CHADEMA, when will you master the Political Game?

Wakati mwingine turudi nyuma tujiulize! CDM watasemea wapi wakati wakinyanyua mdomo tayari wanakamatwa na kutupwa gerezani?
Ungesema hivyo kama mazingira ya kisiasa kwa nchi yetu, yangeruhusu ushindani sawa kwa vyama vyote.

Kwani juhudi za kuiokoa CCM wanazifanyia wapi?
 
Tanzania Tuna chama kimoja Chama Cha Mapinduzi CCM , vilivyobaki ni vyama rafiki kwa ccm, hoja kwamba kuna upinzani Tanzania ni kwamba haupo upinzani, tuwakosoe ccm hao hao wajirekebishe tusonge mbele, hawa wengine utapoteza muda wako bure.
Ili haya uliyoandika yaonekane yana ukweli, waambie CCM wategemee sanduku la kura Kama utawaona wapo! CCM sanduku lao la kura ni TISS na Polisi. Wakurugenzi wanakimbia fomu za wapinzani, kabla ya kupiga kura, CCM tayari wamepata wabunge 80 wa kupita bila kupingwa. Huu ndio udume wa CCM unaosifia? CCM wapo kwa msaada wa jeshi la Polisi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
CHADEMA mnashangaza sana mnaposhindwa kabisa kuitumia kila golden opportunity inayojitokeza kumdhoofisha adui yenu mkuu!

Mmeshaiokoa CCM kwa juhudi zenu wenyewe mara kadhaa sasa. Latest ni hili sakata la Speaker Ndugai. By failing to exploit the gigantic rift that Speaker Ndugai had caused, you basically saved your archenemy. Mungu aipe nini CCM?

Tambueni hili. No matter how much you hate a certain operative of your enemy, akishaanza kuwashambulia wenzake, usimpige; fanya kila uwezalo kukoleza mashambulizi yake kwa wenzake. Ni ajabu ya mwaka na aibu kubwa kwa CHADEMA kumshika shati mchezaji wa CCM anayekwenda kujifunga goli.

Seriously, it’s high time you hired effective coaches. Vinginevyo, mtaendelea kuchezea timu ya adui yenu bila nyie wenyewe kujitambua!
Ile CHADEMA ya Dr haiji kurudi tena mkuu.
Issues nyingi sana zinajitokeza hauoni wakizitumia. Mfano Tozo ilikuwa ni fursa nzuri saaana kwa sababu inamgusa kila mwananchi lakini wamelala fofofo. Sasa inaweza kwenda kumtoa Ndugai wa CCM
CHADEMA haina strategies. wamebaki kulalamika lalamika tu.
 
Nani anaejidanganya..mimi au wewe? Huwezi kuendesha chama cha siasa za ushawishi huku umetanguliza polisi mbele wanaumiza watu. Mwisho wa siku utaishia kumwaga damu tu
Nimekwambia hamna vyama hapo. CCM na Chadema wote ni hovyo tu.
 
Naona unajaribu kunijibu for the sake of it. Unasema kuna udhaifu upande wa bunge halafu ku justify ujinga wako unasema tena kuna udhaifu upande wa Chadema, mwambie Spika afanye kazi yake uone kama patakuwepo na huo udhaifu upande wa CDM.

Mwisho nikwambie tena, mwerevu habebi kila ushauri anaopewa hata kama ni wa hovyo, lazima achanganue kwanza, mjinga ndio hujibebea kila anaachoambiwa na yeyote. Umekalia kusema kuna uhuni CDM ukiambiwa weka ushahidi hapa unalia unatukanwa, tafuta saizi yako umfundishe kuimba haya mapambio yako.
🤣🤣
 
Kwa issue ya Ndugai na Polepole hata maoni ya viongozi wengi wa CDM twitter yana akisi mawazo ya wanachama na wapenzi wao mtandaoni, bado nasimama kwa pointi yangu pale juu.

Na chama kikishindwa kutoka hadharani na kujitenga na positions za makada wake, hakuna sababu ya mtu kuamini kwamba hizo positions ni positions binafsi za makada wa hicho chama!
 
Nimegundua wengi upinzani wanafanya siasa za kukariri, hawashughulishi bongo zao, wao kama anayezungumziwa alishaharibu jambo fulani suku za nyuma watabebana na jambo hilo hilo waendelee kumshambulia mtu huyo bila kujali athari za mashambulizi yao.

Walianza kwa Polepole wakapiga kelele hawakujua kwa kufanya vile wanaitetea CCM ambae ndie adui yao mkubwa zaidi, na mbaya zaidi kwa Polepole walikuwa wanapinga asipewe haki yake ya kujieleza ambayo wao wenyewe kila siku wanaikilia kupitia mikutano ya kisiasa waliyonyimwa.

Hapo nikashindwa kuwaelewa, unakataa Polepole asipewe ila wewe utataka kupewa maana yake nini?. Leo unaungana na yule anayemnyima Polepole halafu kesho utarudi kwake akupe wewe, akikunyima utalalamika kwa nani akusikilize? wanajua wenyewe.

Likaibuka tena hili la Ndugai, wengi wanapiga kelele zao zile zile za kukariri, "Sukuma gang wameshindwa" najiuliza hivi hawa kweli wana upeo atleast wakujua wanachokipigania au wameshaigeuza siasa kuwa ushabiki kama wa Simba na Yanga?

Ndugai ameongea point, stick with him, walete ufafanuzi wa hoja yake, sio kumtisha na vijembe vyao. Kesho wao wakianza kuipinga serikali then CCM wale wale wataanza kuwajibu kwa ile mipasho yao kule bungeni wataanza kulalamika CCM hawajibu hoja, kama ya Ndugai hamkutaka ijibiwe vizuri kwanini yenu ijibiwe toka kwa watu wale wale wenye majibu mabaya?

Sometimes wanaendekeza tabia mbovu ambazo wao wamekuwa wakizipinga bila kujua, majority of them wanatumia same level of thinking kwenye kuamua kila jambo linaloibuka mbele yao, hapa siioni tofauti yao na CCM tofauti yao ni playing ground ndio tofauti.

CCM wana uwanja mpana zaidi wa kuamua mambo mengi ya nchi kwa mazoea ndio maana wale maadui watatu wa tangu tupate uhuru bado tunao mpaka leo, wakati wao Chadema wana kauwanja kao kadogo cha kujifanyia mambo yao kwa mazoea.

Hapa mambo ya kunyimwa haki zao na msajili au polisi hayahusiki kabisa, ni level of thinking yao ndio inajadiliwa hasa kwenye kuicheza michezo ya kisiasa. Kwa namna hii sioni kama kuna lolote la maana watakalo achieve, wanajidumaza huku wao wanashangilia kwa mapambio ya kujipa moya kama vile "Chadema ni mpango wa Mungu" na mengineyo.
Acheni kutafuta huruma kwa madai mfu juu ya chadema. Hata kama chadema wangemsapoti Ndugai au poleepole haiwezi na haitaweza kubadili misimamo ya kisiasa au nguvu ya ccm.

Na bila kumung'unya maneno wote wanaoleta hoja hii ni wale walioumizwa na pigo hili kwa Polepole na Ndugai wakitaka walau sapoti hata ndogo ili kupoza machungu.

Wapi chadema kama chama kimezungumzia suala la Ndugai au polepole.

Hata hivyo sioni mtu yeyote makini na mkweli anayeweza kuwaunga mkono Ndugai na polepole si kwa sababu hoja zao hazina mashiko la hasha bali kwa ushiriki wao wa kinyama na kibedui katika kuumiza wenzako waliokuwa na mawazo kama hayo ila wakati huo wakawa wanatetea matumbo yao. Je uhalali wanaopata wapi?

Acheni kupotosha eti ufundi wa siasa. Kwa matukio haya ya polepole na ndugai awe ccm, chadema, act, nccr na wengineo watajifunza na kufanya siasa safi zisizo za kinafiki maana sasa wanaiona karma inavyofanya kazi.
 
Nyie endeleeni kusubiri kuvushwa na karma!
 
Just to put the record clear, majina hayo 19, hayakujipeleka, yalipelekwa rasmi, na wakati walipoapishwa walikuwa ni wanachama halali wa Chadema.
Hivi hamjiulizi kwanini kikao cha Baraza Kuu hakiitishwi?. Kama ni kweli Chadema hawakupeleka rasmi majina, that means kuna forgery ni kosa la jinai, hamjiulizi kwanini mpaka leo Chadema haijairipoti polisi jinai hii ili uchunguzi wa kijinai ufanyike kubainisha ni nani alifoji barua za Chadema zenye offical letter head na signature zilizo peleka majina yale NEC.

Nawapongeza Chadema kwa kuuzingatia ushauri huu
P
Unafiki unakutesa we baba, eti polisi!
 
Baadhi ya wana CCM wakitaka ajenda zao zifanikiwe huwa wanai- frustrate CDM iongelee hizo ajenda, pambaneni na hali yenu.
 
Hakuna bingwa wa gemu la siasa Tanzania.

CCM wako madarakani tu kwa sababu walipata ukiritimba wa kumiliki siasa za nchi kabla ya ujio wa vyama vingi, ujanja wa ku exploit katiba mbovu, na umbumbumbu wa watanzania kwenye masuala ya siasa(low political literacy).
Kuna mtu nilikuwa namwambia hili leo jioni, exactly the same thing, ukimaster hiki leo, kesho CCM wanakuja na jipya na ovu, hilo jipya utalimaster je hilo ovu utalimaster kwa kutumia nini? una jeshi? una polisi? Tiss je!?

Amini nakwambia kama CDM ingeungana na polepole basi CCM wote wangeungana against CDM, kwa ujumla CDM wangewaunganisha CCM.

Salama ya CDM ni kuendelea kuwa na ajenda zake za muda mrefu ambazo nazo zitachukua muda mrefu kuziachieve. Hapa tunazungumzia CDM kama taasisi, Wanachama wanaweza kucomment chochote, popote muda wowote.
 
CHADEMA mnashangaza sana mnaposhindwa kabisa kuitumia kila golden opportunity inayojitokeza kumdhoofisha adui yenu mkuu!

Mmeshaiokoa CCM kwa juhudi zenu wenyewe mara kadhaa sasa. Latest ni hili sakata la Speaker Ndugai. By failing to exploit the gigantic rift that Speaker Ndugai had caused, you basically saved your archenemy. Mungu aipe nini CCM?

Tambueni hili. No matter how much you hate a certain operative of your enemy, akishaanza kuwashambulia wenzake, usimpige; fanya kila uwezalo kukoleza mashambulizi yake kwa wenzake. Ni ajabu ya mwaka na aibu kubwa kwa CHADEMA kumshika shati mchezaji wa CCM anayekwenda kujifunga goli.

Seriously, it’s high time you hired effective coaches. Vinginevyo, mtaendelea kuchezea timu ya adui yenu bila nyie wenyewe kujitambua!
Chadema is another version of a utopian political infantry party. They aren't after statehouse.
 
Why should I leave Chadema alone?. Hujui kuwa Chadema sio a private party or a saccos, it is public party na inaendeshwa kwa kodi yangu? na ndio maana inakaguliwa na CAG. Nina haki zote za kusema lolote kuhusu Chadema.
P
Watu huwaga wanasahau Hilo, eti unaongelea chama, mtu anafikir kuwa ni Ka Saccos Ka kwao, kumbe ni chama cha umma na kinalipwa ruzuka kma kawa!
 
CHADEMA tatizo hamuweki wazi mambo yenu,mnasema chaguzi zinazofanywa nchini waamuzi tayari wana washindi, I mean CCM tayari wanaweka wagombea wao kuwa washindi, the problem is; kwa nini bado mnashiriki hizo chaguzi?? Its seems mnafaidika nayo,na agenda yenu sio kushinda uchaguzi na kuongoza nchi yetu bali mnajua wenyewe ni kupata mnachopata kwenye chaguzi...what a pitty
 
CHADEMA mnashangaza sana mnaposhindwa kabisa kuitumia kila golden opportunity inayojitokeza kumdhoofisha adui yenu mkuu!

Mmeshaiokoa CCM kwa juhudi zenu wenyewe mara kadhaa sasa. Latest ni hili sakata la Speaker Ndugai. By failing to exploit the gigantic rift that Speaker Ndugai had caused, you basically saved your archenemy. Mungu aipe nini CCM?

Tambueni hili. No matter how much you hate a certain operative of your enemy, akishaanza kuwashambulia wenzake, usimpige; fanya kila uwezalo kukoleza mashambulizi yake kwa wenzake. Ni ajabu ya mwaka na aibu kubwa kwa CHADEMA kumshika shati mchezaji wa CCM anayekwenda kujifunga goli.

Seriously, it’s high time you hired effective coaches. Vinginevyo, mtaendelea kuchezea timu ya adui yenu bila nyie wenyewe kujitambua!
Tarumbeta

Screenshot_20220109-070158_Twitter.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom