CHADEMA: Watanzania tusiwanyanyapae wenye ulemavu

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
VIONGOZI na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameomba wanancvhi kutowanyanyapaa na kuwabagua watu wenye ulemavu nchini na badala yake wajenge utamaduni wa kuwasaidia kila pale inapowezekana.

Ombi hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,
Bw. Freeman Mbowe alipokuwa akikabidhi msaada kwa mlemavu wa miguu, Bi. Edna Katinga (20) mkazi wa Kijiji cha Kitendaguro Manispaa ya Bukoba ambaye pamoja na mwanawe, Joanes George (5) ni walemavu wa miguu na hutembea kwa kutambaa chini.

Bw. Mbowe alimkabidhi Bi. Katinga sh. 6,393,000 ambazo zilichangwa na viongozi na wanachama wa CHADEMA wa mkoani Kagera katika hafla fupi ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na uongozi wa CHADEMA mkoani humo juzi usiku.

Katika kiasi hicho, Bw. Mbowe binafsi alichanga sh. 2,000,000 taslimu ambapo mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMA kutoka mkoa wa Morogoro,
Bi. Regia Mtema alijitolea kumchangia mlemavu huyo shilingi 100,000 kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia hiyo juzi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Dkt. Wilbroad Slaa alijitolea kumpeleka mtoto Joanes katika hospitali maalumu ya watu wenye ulemavu wa viungo ya CCRBT iliyoko Dar es Salaam ambako atafanyiwa uchunguzi wa kitalaamu ili kuangalia uwezekano wa kumwezesha kutembea kawaida.

Nenda hapa:http://majira-hall.blogspot.com/2011/03/chadema-wamchangia-mlemavu-mil-6.html
 
VIONGOZI na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameomba wanancvhi kutowanyanyapaa na kuwabagua watu wenye
ulemavu nchini na badala yake wajenge utamaduni wa kuwasaidia kila pale inapowezekana.

Ombi hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alipokuwa akikabidhi msaada kwa mlemavu wa miguu, Bi. Edna Katinga (20) mkazi wa Kijiji cha Kitendaguro Manispaa ya Bukoba ambaye pamoja na mwanawe, Joanes George (5) ni walemavu wa miguu na hutembea kwa kutambaa chini.

Bw. Mbowe alimkabidhi Bi. Katinga sh. 6,393,000 ambazo zilichangwa na viongozi na wanachama wa CHADEMA wa mkoani Kagera katika hafla fupi ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na uongozi wa CHADEMA mkoani humo juzi usiku.

Katika kiasi hicho, Bw. Mbowe binafsi alichanga sh. 2,000,000 taslimu ambapo mbunge wa viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMA kutoka mkoa wa Morogoro, Bi. Regia Mtema alijitolea kumchangia mlemavu huyo shilingi 100,000 kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia hiyo juzi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa alijitolea kumpeleka mtoto Joanes katika hospitali maalumu ya watu wenye ulemavu wa viungo ya CCRBT iliyoko Dar es Salaam ambako atafanyiwa uchunguzi wa kitalaamu ili kuangalia uwezekano wa kumwezesha kutembea kawaida.

Nenda hapa:GAZETI HURU LA KILA SIKU:: CHADEMA wamchangia mlemavu mil. 6/-

safi sana
 
Najua viongozi hawa walivyo na uchungu na wananchi wao,lakini isiwe kwa hawa tu wawe na utaratibu wa kuchangia na kuchangisha wanachadema na wapenda mabadiliko na maendeleo kwa makundi mbali mbali yenye shida.
 
Yaani hiyo imekaa vizuri kwa kuwa mmoja wa viongozi mafisadi wa vyama vya walemavu aliyenunuliwa alikuwa ukumbi wa maelezo akidai eti walemavu wanatishiwa na maandamano, mfano hai mama mlemavu na mtoto wake mlemavu wakaingia katika maandamano ya CHADEMA kwa hiari yao.

Mungu amewajaalia kupata milioni 6 na matibabu ya mtoto ambaye alishindwa kupata matibabu kutokana na ufisadi wa viongozi wa ccm
 
Haya ndio mambo tunayotaka sisi,kwa staili hii lazima watu watatoa haja kubwa bila kujijua kutukana na wasiwasi kwamba nchi inachukuliwa na CDM.Wasiwasi hautakaa umwishe Mkwere kwa kweli.Pipoooooooooooooooooooozzzzzzzzzzzzzzzz Poweeeeeeeeeeeeeer....!!!
 
Yaani hiyo imekaa vizuri kwa kuwa mmoja wa viongozi mafisadi wa vyama vya walemavu aliyenunuliwa alikuwa ukumbi wa maelezo akidai eti walemavu wanatishiwa na maandamano, mfano hai mama mlemavu na mtoto wake mlemavu wakaingia katika maandamano ya CHADEMA kwa hiari yao.

Mungu amewajaalia kupata milioni 6 na matibabu ya mtoto ambaye alishindwa kupata matibabu kutokana na ufisadi wa viongozi wa ccm

natamani waende wakaongee na waandishi wa habari tena tusikie watasemaje
 
Regia nakupa hongera...

Kwa kweli nazidi kumuelewa kadri siku zinavo enda mbele,nakumbuka mara ya kwanza nilimuona pale mabibo kwenye mkutano na wanachuo,....toka siku hiyo napenda kujua kitu kimoja toka kwake!
 
Kweli mungu yupo pamoja na cdm.hadi kieleweke kwani kuwasaidia wasiojiweza ni moja ya kuteka baraka vitabu vinasema ni bora kutoa kuliko kupokea.
 
peoples power, CCM hadi JK atoe za serikali. mwenye macho haambiwi sikia na mwenye masikio haambiwi ona, kazi ndio imeanza ya kuwaletea maendeleo wananchi.

hadi waseme tusiwachangie watu na wanafunzi, majuzi tu mrema kato mil 400 kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa wasio na uwezo.

Mtabaki mnabana pua tu.

peoples power??????!!!!!!!!
 
Mkuu ni Lema bana sio Mrema,huyo mzee akitoa hizo hela si atakufa kwa presha
 
Hongera CDM kwa msaada mnono kwa huyo mlemavu ila naomba kuuliza. Hivi Bukoba kuna mlemavu mmoja tu? Na kama ni mmoja sawa ila ninavyokumbuka yule mdada albino aliyekatwa mikono yote yuko hai na yuko hapo hapo Bukoba mbona hajapewa msaada? Au huyo ni ndugu yake shemeji?
 
Huyo tumekuachia wewe umchangie...........
Hongera CDM kwa msaada mnono kwa huyo mlemavu ila naomba kuuliza. Hivi Bukoba kuna mlemavu mmoja tu?? na kama ni mmoja sawa ila ninavyokumbuka yule mdada albino aliyekatwa mikono yote yuko hai na yuko hapo hapo bukoba mbona hajapewa msaada? au huyo ni ndugu yake shemeji????
 
peoples power, CCM hadi JK atoe za serikali. mwenye macho haambiwi sikia na mwenye masikio haambiwi ona, kazi ndio imeanza ya kuwaletea maendeleo wananchi.

hadi waseme tusiwachangie watu na wanafunzi, majuzi tu mrema kato mil 400 kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa wasio na uwezo.

Mtabaki mnabana pua tu.

peoples power??????!!!!!!!!

mkuu kuna mtu kasema mil400,mrema,LEMA? Aweke sawa mkuu. Hata ivo cdm haiwezi kumsaidia kila mhitaji,labda tuwakabidhi usukani,waambie ccm wakae pembeni ili cdm iongoze taifa wajameni!!
 
Back
Top Bottom