kuhusu uchaguzi mdogo wa hususan Igunga 2011, je haukua na madeni??)

  ...........Nachokoza tu........

  Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane kisha tusameheane.....R. Mtema (as she then was)
  Dada Amavubi-Rwanda
   
 10. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #10
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani bado siri kubwa sana! Mazungumzo kati ya kamati maalum na Ikulu na vp kuhusu marekebisho ya huo muswada, kweli ccm wamekubali kufanya hivyo! CHADEMA sasa na usanii wa ikulu.
   
 11. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #11
  Jan 24, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwanza nikupongeze Mh JJM lakn nimpongezi bwana Makene hakika unastahili hiyo nafasi na zaidi nimependa namna ambavyo mnatupa mrwjesho kwa kile mkifanyacho pamoja na CC yenu,Bravo CDM
   
 12. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Bw mnyika!,kwanza ni vema kushukuru na kukupongeza walau kwa kutoa taartfa hii,ninavyoona mimi si mbaya kama ungeweka paragraph inayosema walau hayo mazungumzo yanalenga nini kwa undani,na kama muda muafaka wa kuyatoa hadharani bado.basi pia ungeujulisha umma wa wapenda demokrasia ili na sisi tuendelee kuwa na subira.kumbuka kuwa uhai wa mti huanzia shinani, ambako ndiko tuliko sisi chimbuko la peoples power.

  Binafsi ninakukubali kwa kujitokeza kuwa kijana mwanasiasa makini,mwenye kutumia busara zaidi katika utendaji wa majukumu yako kuutumikia umma wa watanzania,na pia katika chama chako cha CDM.
  Lakini naomba pia ujitofautishe na makatibu wenezi (mazoea) wa hivi vyama vingine waliozoea kutulisha taarifa zenye walakini na za kijumla jumla kama hii uiyoanza nayo.nikutakie heri na mafanikio katika vita hii kubwa tuliyonayo dhidi ya Dhulma za mchana mchana .....Alutta Continuaaaaaaaaa
   
 13. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #13
  Jan 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,152
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Bw mnyika!,kwanza ni vema kushukuru na kukupongeza walau kwa kutoa taartfa hii,ninavyoona mimi si mbaya kama ungeweka paragraph inayosema walau hayo mazungumzo yanalenga nini kwa undani,na kama muda muafaka wa kuyatoa hadharani bado.basi pia ungeujulisha umma wa wapenda demokrasia ili na sisi tuendelee kuwa na subira.kumbuka kuwa uhai wa mti huanzia shinani, ambako ndiko tuliko sisi chimbuko la peoples power.

  Binafsi ninakukubali kwa kujitokeza kuwa kijana mwanasiasa makini,mwenye kutumia busara zaidi katika utendaji wa majukumu yako kuutumikia umma wa watanzania,na pia katika chama chako cha CDM.
  Lakini naomba pia ujitofautishe na makatibu wenezi (mazoea) wa hivi vyama vingine waliozoea kutulisha taarifa zenye walakini na za kijumla jumla kama hii uiyoanza nayo.nikutakie heri na mafanikio katika vita hii kubwa tuliyonayo dhidi ya Dhulma za mchana mchana .....Alutta Continuaaaaaaaaa
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni Kamati kuu kwa kazi nzuri
   
 15. O

  Omr JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CDM bana, sasa mnashabikia nini hapo? Nini cha maana kimeandikwa humo? Hawa ndio wanata kuongoza hii nchi?
   
 16. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,502
  Likes Received: 5,613
  Trophy Points: 280
  Taarifa imejitosheleza ingawa taarifa ya fedha ipo shallow kiasi nafikiri ingawa itajadiliwa kikao kijacho lakini kuna kitu kimeepukwa kutotaja takwimu! Wale wanaolazimisha mazungumzo kati ya CDM na mheshimiwa Rais kuwa wazi nafikiri hawako sahihi hasa kwa mkutano wa juzi maana uliopita kila kitu kipo wazi.inapotokea Mh Rais akataka ushauri kutoka CDM lazima kila kitu kiwe wazi? Nafikiri tunapaswa kujadili mchakato wa katiba unavyokwenda kwa kila hatua hata sasa kuna hatua mbovu nyingi tuzikemee wakati tunasubiri matunda ya haya maridhiano.tuache viongozi wafanye kazi tutayajadili matunda yake na tuendeleze majadiliano juu ya katiba ili viongozi wetu wajue msimamo wa sisi wananchi.Wanasiasa na serikali wana namna yao ya kufanya kazi na sisi wananchi yatupasa kuwasimamia wasiende kinyume tusiwape Chadema hadi akili zetu tukabweteka ingawa wanafanya kazi nzuri sana! Wananchi wenzangu tuwaache waendelee na maridhiano which is good kwa afya ya nchi lakini na sisi kwa nafasi zetu tuendeleze mapambano! Aluta Continua!
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona sioni taarifa ya majadiliano ya juzi? Mbona sioni taarifa juu ya mkutano wa Mbowe na Rais?
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii tulishaijadili humu muda mrefu. Kuna magari mwenyekiti aliyatoa kwa ajili ya uchaguzi lakini baadaye akasema yamechakazwa hivyo chama kiyanunue! Limekuwa deni. Nadhani helkopita pia ni sehemu ya deni!
   
 19. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mimi naona kila kitu kiko sawa. Kinachojadiliwa ikulu ni KATIBA na kwamba JK amekubali hoja za CDM na hivyo anarudisha ngoma bungen4 ikafanyiwe marekebisho. Kwangu mimi hayo ndo ya msingi, kwamba undani wa mazungumzo yalikuwaje, nani kasema nini mfano 'nisiposain wenzangu hawatanielewa' hayo tuache ila tupate conclusion za vikao kama hivi sasa
   
 20. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #20
  Jan 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tuache unafiki na unazi wa vyama.Hii taarifa haijajitosheleza na imeacha maswali mengi kwa umma. No clarity of content!
   
Loading...