CHADEMA wanapata ruzuku kubwa kila mwezi nini kinachosababisha wasifungue matawi kila kijiji?

Kwa taarifa nilizonazo CHADEMA ni chama pekee kilichofungua matawi mapya mengi kuliko vyama vingine vyote baada ya uchaguzi 2010, Mfano mzuri ni jimbo la Njombe Magharibi chini ya uongozi wa aliekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo Ndugu Thomas Nyimbo CHADEMA imefungua matawi ktk vijiji vyote na sasa mikakati ya kujenga ofisi inaendelea. Nakushauri mtoa mada kufanya utafiti kabla ya kupost humu javini.
 
Mkuu nashukuru sana kwa mawazo na majibu yako,naheshimu sana sana mawazo hayo,lakini naomba nipishane nawewe katika mambo haya.Mkuu mtazamo ulioutumia kujibu ndio mtazamo wa viongozi wetu wa juu karibu wote,amabo kimsingi wanakosea sana,wewe umejibu kama mwanasiasa(Politician),na uko sahihi kabisa kwa mtazamo wa kisiasa,lakini kwa mtazamo wa kitaaluma ya kisiasa umekosea sana sana tena sana,na nikili viongozi wetu wengi sana wanalizalau hili na hawaoni umuhimu wake.

nikianza kunukuu huja hii,"kwanza nikukumbushe kwamba mikakati(strategies) ya chama inabadilika kila leo, labda tu wewe ndiye hufahamu hilo kwakuwa mikakati ya chama haitangazwi hadharani, inajadiliwa kwenye vikao na kuwekewa mpango wa utekelezaj".

Katika maelezo yako mwenyewe kama mtaalamu wa siasa umekili wazi kwamba kuna tatizo nalilolisema mwanzao,kusema kwamba startegies za chama zinabadilika kila siku labda mimi sijui,inaonesha wazi kunatatizo nalolisema kwamba bado tunajiweka kama chama pinzania na badala ya chama Dola tarajiwa.kama strategies hazijulikani kwa wanachama na hata ambao sio wanachama zaitakifaa nini sasa chama?? tutachukuwaje madaraka na kupata wanachama wengi kama wananachi hawajui nini mikakatai yetu?,

Na pili mkuu wewe na viongozi wetu wengi wanachanganya Strategies (Mikakati) na Tactics(miundo tekelezi),hivi ni vitu viwili tofauti kabisa,startegies zenu zote lazima zijulikane kwa watu wote,ila tactics ambazo mtatumia kufikia mikakati yenu hiyo mliopanga ndio haitakiwi kujulikana kwa watu wote-sasa wengi wa viongozi wetu wanachanganya hili ndio hapo naposema utaalamu unaitajika.


Naomba kukunukuu tena mkuu "Makao makuu kazi yao ni kuweka mikakati ya jumla na ya kitaifa, then ngazi husika za uongozi za chini zina tafsiri mikakati hiyo kulingana na mazingira yao.

Mazingira ya dsm ni tofauti na Mbeya na ni tofauti na Mara ama Arusha. Na wewe kama ni mwanachama una haki ya kutoa mawazo yako katika vikao husika, iwe kwenye tawi, kata, jimbo, mkoa na hata taifa. Then yatafanyiwa kazi kadri uuongozi utakavyo ona inafaa.

Mkuu nukuu yako hapo juu ni tatizo lingine la msingi sana viongozi wetu wanalolifanya sasa,kusema viongozi wa juu wanakazi ya kuweka mikakati ya jumla ya kitaifa,na viongozi wa chini watekeleze kutokana na mazingira yao na hali halisi ya mahalia,ni kosa kubwa sasa,kwa chama kama chetu amabacho kinaitaji kuchukua dola ni lazima viongozi wa juu wawe seehemu kabisa ya utekelezaji wa mikakati ya chini kabisa na pia katika kufikisha ujumbe na malengo ya chama moja kwa moja kwa wananchi,hili linasaidia sana kwanza kuhakikisha chama kinakua na agenda kuu chache na zinazowafikia wananchi wote moja kwa mmoja na bila kupotosha maana halisi,kwani kumbuka watu wengi sana wanaogopa kuchagua chama pinzania kwa kuogopa mabadilioko hii ndio hofu kubwa kabisa ya kwanza.

Kwani kwa uzoefu na utaalamu chama tawala hutumia njia zote kupotosha maana na nia halisi ya agenda za chama pinzania,mfano vita zidi Ufisadi,imepotoshwa sana sana,na hata sasa watu wengi wanazani mtu yoyote mwenye mali ni fisadi,sasa ukienda kijijini kwa bibi yangu mtu mwenye ngomb'e wa 5 na nyumba mbili anaonekana tajiri na hata kuitwa fisadi kwa madhingira ya pale kijijinini.

Halii kama hii inatokea kwa kukosa muunganiko naousema wa kwenda kwa watu sasa na nguvu yote kupelekwa huko ili kutoa tafasiri halisi ya agenda na sera za chama kwa watu.

Kitaalamu chama kinachojiaanda kuchukua dola lazima kiwe na agenda chache za kitaifa bila kujali umahalia,kwanu ukiacha kila mahali wachague nini cha kufanya kwa mujibu wa mazingira yao kamwe hautafikia lengo la kuchukua dola.

Ushauri wangu mkuu ni mmoja tu hakuna chama chochote duniani kilichofanikiwa kuchukua uongozi kwa kutegemea nguvu ya siasa tu au uwezo wa viongozi fulani kutawala majukwaa vizuri,chama kama chadema katika hatua hii ni lazima kitoe nguvu kubwa kwa wataalamu wa siasa(sio wasomi wowowte tu).

Nitakupa mfano katika siasa za chama kinachoelekea kuchukua dola kuna miiko 180,mmoja kati ya miiko mikubwa kabia ni huu "Never personalize Party Agenda",ikiwa na maana usifanye agenda ya chama ikawa agenda ya mtu,hili ndio linatokea sana sasa Chadema kwani agenda nyingi zikitolewa mtu amaitoa kama yake na sio ya chama na inaenda mabli hata baadhi ya viongozi kuipinga agenda ile au msimamo ule.ukiacha agenda za chama zitawaliwe na watu au awatu wafanye agenda za cha ziwe zao binafsi utachochea mgawanyiko ndani ya chama na kuanzisha vita ndani ya chama vya kujitakia umaarufu binfsi au wengine kukaataa hoja za wengine kwa kuzani watawazidi umaarufu hata kama hoja hizo zina tija kwa chama.
Nawasilisha.


Mkuu Kulwa12,

Nakushukuru kwa changamoto uliyoitoa, ni mawazo mazuri na yatafanyiwa kazi. Zaidi ya hapa JF unaweza kuyapeleka kunako ofisi za chama kadri utakavyoona inafaa, iwe jimbo/wilaya, mkoa ama makao makuu.

Hata hivyo ningependa ku comment kidogo kwenye hoja zako.

Kwanza naomba nikukumbushe tena kwamba Dr. Slaa na Mbowe hawawezi kupita kila siku kila kona ya nchi kufungua matawi. Kwakuwa kuna uongozi katika ngazi husika i.e msingi, tawi, kata, jimbo/wilaya na mkoa hao ndio wanaandaa shughuli na kuwaalika viongozi wa kitaifa. Sasa kama katika eneo lako viongozi wa msingi hadi mkoa hawatimizi wajibu wao huwezi kuwatupia lawama viongozi wa kitaifa. Chama chetu ni taasisi inayotakiwa kuonekana iki operate kama taasisi, si kila ujambo wafanye viongozi wa kitaifa, na huu ndio ugonjwa unaowakumba watu wengi kwamba kila siku wanataka kumuona Dr. slaa kwenye maeneo yao akifungua matawi na kufanya mikutano, usisahau kwamba kuna mambo mengi ya uendeshaji wa chama yanamtegemea atekeleze.

Pili, nataka niseme kwamba kama chama tunachopeleka kwa wananchi ni sera na mipango ya kumkomboa mwananchi, wananchi wanasoma sera zetu na mipango yetu wakiridhika nayo watatukabidhi uongozi wa nchi. Pamoja na kwamba unasema wewe ni "political scientist" by profession, nataka nikueleze kwamba huwezi kuweka hadharani mikakati yako ya kufikia ushindi, wananchi hawahitaji kujua mikakati ya kutupatia ushindi, kikubwa kwao kama nilivyosema hapo awali wananchi wanahitaji sera bora zitakazowakwamua kwenye lindi la umaskini na kuboresha huduma za kijamii.

Tatu, kama wewe ni mwanachama na hauna taarifa ya mikakati ya chama, jitahidi kumtafuta kiongozi wako wa jimbo/wilaya utapata taarifa zote. Lakini ukikaa ukasubiri chama kitangaze mikakati yake kwenye vyombo vya habari, hutoiona na utaishia kulalamika, na bahati mbaya kuna wanachama ambao hata vikao vikiitishwa hawahudhurii(simaanishi kuwa ni wewe) lakini ni wepesi sana kunung'unika. Na kama unaona viongozi wako wa ngazi za chini wanakurudisha nyuma ama wanakwamisha juhudi za kukieneza chama basi unatakiwa kuingia mstari wa mbele. Mimi binafsi nilipoona viongozi wangu wanalegalega niliamua kuingia mstari wa mbele na sasahivi kata yangu yenye mitaa minne ya kiserikali tumefanikiwa kufungua matawi manne(kila mtaa kuna tawi la chama na uongozi uliochaguliwa) ndani ya kipindi kifupi tu cha miezi sita, sikusubiri kulalamika kamanda.

Mwisho, katika personalized party agenda, nakushauri utafute ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 ili ujiridhishe kama yale aliyokuwa anayasema dr.slaa akiwa mgombea uraisi pamoja na wagombea ubunge na udiwani ni ya kwao ama ni ilani ya uchaguzi ya chadema. Ingawa pia usisahau kwamba mgombea mwenyewe hazuiliwi kutoa ahadi nyengine tofauti na zilizoko ndani ya manifesto ilimradi haiendi kinyume na sera za chama. Lakini pia usisahau kwamba katika siasa za ushindani kila mwanasiasa anatafuta namna ya kujitanabaisha kwa wananchi, na hapo ndipo ubunifu unapotakiwa, sasa ikitokea kuna mtu ni mbunifu kuliko wengine na mawazo yake yanakubalika hakuna sababu ya kumuonea wivu ni suala la kumuunga mkono kwakuwa anapopata umaarufu na chama nacho kinanufaika kama agenda yake imekubalika kwa wananchi na chama kimeitumia.
 
Nadhani ni wakati sasa wa wanachama wa Chadema kukaa chini na kuamua ni namna gani ya kuendesha chama na lazima muendane na mabadiliko ya kisasa na si kubaki na mawazo ya kale...
 
hivi waswahili mpaka lini mtaeendelea kulalamika paipo kufanya hata research, tatizo lako unablame tuuuu wala pasipo kuwa na uhakika na unachokisema pia my simple analysis nimegundua kwamba we mleta hii thread umekurupuka bkoz hujui nini kinaendelea yani kama vile upo dunia nyingine, chadema kila siku inafungua matawi na sisi wenyewe huku tunashuhudia au unataka kila wakifungua tawi wawe wanakuja mpaka chooni kwenu kukuletea habari.
 
Hivi mbona unatumia makamasi kufikiri, mil200 kweli zinaweza zikafungua matawi nchi zima yani bara na visiwani ktk kipindi cha 2 tu, hiyo hiyo ruzuku itumike kuwalipa watu ndani ya chama pia hiyo hiyo ruzuku itumike kuendesha shuguli za chama at the same time, najua kwamba una f ya mathematics but tumia basi hata knowledge ya history kuanalyse hata vitu vidogo kama hivi, pia ni vyema mda unaotumia kublame cdm ungetumia kuhoji fedha za richmond, dowans, epa, meremeta, uda, ungeweza kuwa chanzo cha ukombozi wa taifa letu.
 
Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA

Nadhani hapo kwenye red ndipo kwenye hoja ya msingi ambayo hata hivyo imejificha. Pengine mleta mada amesema kwa ufupi sana kutokana na uvivu wa kuandika lakini maneno yake ukiyatizama kwa undani yana maana kubwa. Bila shaka dhumuni la fedha za ruzuku ni pamoja na kukijenga chama ikiwa ni pamoja na kufungua matawi. Jamaa anahofu huenda pesa hizo zinatumika kinyume na malengo ikiwa ni pamoja na kugharamikia shughuli za maandamano. Hapo chini kwenye blue nadhani amekwenda mbali saana..
 
Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA


Mawazo haya ni mazuri sana kwa chama cha siasa kuwa na matawi kwenye ngazi za vijiji ili kujiimarisha, ni somo zuri sana si kwa CHADEMA tu ila vyama vyote ambavyo vina nia ya kushika dola.
Sasa haya maombi kwa msajili wa vyama kufuta Chadema sio busara nzuri maana atakuwa amevunja sheria iliyofanya vyama hivi viwepo.
Lakini kama Chadema haijafungua matawi vijijini, basi ungesema umeenda mikoa mingapi ambayo hukuweza kuona ofisi ya chama hichi kwenye vijiji na vilevile ni vyama vingapi vina ofisi huko vijijini kwa mujibu wa tafiti zako.
Unapoleta post isiwe ya kuamka na kuanza kuandika maadamu una fursa hiyo.
Nakupa taarifa fupi, kijijini kwetu Kishanje hakuna ofisi kuanzia TANU hadi CCM ila wanachama wapo na uongozi upo, pia kwenye kata yetu iitwayo Kishanje yenye vijiji vitatu Bumai, Bushashana Kishanje ofisi za vijiji za CCM hakuna pia ofisi ya kata ya CCM haipo ila uongozi kwenye ngazi hiyo upo na unafanya kazi. Nafikiri kuna kitu umejifunza hapo. Waambie CCM wenzako kuwa ofisi zote za chama hicho ni mali ya Watanzania wote kwa maana awali chama kilikuwa kimoja ingebidi mali zote zirejeshwe serikalini ziwe ofisi za umma lakini ukiritimba haukuruhusu hivyo.
Kama umri wako ni kuanzia miaka arobaini utakuwa na ufahamu kuhusu masuala ya siasa za nchi hii lakini kama upo chini ya miaka ishirini samahani utawauliza waliokutangulia.






 
Ruzuku ya CHADEMA haitoshi hata kufungua matawi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara. Kazi ya kufungua matawi, na hata kugharimia uendeshaji, inabidi ifanywe na wanachama wa sehemu mahalia. Kufikiria kujenga chama nchi nzima kwa "pesa" ni mawazo finyu yanayotumiwa na wanasiasa uchwara wanaopenda mambo yatokee kabla hawajafa (EL?). Siasa ni kazi ngumu ambayo mafanikio yake hayategemei pesa tu. Msingi mkubwa wa kukua kwa chama cha siasa ni kuwa na watu kwanza; na si watu tu, bali watu wenye uelewa wa kati na wa juu.

Wakati ukifika watu wenyewe, bila kushauriwa na mtu yeyote, watafungua matawi ya CHADEMA au chama kingine chochote kinachowavutia kwa nguvu zao, hata ikiwezekana kwa pesa yao kidogo watakayo kuwa nayo. Hiyo itakuwa ni nguvu ya umma.

Mfano mzuri wa mahali ambapo nguvu ya umma imejionesha ni kisiwa cha Pemba. Sidhani kama Mpemba anahitaji mtu wa kumfungulia tawi la CUF, au kuhongwa pesa ili akichague CUF. Hiyo ndiyo nguvu ya umma na ndiyo inayokijenga chama na wala si pesa wala dhahabu.
 
Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA







wewe unapenda kutendwa na Tendwa au?
 
Ruzuku ya CHADEMA haitoshi hata kufungua matawi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara. Kazi ya kufungua matawi, na hata kugharimia uendeshaji, inabidi ifanywe na wanachama wa sehemu mahalia. Kufikiria kujenga chama nchi nzima kwa "pesa" ni mawazo finyu yanayotumiwa na wanasiasa uchwara wanaopenda mambo yatokee kabla hawajafa (EL?). Siasa ni kazi ngumu ambayo mafanikio yake hayategemei pesa tu. Msingi mkubwa wa kukua kwa chama cha siasa ni kuwa na watu kwanza; na si watu tu, bali watu wenye uelewa wa kati na wa juu.

Wakati ukifika watu wenyewe, bila kushauriwa na mtu yeyote, watafungua matawi ya CHADEMA au chama kingine chochote kinachowavutia kwa nguvu zao, hata ikiwezekana kwa pesa yao kidogo watakayo kuwa nayo. Hiyo itakuwa ni nguvu ya umma.

Mfano mzuri wa mahali ambapo nguvu ya umma imejionesha ni kisiwa cha Pemba. Sidhani kama Mpemba anahitaji mtu wa kumfungulia tawi la CUF, au kuhongwa pesa ili akichague CUF. Hiyo ndiyo nguvu ya umma na ndiyo inayokijenga chama na wala si pesa wala dhahabu.[/QUOTE
Tawi si lazima liwe jengo la gharama kwani ata nyumba ya makuti inaweza kuwa ofisi ya tawi hivyo mnaposema ya kuwa chama hakina pesa bado ni hoja duni sana. pia watu wanaweza kujitolea kwenye sehemu ya vyumba vya nyumba zao kuwa matawi si lazima kuwa na gharama kubwa
 
Back
Top Bottom