CHADEMA Yafanya kufuru Ukonga

CHADEMA Yafanya kufuru Ukonga

Wapo wapuuzi ndani ya chama cha majizi ambao wao kila mara ni kudanganya watu mara Chadema ni chama cha Wakristo mara chama cha wachaga mara chama cha watu wa kaskazini,ni jinsi gani wameishiwa hoja vichwani mwao hivyo wanatafuta hoja nyepesi kwa kudanganya watu

Sasa hivi walikuwa wakimsakama Dr Slaa wameishiwa hawana mpya wametulia au bado mnatunga uongo mwingine?
 
magamba mpaka wakimbie hapo kiukweli wameshikwa vibaya sana

Mkuu big victor Kwa Ukonga magamba watapata kipigo cha mbwa kwenye uchaguzi.Ni jimbo pekee ambalo huwezi kuamini kama liko Dar.Barabara zake zote ni mbovu na kipindi cha mvua nauli ya daladala hufika mpaka 1000/-
 
Last edited by a moderator:





[h=3][/h]
IMG-20130804-WA0010.jpg
​
Kama ilivyotangazwa awali CHADEMA jana wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Ukonga Eneo la Mazizini.Mkutano huo ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche akishirikiana na vijana wa Bavicha Jimbo na viongozi wa Jimbo na Kata.​
--
​
Yaliyojiri mkutanoni:

Mkutano huu ulikuwa ni wa Kata tu lakini cha kustaajabisha ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi kwamba ulionekana ni mkutano wenye hadhi ya kitaifa.Mjumbe wa Sekretariati ya Bavicha Taifa aliyeongozana na Heche alisema vijana wameamua kuleta mageuzi na watapambana bila kuogopa chochote alimradi wanafuata sheria na taratibu.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Sheikh Mwaipopo akihutubia umati mkubwa wa watu alilaani CCM kwa kuendesha propaganda za udini na sasa zinahatarisha amani ya nchi.



Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema.



Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Mkiti wa Bavicha Taifa John Heche alilaani CCM kwa kukataa mapendekezo yote ya msingi yaliyoko katika Rasimu ya Katiba mpya.

Heche amewaambia wananchi kwamba kuanzia kesho Chadema inaanza ziara katika nchi nzima kutumia anga na nchi kavu kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu katiba mpya.

Katika hali ya kusikitisha wananchi walihuzunika sana baada ya Heche kuwaeleza jinsi wabunge wa CCM walivyovizia kipindi ambacho Chadema hawakuwepo bungeni na kupitisha harakaharaka kodi ya laini za simu.



Mara baada ya mkutano huo wananchi waligawiwa bure Nakala za rasimu ya katiba bure.Kwa muda mchache nakala zaidi ya mia mbili ziliisha na pia mamia ya wanachama wapya walichukua kadi za Chadema na mpaka naandaa taarifa hii bado kulikuwa na foleni kubwa ya wanachama wanaosubiri kadi mpya.



​



 
CDM songa mbele kwa kasi ya Anga, Nchi kavu , na majini hadi hawa magamba CCM wanyooshe miko. Kudadadeck!!
 
CCM ni Chama Cha wauza Madawa, na wanajuana kwa majina lakini hawatajani kama unabisha muulize yule mpangaji aliyepangishwa kinguvu kule magogoni na NEC, atakakwambia anawajua lakini hawataji
 
CCM ni Chama Cha wauza Madawa

Kuanzia mwenyekiti wao wa Taifa - Teja, mawaziri balaa, wabunge wa CCM ndiyo usisema. Hawa jamaa sijui akili zao ziko wapi. Kazi kweli kweli kuongozwa na akili za Teja na wauza unga!
 
Kuanzia mwenyekiti wao wa Taifa - Teja, mawaziri balaa, wabunge wa CCM ndiyo usisema. Hawa jamaa sijui akili zao ziko wapi. Kazi kweli kweli kuongozwa na akili za Teja na wauza unga!
CCM ni sawa na UKOO WA PANYA. Kwani Baba mwizi, Mama mwizi, Mtoto mwizi, Dada mwizi, Kaka mwizi, Babu mwizi, Bibi mwizi, Shemeji mwizi, Mkwe mwizi. UNABISHA? Sasa tumia dawa itwayo CHADEMA kuangamiza kabisa ukoo huu wa wadudu waharibifu wa mali asili ya nchi yetu. UPATAPO UJUMBE HUU MTARIFU NA MWINGINE.
 
Back
Top Bottom