CHADEMA Yajitoa mchakato wa Katiba; Yadai Rais kawauza!

Hivi kama asingesaini kingetokea nini? Mimi nafikiri anasaini halafu kama kuna marekebisho yanapelekwa tena Bungeni. Kwa hiyo inawezekana marekebisho yaliyopendekezwa na Chadema yakapelekwa tena vikao vijavyo.
 
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011, kimekiuka makubaliano yao, hivyo kimeamua kususia mchakato mzima wa kuratibu maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kwa kutumia sheria hiyo. Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kuonyesha kutoridhishwa na namna kiongozi huyo wa nchi, alivyowachezea akili.

"Kitendo cha Rais Kikwete kuusaini muswada huo bila ya kuupitia ni kinyume na makubaliano, jambo ambalo linatufanya tususie mchakato mzima wa kuuratibu maoni ya kwa ajili ya Katiba Mpya kupitia sheria ailiyoisaini,"alisema Mnyika na kuendelea: “Tumeamua kujitoa kwenye mchakato mzima wa kuratibu Marekebisho ya Muswada wa Sheria ya Katiba kutokana na Rais kukiuka makubaliano yetu Ikulu yaliyomtaka aupitie kwanza kabla ya kuusaini.”

Mnyika aliendelea kueleza kuwa Chadema iliwasilisha waraka wa mapendekezo sita kwa Rais ikiwa ni pamoja na kumtaka asiusaini muswada huo kutokana na wananchi kutoshirikishwa ipasavyo kwenye mchakato wa ukusanyaji wa maoni.

Zaidi: Chadema: Rais ametuuza

Hivi katika makubaliano aliyosaini Mnyika kulikuwa na kipengele kwamba Rais asisaini mswada? Au ile haikuwa sahihi ya Mnyika? Mnyika rejea hati uliyosaini wewe na Nchimbi na kama ni ya kughushi utuambie ila kama ni yako kwako wewe ndio inakiuka makubaliano. Vinginevyo useme ulisaini kitu ambacho hukukijua (kitu ambacho siamini). Ukiwa kama Mbunnge wangu mimi binafsi nakuamini sana.
 
Hivi mnaamini CDM kweli hawakujua wanachofanya? Mlitaka wakurupuke tu na maandamano bila kuonyesha utashi wa kisiasa kwenye 'mgogoro' huo? Mnataka kuamini kabisa kuwa JK/CCM wangekubaliana kikamilifu na madai ya CDM wakati ambapo CCM na Serikali hawakutaka hata Wananchi watoe maoni yao?
Naamini tumeona nia ya CDM na pia nia ya CCM na Serikali, sasa CDM wanayo haki kufuata njia mbadala na hakuna wa kuwalaumu, Wananchi tuna wajibu wa kuwaunga mkono.
 
Ifike mahala CHADEMA wajiulize kama matamshi, kauli, hatua na vitendo vyao mara kwa mara wanatumwa na WANACHAMA wao au wafuasi wa chama chao? CHADEMA inataka kuwa himaya ya VIONGOZI pekee? Wanapoibana serikali ya JK izingatie maoni ya wananchi wao wanalifanya hili kwenye maamuzi yao mbalimbali? CHADEMA isiwasemee WATANZANIA kwa ujumla wao kwani hata CCM si ya WATANZANIA wote.
 
Ninachohisi mimi hata huo mswada ukirudi tena bungeni kufanyiwa marekebisho. Cdm watatoka kama kawaida yao maana sio rahisi yanayotaka wao yote wakubaliwe.wamekwisha poteza hiyo bahati sasa wao watakuwa kama sisi raia tu.
 
Mnyika ndo katuuza. Katika makubaliano aliyotia saini pale Ikulu wakati anapiga ile 'tea', hakuna hata moja lilosema kuwa mmekubaliana rais asisaini muswada kuwa sheria kabla ya marekebisho. Ni afadhali muheshimiwa Mnyika akae kimya na atuombe radhi kwa kutokutafakari makubalianao kabla ya kusaini. Ni sawa kabisa na wale wanaoingia mikataba mibovu.

Waliamini hata saini kwa7bu ya mazingira ya majadiliano waliyokuwa wakifanya naye. Kwa maana nyinge makubaliano ya kutokusaini muswada huo yalifikiwa by implication in the course of majadiliano na raisi na sio expressly ktk maandishi.
 
Hivi katika makubaliano aliyosaini Mnyika kulikuwa na kipengele kwamba Rais asisaini mswada? Au ile haikuwa sahihi ya Mnyika? Mnyika rejea hati uliyosaini wewe na Nchimbi na kama ni ya kughushi utuambie ila kama ni yako kwako wewe ndio inakiuka makubaliano. Vinginevyo useme ulisaini kitu ambacho hukukijua (kitu ambacho siamini). Ukiwa kama Mbunnge wangu mimi binafsi nakuamini sana.

Nini sababu ya kumuona rais kabla muswada kusainiwa, ili asisaini, turekebishe mapungufu ili tuepuke gharama za kuwalipa sitting allowance wabunge kwa makosa ambayo tumekubali kuyarekebisha, kimsingi tuna rais asiyeheshimu uchumi, anaweza uza nyumba apate hela kumcheza mwanae. ichukie ccm.
 
Tukiachana na malalamiko ambayo baadhi yetu tunawatupia cdm ambao wanawabunge 28 tu wa kuchaguriwa, sisi tumerizika na mswada ambao jk ameusaini, kwa sababu katiba mpya si ya cdm pekee bali watanzania wote, hakuna mwana ccm yeyote anayetaka rais apunguziwe madaraka yake kikatiba na hilo watapigania mpaka mwisho kwa sababu wakikosa ubunge kipindi kijacho rais huwachagua kuwa wakuu wa mikoa,wilaya au makatibu wa wizara.
 
...True.

...Niliposikia Kikwete atakutana na Chadema nikapata wasiwasi, kwani hao jamaa walijua fika Rais hawezi kugeuka nyuma. Walichofanya ni kwenda kuhalalisha matendo yao ya baada.

...And lets not kid ourselves, Serikali haina mwonekano mzuri siku hizi. Tena Kikwete ndio zaidi. Chochote watakachoongea Chadema juu ya hili kitaaminiwa tu.

...I smell lots of trouble.
Mkuu, nnamisi sana jamvini, namisi pointi zako za nguvu.
Wapi Mwiba, Kibunango na Mtu wapwani?
 
Mnyika ndo katuuza. Katika makubaliano aliyotia saini pale Ikulu wakati anapiga ile 'tea', hakuna hata moja lilosema kuwa mmekubaliana rais asisaini muswada kuwa sheria kabla ya marekebisho. Ni afadhali muheshimiwa Mnyika akae kimya na atuombe radhi kwa kutokutafakari makubalianao kabla ya kusaini. Ni sawa kabisa na wale wanaoingia mikataba mibovu.

Kama raisi kawauza chadema na ninyi viongozi wa chadema mmetuuza wananchi tuliokuwa tunawategemea kurekebisha mambo. Kama ulivyosema hapo juu, ile karatasi yenye para mbili tu iliyosainiwa sijui kama mheshimiwa mnyika aliisoma kabla hajasaini au alikuwa ameshalewa juice ya ikulu, kwa sababu inatamka wazi kuwa "hata kama muswada huu utasainiwa utaendelea kuboreshwa na mawasiliano ya mara kwa mara yatafanyika".

Utaona kwamba hapa ni wazi makubaliano yalikuwa muswada usainiwe bali maboresho yaendelee. Sasa hapa cdm ndipo walipochemka kwa kujua au kutokujua. Hapa sijui wamesaini baada ya kuchanganyikiwa kwa kuingia ikulu au ni vipi sijui. Nadhani wangesaini baada ya kuandika "hata kama muswada utasainiwa na kuwa sheria hautaanza kutumika mpaka utakapofanyiwa marekebisho" hapa ingeeleweka lakini kilichosainiwa kinatoa idhini kwa serikali na magamba yake kuendelea na mchakato. CHADEMA MMETUANGUSHA INAFAA MKIRI HILI NA KUFIKIRIA SASA NINI KIFANYIKE.
 
Ifike mahala CHADEMA wajiulize kama matamshi, kauli, hatua na vitendo vyao mara kwa mara wanatumwa na WANACHAMA wao au wafuasi wa chama chao? CHADEMA inataka kuwa himaya ya VIONGOZI pekee? Wanapoibana serikali ya JK izingatie maoni ya wananchi wao wanalifanya hili kwenye maamuzi yao mbalimbali? CHADEMA isiwasemee WATANZANIA kwa ujumla wao kwani hata CCM si ya WATANZANIA wote.

..kwani wajibu wa Chama cha Siasa ni kuwasemea na kuwatetea wanachama wake na viongozi wake tu??
 
Ifike mahala CHADEMA wajiulize kama matamshi, kauli, hatua na vitendo vyao mara kwa mara wanatumwa na WANACHAMA wao au wafuasi wa chama chao? CHADEMA inataka kuwa himaya ya VIONGOZI pekee? Wanapoibana serikali ya JK izingatie maoni ya wananchi wao wanalifanya hili kwenye maamuzi yao mbalimbali? CHADEMA isiwasemee WATANZANIA kwa ujumla wao kwani hata CCM si ya WATANZANIA wote.

Wewe subiri chausta watakusemea, acha chadema watusemee sisi.
 
Hivi katika makubaliano aliyosaini Mnyika kulikuwa na kipengele kwamba Rais asisaini mswada? Au ile haikuwa sahihi ya Mnyika? Mnyika rejea hati uliyosaini wewe na Nchimbi na kama ni ya kughushi utuambie ila kama ni yako kwako wewe ndio inakiuka makubaliano. Vinginevyo useme ulisaini kitu ambacho hukukijua (kitu ambacho siamini). Ukiwa kama Mbunnge wangu mimi binafsi nakuamini sana.
Yale makubaliano sio by law mkuu, ni utashi tu kisiasa uliokuwa unahitajika, hakuna upande wowote ambao unaweza kumshitaki mwenzake kisheria kwa kukiuka makubaliano yale.
Kwa mtu mchokonozi ni lazima ajiulize ni kwa nini Dr Slaa asiwepo kwenye vile vikao vyote viwili, kumbuka sababu ya kutohudhuria kwake ni ya kufikirika haiingii akilini. Think loud!
 
WanaJF

Hakika Mhe. Zitto ni kichwa. Nina uhakika kama Mhe. Zitto angekuwepo, hicho wanachoita "makubaliano na Mhe. Rais" asingeweza kukikubali. Mhe. Rais kusaini huo Muswaada ni sawa, kwa sababu "makubaliaono" hayakuwa na chochote kitakacho mzuia asiusaini.

Mhe. Rais kwa mujibu ya Sheria hii, atateua TUME ya kukusanya maoni na kuratibu zoezi zima la uundwaji wa Katiba Mpya. Nina amini, Mhe. Mnyika, Mhe. Mrema, Mhe. Cheyo, Mhe. Kafulila ni miongoni mwa watakaoteuliwa kuwa kwenye hiyo Tume. CDM mkisusia hilo zoezi, bado maoni yatakusanya...na Katiba Mpya itaundwa.

Wito wangu: Kubalini kuwa HESABU zenu hazikwenda sawa.....kuanzia siku ile mnatoka nje ya ukumbi wa Bunge....mkisusia kuchangia kwenye Muswaada ambao sasa ni Sheria......tena kali sana!
 
Na huyu ni nani?

  • [h=6]Zitto Z Kabwe

    Serikali na Chadema kukubaliana kujenga kuaminiana, kuwasiliana mara kwa mara na kushauriana ili kujenga Mwafaka wa Kitaifa kuhusu Katiba ni hatua nzuri na ya kupongeza katika demokrasia yetu. Nampongeza Rais Kikwete na Mwenyekiti Mbowe. Pia nawapongeza Wazee waliosaidia kutufikisha katika Mwafaka huu. Katiba inaweza kutafutwa Barabarani lakini inaandikwa mezani. Daima Maslahi ya Taifa kwanza, vyama baadaye. Mungu ibariki Tanzania[/h]

Nimesikitika maoni ya Dr. Bana na Ndg. Mtatiro, kuwa eti tusubiri kuona ubora wa tume. Kwa mwendo huu tuamini kuwa tayari katiba ya CCM imeshaandikwa, kinachosubiriwa ni formalities tu za kuipitisha.

Upuuzi ulishafanyika tangia Bunge kuukubali mswada ule, hata CDM wasingeenda Ikulu ilikuwa lazima JK asikiangushe chama chake, kwani katiba inamaslahi zaidi kichama (4milion people) dhidi ya wananchi (over 40 million). Nimesikitika sana na usanii huu unaoendelea katika nchi hii....
 
Back
Top Bottom