Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,446
- 5,647
Ukishagundua kwamba jukumu la kujiletea maendeleo wewe na familia yako ni LAKO na hakuna mwanasiasa, hakuna chama, wala hakuna kiongozi mwenye manufaa na wewe, utaishi maisha mazuri na ya amani sana.
Tuseme elimu tunayopata kuhusu umuhimu wa sera na mikakati bora ya kisiasa katika kutengeneza mazingira wezeshi kiuchumi kwa wananchi ni porojo tu? Yaani haijalishi kama nchi inaongozwa na mtu aina ya Mugabe, Nyerere, Obama, Kuffuor, Kim Jong Il, Biya, Mao, Deng, Merkel - wote sawa tu, hawaongezi wala kupunguza kitu kwenye maisha ya mtu?
Umeshawahi kujiuliza inakuwaje wahabeshi wanakufa kwenye malori kukimbia nchi yao? Au maelfu wanazama Mediterranean kukimbilia ulaya? Nchi kama Nigeria na DRC zinakimbiwa! Unafikiri hizi nchi hazina rasilimali za kuwawezesha kuishi na kufanikiwa kimaisha? Think again, ndipo utaelewa kwa nini nchi za watu makini hawachezei chaguzi za viongozi wao wa kisiasa.