CHADEMA, when will you master the Political Game?

Watamsikitikia Ndugai kwa kutokuwa na msimamo wakati yeye ni kiongozi wa mhimili wa serikali. Kiongozi wa Mhimili ambao uchaguzi wake haohao wanauita uchafuzi.
CHADEMA hawana muda na maigizo ya kina Ndugai kwenye PC ya Leo maana haiwahusu. Wao wana mikakati yao isiyohusisha Mazuzu wanaolialia hapo Dodoma.
Yaani watu nyie ni wasahaulifu kweli, kwa hiyo mlotegemea CHADEMA wangetoka hadharani kumsapoti Ndugai halafu ingewasaidia nini kisiasa baada ya Ndugai kuomba radhi. Mbatia kamsapoti unaona alivyobaki peke yake baada ya mwenye hoja kuachana nayo?
 
Siasa za CDM siyo zenu!

Pili pili msizozila kuwa washa namna gani?

CDM ina vipaumbele vyake:

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kwenye madai yetu ya katiba mpya.
2. Mwendazake hayupo tena, makando kando yake tuhangaike nayo kwenye "haki na maridhiano" baada ya katiba mpya.
3. Agenda zetu ni za kudumu si marafiki.


Juu ya hivi ni muhimu pia ikafahamika ni nia yetu kujua hapo #2 hizi 29tr/- Mikopo ya awamu ya tano zilitumika wapi.

Kwa sisi observers, siasa za matukio na jitihada za CDM za kuiokoa CCM dhidi ya minyukano yake ya ndani ndivyo vimekuwa vipaumbele vya CDM!
 
CCM ndo Wana mbinu za kistaarabu za kisiasa?
1) Kupiga risasi wapinzani mchana kweupe
2) Kuua wapinzani
3) Kuwabambikia kesi za mauaji wapinzani nchi nzima
4) Kufilisi na kuwahujumu wapinzani
5) Kununua wapinzani
Niambie nini cha kistaarabu hapo? CCM ni chama kilichokufa na kinategemea polisi kufanya shuguli zake, na hili hata JK alilisema wazi. Kuwe kuna tume huru na ya haki, vijana waingie mitaani kupiga kura..watatoboa?

Wewe utakuwa umedandia train kwa mbele!
 
Mkuu brazaj , elimu ya uraia inahitajika sana kujua kitu kinachoitwa haki jinai.
Kuna jinai za aina mbili, public and private or personal.

Ukifanya jinai ya public, unakamatwa na kufunguliwa mashitaka na republic bila mtu kuripoti.

Lakini jinai ya private ni lazima wewe uliyetendewa ukaripoti polisi kulalamika ndipo polisi waanzishe uchunguzi wa kijinai.

Lissu alipotangaza anafuatiliwa hadi kutaja number ya gari, jeshi la polisi walifanya nini?. They did nothing kwasababu Lissu alipaswa kuripoti polisi na sio kuripoti kwenye press conference.

Forgery ikifanywa popote, bila hiyo forgery kuripotiwa polisi will do nothing!.

Hata majambazi wakivunja nyumba yako wakapiga, wakaua, usiporipoti, its the end.

Katibu Mkuu wa Chadema, JJ. Mnyika alienda NEC kuomba kuonyeshwa hiyo barua ya uteuzi ya Chadema ilioleta hayo majina 18, aligomewa kwasababu who is he?!. Alipaswa kuripoti polisi, then polisi ndio waombe barua ya Chadema ilipelekwa NEC, kama hakuna mtu wa Chadema aliyelalamika, polisi wanaanzia wapi?.

Hata jinai ya kubakwa, unless aliyebakwa minor, lakini mwanamke alifikisha the age of the majority, akibakwa, asiporipoti, anahesabika ame consent!.

Kwenye ku deal na serious issues, Handling of Serious Security Issues: Kama CHADEMA Takes Things For Granted Kwa Uzembe Hivi!, Jee Ikulu Yetu Wangeiweza?
Chadema are very poor!.
P

Bwana pascal hizi sheria za wapi?

Jinai ni moja na wajibu wa polisi ni kushughulikia na jinai. Jinai zote mwenye kesi ni jamhuri. Huyo ndiye mwenye wajibu wa kufanya uchunguzi na kushtaki.

Wameitwa kina Pascal Mayalla na wengi wengine kwenye tume ya maadili kwa tuhuma za kuvunjia baadhi ya mihimili hadhi zao.

Rejea tuhuma kumhusu bwana Pascal kwenye lililokuwa swali: "je bunge ni dhaifu?"

Sembuse forgery?

Kwenye saga hii huoni hata hadhi zilizovunjwa? Kwanini umewakomalia Chadema tu? Hawa wenye hadhi zao nao je?

Au ni yale mambo ya hoja za upande mmoja automatically kutotingishika?

Si kuwa tunayoyaona ni matokeo ya kuwa na katiba iliyowekwa kijanja kijanja kwa ajili ya walio madarakani?

Hudhani kuwa Chadema wana hoja kuachana na yote kuwekeza kwenye katiba mpya kama muarobaini kamili wenye ufumbuzi kwa yote?
 
Nimegundua wengi upinzani wanafanya siasa za kukariri, hawashughulishi bongo zao, wao kama anayezungumziwa alishaharibu jambo fulani suku za nyuma watabebana na jambo hilo hilo waendelee kumshambulia mtu huyo bila kujali athari za mashambulizi yao.

Walianza kwa Polepole wakapiga kelele hawakujua kwa kufanya vile wanaitetea CCM ambae ndie adui yao mkubwa zaidi, na mbaya zaidi kwa Polepole walikuwa wanapinga asipewe haki yake ya kujieleza ambayo wao wenyewe kila siku wanaikilia kupitia mikutano ya kisiasa waliyonyimwa.

Hapo nikashindwa kuwaelewa, unakataa Polepole asipewe ila wewe utataka kupewa maana yake nini?. Leo unaungana na yule anayemnyima Polepole halafu kesho utarudi kwake akupe wewe, akikunyima utalalamika kwa nani akusikilize? wanajua wenyewe.

Likaibuka tena hili la Ndugai, wengi wanapiga kelele zao zile zile za kukariri, "Sukuma gang wameshindwa" najiuliza hivi hawa kweli wana upeo atleast wakujua wanachokipigania au wameshaigeuza siasa kuwa ushabiki kama wa Simba na Yanga?

Ndugai ameongea point, stick with him, walete ufafanuzi wa hoja yake, sio kumtisha na vijembe vyao. Kesho wao wakianza kuipinga serikali then CCM wale wale wataanza kuwajibu kwa ile mipasho yao kule bungeni wataanza kulalamika CCM hawajibu hoja, kama ya Ndugai hamkutaka ijibiwe vizuri kwanini yenu ijibiwe toka kwa watu wale wale wenye majibu mabaya?

Sometimes wanaendekeza tabia mbovu ambazo wao wamekuwa wakizipinga bila kujua, majority of them wanatumia same level of thinking kwenye kuamua kila jambo linaloibuka mbele yao, hapa siioni tofauti yao na CCM tofauti yao ni playing ground ndio tofauti.

CCM wana uwanja mpana zaidi wa kuamua mambo mengi ya nchi kwa mazoea ndio maana wale maadui watatu wa tangu tupate uhuru bado tunao mpaka leo, wakati wao Chadema wana kauwanja kao kadogo cha kujifanyia mambo yao kwa mazoea.

Hapa mambo ya kunyimwa haki zao na msajili au polisi hayahusiki kabisa, ni level of thinking yao ndio inajadiliwa, hasa kwenye kucheza michezo ya kisiasa. Kwa namna hii sioni kama kuna lolote la maana watakalo achieve, wanajidumaza huku wao wanashangilia kwa mapambio ya kujipa moya kama vile "Chadema ni mpango wa Mungu" na mengineyo.

You’re absolutely right!
 
CHADEMA kitafanya lolote lile ambalo Lisu atasema, hata kama halina manufaa makubwa kwa chama. Lisu ndiye 'think tank' la CHADEMA. Bahati mbaya Lisu ni mwanaharakati zaidi, hana mbinu na mikakakati thabiti ya kisiasa.

You’re right. Lissu akisema kitu, hata kama ni bullshit, twende kazi. Na hiyo ni moja ya sifa za unyumbu wao unaosemwa kila siku!
 
Mkuu Denoo umechambua vizuri sana sana. Hilo ndio tatizo kubwa la CDM: kutokuwa strategic katika kufanya siasa zao. Wao badala ya kuangalia issues and the BIG STRATEGIC PICTURE, wanarukia petty issues na personalities, na visasi.
Mfano suala hili la Ndugai, hoja aliyoiibua Ndugai ni hoja muhimu yenye maslahi ya Taifa, lakini kwa sababu tu wana ugomvi binafsi na Ndugai, wameshindwa kumuunga mkono kwa hilo jambo ambalo lingewapa political mileage na kuonekana watetezi wa rasimilimali za nchi lakini pia ingokoleza zaidi madai ya KATIBA MPYA. Cha ajabu, nao wakaungana kumshambulia Ndugai kwa kuwa tu alishawaonea huko nyuma! VERY CHILDISH. Unaounga mkono agenda au issue ya mtu haina maana ya kuwa unaamuunga mkono au kumubali mtu huyo.
Hata suala la Polepole ni hivyohivyo, ingebidi wajitokeze hadharani kutetea haki yake ya kuelimisha umma kama PRINCIPLE na sio kumkejeli kwa kusema Polepole alikuwa kinara wa uchafuzi wa uchaguzi 2020.

Kwa kweli CDM na upinzani kwa ujumla wanahitaji kupata viongozi weledi na wenye akili kubwa zaidi. Otherwise, hawawezi kufika mbali na pia HAWAWEZI KUPEWA DOLA KAMWE kwa mentality hii.
Atleast mmoja umenielewa.
 
Ushiriki wa Chadema kwenye mambo yapi? mazuri au mabaya? kama ni ushiriki wa kuiandikia barua ofisi ya Spika kuijulisha juu ya uamuzi wa kuwavua uanachama hao wanawake 19 kwangu ni ushiriki mzuri.

Lakini kama ni ushiriki wa kusema kwakuwa hao wanawake wana uhusiano wa kimapenzi na baadhi ya viongozi wa Chadema ndio wakapeleka majina yao kwa Spika, hilo nataka ushahidi zaidi toka kwenu, hisia zenu pekee hazitoshi kujustify anything hapa.

Nasimama na kauli ya KM Mnyika kwamba kwa upande wao walimaliza kila kitu kuhusu kuijulisha ofisi ya Spika kwa maandishi juu ya uamuzi waliochukua dhidi ya wale wanawake, then burden of proof now ipo kwenu mnaosema mapenzi sijui yalifanya nini.
Ni kweli mmemaliza na mmenalizwa. Nilichosema ni kuwa wengine tunaumia sana kuona akili ndogo zikiendesha akili kubwa. Covid-19? Mbona mnaomba masndamano ya katiba,. Nachojaribu kusema ni kuwa kuna udhaifu upande wa bunge lakini unasaidiwa sana na uhuni ndani ya CHADEMA then mnaanza kuaminishwa au kuhalalisha huo uhuni kwa sababu za uongo na upuuzi kama ulizotoa hapo mwanzo.
 
Just to put the record clear, majina hayo 19, hayakujipeleka, yalipelekwa rasmi, na wakati walipoapishwa walikuwa ni wanachama halali wa Chadema.
Hivi hamjiulizi kwanini kikao cha Baraza Kuu hakiitishwi?. Kama ni kweli Chadema hawakupeleka rasmi majina, that means kuna forgery ni kosa la jinai, hamjiulizi kwanini mpaka leo Chadema haijairipoti polisi jinai hii ili uchunguzi wa kijinai ufanyike kubainisha ni nani alifoji barua za Chadema zenye offical letter head na signature zilizo peleka majina yale NEC.

Nawapongeza Chadema kwa kuuzingatia ushauri huu
P
Kwa hiyo CDM wanakula tu Ruzuku.Jamani siasa za bongo full maigizo.
 
CHADEMA mnashangaza sana mnaposhindwa kabisa kuitumia kila golden opportunity inayojitokeza kumdhoofisha adui yenu mkuu!

Mmeshaiokoa CCM kwa juhudi zenu wenyewe mara kadhaa sasa. Latest ni hili sakata la Speaker Ndugai. By failing to exploit the gigantic rift that Speaker Ndugai had caused, you basically saved your archenemy. Mungu aipe nini CCM?

Tambueni hili. No matter how much you hate a certain operative of your enemy, akishaanza kuwashambulia wenzake, usimpige; fanya kila uwezalo kukoleza mashambulizi yake kwa wenzake. Ni ajabu ya mwaka na aibu kubwa kwa CHADEMA kumshika shati mchezaji wa CCM anayekwenda kujifunga goli.

Seriously, it’s high time you hired effective coaches. Vinginevyo, mtaendelea kuchezea timu ya adui yenu bila nyie wenyewe kujitambua!
Golden opportunity ya CCM kuanguka ilikuwa ni 1995 siyo sasa hivi lakini Nyerere aliiokoa CCM na akautia vilema upinzani ambavyo wanavyo mpaka leo. Wakati ule Mrema alivyowageuka CCM ndiyo CCM ilikuwa vulnurable. Na kama si Nyerere kuingilia kati, kumbeba Mkapa across the finish line, CCM ingeangushwa. Leo hii hakuna golden opportunity.
 
Walisema baraza kuu la chama litakaa, liliketi kujadili? Chadema walienda mahakamani kushati kihusu forgery za signatures, majina na mihuri ya chama? Wanasiasa wa nchi hii ni zaidi ya ufikiriavyo.
Chadema kwasasa Ina mambo mengi ya msingi ya kufanya Kama kuimarisha chama ( Tunasonga kidigitali), Kesi ya mwenyekiti Mbowe, na kujenga ofisi nchi nzima. Kuliko kukaa mnawajadili kila siku watu mliokwisha kuwafukuza uanachama lakin serikali inawakingia kifua
 
Mkuu Denoo umechambua vizuri sana sana. Hilo ndio tatizo kubwa la CDM: kutokuwa strategic katika kufanya siasa zao. Wao badala ya kuangalia issues and the BIG STRATEGIC PICTURE, wanarukia petty issues na personalities, na visasi.
Mfano suala hili la Ndugai, hoja aliyoiibua Ndugai ni hoja muhimu yenye maslahi ya Taifa, lakini kwa sababu tu wana ugomvi binafsi na Ndugai, wameshindwa kumuunga mkono kwa hilo jambo ambalo lingewapa political mileage na kuonekana watetezi wa rasimilimali za nchi lakini pia ingokoleza zaidi madai ya KATIBA MPYA. Cha ajabu, nao wakaungana kumshambulia Ndugai kwa kuwa tu alishawaonea huko nyuma! VERY CHILDISH. Unaounga mkono agenda au issue ya mtu haina maana ya kuwa unaamuunga mkono au kumubali mtu huyo.
Hata suala la Polepole ni hivyohivyo, ingebidi wajitokeze hadharani kutetea haki yake ya kuelimisha umma kama PRINCIPLE na sio kumkejeli kwa kusema Polepole alikuwa kinara wa uchafuzi wa uchaguzi 2020.

Kwa kweli CDM na upinzani kwa ujumla wanahitaji kupata viongozi weledi na wenye akili kubwa zaidi. Otherwise, hawawezi kufika mbali na pia HAWAWEZI KUPEWA DOLA KAMWE kwa mentality hii.
Kaanzishe chama chako au uungane na Zitto mumuunge mkono Ndugai
 
Wewe ulisema kuwa chadema hawana siasa za kistaarabu...ndo nikakuandikia hayo na nilikukopi ulichoandika nikakujibu. Umeona uliandika ujinga ndo unasema nilidandia treni kwa mbele

Again, umedandia train kwa mbele! Hakuna mahali popote mimi nilisema chama fulani ndiyo wana siasa za kistaarabu. Mimi niliandika kukataa argument kwamba CDM sio watu wa siasa majitaka!
 
CDM haina siasa za kistaarabu hata kidogo bali ina ukosefu mkubwa wa mbinu za medani na umahiri wa siasa majitaka. Jambazi hawezi kuchukuliwa kuwa raia mwema kwa sababu tu ameshindwa kuwa na sophisticated techniques za uhalifu!

Viongozi wa CDM wamebadili gia angani au wamekengeuka mara ngapi katika maswala makubwa na ya msingi?
Unajua kusoma wewe? Umeandika nini hapo? Unakuwa kama Ndugai, unasema kitu halaf unakuja kukataa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom