CHADEMA Yafanya kufuru Ukonga

CHADEMA Yafanya kufuru Ukonga

Daaaaah! Nafsi yangu imefarijika sana yaani nina amani mpaka bhaaaaaaaas!!
 
Wekeni mikutano iyo live through jf. inaleta matumaini. kila mara mwisho wa mikutano wakumbusheni watu kujiandikisha na kpiga kura wakati ukiwadia.

...kweli mkuu,hapo kwenye kujiandikisha na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ndo tuweke msisitizo...
 
Waooh!
Hii thread imenifanya niagize konyagi bila kupenda.
Very interesting! Propaganda za ccm zimefeli na kufika kikomo.
Ukisoma thread zingine huko utaona jinsi Mkutano wa Mwgulu ulivyoaibisha hapo jana.
Ccm ni lazima mkubali kuwa muda wa kuitwa WAPINZANI umefika.
Msiue watu kwa kuwakataa bana.

.....Arusha Elerai na Kaloleni Waislam waliongoza kwa kuipa kura Chadema!!!
 
Salute sana kamanda Molemo kwa kuwasilisha taarifa hii kwa wadau wa JF!
Kama ulivyosema ni kweli huo ni mkutano ulioandaliwa na Tawi la Chadema Mazizini chini ya usimamizi wa uongozi wa kata ya Ukonga. Sasa unaweza kuona ni kwa kiasi gani makamanda wameiva kiasi kwamba wanaweza kuandaa mkutano mkubwa kiasi hicho katika ngazi ya mtaa/tawi!
Bahati mbaya mimi nilipata dharura majira ya saa saba wakati tunakaribia kuanza mkutano na nikalazimika kuelekea hosoitali mwanangu aliugua ghafla lakini nilikuwa napata taarifa toka kwa makamanda wakinijulisha jinsi mkutano ulivyokuwa umefana!
Tunaendelea na maandalizi muda si mrefu tutaandaa mkutano mwingine mtaa wa Mongolandege ili kuhakikisha kuwa kata ya Ukonga inaongoza harakati za kuifuta ccm katika jimbo la Ukonga!
Mura,
Hope kijana anaendelea vyema mpe pole, lakini unatakiwa uwe karibu kidogo na familia hao chadema wanakuzeesha tu jamaa yangub

Mkono wa binadamu hautaanguka, jaribu dili nyingine
 
.....

........Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema........

Hii kitu kama ni kweli, itawamaliza kabisaaaa Magamba...maana wa mewatumia sana maseikh kupropagate!!
 
Kama ilivyotangazwa awali CHADEMA leo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Ukonga Eneo la Mazizini.

Mkutano huo ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche akishirikiana na vijana wa Bavicha Jimbo na viongozi wa Jimbo na Kata.

Yaliyojiri mkutanoni:

Mkutano huu ulikuwa ni wa Kata tu lakini cha kustaajabisha ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi kwamba ulionekana ni mkutano wenye hadhi ya kitaifa.

Mjumbe wa Sekretariati ya Bavicha Taifa aliyeongozana na Heche alisema vijana wameamua kuleta mageuzi na watapambana bila kuogopa chochote alimradi wanafuata sheria na taratibu.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Sheikh Mwaipopo akihutubia umati mkubwa wa watu alilaani CCM kwa kuendesha propaganda za udini na sasa zinahatarisha amani ya nchi.

Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Mkiti wa Bavicha Taifa John Heche alilaani CCM kwa kukataa mapendekezo yote ya msingi yaliyoko katika Rasimu ya Katiba mpya.

Heche amewaambia wananchi kwamba kuanzia kesho Chadema inaanza ziara katika nchi nzima kutumia anga na nchi kavu kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu katiba mpya.

Katika hali ya kusikitisha wananchi walihuzunika sana baada ya Heche kuwaeleza jinsi wabunge wa CCM walivyovizia kipindi ambacho Chadema hawakuwepo bungeni na kupitisha harakaharaka kodi ya laini za simu.

Mara baada ya mkutano huo wananchi waligawiwa bure Nakala za rasimu ya katiba bure.Kwa muda mchache nakala zaidi ya mia mbili ziliisha na pia mamia ya wanachama wapya walichukua kadi za Chadema na mpaka naandaa taarifa hii bado kulikuwa na foleni kubwa ya wanachama wanaosubiri kadi mpya.

NB:
Nimeshindwa kupiga picha kutokana na aina ya simu niliyokuwa nayo.Hata hivyo nikifanikiwa kupata picha kutoka kwa makamanda waliokuwepo nitaziweka.
tundu2.jpg


tundu1.jpg


tundu3.jpg
 
Mkuu Molemo nimefanikiwa kupata baadhi ya picha zilizopigwa.
IMG-20130804-WA0010.jpg
Mwenyekiti wa Bavicha Kamanda John Heche akihutubia wakaazi wa Ukonga Mazizini.
IMG-20130804-WA0011.jpg
Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano mtaa wa mazizini wakimsikiliza kamanda Heche.
 
Last edited by a moderator:
Salute sana kamanda Molemo kwa kuwasilisha taarifa hii kwa wadau wa JF!
Kama ulivyosema ni kweli huo ni mkutano ulioandaliwa na Tawi la Chadema Mazizini chini ya usimamizi wa uongozi wa kata ya Ukonga. Sasa unaweza kuona ni kwa kiasi gani makamanda wameiva kiasi kwamba wanaweza kuandaa mkutano mkubwa kiasi hicho katika ngazi ya mtaa/tawi!
Bahati mbaya mimi nilipata dharura majira ya saa saba wakati tunakaribia kuanza mkutano na nikalazimika kuelekea hosoitali mwanangu aliugua ghafla lakini nilikuwa napata taarifa toka kwa makamanda wakinijulisha jinsi mkutano ulivyokuwa umefana!
Tunaendelea na maandalizi muda si mrefu tutaandaa mkutano mwingine mtaa wa Mongolandege ili kuhakikisha kuwa kata ya Ukonga inaongoza harakati za kuifuta ccm katika jimbo la Ukonga!

.........Mwita Maranya Pole Kamanda usihofu Junior Kamanda atapona haraka .....Magamba wanazidi kuhombokela!!!!
 
... Katikati ya eneo lenu kuna sehemu pale inaitwa MARKAZ
wakazi wote wa enoe hilo ni wafuasi wa CUF "je CDM mmeweza kufungua shina (tawi) eneo hilo?"

Mkuu nimeshafungua tawi hapo Markazi na muda si mrefu ninaizika rasmi cuf. Nilifungua tawi hapo Marikazi mwishoni mwa mwaka jana tukiwa na wanachama 39 lakini hadi kufikia mwezi wa tatu mwaka huu tulikuwa na wanachama 72.
 
Asante sana kwa taarifa , japo nimefuturu uji na maharage lakini kwa uzi najiona kama nimefuturu mchemsho wa mbuzi !
 
...we heche wewe utamuua savimbi kwa presha...
 
Back
Top Bottom