mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,503
- 252
hapo kwenye ulipaji wa madeni ya 2010, kumbe baadhi ya wafadhili wameamua kukidai chama? Inaacha maswali kuliko majibu!
kaka lende acha unazi wa sisiem
hapo kwenye ulipaji wa madeni ya 2010, kumbe baadhi ya wafadhili wameamua kukidai chama? Inaacha maswali kuliko majibu!
Mzee heshima mbele
Mimi sitaki details nyingi ila mazungumzo na Ikulu lazima yawekwe wazi kila baada ya wao kukutana la sivyo hali ya CUF inatutisha. Hali na siasa sio siri lazima washika dau wapewe ni nini CDM wanafuata ikulu na kila hatua ili kutoa maswali na wasiwasi, kumbuka kule mwenye Ikulu ni CCM na CCM sio mwema hata kidogo kwa demokrasia ya TZ haipendi wala haitaki anajaribu kumrubuni yeyote kwa gharama yeyote.
Hivi hili lakusimamisha mgombea visiwani CDM wapo serious au wanabeep?Mmmh! Yangu macho!!
Sasa ulitaka ujue nini kilizungumzwa Ikulu? nilidhani watu wengi walikuwa wanataka picha sasa picha inaonekana hazitoshi tena. Ila tusubiri tuone je Kikwete atateua tume ya kupitia Katiba bila kubadilisha sheria na je itaanza kazi kabla ya mabadiliko ya sheria Bungeni? Huo ndio mstari uliochorwa.
Watanzania bwana, sasa watu mko kwenye mapambano, majenerali wamekaa na kupanga mikakati na kufanya mazungumzo; wanakuja kwa wapiganaji na kuwaambbia yale ambayo ni muhimu kw awapiganaji na kuonesha njia ya kuelekea ushindi. Wapiganaji wanaanza kuuliza details za kila kitu kilichozungumzwa? really?
Unless wanaotaka hivyo siyo wapiganaji isipokuwa wajumbe wa adui ambao wangependa kujua taarifa za ndani. CHADEMA wametoa taarifa inatosha kwa wakati huu mambo ya gharama zote n.k huwezi kuweka kila kitu hadharani ukiweka hesabu zako zote wazi adui zako wanaweza kujua una nguvu kiasi gani. Hawa wanaosema wanataka details zaidi hutawaona wakidai CCM iweke zaidi taarifa zake. why not?
Moja: Taarifa haijitoshelezi, mfano-Kulitokea nini huko Uzini mpaka sasa ufanyike uchaguzi na uteuzi wa mgombea wa chadema? Mwakilishi aliyechaguliwa 2010 amefariki au kavuliwa uanachama?Mbili: Vyama vyetu vijifunze kutumia fedha kwa umakini. Hii itatupa moyo kwamba hata wakiingia madarakani hawatatapanya mali na raslimali za watanzania. Chadema wana pesa sana siku hizi kiasi cha kufanyia mikutano New Africa Hotel? Mi nilidhani wangebana sana matumizi ili sehemu ya mapato yao yaelekezwe kijijini kuimarisha chama!!?
Yaani nimeisoma hii taarifa nilichopata zaidi ni lugha tamu ya porojo kuliko utendaji, kweli hilki ni chama maini na si makini !
Inaonyesha hata usivyo makini kutumia nafasi katika mtandao, una-quote habari kuu! Kweli wewe ni maini!
Demokrasia inaruhusu usipojaribu huwezi kujipima. After all mwanya wa vyama vingine vya upinzani kujipenyeza katika siasa za Zenji umeanzakuonekana. Watapanua tu!aahahaha.chadema imeingia kwenye Uchaguzi kwa nia ya kusindikiza wenyeji. akifika nyjiani atarudi kwao
Mkuu Mwanakijiji ni kwamba ukishaumwa na nyoka hata unyasi unaukimbia!! Usiri katika mazungumzo una historia mbaya hapa nchini ndio maana watu wanaogopa! Na mara nyingi usiri huwa hauna mwisho mwema kwa wale ambao hawana dola. Mwezi November 2011 walipokutana pande zote zilisaini communique lakini sasa tunaona vipande vipande vya taarifa.
Sasa ulitaka ujue nini kilizungumzwa Ikulu? nilidhani watu wengi walikuwa wanataka picha sasa picha inaonekana hazitoshi tena. Ila tusubiri tuone je Kikwete atateua tume ya kupitia Katiba bila kubadilisha sheria na je itaanza kazi kabla ya mabadiliko ya sheria Bungeni? Huo ndio mstari uliochorwa.