GE2025 CHADEMA yalia na idadi ya wapiga kura: "Hao milioni 2.6 wametoka wapi?"

GE2025 CHADEMA yalia na idadi ya wapiga kura: "Hao milioni 2.6 wametoka wapi?"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,599
Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi wa CHADEMA, John Pambalu amekosoa takwimu zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwa idadi ya wapiga kura mwaka huu inafikia zaidi ya 37.6, wakisema idadi hiyo inapingana na takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotoa idadi ya Watanzania katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Akizungumza katika uzinduzi wa ratiba ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Tanzania Bara, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC), Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema jumla ya Wapiga Kura walioandikishwa kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 ni Milioni 37.6.

Aliongeza kuwa kati ya idadi hiyo, Milioni 18.9 ni Wanawake, sawa na Asilimia 50.31, huku Wanaume wakiwa Milioni 18.7, sawa na Asilimia 49.6. Aidha, Watu wenye Ulemavu walioandikishwa ni 49,174.

Msikilize:



 
Back
Top Bottom