CHADEMA wateka Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wateka Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  16 NOVEMBER 2011


  *Wabunge walia na Lissu, wahoji usomi wake
  *Waionya serikali kutochukua hatua mapema
  *Mnyika: Kikao cha Kamati Kuu kukutana kesho


  Na Godfrey Ismaely, Dodoma

  SIKU moja baada ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na NCCR-Mageuzi, kususia mjadala wa
  Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, uamuzi huo unadaiwa kutokuwa na tija kwa Watanzania badala yake unalenga kuwapotosha.

  Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliyasema hayo Bungeni mjini Dodoma jana wakati wakichangia mjadala huo na kudai kuwa, Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tindu Lissu (CHADEMA), anatumia vibaya usomi wake kupotosha Watanzania.

  Walisema maoni yaliyowasilishwa bungeni na Bw. Lissu ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Sheria na Katiba, yalilenga kupotosha Watanzania na kulichafua jina la Muasisi wa Muungano, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Mbunge wa Simanjiro, mkoani Manyara, Bw. Christopher Ole Sendeka (CCM ), alisema Bw. Lissu ameshindwa kutumia vyema usomi wake kuelimisha Watanzania badala yake anajenga hoja za kuwagawa jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa taifa.

  "Kwa mara ya kwanza namsikia msomi anayejiita mwanasheria kupitia hotuba yake akimkashifu Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kudai alimomonyoa uhuru hii haiwezekani, naomba arudi tena darasani kwani usomi wake bado haujamsaidia, inakuweje anamtuhumu Baba wa Taifa na kuwapotosha Watanzania," alisema.

  Bw. Sendeka alisema elimu aliyonayo Bw. Lissu, haijamsaidia hivyo anapaswa kupatiwa mafunzo ya ziada ili yaweze kumkomboa kifikra.

  "Katika hili tupo tayari kumpatia mafunzo ya ziada, tutamfundisha bure bila gharama yoyote, Watanzania mnapaswa kutambua kuwa, kinachojadiliwa hapa si uidhinishwaji wa Katiba Mpya kama wanavyopotoshwa bali ni mchakato wa kupata maoni ya kuunda tume huru ambayo itakusanya maoni ya wananchi kuunda Katiba Mpya," alisema Bw. Sendeka.

  Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Mohamed Rashid (CUF), alisema inasikitisha mbunge anapokula kiapo cha kuitumikia na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini anatumia nafasi hiyo kupotosha umma hali ambayo inaweza kuleta vurugu.

  "Ukisoma katika muswada huu, kuanzia kipengele cha kwanza hadi hitimisho, hakuna sehemu inayoeleza kwamba nchi yetu inatawaliwa kwa misingi ya kidikteta wala ufalme, jana (juzi), Bw. Lissu wakati akiwasilisha hotuba yake, alipotosha Watanzania...hii ni hatari.

  "Ukisoma ukurasa wa 20 wa hotuba ya Bw. Lissu, sisi wabunge tunaambiwa hatuna mawazo...hii ni aibu kubwa, dharau hizi hatuzitaki mimi Rashid nimekaa katika bunge hili muda mrefu, haijawahi kutokea hali kama hii," alisema Bw. Rashid.

  Aliongeza kuwa, kinachofanyika kwa sasa si kupitisha katiba mpya, bali ni mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya kuandika katiba.

  Alisema haiwezekani Tanzania igawanyike vipande kwa sababu ya ya watu fulani bali katika hatua ya kupiga kura, tume zote za uchaguzi zishiriki kuandaa vitengo vyao ili kila mwananchi aweze kushiriki kupiga kura.

  Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wabunge wa CHADEMA, Bw. John Mnyika, amesema baada ya kutafakari, wabunge wa chama hicho kwa pamoja wamefikia uamuzi wa kuitisha Kikao cha Kamati Kuu cha dharura ambacho kitafanyika kesho na kutoa mwelekeo wao juu ya muswada huo.

  "Msingi wa kikao hiki ni kutoa mwelekeo jinsi muswada huu ulivyokaa vibaya kwa wananchi kwani haujawatendea haki ya kuwasilisha maoni yao kama wanavyotaka," alisema.

  Alisema chama hicho kinatambua kuwa, muswada huo ulipowasilishwa bungeni ulitoka kwa mara ya kwanza si kwa mara ya pili kama ulivyowasilishwa na Waziri mwenye dhamana.

  Katika hatua nyingine, wabunge hao walienda mbali zaidi na kuionya Serikali kuchukua hatua mapema dhidi ya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani na uhamasishaji wananchi kushiriki vurugu kinyume na sheria za nchi kwani machafuko yaliyotokea nchi za Rwanda na Burundi yalianza kwa kauli kama zinavyotolewa na viongozi wa CHADEMA.

  "Mimi naona hawa wana lao, tena nia yao ni mbaya, nchi ya Rwanda na Burundi, walianza hivi hivi, hapa lazima Serikali ichukue hatua," alisema Mbunge wa Kibakwe, Bw. George Simbachawene.   
 2. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Bahati mbaya wabunge wa CCM wameshazoea sera za 'Ndiyo mzee' wakiambiwa ukweli wanakuwa wakali kama pilipili. Nadhani hata hawajaisoma Hotuba ya Kamanda Lissu. Hotuba ya Lissu naifananisha kama Biblia au Kurani ambayo ukiisoma ili Upate sababu za kuipinga huwezi kuielewa hata kidogo! Kama ni Darasa wabunge wa CCM wanahitaji kwenda wao kwanza.....
   
 3. R

  RMA JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tundu Lisu ana makosa gani kueleza mabaya ya Nyerere? Kwani Nyerere ni Mungu? Kwani kila kitu alichokifanya Nyerere kilikuwa ni sahihi? Hata Nyerere mwenyewe alipata kukiri kuwa katika utawala wake alifanya na makosa kwa vile yeye sio malaika! Hiyo kauli iliwapita CCM kushoto? Sasa Nyerere amekuwa kanuni ya imani? Iwapo ccm wanamuenzi Nyerere mbona siasa ya ujamaa wameizika? Unafiki mtupu!
   
 4. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,971
  Trophy Points: 280
  Nyie kiboko yenu ni godfrey dilunga wa raiamwema.MTAACHA LINI KUTAFUTA UMAARUFU WA KIJINGA?.
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  yeye ole sendeka ameelimika nini mpaka anamdharau lissu!? Au kutishia watu kwa bastola ndio kuelimika!?
   
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tatizo wanaendekeza propaganda badala kukabiliana na ukweli wakajenga hoja, wanaanza kushambulia wakidhani bado kuna mtu hajui pumba na mchele. Waelewe saizi kuna idadi kubwa ya watanzania wanaoelewa sheria, katiba na mambo mengi yahusuyo nchi yao kwa hiyo wabadilike au wang'atuke siyo kulia lia kwa kutoa vitisho ambavyo havisaidii kwa vizazi vya leo.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sijui kama walimsikia au walimwelewa tindu lisu usikute walikuwa wamelala wakaja kushituli kuwa lisu kamwaga sumu bungeni..chadema tunataka maanamano si ya kwenda na kurudi ni ya kambi..
   
 8. T

  T.K JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lissu kweli anawakosesesha raha magamba
   
 9. v

  valbert Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM vp?mbn cwa elewi kila anae cmama yaleyale ina maana akili zenu sawa?acheni unafiki.
   
 10. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli daima unaumaa lissu amesema ukweli na anatumia usomi wake kuwasaidia wananchi kwa kuwafumbua macho dhidi ya serikali ambayo inawaada kwa kufanya vitu ambavyo wananchi walio wengi siyo rahisi kugundua hiyo mitego. Bunge letu lina wafanyabiasha na wasema hovyo wanashindwa kuanalyse issues wao wanakalia kuattack mtu na chama kitu ambacho hakina msingi wowote kwa mustakabali wa taifa letu.bottom line wananchi wanachotaka ni katiba mpya ambayo itakuwa imefuata misingi ya haki,ushirikishwaji na uwazi.
   
 11. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jamani, lazima tuwe honest, hivi kweli Ole Sendeka ni mtu wa kupima elimu yake na ya Lissu? Yaani baba mzima unajikosha na kujificha kwenye Ukuta wa Mwl Nyerere. Who is Nyerere ambaye hapaswi kuelezewa mabaya yake? Ukiwa mpambanaji lazima uwe tayari kukosolewa lakini sioni upambanaji wa Sendeka ila naona pumba zilizokubuhu.
   
 12. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la magamba wanajaribu kumtumia mwl. Nyerere kuficha maovu yao kwamba kwa kutumia nukuhu zake basi utakubalika.laah asha unyerere siyo upele useme utakumbukiza.nyerere hakuwa malaika hata yeye alikiri hilo.
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi kinachofanya nisifuatilie BUNGE,ni suala la kutoujadili MUSWADA na kujadil watu!
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wasifu wa MH Sendeka.

  Yaani huyu kiilaza na shule ya kuunga kwa ukoka anathubutu kufungua domo lake la chewa na kukashifu Elimu ya mtu?

  Highest Level of Education ni Community Development Course Hiyo ni Diploma ya kutunga.
  Kashindwa kusema ana Diploma ya Utapeli ya SKY Hoteli enzi zileeee!

  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]MS.TCDC & Kimage Manor College (IRELAND)[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]Community Development Course[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1995[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1997[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]DIPLOMA[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  Eti anadai alikuwa leader of student union wa UVCCM tangu 1975??? CCM imezaliwa 1977
  Shule kaanza 1974, ina maana alikuwa kiongozi wa CCM tangu yuko darasa la pili???

  Sendeka ni mjinga na anatumiwa kama kaptula ya ndani na Viajuza na Vigagula vya CCM

  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]alutation[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Honourable[/TD]
  [TD]Member picture
  [​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]First Name: [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Christopher[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Middle Name:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Olonyokie[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Last Name:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Ole-Sendeka[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="width: 20%, bgcolor: #E9F0F0"]Member Type:[/TD]
  [TD="width: 38%, bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Constituent:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Simanjiro[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Political Party:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]CCM[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office Location:[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]P.O.Box 14384, Arusha[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office Phone: [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]+255 768 300000[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Ext.: [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office Fax: [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Office E-mail: [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]csendeka@parliament.go.tz[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Member Status: [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Current Member[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #CCFFFF"]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Date of Birth [/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 5"]EDUCATIONS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]School Name/Location [/TD]
  [TD="width: 27%, bgcolor: #B4C6DB"]Course/Degree/Award [/TD]
  [TD="width: 15%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Start Date[/TD]
  [TD="width: 13%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]End Date[/TD]
  [TD="width: 10%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Level[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Naberera Primary School[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]Primary Education[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1974[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1980[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]PRIMARY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Monduli Secondary School[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]O-Level Education[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1981[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1984[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]SECONDARY[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Oldmoshi High School[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]A-Level Education[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1985[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1987[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]MS.TCDC & Kimage Manor College (IRELAND)[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]Community Development Course[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1995[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1997[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]DIPLOMA[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]CERTIFICATIONS [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Certification Name or Type[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Certification No. [/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Issued[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Expires[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]EMPLOYMENT HISTORY [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB"]Company Name [/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Position [/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]From Date[/TD]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, align: center"]To Date[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]The Parliament of Tanzania[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Member - Simanjiro Constituency[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]2005[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]2015[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Non-Government Organisations- NGO's[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Programme Coordinator/ Officer[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1994[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1997[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Prime Minister's Office[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Secretary[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1990[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1993[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]POLITICAL EXPERIENCE [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu"]Ministry/Political Party/Location[/TD]
  [TD="class: text_menu, width: 31%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]Position[/TD]
  [TD="class: text_menu, width: 12%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]From[/TD]
  [TD="class: text_menu, width: 10%, bgcolor: #B4C6DB, align: center"]To[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Head of Admnistration (UVCCM-HQ)[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1999[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]2001[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Member of National Executive Council(NEC)[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1997[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]2002[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chairman - Simanjiro District[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1993[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]2007[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chairman -UVCCM[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1989[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1994[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Chama Cha Mapinduzi - CCM[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"]Leader of Student Union(UVCCM)[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1975[/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0, align: center"]1987[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 2"]PUBLICATIONS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Description[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Published Date[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [TD="bgcolor: #E9F0F0"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 4"]SPECIAL SKILLS[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB"]Skill Name or Description[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Years Experience[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Acquired Through[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"]Skill Level[/TD]
  [/TR]
  [TR="class: detail"]
  [TD="colspan: 7"]No items on list[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [TD="bgcolor: #EDEEEE"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B4C6DB, colspan: 5"]RECOGNITIONS [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"] Recognition Type[/TD]
  [TD="class: text_menu, bgcolor: #B4C6DB"] Recognition Date[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm tatizo lenu ni uwezo mdogo wa kufikiri.
   
 16. H

  Haika JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  waliobaki bungeni kazi ni kusinzia na kujadili hotuba ya Lissu!!!
  Wameusoma mswada wenyewe kwanza?
   
 17. H

  Haika JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Naomba waheshimiwa wabunge waliousoma mswada wanyooshe mokono juu, naona mikono nje kwa wabunge wa chadema, ndani naona vidole ama vinne tu,
  basi tujadili hotuba ya Lissu
   
 18. Niconqx

  Niconqx Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wapinzani wachache waliopo bungeni wakipewa nafasi ya kusikizwa itaokoa maafa yanayoweza kutokea.watanzania wa leo wamebadilika kutokana na nguvu ya taarifa 'power of information'
  itumike busara ya hali ya juu kufanya maamuzi kabla ya kuja kujuta baadaye.
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Hawa mafisadi siku zao ina idadi ndogo sana kwa hali wanayenenda nayo! Hawa tusiwashtue hata kidogo maana hili neno litakamilika."ASIYEFUNZWA NA MAMAE UFUNZWA NA ULIMWENGU" Hapo ndipo watagutuka kwamba Watanzania wa leo kumbe siyo wale tena.
   
 20. B

  Balozi Chriss Senior Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo la wabunge wa CCM hawajui ni kwa nini wamechaguliwa kuwakilisha wananch....Sasa aliyosema Tundu Lisu mbona ni mambo ya msingi sana na kama wao ni wasomi kwanini wasikosoe misingi ya kipuuzi ambayo kwa namna moja au nyingine aliwekwa na Baba wa Taifa kama ipo...Hivi unadhani hoja ya usomi anaoongelea Ole Sendeka kweli inamashiko?
  SASA watake wasitake wananchi tunaungana na CDM mpaka kieleweke.
   
Loading...