CHADEMA wateka Bunge

Lissu kawashika pabaya, wanahaha kutafuta namna ya kupotosha ukweli wa wazi alousema Lissu. Ndo maana kila anayesimama haachi kumtaja lissu kwa mambo binafsi badala ya kujikita kuchangia mswada wao. Wamekuwa kama waimba mipasho na kiitikio ni Lissu na chadema. Shame on magamba!
 
Jamani, lazima tuwe honest, hivi kweli Ole Sendeka ni mtu wa kupima elimu yake na ya Lissu? Yaani baba mzima unajikosha na kujificha kwenye Ukuta wa Mwl Nyerere. Who is Nyerere ambaye hapaswi kuelezewa mabaya yake? Ukiwa mpambanaji lazima uwe tayari kukosolewa lakini sioni upambanaji wa Sendeka ila naona pumba zilizokubuhu.

jamaa anaka div sifuri form six kama mimi halafu anabishana na mwadhili wake kweli siasa haina heshima..
 
Nyie kiboko yenu ni godfrey dilunga wa raiamwema.MTAACHA LINI KUTAFUTA UMAARUFU WA KIJINGA?.

G. Dillunga ni mwandishi mzuri kweli, na anatoa maoni yake kama waandishi wengine!
Akiwa mtu mwenye kujua ukweli, kuna vitu ameviruka kwenye makala yake ya jana na nlimwambia pia asome makala ya Msomaji Raia.
Tulia, chukua mda linganisha kati ya G. Dillunga na Msomaji Raia nani stori yake inajenga msawazo na ulinganifu katika kujenga tafakuri bila kuweka hisia binafsi!?
Ni rahisi kuona hisia za Dillunga....
 
muswada usomwe upya na mjadala uanze upya kwa kuwa wabunge wa ccm na cuf wamekuwa wakijadili hotuba ya tundu lissu badala ya kutoa maoni yao kutokana na muswada uliokuwa mbele yao, siku zote wabunge wa ccm kazi yao ni kujibu hoja za wabunge wa upinzani badala ya kutoa maoni yao juu ya muswada wanasahau kuwa kazi ya kujibu hoja ni ya yule aliyeleta muswada(waziri), sasa waziri kazi yake bungeni itakuwa nini!? kuleta miswada bungeni tu!? wabunge wa ccm wamezoea mipasho hawana hoja za msingi kazi yao ni kusikia wapinzani wametoa hoja au maoni gani halafu wao wanadandia kwa mipasho!
 
wapinzani wachache waliopo bungeni wakipewa nafasi ya kusikizwa itaokoa maafa yanayoweza kutokea.watanzania wa leo wamebadilika kutokana na nguvu ya taarifa 'power of information' itumike busara ya hali ya juu kufanya maamuzi kabla ya kuja kujuta baadaye.
CCM WANASEMA WABUNGE WA UPINZANI WAKO WACHACHE SANA NA WAKIPEWA NAFASI WATALIPOTOSHA TAIFA NA KULIPELEKA KWENYE MACHAFUKO MAKUBWA, wanasema njia ya kuwadhibiti chadema na nccr ni kuhakikisha wanaupitisha mswada
 
Tundu Lisu ana makosa gani kueleza mabaya ya Nyerere? Kwani Nyerere ni Mungu? Kwani kila kitu alichokifanya Nyerere kilikuwa ni sahihi? Hata Nyerere mwenyewe alipata kukiri kuwa katika utawala wake alifanya na makosa kwa vile yeye sio malaika! Hiyo kauli iliwapita CCM kushoto? Sasa Nyerere amekuwa kanuni ya imani? Iwapo ccm wanamuenzi Nyerere mbona siasa ya ujamaa wameizika? Unafiki mtupu!


Nop, Nyerere sii Mungu na hajawahi kupenda kuabudiwa! Mungu ni Slaa. mnaye muabudu..
 
Hawa wabunge wa CCM ni wanafiki kabisa.Toka lini wakamuenzi Nyerere? Alipoaga dunia tu Nyerere maadili aliyoyaacha wameyatupa mbali wamebakiza unafiki tu.Hivi kwanza watueleze hii nchi tunafuata ujamaa na kujitegemea au ufisadi,ubinafsi,ushikaji,uswahiba na kula rushwa?Magamba acheni wasomi kama Lissu na wanaharakati kuyaeleza maovu yote toka enzi za Mwalimu,Mwinyi,Nkapa na sasaJK.Katiba mpya maana yake tunaunda taifa jipya siyo kucopy yaliyopo kwenye katiba ya sasa na kuyapest na kuuita tumeunda katiba mpya.Hivi hawa wabunge wa chama cha magamba wanaelewa au ni vilaza kupita kiasi.
 
CCM na mkewe CUF sasa wamejidhihirisha kuwa wana akili za kushikiwa, badala ya kujadili hoja wanamjadili mtu.Hii ndiyo taabu ya kutumia masaburi kufikiri.
 
Jamani let us be serious hivi Ole Sendeka ambaye hajawahi kusoma hata LLB 101, leo hii kweli mbele ya
Bunge anajitapa kwamba anaweza kumfundisha lawyer Tundu Lissu graduate law? This is Only Possible in
Tanzania Parliament!

Yale yale ya UPE, STD VII failure anakwenda kufudisha shule ya msingi. Ole Sendeka is still living in that age.
No wonder hajui hata chama chake CCM kimezaliwa lini. Anachakachua kwamba eti alikuwa chairman wa
UV-CCM 1975. Wakarti dunia nzima inafahamu CCM ilizaliwa 1977. Ubunge wake kwanza unaweza kufutwa
kwa kosa hilo (udanganyifu) refer kesi ya Kihiyo wa Temeke.

Shame on your masaburi Ole Sendeka
 
Its shame kuona jinsi ambavyo wabunge wa ccm walivyo na uelewa mdogo,hapa ndipo panakuwa na haja ya wabunge kuwa na kiwango fulani cha elimu.hoja alizotoa lissu ni za mantiki kubwa na za kisomi na ziko very analytical..hakuna asiyejua kuwa mswada huu ni ya namna ya kuandaa tume ya kuratibu mchakato wa ukusanyaji maoni,lakini sheria ikishatungwa ikasema terms of reference atatoa rais,kama kuna jambo rais hapendi lipigiwe kura litapigiwa? Atakayesimamia ukusanyaji wa maoni ni tume ya uchaguzi,watanzania wana imani na tume ya uchaguzi kwa kiasi gani? Ikishasema bunge la katiba litakuwa na wajumbe sawa bara na visiwani kuna uwiano sahihi wa uwakilishi? Kumbuka bara tunao viongozi ambao tayari ni wazenji,ikishasema ripoti itawasilishwa kwa rais,kama haipendi atairidhia? NASEMA WABUNGE WA CCM MNACHEMKA,ZITENDEENI HAKI ELIMU ZENU.Nimesikitishwa na mwigulu mchemba na maoni yake? Wapi makamba? Ole sendeka,mama kilango,yule mbunge wa kisarawe,lusinde NIMEWASAMEHE BURE.
 
The eagle has landed, under the pilot-ship of admiral TUNDU LISSU, the real patriot and statesman.The Tanzania Parliament has been set ablaze, and them ccm members of it are perturbed by the emission of heat from Lissu's presentation.
 
Iv hwa ccm wananini ivi wao ndo wanamwenzi mwalimu? Tena ccm ndo wanamdharau mwalimu kwa vitendo ili niwaelewe wanachokiongea waludishe azimio la arusha kama wao wamemdharau mwalimu tena kwa kufuta miiko ya taifa na wamepoteza heshima kabisa sembuse maneno ya lissu ambayo ni ya ukweli Mbona wakiambiwa ukweli wanakuwa wakali sasa hizo ngonjela wanazoziimba bungeni hazna impact kabisa bila wapambanaji wetu wa upinzani hasa cdm
 
Huyo Ole Sendeka anaposema eti kukosoa yaliyofanywa kwenye awamu ya kwanza ni kumdharau baba wa taifa, si kweli:

Naomba nimkumbushe ole Sendeka maneno ya Mwl aliposema: Awamu ya kwanza tuefanya mazuri mengi na vile vile tumefanya makosa/Mabovu mengi tu! Ndiyo,!! tusifanye makosa sisi malaika!!. Akaendelea: Kazi ya awamu inayofuata ni kuendeleza yaliyo mema na kuacha yale mabovu/ya kijinga. Akamalizia kwa kusema:

Taabu yenu mnaacha yale mema mnachukua yale ya kijinga/ mabovu, watu wa ajabu kabisa!! Akashangaa.
Sasa Sendeka anajifanya haya maneno hajapata kuyasikia.

Wanachofanya kambi ya upinzani ni kuachana na yale mabovu aliyofanya baba wa taifa na awamu yake ya kwanza, badala yake wanataka kurekebisha ili mambo yaendane na hali halisi tuliyo nayo kwa sasa. Big up CDM/Upinzani.
 
Jamani let us be serious hivi Ole Sendeka ambaye hajawahi kusoma hata LLB 101, leo hii kweli mbele ya
Bunge anajitapa kwamba anaweza kumfundisha lawyer Tundu Lissu graduate law? This is Only Possible in
Tanzania Parliament!

Yale yale ya UPE, STD VII failure anakwenda kufudisha shule ya msingi. Ole Sendeka is still living in that age.
No wonder hajui hata chama chake CCM kimezaliwa lini. Anachakachua kwamba eti alikuwa chairman wa
UV-CCM 1975. Wakarti dunia nzima inafahamu CCM ilizaliwa 1977. Ubunge wake kwanza unaweza kufutwa
kwa kosa hilo (udanganyifu) refer kesi ya Kihiyo wa Temeke.

Shame on your masaburi Ole Sendeka

Hii tamu sana. Ningefurahi kuona mchango wa hawa wafuatao kuhusu hii: rejao, mzee, faizafoxy, fiksiman, zakazaka, nyantella, na yule mwenye malaria sugu
 
Amani yetu ndio tatizo la ccm kutojua tunataka katiba mpya...yenye 1. tume huru ya uchaguzi 2.kulinda uchumi wetu 3. kuwawajibisha viongozi mafisada
 
Tundu Lissu na Makamamnda wetu wa CDM msikate tamaa Watanzania wengi tuko pamoja nanyi! hii sio miaka ile ya kudanganywa tena! Mageuzi ya Technoligia ya habari yamefanya sasa watu wengi wanajua mambo mengi yanayoendelea na wanajua utapeli na ukweli! CCM wamegeuza Mjadala,wamekwepa hoja za Msingi wameamua kushambulia watu! wamekuwa vituko tu.Ole sendeka kumbe hanakitu kichwani du! aisee ndiyo anataka kumfundisha Tundu Lissu kazi kwelikweli. CV yake inatia huruma jamani!

Hamad rashid yeye anatetea maslahi ya Wazanzibar nashangaa CCM bara hagundui hilo,wenzenu wamekuwa favored lazima waishabikie,CCM bara wanasujudia sana wazanzibar ndiyo maana wanafoka bungeni wakati wengine tunawaona kama wageni wa nchi nyingine wanao tuchezea hapa kwetu.
 
Kuna hoja kama mbili tatu hivi Watanzania tunapaswa kuzifahamu
  1. Ikumbukwe CCM si kwenye Ilani yao (2010-2015) na wala kwenye mikutano yao ya kampeni si ya udiwani, ubunge, wala urais hakuna hata sehemu moja walisema kwamba watabadili Katiba. Hivyo ni busara kwao kuwasikiliza wale waliosema watabadilisha!!
  2. Msimamo wa CCM juu ya Katiba Tanzania ni kwamba katiba ya sasa kwao haina matatizo (Ushahidi wa hili lipo Ibara ya 32(4) kwamba wananchi wakikataa kwa 50+% tutarudi kwenye katiba ya zamani na si kuanza upya mchakato).
  3. Ni Rais mwenyewe na chama chake ndio wamepoteza imani ya watanzania kwa maneno na vitendo mfano kusamehe wezi wa EPA waliorudisha pesa walizokwapua na kupigia kampeni watu wabadhirifu (watuhumiwa) na ambao serikali yake imewashitaki mahakamani.
  4. Tunatengeneza katiba itakayo tupeleka kwa zaidi ya miaka 100 ijayo hivyo si vema maslahi ya vyama yakawa mbele kama CCM wanavyotaka. Nani anamjua Rais wa Tanzania wa 2015 au 2020 au 2025 nk.........!!? Kwanini maslahi ya vyama yako mbele??
  5. Si yote wayatakayo CDM (Upinzani wakiwemo NCCR) lazima yaingie kwenye Katiba na sio yote wayapendayo CCM yawe hivyo kwa sababu ya wingi wao (to strike a balance ni muhimu).
Rai yangu kwa watawala ni kusoma alama za nyakati, ubabe na vitisho vina mwisho na mwisho ni mbaya. Tujenge Tanzania yenye neema na ustawi mzuri wa kiuchumi, kisiasa, kijamii, na kiutamaduni. Kudhani kwamba Mwlimu hakuwahi kukosea ni MAKOSA. Rasimu ya muswada uliowasilishwa bungeni unamapungufu mengi na waliobaki badala ya kuujadili muswada wanajadili watu (CDM). Waliobaki na waliotoka nani ni mbora sijui!!??
Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom