Ndugu yangu hoja si CHADEMA kufutika, suala kubwa ni 50% ya watanzania wanaohitajika kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wao wataowaongoza kuamua kukaa nyumbani, vijiweni au mashambani na kupuuzia haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Jiulize ni kwanini?
Soma taarifa ya KATIBU WA CCM (Mh Bashiru) juu watanzania 50% kutoshiriki kuchagua viongozi wao mwaka 2010. Mbaya zaidi kaeleza kuna chaguzi ambazo walioshiriki walikuwa ni 30%, jiulize hivi 70% ilikuwa wapi? Kama hii namba haina maana kwako, ina maana sana katika process nzima ya demokrasia.
“(Wameanza tabia) Ya kukaa nyumbani kwa sababu wanaona ni kituko, ni mchezo wa kuigiza. Ndio maana leo kupata watu kwenda kupiga kura imekuwa shida. Note (angalia), tunakoshinda ni chini ya asilimia 30, chini ya asilimia 40. Hakuna mahali ambako wapigajikura wamejitokeza kwa asilimia 50," alisema Dk Bashiru.
"Na mwaka 2010 ulitia fora. Watu wengi walijiandikisha, kumbe walikuwa wanataka kile kiparata (kitambulisho cha mpigakura), kwa sababu kinatumika kwenda polisi kudhamini, kujitambulisha.
“Walipokipata wakaingia mitini. Kwa Mara ya kwanza katika historia ya nchi hii tulipata Serikali ambayo haina uhalali wa kisiasa kwa sababu wapigajikura wengi zaidi ya ailimia 50 walibaki nyumbani." Nukuu tka kwa Dr Bashiru.
Hii namba ya watanzania wanaojiandikisha na kutokwenda kupiga kura ndio ya kukuumiza wewe kichwa sio CHADEMA au CUF kama unavyofikiri wewe.
Mashabiki/wafuata bendera/wapambe/walia tumbo fungueni akili zenu na muelewe kuwa kinachohitajika ni kuboresha hali ya wananchi na sio kupoteza muda wenu mwingi kufa na CHADEMA na vyama vingine vya upinzani. Kutumia pesa kununua wabunge/madiwani na viongozi wa upinzani si dawa ya kuboresha maisha ya wananchi. Ni siasa chafu, siasa za ujima na potofu na inayoitoa Tanzania katika medani za siasa. Tanzania oyeeeeeeeeeeeee.