CHADEMA wapelekana kortini

Koffie

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
433
92
DIWANI wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata ambaye amevuliwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema, amewasilisha mahakamani zuio la kutekelezwa kwa uamuzi huo.

Matata aliwasilisha hati ya kuomba Mahakama izuie uamuzi huo wa Chadema jana, kwa madai kuwa umekiuka Katiba ya chama hicho.

Akizungumza jana baada kuwasilisha hati hiyo mahakamani, Matata alidai kuwa kabla ya uamuzi huo wa Kamati Kuu, alipaswa kujadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Wilaya na Mkoa.

"Hakuna mwenye ubavu wa kuzuia Mahakama kufanya uamuzi, wanapaswa kuheshimu uamuzi wa Mahakama … mimi nimechaguliwa na watu zaidi ya 3,000, Kamati Kuu yenye watu 20 haiwezi kunyima haki watu wangu walionichagua kutokana na majungu ya wachache," alidai.

Alidai kushangazwa kuona kuwa Kamati Kuu inatoa uamuzi wa kumvua uanachama kabla ya kujadiliwa katika ngazi ya wilaya na mkoa.

Matata alidai kuendelea kupigania haki yake ya msingi kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho na kueleza kuwa uamuzi wa kumfukuza ulikuwa kinyume cha Katiba ya Chadema na ulilenga kumdhoofisha kisiasa, kutokana na viongozi wa ngazi za juu na wabunge wa chama hicho kumhofia kisiasa.

Mbali na kwenda mahakamani, Matata pia alitangaza nia yake ya kuwania umeya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela.

Matata alidai kuwa chokochoko dhidi yake zilianza mapema, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka juzi ambapo alichukua fomu ya kuwania umeya wa Jiji la Mwanza, lakini Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliamua kupindisha Katiba ili kumwengua.

Alidai kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema, Meya anapaswa kuchaguliwa na kamati tendaji za wilaya na mkoa, baada ya kupigiwa kura, lakini Dk Willibrod Slaa na baadhi ya wabunge wa chama hicho, waliingilia kati na kumpendekeza meya aliyetimuliwa, Josephat Manyerere.

Mbali na Matata, Diwani wa Kata ya Igoma, Adam Chagulani (Chadema) amelazimika kusitisha mkutano wake wa hadhara wa kuelezea wananchi wake sakata la kuvuliwa uanachama, baada ya kudai kuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema), amekuwa akitumia watu kumfanyia vurugu.

Alidai baada ya kutangazwa kuvuliwa uanachama, alifanya mkutano na wananchi wake kuwaelezea kilichotokea na uamuzi ambao atachukua.

Chagulani alidai kuwa ingawa polisi walisitisha mkutano, kabla ya hapo Wenje alikuwa amepeleka wapambe wake kutoka mjini kwenda Igoma kwa kukodi magari na kuwanunulia ‘viroba' ili wafanye fujo.

Hata hivyo, Wenje akizungumza kwa simu na gazeti hili alielezea kushangazwa na tuhuma hizo kwani yeye aliondoka Mwanza tangu Septemba 7, kushiriki kikao cha Sekretarieti na Kamati Kuu na bado hajarudi.

Naye Arnold Swai anaripoti kutoka Moshi, kwamba Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amepinga safari ya madiwani wa Manispaa ya Moshi inayoongozwa na Chadema kwenda Kigali, Rwanda kwa madai kuwa bajeti iliyotengwa ya Sh milioni 123 ni kubwa.

Gama alitoa uamuzi huo jana, wakati akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, kilichohudhuriwa na madiwani hao na baadhi ya wakuu wa idara wa Manispaa ya Moshi.

Kwa mujibu wa Gama, safari hiyo haina tija, endapo watatumia kiasi kikubwa cha fedha hizo. Alisema madiwani kwenda kujifunza ni jambo la msingi lakini si kutumia fedha nyingi kiasi hicho, ambazo ni kodi za wananchi wanaohitaji maendeleo.

"Si kwamba nawakatalia lakini nasema safari kama hii ya wakati mmoja na mara moja tu kwa mwaka, siwezi kuikubali kutokana na matumizi makubwa ya fedha, wakati shida za wananchi hapa ni nyingi, kama mnataka, basi waende wachache watumie Sh milioni 20, hapo sina pingamizi," alisema Gama.

Alisema kabla hajamshauri Waziri husika kutoa kibali cha kuwaruhusu kusafiri nje ya nchi ilibidi ajiridhishe kwanza na ndipo alipobaini kuwapo kwa kasoro ambazo ni kikwazo cha safari hiyo.

Gama alisema moja ya matatizo ni msafara wa watu 57 wanaotarajiwa kwenda Kigali kwa siku saba huku malipo ya posho zao yakionesha watalipwa siku tatu, jambo ambalo si sahihi.

Alieleza, kwamba kutokana na msafara huo zaidi ya Sh milioni 200 zingetumika na kuagiza waende wachache, ili fedha zingine zitumike kwa maendeleo.

Meya wa Manispaa hiyo, Japhary Michael (Chadema) alisema anashangazwa na uamuzi wa Gama kupinga safari hiyo wakati ipo kikanuni na kulaumu kitendo cha kuzungumzia suala hilo kwa vyombo vya habari.

Michael alisema wamekubaliana vizuri na uamuzi uliotolewa na Gama na hawana pingamizi juu ya hilo, lakini alieleza kuwa ushauri huo wangepewa kwenye vikao vya ndani na si mbele wanahabari.

Chanzo: HabariLeo

Uchu wa madaraka
 
lowahasa na nape mbona hawali pamoja?Sendeka na millya walikuwa cdm..masuala ya personal comflict usirelate na chama ama tasisi..ur not GT at all

Hey GT,, hapo kwenye Red huwa wanasema CONFLICT,, ok?? Stay tight, hahahaha I mean hii ni Wasup sana you know!
 
hapo hawajachukua dola!! ugomvi moja kwa moja, je wakichukua??

Huyo diwani ametekeleza wajibu wake kidemokrasia. Hajakubaliana na kamati kuu, ameenda mahakamini ambako haki itatendeka. walioridhika, hawakwenda. That is good
 
Hiyo ndiyo Democracy ya kweli, kama hukubaliani na jambo unapeleka shauri lako kwenye chombo cha kutafsiri sheria ili haki itendeke na sio 'kumpiga mtu bomu' au 'kitu kizito'.
 
hapo hawajachukua dola!! ugomvi moja kwa moja, je wakichukua??

Mahakama kwa uelewa wa kawada n chombo cha kutoa haki,kiongozi anayefuata haki yake huko ni kuigwa wale wa upande wa pili si wanatumia umwamba na kuoneshana bastola...............elewa maana halsi ya mahakama,mahakama si genge la wizi kama viongoz wa serikali hii wanavyochafua mahakama kwa kuficha maovu yao huko........
 
Nilijua habari lazima imetoka kwenye kipeperushi cha serikali...Habarileo. Hawa nao ni janga kama ilivyo kwa TIBISIII
 
lowahasa na nape mbona hawali pamoja?Sendeka na millya walikuwa cdm..masuala ya personal comflict usirelate na chama ama tasisi..ur not GT at all

Jifunze spelling ndugu yangu, pamoja na hayo fuata link iliyotolewa ili ujue kama suala hili ni personal interest au ni suala la wakubwa wa chama kuminya democracy. Hiki ndio chama ambacho kinatuomba watanzania ridhaa ya kutuongoza wakati wanashindwa kujali maamuzi ya watu zaidi ya 3000 waliomchagua Mhe. Henry Matata. Wanajifungia watu 20 wanatoa maamuzi bila maamuzi hayo kujadiliwa na Kamati ya utendaji ya Wilaya ambapo diwani huyo anatokea. Suala hili linafanyika kwa sababu tu ya kumfurahisha Baba Junior.
 
Hey GT,, hapo kwenye Red huwa wanasema CONFLICT,, ok?? Stay tight, hahahaha I mean hii ni Wasup sana you know!

nenda ktk hoja wewe..hao wa chadema walioenda mahakamani arusha mbona juzi walifuta rufaa baada ya kubaini kuwa watashindwa vbaya? Pili,mbona madiwani wa ccm arusha wametumia ml 250 kwenda kigali ktk michezo last year mkuu wa mkoa hakuwazuia..ndo maana tunasema tuna hasara kuwa na Ma RC makada wanaoingiza itikadi ktk kazi.
 
Moshi ni moja ya manispaa zilipiga hatua kubwa ya maendeleo hapa nchini,hakuna sababu ya kutumia mamilioni ya kodi ya walala hoi kwenda kutembea kigali,hii ni anasa ya wazi.
 
Back
Top Bottom