CHADEMA Yajitoa mchakato wa Katiba; Yadai Rais kawauza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Yajitoa mchakato wa Katiba; Yadai Rais kawauza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Dec 1, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ya mwaka 2011, kimekiuka makubaliano yao, hivyo kimeamua kususia mchakato mzima wa kuratibu maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya kwa kutumia sheria hiyo. Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa hatua hiyo imefikiwa ili kuonyesha kutoridhishwa na namna kiongozi huyo wa nchi, alivyowachezea akili.

  "Kitendo cha Rais Kikwete kuusaini muswada huo bila ya kuupitia ni kinyume na makubaliano, jambo ambalo linatufanya tususie mchakato mzima wa kuuratibu maoni ya kwa ajili ya Katiba Mpya kupitia sheria ailiyoisaini,"alisema Mnyika na kuendelea: "Tumeamua kujitoa kwenye mchakato mzima wa kuratibu Marekebisho ya Muswada wa Sheria ya Katiba kutokana na Rais kukiuka makubaliano yetu Ikulu yaliyomtaka aupitie kwanza kabla ya kuusaini."

  Mnyika aliendelea kueleza kuwa Chadema iliwasilisha waraka wa mapendekezo sita kwa Rais ikiwa ni pamoja na kumtaka asiusaini muswada huo kutokana na wananchi kutoshirikishwa ipasavyo kwenye mchakato wa ukusanyaji wa maoni.


  Zaidi: Chadema: Rais ametuuza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hawa CHADEMA nao kama hawaeleweki eleweki vile...
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  chadema mliyataka wenyewe hakuna wa kumlaumu ndoa na ccm imewashinda mnaleta visingizio
   
 4. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mnyika kwani ulitaka mapendekezo yote lazima Jk ayakubali? kama yalikuwa sita unajuaje labda matano yalibaki kayakubali?
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kusema lakini Chadema inaonekana kutokujua inachofanya.
   
 6. i

  iMind JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,906
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Yaani hata mimi siwaelewi, nilitegemea wangevuta subira ili kuona kama serikali itapeleka mapendekezo ya kurekebisha sheria hii katika bunge lijalo. Job true true
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kukataa pendekezo moja tu kati ya sita sio kukiuka mapendekezo. chadema wakubali win win situation katika mazungumzo na Rais. kama walikwenda Ikulu ili matakwa yao yote yatekelezwe ni kumjaribu JK vibaya
   
 8. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Walitakiwa wafanye nini?
   
 9. s

  shukia Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa makubaliano yale na JK ambayo yalisainiwa na Mnyika na Nchimbi hakuna hata moja lililosema kuwa Rais asisaini Muswada kabla ya marekebisho.

  Ila nakumbuka la kwanza lilikuwa linasema "Pamoja na sheria hiyo kupitishwa na Bunge ipo haja ya kuendelea kuiboresha ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa".

  Sina hakika kama mlilielewa hili. Yawezekana mlinogewa chai ya Ikulu na kushindwa kulitafakari hili kabla ya kulisaini. Kwa maana hiyo kusema kwamba rais kawauza mmeniboa
  .
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Kumbe na wewe umeona eeh
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kurugenzi za mawasiliano Magogoni, hebu jitulize kidogo; taratibu mkuu!!

   
 12. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  unataka kutuaminisha kwamba swala la hii sheria ni swla la hisani ya Kikwete?
  kwamba anweza kuamua atakavyo kwasababu he is the president na sisi tunyamaze kwasababu ameamua hivyo?

  the bigger issue here is, issue za msingi zizingatiwe..........binafsi najua kwamba hakuna jema linaloweza kutoka kwa CCM wala JK wa CCM.......sio katiba mpya wala tanzania tuitakayo.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mnyika huko sio kujitoa mlishajitoa muda mrefu mlikwenda ku-mbeep Jk na yeye kawapigia hamtaki kupokea simu
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  kurugenzi ya mawasiliano chadema, hebu jiulize kidogo, taratibu mkuu!!!
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  mama porojo hao chadema ni porojo tupu
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwani ni nani anyeongoza nchi hii?
  Haiwezekani kupata katiba kwa njia wanayoitaka mpaka waingie madarakani.
  Mbona Lema kimya?....
   
 17. s

  shukia Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyika ndo katuuza. Katika makubaliano aliyotia saini pale Ikulu wakati anapiga ile 'tea', hakuna hata moja lilosema kuwa mmekubaliana rais asisaini muswada kuwa sheria kabla ya marekebisho.

  Ni afadhali muheshimiwa Mnyika akae kimya na atuombe radhi kwa kutokutafakari makubalianao kabla ya kusaini. Ni sawa kabisa na wale wanaoingia mikataba mibovu.
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Mnyika naona unaona maoni ya watu wengi hapo juu, hata kitaani ni hivyo hivyo

  All I can say to you guys please STICKY to your decision, chadema ijulikane ina mlengo gani, mlengo wa kulia, kushoto au kati, amueni kuwa radicals na dunia ijue hivyo...au muwe kondoo na dunia itawajua hivyo. Mmekuwa mnabadilika badilika sana.....

  Hata iwe vipi hamtakuwa na uwezo wa kumfurahisha kila mtu.....ila amueni muwe vipi na mtavuta wengine kwa vile mtakavyokuwa!!

  Leo mtakasirika, kesho mtamchekea yule yule aliyewakasirisha jana, kitu gani huwa kinatokea??...hatujui

  Lingine, jamani ikiwezekana hiyo ruzuku ichukue nafasi ya posho zenu za bungeni...susieni vikao vya bunge na DUNIA ijue hivyo CCM wanajua kuwa huwa mnatisha leo....mnakuja kesho! this aint good not neither for your supporters nor for your members.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  pepoooooooooooooooooooo mnalo hilo kachukueni barua yenu mlango wa Ikulu
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  They never seem to have plan B before taking plan A.

  Nakupa guarantee hawawezi kususa hadi mwisho wa huo mchakato.
  Watakuja kubadili maneno tu baadae kuwa hatukuwaelewa kama madai yao ya kutomtambua rais
   
Loading...