CHADEMA wapelekana kortini

Kifarutz;Kila siku huwa sikubali siasa hizi zilizoibukia CHADEMA za kufukuza viongozi waliochaguliwa kwa kura za wananchi!Haiwezekani na ni kuiminya demokrasia kwa KAMATI KUU-CHADEMA yenye wajumbe si zaidi ya 20 KUWAFUKUZA MADIWANI/WABUNGE waliochaguliwa kwa kura nyingi za wananchi tena wengine wasio shabikia chama chochote(independents)!

Siasa hizi za kufukuzana nazipinga;kama mwakilishi kaenda kinyume na CHADEMA na hataki kujirekebisha inabidi tu ATENGWE NA APUUZWE hadi mwaka 2015!
hilo linaweza kufanyika kama hasara za kumpuuza hazirudishi nyuma kasi ya mabadiriko na kama haumizi chama vinginevyo bora kumkosa na kuanza upya kwa sababu anakuwa mzigo wa misumari hamuwezi kubeba
 
Tatizo apo ni umeya tu chagulani alipigwa chini ndani ya vikao vya ndani akapewa manyerere asa amejenga bifu na meya
 
nenda ktk hoja wewe..hao wa chadema walioenda mahakamani arusha mbona juzi walifuta rufaa baada ya kubaini kuwa watashindwa vbaya? Pili,mbona madiwani wa ccm arusha wametumia ml 250 kwenda kigali ktk michezo last year mkuu wa mkoa hakuwazuia..ndo maana tunasema tuna hasara kuwa na Ma RC makada wanaoingiza itikadi ktk kazi.

Kwamba Arusha walitumia Mil. 250 sasa na CDM watumie kama wenzao CCM HAPANA, kiukweli CDM kubalini kuwa hapo kwenye hiyo Manispaa ya Moshi mlitaka kuingizwa mkenge na hiyo naamni ilipangwa makusudi mazima na watendaji wa hiyo manispaa ili wahakikishe CDM hiyo kashifa inaangukia kwenu. Jiulize kwanini hilo katazo hadi Gama (Kada wa CCM na Mkuu wa Mkoa ndiyo ache kutoa katazo hilo mbele ya wanahabari?)
Ni fedha kiasi gani zinazopote kwenye H/wilaya ambazo zinasimamiwa na CCM na akuu wa mikoa wapo lakini hakuna kinachotokea kama hicho. CDM kuweni makini sana hasa kwenye halmashauri mnazoongoza ambazo kiukweli bado zinasimamiwa na watendaji wakuu ambao wengi wao wako pale kwa ajili ya maslahi ya CCM, mf. ni Mkurugenzi gani ambaye hana maslahi na CCM ukizingatia namna wanavyopata hizo nafasi.

Chondechonde CDM kuweni makini sana na mitego kama hiyo vinginevyo umma utaaminishwa kuwa na ninyi hamna tofauti na magamba
 
Jifunze spelling ndugu yangu, pamoja na hayo fuata link iliyotolewa ili ujue kama suala hili ni personal interest au ni suala la wakubwa wa chama kuminya democracy. Hiki ndio chama ambacho kinatuomba watanzania ridhaa ya kutuongoza wakati wanashindwa kujali maamuzi ya watu zaidi ya 3000 waliomchagua Mhe. Henry Matata. Wanajifungia watu 20 wanatoa maamuzi bila maamuzi hayo kujadiliwa na Kamati ya utendaji ya Wilaya ambapo diwani huyo anatokea. Suala hili linafanyika kwa sababu tu ya kumfurahisha Baba Junior.

lipi bora kwako watu 3000 wakose hicho unacho dai haki .wa kata ya diwani matata au watu laki moja wa ilemele ,iwapo matata angeingia kuwa meya kwa mgogo wa mafisadi fulani wasio zidi 20 wa gamba .nakufanya ufisadi ambao utawanyima haki watu laki moja ,eti we gamba ?? Think big boy .or otherwise ur in a green bottle .try hard to cum out of it .and meet the great thinkers ,just out here
 
DIWANI wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata ambaye amevuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema, amewasilisha mahakamani zuio la kutekelezwa kwa uamuzi huo.

Matata aliwasilisha hati ya kuomba Mahakama izuie uamuzi huo wa Chadema jana, kwa madai kuwa umekiuka Katiba ya chama hicho.

Akizungumza jana baada kuwasilisha hati hiyo mahakamani, Matata alidai kuwa kabla ya uamuzi huo wa Kamati Kuu, alipaswa kujadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Wilaya na Mkoa.

"Hakuna mwenye ubavu wa kuzuia Mahakama kufanya uamuzi, wanapaswa kuheshimu uamuzi wa Mahakama … mimi nimechaguliwa na watu zaidi ya 3,000, Kamati Kuu yenye watu 20 haiwezi kunyima haki watu wangu walionichagua kutokana na majungu ya wachache," alidai.

Alidai kushangazwa kuona kuwa Kamati Kuu inatoa uamuzi wa kumvua uanachama kabla ya kujadiliwa katika ngazi ya wilaya na mkoa.

Matata alidai kuendelea kupigania haki yake ya msingi kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na kueleza kuwa uamuzi wa kumfukuza ulikuwa kinyume cha Katiba ya Chadema na ulilenga kumdhoofisha kisiasa, kutokana na viongozi wa ngazi za juu na wabunge wa chama hicho kumhofia kisiasa.

Mbali na kwenda mahakamani, Matata pia alitangaza nia yake ya kuwania umeya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela.

Matata alidai kuwa chokochoko dhidi yake zilianza mapema, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka juzi ambapo alichukua fomu ya kuwania umeya wa Jiji la Mwanza, lakini Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliamua kupindisha Katiba ili kumwengua.

Alidai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Meya anapaswa kuchaguliwa na kamati tendaji za wilaya na mkoa, baada ya kupigiwa kura, lakini Dk Willibrod Slaa na baadhi ya wabunge wa chama hicho, waliingilia kati na kumpendekeza meya aliyetimuliwa, Josephat Manyerere.

Mbali na Matata, Diwani wa Kata ya Igoma, Adam Chagulani (Chadema) amelazimika kusitisha mkutano wake wa hadhara wa kuelezea wananchi wake sakata la kuvuliwa uanachama, baada ya kudai kuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema), amekuwa akitumia watu kumfanyia vurugu.

Alidai baada ya kutangazwa kuvuliwa uanachama, alifanya mkutano na wananchi wake kuwaelezea kilichotokea na uamuzi ambao atachukua.

Chagulani alidai kuwa ingawa polisi walisitisha mkutano, kabla ya hapo Wenje alikuwa amepeleka wapambe wake kutoka mjini kwenda Igoma kwa kukodi magari na kuwanunulia ‘viroba’ ili wafanye fujo.

Hata hivyo, Wenje akizungumza kwa simu na gazeti hili alielezea kushangazwa na tuhuma hizo kwani yeye aliondoka Mwanza tangu Septemba 7, kushiriki kikao cha Sekretarieti na Kamati Kuu na bado hajarudi.

Naye Arnold Swai anaripoti kutoka Moshi, kwamba Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amepinga safari ya madiwani wa Manispaa ya Moshi inayoongozwa na Chadema kwenda Kigali, Rwanda kwa madai kuwa bajeti iliyotengwa ya Sh milioni 123 ni kubwa.

Gama alitoa uamuzi huo jana, wakati akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kilichohudhuriwa na madiwani hao na baadhi ya wakuu wa idara wa Manispaa ya Moshi.

Kwa mujibu wa Gama, safari hiyo haina tija, endapo watatumia kiasi kikubwa cha fedha hizo. Alisema madiwani kwenda kujifunza ni jambo la msingi lakini si kutumia fedha nyingi kiasi hicho, ambazo ni kodi za wananchi wanaohitaji maendeleo.

“Si kwamba nawakatalia lakini nasema safari kama hii ya wakati mmoja na mara moja tu kwa mwaka, siwezi kuikubali kutokana na matumizi makubwa ya fedha, wakati shida za wananchi hapa ni nyingi, kama mnataka, basi waende wachache watumie Sh milioni 20, hapo sina pingamizi,” alisema Gama.

Alisema kabla hajamshauri Waziri husika kutoa kibali cha kuwaruhusu kusafiri nje ya nchi ilibidi ajiridhishe kwanza na ndipo alipobaini kuwapo kwa kasoro ambazo ni kikwazo cha safari hiyo.

Gama alisema moja ya matatizo ni msafara wa watu 57 wanaotarajiwa kwenda Kigali kwa siku saba huku malipo ya posho zao yakionesha watalipwa siku tatu, jambo ambalo si sahihi.

Alieleza, kwamba kutokana na msafara huo zaidi ya Sh milioni 200 zingetumika na kuagiza waende wachache, ili fedha zingine zitumike kwa maendeleo.

Meya wa Manispaa hiyo, Japhary Michael (Chadema) alisema anashangazwa na uamuzi wa Gama kupinga safari hiyo wakati ipo kikanuni na kulaumu kitendo cha kuzungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari.

Michael alisema wamekubaliana vizuri na uamuzi uliotolewa na Gama na hawana pingamizi juu ya hilo, lakini alieleza kuwa ushauri huo wangepewa kwenye vikao vya ndani na si mbele wanahabari.

Chanzo: HabariLeo

Uchu wa madaraka

Hapo kwenye red, This is very low kwa Chagulani kutoa maneno na hoja kama hizo. Anafikiri bado ana hadhi ya udiwani kuweza kuitisha mkutano?Kama nani? Kama Gazeti letu la Serikali I mean Habari Leo linaandika upuuzi kama huu basi limefikia hadhi ya toilet paper, before mtu ungeweza hata kulifungia maandazi.
 
Bado nakitafakari kiswahili....ni lugha yangu ila bado najifunza. Ingawa naongea lugha za wenzetu zaid ya nne ila najivunia kiswahili. Tatizo ni pale kinavyoanza kutafsiriwa,,,yaani matumizi yake hapo ndio utajua lugha hii ni pana mfano ni majibu ya polisi baada ya kuua kwa makusudi wanajitetea kuwa kilichomuua ni kitu kizito, halafu chenye ncha kali....kwani RPG si kitu kizito na tena si kina ncha kali lakini ni bomu? Kwani RISASI si kitu kizito pia na tena si kina ncha kali?

Sasa swali langu ni kwamba hiki kitu kizito kilitokea wapi? polisi hawajakiona? mbona sote tunaona ni risasi iweje wao wasione?

Nimechefukwa na roho.
 
Jifunze spelling ndugu yangu, pamoja na hayo fuata link iliyotolewa ili ujue kama suala hili ni personal interest au ni suala la wakubwa wa chama kuminya democracy. Hiki ndio chama ambacho kinatuomba watanzania ridhaa ya kutuongoza wakati wanashindwa kujali maamuzi ya watu zaidi ya 3000 waliomchagua Mhe. Henry Matata. Wanajifungia watu 20 wanatoa maamuzi bila maamuzi hayo kujadiliwa na Kamati ya utendaji ya Wilaya ambapo diwani huyo anatokea. Suala hili linafanyika kwa sababu tu ya kumfurahisha Baba Junior.

Ni afadhali watu ishirini wamekaa kuliko anavyofanya maamuzi baba mwana asha, huwa ni yeye na familia yake ha ha ha. wewe humjui matata, kama ungekuwa unamjua ungekaa kimya ingependeza zaidi, hata hao watu 3000 unaowasema walimpa kwa kuwa alitokea chama cha chadema hawakuwa na jinsi nyingine, na ndo maana akashinda,
 
lipi bora kwako watu 3000 wakose hicho unacho dai haki .wa kata ya diwani matata au watu laki moja wa ilemele ,iwapo matata angeingia kuwa meya kwa mgogo wa mafisadi fulani wasio zidi 20 wa gamba .nakufanya ufisadi ambao utawanyima haki watu laki moja ,eti we gamba ?? Think big boy .or otherwise ur in a green bottle .try hard to cum out of it .and meet the great thinkers ,just out here

Ni afadhali watu ishirini wamekaa kuliko anavyofanya maamuzi baba mwana asha, huwa ni yeye na familia yake ha ha ha. wewe humjui matata, kama ungekuwa unamjua ungekaa kimya ingependeza zaidi, hata hao watu 3000 unaowasema walimpa kwa kuwa alitokea chama cha chadema hawakuwa na jinsi nyingine, na ndo maana akashinda,

Wakuu tuache dogma, tujaribu kuwa realistic, CDM kinajinasibu kama chama cha Democrasia, na democrasia inatoa madaraka makubwa kwa wananchi kuamua. Pamoja na hilo kulingana na maelezo kwenye habari hiyo kabla ya kamati kuu haijawanyang'anya uanachama Matata haikupata baraka ya kamati ya siasa ya wilaya ya Illemela. Labda niulize katiba yenu inasemaje kuhusu hilo? ......Mkuu Morenja, unaeleza kwamba uamuzi huu umefanyika ili kumzuia Matata asiwe Meya, kwa hiyo hapo tatizo ni Umeya?......Mkuu Kitenuly, Matata mwenyewe ameshalalamika kwamba maamuzi yaliyofanyika ni kutokana na shinikizo la Baba Junior hatuna uhakika kama hakumshirikisha mama junior kwani Kuna Manug'uniko kwamba mama Junior anaki-dictate CDM hadi imepelekea Mwigamba kuhamishwa.
 
habari leo gazeti mama la udaku nchini hizi ndizo habari mlizoona mbona huyu chagulani au matata hamkuwahi kuwasifia kabla ya msuguano ndani ya chama kwa taarifa yenu chadema hailei ugonjwa
 
nilishasema siku nyingi tu cdm ni wasanii
WASANII KIVIPI?kwa nao wamepiga picha na jezi ya barcelona kama kikwete?na wametoa ahadi ya kuileta real madrid kama kikwete?tayari nao wamesema liwalo na liwe kama pinda?Nao wamesema umaskini wa nchi hii haujulikani sababu, kama kikwete?after all umepost mchango wako ulisoma course gani ya chuo cha sanaa na wapi? lini? mwaka gani?je rizmoko aliposema yeye sio tajiri na siku 7 kwa slaa athibitishe sio usanii?jamani tuweke uzalendo na utaifa mbele tusikurupuke ,hii ni nchi yetu na bila mabadiliko ya kweli watu wa mataifa mbalimbali wanatushangaa.Tutaishia kupakia twiga kwenye ndege za jeshi.welediiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hauuzwi kama degree za c.h.u.p.i.korogwe hiyo
 
Kwa nini ang'aninie CDM wakati kuna vyama vingine? Hivi CCK na chenyewe si kipo Tanzania? WHY ONLY CDM?
 
hapo hawajachukua dola!! ugomvi moja kwa moja, je wakichukua??

Nadhani ni vizuri kutoa magugu kabla hawajachukua dola, kwani ccm wamethibitisha kwamba ukishachukua dola hata gamba chafu kama la karamagi linakua gumu kutoka
 
si muondoke tunyinyimmeona chadema ni chama cha kubaatisha ,ONDOKENI NA TAMAA ZETU,CHADEMA CHAMA KINACHOONGOZWA NA MISINGI YA KISHERIA ILIYOJIWEKEA KATIKA KATIBA
 
Back
Top Bottom