CHADEMA watikisa jimbo la Spika Makinda....

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanza kuitikisa ngome ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, baada ya kufungua matawi ya chama hicho katika mkoa mpya wa Njombe na kuingiza wanachama wapya zaidi ya 100 ambao ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hatua hiyo ya Chadema imelenga kujiimarisha katika maeneo ya vijijini, ikiwa ni pamoja na kufuta utamaduni wa baadhi ya viongozi wa chama tawala kupita bila kupingwa katika chaguzi mbalimbali.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chadema kimeingia katika Jimbo la Spika Makinda la Njombe Kusini katika ziara ya viongozi wa chama hicho katika mkoa wa Njombe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza jana na wakazi wa Kata ya Mtwango, Tarafa ya Makambako Wilaya ya Njombe, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Njombe Magharibi (sasa mhamasishaji wa Chadema Mkoa wa Njombe), Thomas Nyimbo, alisema tayari amepokea kadi 10,000 kutoka makao makuu ya chama hicho kwa ajili ya kuzigawa kwa wanachama wapya wanaojiunga na Chadema. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Nyimbo kada wa zamani wa CCM na aliyewahi kuwania mbunge wa chama hicho katika Jimbo la Njombe Magharibi mwaka jana baada ya kushinda katika kura za maoni za chama hicho, jina lake lilienguliwa na kugombea jimbo hilo kupitia Chadema. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Nyimbo, aliangushwa katika uchaguzi huo na Gerson Lwenge, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Maeneo mengine yaliyofikiwa na Chadema na kufanikiwa kuwateka wanachama wa CCM ni Jimbo la Njombe Kaskazini ambalo linaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Deo Sanga (Jah People), ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika mkutano huo, Nyimbo, alisema inashangaza kuona kuwa bado kuna vijiji na kata nchini ambavyo vinakumbatia mfumo wa chama kimoja wakati vipo vyama kama Chadema ambacho kinachochea maendeleo kwa kuisukuma CCM kutekeleza ahadi zake.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Ndugu zangu tumepokea kadi zaidi ya 10,000 kutoka makao makuu ya Chadema Taifa na lengo letu ni kuzigawa kwa wanachama wanaojiunga na chama hiki kule Njombe mjini, tumeshaanza kuingiza wanachama na hivi sasa tunaendelea na zoezi hilo kwa kila jimbo,” alisema na kuongeza:[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Na leo tumefungua ofisi ya tawi hapa Mtwango na kuingiza wanachama 100, kwa kuwa lengo letu ni kujiimarisha na kuwafikia watu wa vijijini.”[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa Nyimbo, Chadema kimepanga kuendelea kuwahamasisha wananchi wa mkoa mpya wa Njombe kujiunga na chama hicho.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ziara hiyo ilianza wiki iliyopita na juzi chama hicho kilipanga kuingia katika Jimbo la Njombe Magharibi kwa Lwenge, lakini ziara hiyo iliahirishwa kutokana na mvua.

SOURCE: NIPASHE[/FONT]
 
Kaza buti twende hii ikifanyika kila mahali naamini mambo yatakuwa mbwitombwito.
 
Viva Chadema, kama Zambia wameweza sisi tushindwe nini, 2015 we need changes, Nia tunayo, Uwezo tunao, Sababu tunazo.
 
Chadema wanashambulia kila kona ya nchi kama nyuki.
 
Nafikiri Chadema wabadilishe mwelekeo na mtazamo.
Mtazamo wenu ni kutangaza sera zenu kwa wananchi wote na sio kukazania wanachama. Mnatakiwa mfahamu kuwa kuwa na kadi zaidi ya moja ya chama cha siasa sio kosa huko tanzania. Hulka ya wabongo ni muhali na hivyo wengi ni walaghai.
 
Nafikiri Chadema wabadilishe mwelekeo na mtazamo.
Mtazamo wenu ni kutangaza sera zenu kwa wananchi wote na sio kukazania wanachama. Mnatakiwa mfahamu kuwa kuwa na kadi zaidi ya moja ya chama cha siasa sio kosa huko tanzania. Hulka ya wabongo ni muhali na hivyo wengi ni walaghai.

Uko sawa mkuu lakini tambua utangazaji/usambazaji wa sera unaendana (hand in hand) na kurecruit wanachama. Binafsi naona anachofanya Nyimbo ni sahihi kabisa, hata wagombea wa majimbo mengine ambao walishindwa last election wangekuwa busy this time wanaeneza sera na kupata wanachama c kusubiri 2015 ndo wanaibuka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom