CHADEMA Yafanya kufuru Ukonga

CHADEMA Yafanya kufuru Ukonga

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Kama ilivyotangazwa awali CHADEMA leo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Ukonga Eneo la Mazizini.

Mkutano huo ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche akishirikiana na vijana wa Bavicha Jimbo na viongozi wa Jimbo na Kata.

Yaliyojiri mkutanoni:

Mkutano huu ulikuwa ni wa Kata tu lakini cha kustaajabisha ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi kwamba ulionekana ni mkutano wenye hadhi ya kitaifa.

Mjumbe wa Sekretariati ya Bavicha Taifa aliyeongozana na Heche alisema vijana wameamua kuleta mageuzi na watapambana bila kuogopa chochote alimradi wanafuata sheria na taratibu.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Sheikh Mwaipopo akihutubia umati mkubwa wa watu alilaani CCM kwa kuendesha propaganda za udini na sasa zinahatarisha amani ya nchi.

Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Mkiti wa Bavicha Taifa John Heche alilaani CCM kwa kukataa mapendekezo yote ya msingi yaliyoko katika Rasimu ya Katiba mpya.

Heche amewaambia wananchi kwamba kuanzia kesho Chadema inaanza ziara katika nchi nzima kutumia anga na nchi kavu kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu katiba mpya.

Katika hali ya kusikitisha wananchi walihuzunika sana baada ya Heche kuwaeleza jinsi wabunge wa CCM walivyovizia kipindi ambacho Chadema hawakuwepo bungeni na kupitisha harakaharaka kodi ya laini za simu.

Mara baada ya mkutano huo wananchi waligawiwa bure Nakala za rasimu ya katiba bure.Kwa muda mchache nakala zaidi ya mia mbili ziliisha na pia mamia ya wanachama wapya walichukua kadi za Chadema na mpaka naandaa taarifa hii bado kulikuwa na foleni kubwa ya wanachama wanaosubiri kadi mpya.

-----------------------------------------

attachment.php



attachment.php
 
Waooh!
Hii thread imenifanya niagize konyagi bila kupenda.
Very interesting! Propaganda za ccm zimefeli na kufika kikomo.
Ukisoma thread zingine huko utaona jinsi Mkutano wa Mwgulu ulivyoaibisha hapo jana.
Ccm ni lazima mkubali kuwa muda wa kuitwa WAPINZANI umefika.
Msiue watu kwa kuwakataa bana.
 
kweli cdm noma!,mi mwenyewe nilikuwepo ckuamini kama hali imefikia hivyo!yaani john heche anajaza watu kiasi kile!utadhani ni viongozi wa taifa!ndio walikuwepo,kiongozi wa bavicha anajaza watu wanawoweza kulingana naa mkutano anaohutubia mwenyekiti wa ccm!hii c hatari.
 
Mungu awalinde makamanda!
Ukombozi umekaribia
ccm imeamua kujiangamiza yenyewe kwa kutumia mabomu na risasi za moto kuwaua raia wake
naye waziri mkuu amethibitisha kwamba ni kweli polccm ndo wanauwaua raia na amri hiyo imetolewa na ccm
na akawadhibitishia uma kwamba bado ccm wametoa amri kwa policcm waendelee kuwaua raia
Asante sana waziri mkuu Pinda tumekusikia tumekuelewa hadi kieleweke
 
Good news, mabadiliko ni kama kimbunga kwani hayazuiliki kwa propaganda.
 
go chadema....watz wengi tuna imani na chadema
 
Mungu awalinde makamanda!
Ukombozi umekaribia
ccm imeamua kujiangamiza yenyewe kwa kutumia mabomu na risasi za moto kuwaua raia wake
naye waziri mkuu amethibitisha kwamba ni kweli polccm ndo wanauwaua raia na amri hiyo imetolewa na ccm
na akawadhibitishia uma kwamba bado ccm wametoa amri kwa policcm waendelee kuwaua raia
Asante sana waziri mkuu Pinda tumekusikia tumekuelewa hadi kieleweke

Twanga kotekote... Wao wanalia na Dr.Slaa,
Kamanda Mbowe,
Lema,
Lisu
Mnyika
Sugu nk..
Hawajui kua kila ilipo flag ya M4C ni campeni tooouuuushaa..
 
.....

........Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema........
 
Salute sana kamanda Molemo kwa kuwasilisha taarifa hii kwa wadau wa JF!
Kama ulivyosema ni kweli huo ni mkutano ulioandaliwa na Tawi la Chadema Mazizini chini ya usimamizi wa uongozi wa kata ya Ukonga. Sasa unaweza kuona ni kwa kiasi gani makamanda wameiva kiasi kwamba wanaweza kuandaa mkutano mkubwa kiasi hicho katika ngazi ya mtaa/tawi!
Bahati mbaya mimi nilipata dharura majira ya saa saba wakati tunakaribia kuanza mkutano na nikalazimika kuelekea hosoitali mwanangu aliugua ghafla lakini nilikuwa napata taarifa toka kwa makamanda wakinijulisha jinsi mkutano ulivyokuwa umefana!
Tunaendelea na maandalizi muda si mrefu tutaandaa mkutano mwingine mtaa wa Mongolandege ili kuhakikisha kuwa kata ya Ukonga inaongoza harakati za kuifuta ccm katika jimbo la Ukonga!
 
Last edited by a moderator:
Wakati wa ukombozi ni sasa.
 
Kama ilivyotangazwa awali CHADEMA leo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Ukonga Eneo la Mazizini.

Mkutano huo ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche akishirikiana na vijana wa Bavicha Jimbo na viongozi wa Jimbo na Kata.

Yaliyojiri mkutanoni:

Mkutano huu ulikuwa ni wa Kata tu lakini cha kustaajabisha ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi kwamba ulionekana ni mkutano wenye hadhi ya kitaifa.

Mjumbe wa Sekretariati ya Bavicha Taifa aliyeongozana na Heche alisema vijana wameamua kuleta mageuzi na watapambana bila kuogopa chochote alimradi wanafuata sheria na taratibu.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Sheikh Mwaipopo akihutubia umati mkubwa wa watu alilaani CCM kwa kuendesha propaganda za udini na sasa zinahatarisha amani ya nchi.

Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Mkiti wa Bavicha Taifa John Heche alilaani CCM kwa kukataa mapendekezo yote ya msingi yaliyoko katika Rasimu ya Katiba mpya.

Heche amewaambia wananchi kwamba kuanzia kesho Chadema inaanza ziara katika nchi nzima kutumia anga na nchi kavu kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu katiba mpya.

Katika hali ya kusikitisha wananchi walihuzunika sana baada ya Heche kuwaeleza jinsi wabunge wa CCM walivyovizia kipindi ambacho Chadema hawakuwepo bungeni na kupitisha harakaharaka kodi ya laini za simu.

Mara baada ya mkutano huo wananchi waligawiwa bure Nakala za rasimu ya katiba bure.Kwa muda mchache nakala zaidi ya mia mbili ziliisha na pia mamia ya wanachama wapya walichukua kadi za Chadema na mpaka naandaa taarifa hii bado kulikuwa na foleni kubwa ya wanachama wanaosubiri kadi mpya.

NB:
Nimeshindwa kupiga picha kutokana na aina ya simu niliyokuwa nayo.Hata hivyo nikifanikiwa kupata picha kutoka kwa makamanda waliokuwepo nitaziwek.



Ulikuwa unatumia simu ya tochi ha ha haa vijana wa Bavicha bwana umeshaandika siku nenda kaedit picha za Arusha uzilete hapa.
 
Kama ilivyotangazwa awali CHADEMA leo wamefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo la Ukonga Eneo la Mazizini.

Mkutano huo ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Bavicha Taifa John Heche akishirikiana na vijana wa Bavicha Jimbo na viongozi wa Jimbo na Kata.

Yaliyojiri mkutanoni:

Mkutano huu ulikuwa ni wa Kata tu lakini cha kustaajabisha ulihudhuriwa na umati mkubwa wa watu kiasi kwamba ulionekana ni mkutano wenye hadhi ya kitaifa.

Mjumbe wa Sekretariati ya Bavicha Taifa aliyeongozana na Heche alisema vijana wameamua kuleta mageuzi na watapambana bila kuogopa chochote alimradi wanafuata sheria na taratibu.

Katibu wa Jimbo la Ukonga Sheikh Mwaipopo akihutubia umati mkubwa wa watu alilaani CCM kwa kuendesha propaganda za & udini na sasa zinahatarisha amani ya nchi
.

Huku akishangiliwa na halaiki ya watu Sheikh Mwaipopo amesema Waislam wamegundua propaganda za CCM na kwa kuthibitisha hilo amesema jana aligawa kadi kwa Masheikh 12 wa Gongolamboto walioomba kwa hiyari yao kujiunga Chadema.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Mkiti wa Bavicha Taifa John Heche alilaani CCM kwa kukataa mapendekezo yote ya msingi yaliyoko katika Rasimu ya Katiba mpya.

Heche amewaambia wananchi kwamba kuanzia kesho Chadema inaanza ziara katika nchi nzima kutumia anga na nchi kavu kuelezea msimamo wa Chadema kuhusu katiba mpya.

Katika hali ya kusikitisha wananchi walihuzunika sana baada ya Heche kuwaeleza jinsi wabunge wa CCM walivyovizia kipindi ambacho Chadema hawakuwepo bungeni na kupitisha harakaharaka kodi ya laini za simu.

Mara baada ya mkutano huo wananchi waligawiwa bure Nakala za rasimu ya katiba bure.Kwa muda mchache nakala zaidi ya mia mbili ziliisha na pia mamia ya wanachama wapya walichukua kadi za Chadema na mpaka naandaa taarifa hii bado kulikuwa na foleni kubwa ya wanachama wanaosubiri kadi mpya.

NB:
Nimeshindwa kupiga picha kutokana na aina ya simu niliyokuwa nayo.Hata hivyo nikifanikiwa kupata picha kutoka kwa makamanda waliokuwepo nitaziweka.

... Katikati ya eneo lenu kuna sehemu pale inaitwa MARKAZ
wakazi wote wa enoe hilo ni wafuasi wa CUF "je CDM mmeweza kufungua shina (tawi) eneo hilo?"
 
Back
Top Bottom