Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Aug 20, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,523
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Katika thread moja humu jukwaani, nimekutana na mchango wa mwana jf huyu

  Kutokana na kauli hiyo, nimekuwa inspired kuandika kidogo kuhusu adui mkuu wa Tanzania wengi wakidhani ni CCM, kumbe sio, bali adui mkuu wa Watanzania ni huyu nimtajae hapa chini na headline imejielekeza kwa Chadema, simply because ndicho chama pekee cha upinzani huku bara, chenye kuonyesha mwelekeo wa matumaini ya uwezekano wa kulipatia taifa letu la Tanzania, ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania!.

  Mkuu Jogi, japo umeniomba "Nikubaalie japo mara hii tu kuwa, tatizo linalotumaliza ni zimwi CCM". Samahani sana, sikukubalii, kwa maoni yangu, japo ni kweli CCM ni zimwi, adui sio zimwi, bali wale wanaolifuga hili zimwi na kulipa chakula ili liendelee kuishi!.

  1. Tatizo kubwa la Watanzania au adui mkubwa wa Tanzania sio CCM, CCM is just the vehicle, haikujiweka hapo ilipo, imewekwa, hivyo tatizo sio CCM iliyowekwa, bali tatizo ni wale walioiweka CCM hapo ilipo!. That simply means, tatizo ni sisi Watanzania tulioiweka CCM madarakani and it plays games on us again and again na sisi tukiendelea kuiweka madarakani again and again and again na sitashangaa kama hata 2015, tukairudisha tena CCM ikulu ya Magogoni!.

  2. Hii dhana ya kudhania adui mkubwa wa Tanzania ni CCM, is a wrong concept, na hili ndilo kosa kubwa la wapinzani, wakiwemo Chadema, katika chaguzi zote za nyuma wapinzani wanaelekeza nguvu nyingi concentration kubwa ya mashambulizi yote kwa CCM wakibeza tuu CCM haikufanya hiki au kile, huku wakijihesabu CCM ndie adui yao mkubwa, hivyo ku miss the real target ya adui halisi ni nani!. Adui sio CCM, adui ni watu wanaoiweka CCM hapo ilipo.

  5. CUF baada ya kujaribu mara 3 ikashindwa, ikaamua kutumia principle ya "if you can't beat them, join them", kwa mara ya 4 katika uchaguzi wa 2010, ikakubali yaishe, ikawajoin ndani ya SUK katika ndoa ya kukubali kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, at the same time, its fighting from within, and it is expected to be hitting them very hard from within, kwa mtindo wa "kikulacho" na kikundi cha "uamsho" ni matokeo chanya ya kipigo hicho kwa serikali ya SUK from within, hivyo kwa 2015 upande wa Zanzibar CUF ni njia nyeupe!.

  6. Kwa sasa, angalau Chadema, kupitia M4C, imeshagundua adui halisi anayewakosesha ushindi, na sasa imejielekeza kwa wananchi ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho na wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, hivyo concentration ikiwekwa kwenye "changing the mindset ya wenye maamuzi, kuacha kuchagua kwa mazoea tuu, bali kuchagua kwa sababu. Wananchi, watafunguka macho, na hawatakuwa na sababu tena ya kuendelea kuichagua CCM!.

  7. Ili hili liwezekane, wapinzani wasiwe ni watu wa kulalamika na kulaumu tuu kuhusu CCM, bali sasa wajikite kueleza where CCM does wrong, lakini wao wakiingia, watafanya nini tofauti na CCM, na kitabadilisha nini, ili wale wanaoichagua CCM kwa mazoea tuu, wapate sababu za msingi za kutoichagua CCM na kuwachagua wapinzani.

  8. Mara baada ya uchaguzi wa 2010 na mafanikio makubwa upande wa Chadema, kwenye ile mada yangu ya "CCM Imechokwa, Chadema Haijajipanga", niliwaeleza kuwa wapinzani bado wako kiuana harakati zaidi, bado hawajipanga mkao wa kushika dola, lakini kwa kwa sasa kupitia M4C, Chadema wanaonyesha dalili za kujipanga japo bado wanakabiliwa na madhaifu haya na yale, yakiwemo, lile koti la ukanda, udini, ukabila na ubinafsi wa "umimi" etc.

  9. Kwa leo naomba nisiingie tena kwenye udini, ukanda na ukabila wa Chadema, bali naomba nijikite kwenye ubinafsi au "umimi" kwa Chadema kujiamini kupita kiasi kuwa peke yao wataweza!, nilisema peke yao hawawezi, na leo nasema te na na tena, "Chadema peke yenu hamuwezi Kuiondoa CCM Madarakani" kwa sababu hili CCM ni dubwana kubwa sana ambalo haliwezi kung'oka bila umoja ambao ni nguvu ya Watanzania wote wenye kuliutakia mema taifa hili.

  10. Kabla ya kauli ya majuzi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kule bungeni, nilikuwa najua ma RC na ma DC ni watendaji wakuu wa serikali mikoani na wilayani baada ya kutenganisha zile kofia mbili za chama kushika hatamu za kuiongoza serikali, kumbe wamevua tuu hizo kofia na kutovaa sare, lakini kiutendaji kumbe wako pale kuhakikisha CCM inatawala milele!, hivyo bila joint foces, hakuna jinsi ya kuipumzisha CCM na ni kweli itatawala milele!.

  11. Chadema na wapinzani wengine wote wa ukweli, ni lazima wa join forces kutafuta the common working grounds na wenzenu wengine wote mu work together towards a common enemy hata na nyinyi wenyewe kwa wenyewe lazima mkubali kushirikiana kwa kukubali kutokubaliana kwa hayo madogo madogo lakini lazima mkubaliane kwenye kubwa la msingi kwa kukubali "umoja ni nguvu" vinginevyo matokeo ya 2015 yatakuwa ni yale yale ya, vyama vile vile, na watu wale wale!.

  12. Mfano, japo CUF ni mke wa CCM kwa upande wa Zanzibar, hiyo ni "marriage of convinience", hivyo inavunjika wakati wowote "conveniences" zikimalizika, hivyo Chadema inacho kibarua kigumu cha kum..ngoza huyu mke wa mtu kwa kumhakikishia akikubali kutoka nje ya ndoa, yeye sasa hatakuwa mke tena, bali atageuka mume na 2015 ni yeye sasa ndie atageuka kidume na kumuoa huyo mume aliyenae sasa kwa sababu mume huyo ategeuzwa mke!.

  13. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya CUF kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia njia nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2015, ni lazima ikubali kuisupport ya CUF kwa upande Zanzibar ili CUF nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na CUF, waainishe maeneo ya strong holds za kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2015, kuepuka kumfaidisha kunguru kwa vita vya panzi!.

  14. Voting statistics

  Tanzania: 2010 Presidential election results
  Updated January 2010

  The United Republic of Tanzania elections for parliament and the presidency were held on 31 October 2010.

  Voting statistics
  Registered Voters 20 137 303
  Total votes 8 626 283
  % Turnout 42.84
  Valid votes 8 398 394
  Spoilt votes 227 889
  % Spoilt votes 2.64

  Table source
  Commonwealth 2010, 31.

  Results
  Candidate Party Votes % Vote
  Jakaya Kikwete Chama Cha Mapinduzi (CCM) 5 276 827 62.83
  WP Slaa Chama Cha Demokiasia na Maendeleo (CHADEMA) 2 271 941 27.05
  Ibrahim Lipumba Civic United Front (CUF) 695 667 8.28
  Peter Mziray Kuga Progressive Party of Tanzania (PPT-MAENDELEO) 96 933 1.15
  Rungwe Hashim Spunda National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi) 26 388 0.31
  Muttamwega Bhatt Mgaywa Tanzania Labour Party (TLP) 17 462 0.21
  Yahmi Nassoro Dovutwa United People's Democratic Party (UPDP) 13 176 0.16
  Total
  8 398 394 99.99

  Table source
  Commonwealth 2010, 31.

  References
  COMMONWEALTH 2010 Report of the Commonwealth Observer Group: Tanzania General Elections 31 October 2010.

  15. Kwa mujibu wa data hizo, JK amechaguliwa kura milioni 5 tuu kati ya watu milioni 40!. Waliojiandikisha ni milioni 20, lakini waliopiga kura ni milioni 8 tuu!, hii inamaanisha kuna watu milioni 12, ambao walijiandikisha lakini hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwemo wale waliokata tamaa na kuona kupiga kura ni wastage of time, hata upige vipi kura, matokeo ni yale yale lazima CCM ishinde, hivyo kuliko kupoteza muda wakaachana kabisa na kupiga kura!

  16. Suppose 2015, Watanzania tutakuwa Milioni 50 wenye sifa za kupiga kura ni milioni 35, hawa wote wakihamasishwa kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura, mgombea wa CCM atajipatia kura zao zile milioni 6 za wanachama wao kwa mujibu wa tovuti ya CCM, halafu hizo kura milioni 29 zimuangukie mgombea wa upinzani, hata NEC ya CCM, wachakachue vipi, there will be no way out!, hivyo adui yetu mkubwa sio CCM, bali ni Watanzania wanaipigia kura CCM!.

  17. Sasa ili kuwafikia Watanzania wote na kuwaamsha waliolala, Chadema haiwezi kuwafikia Watanzania wote kwa kutegemea mikutano ya hadhara na mass media za wengine. Chadema lazima wawe na mass media yake ambayo ita propagate the message of changing the mindset ya Watanzania. Chadema wana all the resource kumiliki media yake lakini very unfortunately they are myopic, hawana vision ya kuona mbali kuangalia nje ya box and see a bigger picture. Hawajui kupanga priorities zao. Bei ya gari moja tuu la M4C linatosha kununua transmitter ya Digital ya redio na TV. Chadema bila media yake, ni kutwanga maji kwenye kinu, CCM ina media yake na TV yake TBCCM, radio zake na magazeti yake, Chadema bila media yake, ikulu wataendelea kuisikia tuu kwenye bomba, 2015 ni CCM tena! .

  Wasalaam.

  Paskali

  NB. Paskali, sio mwanachama, mfuasi wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni Mtanzania wa kawaida mwenye kuweka mbele maslahi ya taifa.
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hoja yako ni njema ila hii kauli hapo juu ndio uwa inaniacha hoi..ati Pasco wa JF sio mwanachama wala mshabiki wa chama cha siasa...huu ni unafiki, ukweli ni kuwa unaweza usiwe mwanachama au mfuasi wa chama chochote ila lazima uwe na hisia za chama fulani..kwa asili ya binadamu ni ngumu kuwa at the between. Jaribu kuacha unafiki huu nadhani hoja zako zitakuwa bora zaidi. Ukweli ni kuwa hoja yako ina mashiko, isipokuwa unafiki weka pembeni.
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Pasco

  Mkuu chukua tano umenena ukweli ambao wenye makengeza hawataki kuuona.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  Naogopa kusema kuwa wewe ndiyo una makosa.

  Kwa haraka haraka na kwa kutumia KATIBA zetu hizi za Tanzania zilizo na matundu mengi kama Mipaka yetu ya nchi, nasikitika kukuambia kuwa CCM IMEJIWEKA MADARAKANI na si kuwa TUMEIWEKA MADARAKANI.

  Tukianzia na uchaguzi wa Rais, ni wewe ulitutangazia matokeo siku kadhaa hata kabla ya uchaguzi. Ukatuambia na maandalizi ya kumuapisha KIKWETE (siyo RAIS) kuwa Rais kwa muhula wa pili yameshaanza (tulishangaa hata wageni waalikwa kuwepo). Hii haikujalisha kama ameshinda au kashindwa kwa sababu katiba ya Tanzania, MTU AKITANGAZWA NA TUME KUWA NDIYO RAIS, basi imetoka na huwezi kwenda kupinga matokeo hayo popote pale. Nina imani ingelikuwepo kifungu hicho, sasa hivi uchaguzi ungelirudiwa tena na watu kufungwa..... (wafungwe na nani? Majaji waliochaguliwa na Kikwete? Jaji gani aamue uchaguzi urudiwe wakati wamewekwa hapo na huyo huyo Kikwete? Polisi gani apeleleze? Usalama gani wa Taifa apeleleze? Takururu gani apeleleze ... wakati Maboss wote wamewekwa na Kikwete/Mwenyekiti wa CCM???)

  Hapo unaona kuwa Mduara unafunga kama wimbo wa P-SQUARE (If you do me, I do you). JWTZ gani aje juu wakati ndiyo hao akina Shimbo na mtani wangu Mwamunyange walikuwa kwenye mkutano wa MBAYUWAYU?

  CCM ni kama mashidano ya ngumi na CHAMPION. Ukitaka kumshinda, mpeleke chini kwa KNOCK OUT maana vinginevyo utaambiwa mmetoka droo na hapo mshindi bado ni YEYE.

  Adui wa Tanzania wapo wengi ila namba moja ni CCM (kama 40%) ila ndiye mwenye asilimia nyingi. Huyo akiondoka, bado kutakuwa na kazi kubwa sana ya kuwaondoa hawa wengine wengi ila wadogo wadogo - Katiba, Polisi, Takururu, Usalama wa Taifa, Mahakama, Bunge, Umasikini, Elimu ya uraia, kusoma na kuandika, Muungano na Zanzibar nk nk.
   
 5. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nitarudi
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi kulikuwa na haja gani ku-quote HABARI NZIMA na unakuja kuandika kimstari kimoja? HEBU angalia mwenzako hapo juu.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  [h=2]Sikieni hii kauli ya mwanasheria mkuu wa serikali dhidi ya takukuru/dr hosea[/h]
  NI KUHUSU SHERIA KUIKWAZA TAKUKURU KUWASHTAKI VIGOGO WA UFISADI

  Kizitto Noya
  MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amesema Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), ni nzuri na kwamba haipaswi kufanyiwa mabadiliko kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.

  Jaji Werema aliliambia gazeti hili jana kuwa haoni haja ya sheria hiyo kufanyiwa mabadiliko sasa kwa kuwa haina tatizo na ipo kutekeleza misingi ya utawala wa Sheria.

  "Mimi nakubaliana na Sheria hii ya (Takukuru) kwamba iendelee kuwapo. Hakuna haja ya kuifanyia mabadiliko sasa. Ni nzuri kwa kuwa inazingatia misingi ya utawala wa sheria," alisema Jaji Werema.

  Kauli ya Jaji Werema inapingana na ile iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah kwamba sheria hiyo imekuwa ikiwakwaza kuwashughulikia wala rushwa wakubwa, kwani majalada ya kesi zilizokwishafanyiwa uchunguzi yamekwama kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP).

  From: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/310536-re-sikieni-hii-kauli-ya-mwanasheria-mkuu-wa-serikali-dhidi-ya-takukuru-dr-hosea.html

  Habari ndiyo hiyooo. Hao ndiyo utegemee watangaze Matokeo na kusimamia UCHAGUZI.
   
 8. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Sikonge

  ...naunga mkono hoja(LIKE)...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,523
  Trophy Points: 280
  Only83, mimi kiukweli wa toka ndani ya moyo wangu sio mwanachama, sio mfuasi na sio mshabiki wa chama chochote!.

  Ndio maana nilipo waambia CCM wamechokwa na niliwaambia na jinsi ya kujinasua toka mchoko iliopo na walianza kujinasua japo wanajizamisha kwenye tope zito zaidi!.

  Nilipowaambia Chadema hawajajipanga, niliwaelekeza na jinsi ya kujipanga japo niliambulia kutukanwa sana, ujumbe ulifika na kujipanga kumeanza!.

  CUF nao walipofunga ndoa yao na CCM kwa kula kiapo cha kuitekeleza ilani ya CCM, niliwaambia that is the begining of an end of era for CUF bila kujua kuwa kumbe walifunga tuu ndoa of "canvenuence" kwa principle ya " if you can't beat them, join them" na sasa ndio wana hit'em hard from within!.

  Kwa mujibu wa kazi yangu mimi ni daiwaka kama taxi driver, wote ni abiria wangu, ukitokea mzigo wa CCM, napiga kazi, watakaosema mimi CCM na waseme.

  Ukitokea mzigo wa Chadema au CUF mimi napiga tuu kwa maslahi ya taifa mbele na kuziacha siasa za vyama nyuma.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,523
  Trophy Points: 280
  Mkuu Sikonge, CCM is a wrong target the right target ni " people" na sio CCM, in targeting the people you'll hit them all including CCM kwa sababu iko among the people!. Ukiitarget CCM, you will only hit CCM and miss the people wanaoichagua CCM hivyo to miss the point and the target,2015 watu wataichagua tena CCM na tena na tena mpaka ilitimie ile miaka 100 tulioelezwa humu!.

  Lets now deal with the source and not outcome, CCM sio msingi, bali ni matokeo tuu, watu ndio msingi, ukideal na matokeo ukaacha msingi, msingi utaendelea kutoa matokeo yale yale!.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Pasco

  na wewe kumbe umekaririshwa kwamba chadema kuna ukanda, udini, ukabila na ubinafsi wa "umimi"?

  unaweza kuthibitisha kwa mifano?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. T

  Temple Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Pasco,
  Hayo mawanzo ya kutaka consensus kati ya vyama vya upinzani ni nzuri, lakini kumbuka yalitaka kuisambaratisha CHADEMA kwa sababu hakika ulikuwa mpango wa CCM ku penetrate katika vyama hivyo. CHADEMA kiliamini hivyo na kuwa baadhi ya waandishi wa habari na baadhi ya vyombo vya habari vilipewa task hiyo kuhakikisha CHADEMA inaingia mkenge. Uchaguzi mdogo wa Tarime ulidhihirisha hivyo. Hata hivyo siingilii mawazo yako kuwa CCM is too strong kwa CHADEMA peke yake kuitoa. Kwa mimi naiona is not strong that much ila baadhi ya watu kuto mini mabadiliko kama ilivyo kwa Rais wa Syria kwa sasa.
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pasco,

  CCM ni WATU na siyo Chombo. System ni WATU na siyo Chombo.

  Ukishamfahamu ADUI wako vizuri, utajua tu jinsi ya Ku-deal naye.

  Ndiyo maana wakati ZITTO anatamba kuwa anataka kuwa RAIS na hayo maneno anayasema akiwa Bungeni au Mitaani, M4C wapo vijijini wakiishambulia CCM kwenye Mioyo ya watu.  Emancipate yourselves from mental slavery; - CCM
  None but ourselves can free our minds.

  Have no fear for atomic energy,
  'Cause none of them can stop the time.
  How long shall they kill our prophets,
  While we stand aside and look? Ooh!
  Some say it's just a part of it:
  We've got to fullfil the book.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Pasco, unajua mada zako unazipanga vizuri, unaziandika vizuri na unazifafanua vizuri kwa lugha rahisi kiasi kwamba hata kama kimantiki si kweli watu wengi wanaweza kukubaliana na hoja zako? Ndivyo ilivyo hata kwa hoja yako hii ya leo.

  Kiukweli kulekea elfu mbili na kumi na tano adui mkubwa wa Chadema ni…..CCM.

  Mimi si mwandishi mzuri hivyo nitaenda straight to the point.

  1. Well, kuhusu watanzania kuichagua CCM over and over again, wewe unatarajia nini? The whole system is fine-tuned kuiweka CCM madarakani na kimsingi hilo ndilo linalowapa kiburi baadhi ya wasemaji wa CCM kwamba "CCM ipo ili kutawala milele…" na mwingine kuongeza kwamba "ni heri afe kuliko kuona Chadema inatawala…" We unadhani hii ni exercise in political rhetoric tu? Wanamaanisha wanayoyasema na kiukweli kuna kila sababu ya watawala wetu wa sasa na makada wa CCM kutopata hamu au kuogopa kabisa kuona upinzani unachukua serikali. Sababu zinajulikana.

  2. Dhana kwamba adui mkubwa wa watanzania si CCM bali ni sisi wenyewe siyo sahihi sana. Ni kweli kwamba kuna vi element fulani vya utamaduni wa kitanzania vinavyotubakisha sana nyuma lakini adui mkubwa ni yule anayecapitalize kwenye udhaifu wetu ili kuendelea kutunyonya na kutukandamiza. CCM haina huruma, haina tofauti na mkoloni wa kiarabu au kijerumani aliyetumia ukarimu wetu, upole wetu na kukosa elimu kwetu ili kujinufaisha juu ya migongo yetu. Ni kweli, hata hivyo, kwamba njia ya kumshinda adui wa namna hii ni kusambaza elimu ya uraia. Hii inatusaidia sana kuongeza ukali kidogo tunapodai haki zetu za kikatiba na kumpinga hasa pale anapoleta uhuni na ndicho Chadema wanachofanya.
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Good point... Watu wana njaa shida na taabu nyingi lakini utashangaa ccm wanafanya mkutano watu wanajaa na kuwasikiliza na bado wanawapigia kura. Nini ambacho ccm inataka kutuambia ambacho hatujasikia kwa miaka hii 50?
   
 16. M

  MTK JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Pasco nakupa 4/10; your diagnosis(kutambua ugonjwa) may be right lakini perscription(kutibu) is off track!!

  Hebu tusaidie ni vyama gani ambavyo unaviona viko focused enough kuunganisha nguvu na CDM kuelekea ufanisi, na pia shauri watumie formula gani kufanikiwa kwa sababu wamejaribu mara nyingi wamekwama kutokana na baadhi ya udhaifu uliouainisha hapo juu!

  Binafsi naamini CDM haina sababu ya kuhangaika na vyama vya siasa bali kukusanya nguvu za umma na makundi ya vyama vya wafanya kazi, wakulima na wafugaji, taasisi zisizo sa kiserikali na wanaharakati mbalimbali bila kusahau diaspora(watanzania wanaoishi nje ya nchi)

  Kampeni za Sangara na vuguvugu la M4C na nyingine zitakazofuata kuelekea 2015 zinakusudia kufanikisha uamsho huo; watanzania wajitambue na kuchukua hatua mahsusi.
   
 17. SoNotorious

  SoNotorious JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Sep 11, 2011
  Messages: 2,426
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  It is not a war against ccm or cdm, it is a war against YOU.
   
 18. Yonjolo

  Yonjolo Member

  #18
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakugongea "like" mkuu. Kama watanzania walionesha nia njema kwa nchi yao kwa kukipiga chini chama cha mapinduzi ni dhahiri kabisa bwana pasco unawakosea watanzania na unapaswa utuombe radhi.

  Mimi naamini tulifanya sehemu yetu lakini kwa bahati mbaya wao ccm wameushikilia mpini kwa mabavu yote.

  Kama mtu ana roho mbaya huwa haichukiwi roho bali mwili wa huyo mtu utahesabika kuwa ni mbaya tu.
  ccm ni janga la uhai wa watanzania.
   
 19. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #19
  Aug 20, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
 20. Wilawela

  Wilawela Member

  #20
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pascal nakubaliana nawe kwa kusema umoja ni nguvu na utengano ni udhaif.

  Lakini kumbuka 1995 CDM walijiunga na NCCR mageuzi wakamsapoti Mrema na Kukubaliana kuachiana majimbo ya Ubunge Kumbuka arusha Mjini Makongoro Nyerere alitakiwa amwachi Mzee Mtei as pe MoU ilikiukwa, 2000 Bob Makani baada ya kuvuta fomu aliambiwa amwachi Prof.Lipumba na alifanya hivyo lakini matokeo yake hawakuachiana Ubunge wala Udiwani!

  Miaka yote hiyo CDM wamekuwa wakiwachia CUF urais,ubunge uwakilishi nk, lakini mara zote wamesalitiwa! Unajua mfano last election mambo yalikuwa safi kwa CDM na magumu kwa CUF lakini likaja wazo ya "KURA ZA HISANI KWA KIKWETE MWISLAM MWENZETU NA KUEPUSHA NCHI KUTAWALIWA NA PADRI" uzuri kila kitu hadharani(rejea kanda za wanazuoni wa kiislam) sasa mazingira kama hayo toa Strategies za kuunganisha nguvu na kupata UMOJA.

  Maana wewe unaweza kuwaza very Objectively mwenzio so Subjectively! Maana hata sasa CUF wanasema rais atoke Zenj kwa nia hiyo hiyo!
   
Loading...