CHADEMA wanapata ruzuku kubwa kila mwezi nini kinachosababisha wasifungue matawi kila kijiji?

Godwine ana hoja aidha haelewi ni kwa nini CDM hawafungui matawi vijijini wakati wanapata ruzuku ambayo ana haki ya kuihoji au inawezeka CDM hawatoi taarifa wapi wamefungua na Godwine akazipata.

Huyu hajauliza kwa lengo la kutaka kujua yeye ameanza kulaumu na tena kumuomba tendwa aifute CDM je hapo ni sahihi?
Angekuwa na nia ya kuelewa angejua kuwa matawi ni juhudi za wakazi wa eneo husika tu chama kinakuja ku-support!

Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA

Halafu hapo unakuta wanasema CCM mafisadi wakati wao ndo mafisadinambari one.
 
Na nyie magwanda kama mtu akiwapa ushauri jaribuni kuupokea basi. Msiwe vichwa ngumu kama moderators wa JF ambao hata uwashauri vipi wenyewe wanapuuzia tu!
 
Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA

Wewe pia unaweza kufungua tawi katika eneo lako na kuomba kutambuliwa kama tawi la CDM kupitia uongozi wa CDM wilayani kwako.

Neno kubwa ni pana. Unaposema chadema wanapata ruzuku kubwa, unalinganisha na ruzuku ya CCM au ya TLP?.
Acha kulalamika chukua hatua...
 
Mtoa hoja umekwenda mbali, hawawezi kufungua matawi kila kijiji wakati hata ofisi kila wilaya wameshindwa. Rufiji, Mafia na Mkuranga mifano michache hawana ofisi za wilaya. Ruzuku yao inaishia mshahara wa Dr. Slaa na posho za maandamano
 
feedback,

kwa taarifa yako na wengine ni kwamba mwaka kesho tunaanza mchakato wa uchaguzi ndani ya chama. Tutaanza na ngazi ya chini kabisa ya msingi, tawi, kata, jimbo/wilaya, mkoa na hatimaye taifa.

Maelekezo ya ofisi ya katibu mkuu ni kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa tawi bila chaguzi za misingi kukamilika, hakutakuwa na uchaguzi wa kata bila uchaguzi wa matawi kukamilika, hakutakuwa na uchaguzi wa jimbo/wilaya bila chaguzi za kata kukamilika, na utaratubu utakwenda hivyo hivyo hadi ngazi ya taifa, kwa mujibu wa katiba ya chama.

Na kwakuwa ni lazima chaguzi ngazi zote zifanyike, na kwa kuzingatia mwitikio wa wananchi katika kujiunga na chadema, hatuna shaka kwamba kabla ya kuwa na uchaguzi wa ngazi za majimbo/wilaya, kila kijiji na mtaa kutakuwa na ofisi ya chadema. Jambo la msingi ni kuunganisha nguvu na wanaharakati wote kujiunga na chadema ili tupate viongozi wazalendo na watakao kuwa commited ili hatimaye chama kiwe na uongozi imara toka ngazi za chini kabisa kama ilivyo kwenye level ya kitaifa.
wadau tukubali au tukatae chadema tuna tatizo kubwa la kimsingi la political startegist,kunavitu vya msingi sana katika ujenzi wa chama dola(kinachojiaandaa kuchukua madaraka) viongozi wangu hawavipi kipaumbele,bado wanaendelea na startegis ya chama pinzania.kwa sisi politica scientists na strategist hili ni kosa la kimsingi sana,toweni wigo wa wadau wengi zaidi na wenye taaluma hii washauri cha kufanya,kuwa na maprofessa katika kamati kuu haimanishi wao ni wataalamu wa kila fani..hili nitalisema siku zote,tubadilishe strategies za chama sasa,tujikite kwa watu,hata bibi yangu wa kijijini akiambiwa chadema aseme moja kwa moja nini tofauti ya chadema na ccm,na chadema ikipata madaraka itamfanyia nini tofauti.
 
kama Chadema ikiwa na wanachama wengi kama wewe basi kitakuja kuwa chama imara zaidi lakini kama kitaendelea na mfumo wa sasa basi siku akina dr slaa watapoondoka katika mfumo basi hakutakuwa na chama kitachobakia bali litabaki genge la watukanaji kama walivyojaa humu JF
 
Mkuu,kwanza nikukumbushe kwamba mikakati(strategies) ya chama inabadilika kila leo, labda tu wewe ndiye hufahamu hilo kwakuwa mikakati ya chama haitangazwi hadharani, inajadiliwa kwenye vikao na kuwekewa mpango wa utekelezaji.

Pili naomba utambue kwamba Chama ni wanachama. Wanachama wenyewe huko waliko wanatakiwa waji organise kulingana na mazingira yao. Wananchi wanatakiwa wajiunge na chama ili wanachama hao waweze kutekeleza majukumu ya ustawi wa chama katika eneo na ngazi husika.

Makao makuu kazi yao ni kuweka mikakati ya jumla na ya kitaifa, then ngazi husika za uongozi za chini zina tafsiri mikakati hiyo kulingana na mazingira yao.

Mazingira ya dsm ni tofauti na Mbeya na ni tofauti na Mara ama Arusha. Na wewe kama ni mwanachama una haki ya kutoa mawazo yako katika vikao husika, iwe kwenye tawi, kata, jimbo, mkoa na hata taifa. Then yatafanyiwa kazi kadri uuongozi utakavyo ona inafaa.

Tatizo moja na la msingi tulilonalo watu wengi, hasa hapa JF ni wazuri sana kwa kuandika, lakini inapofika kwenye utekelezaji wanakuwa wagumu. Sisi wengine tumejitolea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba chama kinawafikia wananchi kadri iwezekanavyo.
Mathalani mim i binafsi pamoja na kuwa kiongozi katika ngazi ya jimbo lakini nimeamua kuelekeza nguvu zangu kwa kushirikiana na wanachama wenzangu kuanzisha matawi mapya na kuimarisha yale yaliyopo. Tumefanikiwa kufungua matawi katika mitaa yote iliyopo ndani ya kata yetu ya ukonga na juhudi zinaendelea kuona kwamba jimbo zima linakuwa na tawi kila mtaa.

Kwahiyo inatakiwa kila mmoja kwa nafasi yake awajibike, hatuwezi kukaa na kusubiri dr.slaa ama mbowe wafanye kazi ya kuanzisha na kufungua matawi kila kona, hiyo ni kazi yetu wananchi wenyewe.
 
Godwine,

Chadema sasahivi ilipofikia ni zaidi ya Dr. Slaa, ama Mbowe, hilo nataka nikuhakikishie.

Chadema sashivi ni taasisi imara inayoweza kujiendesha bila hao viongozi unaowataja, kuna hazina kubwa sana ya vijana, watu wa makamo na wazee wanaoweza kukiendesha chama bila wasiwasi wowote. Wananchi wanapoamua kutuunga mkono kwa dhati na kwa wingi ni kwa sababu wamekiamini chama, si kwa sababu ya dr.slaa ama mbowe.

Kwahiyo ni vizuri na wewe ukajiondoa katika hilo genge la walalamikaji na watukanaji hapa JF kwa kupost "constructive criticism"!!
 
Daima sina upande wa kushambulia au kusifia daima bali niko katika sehemu ya kutaka taifa lipambane kwa hoja na si ushabiki na matusi kwani kwangu mimi mtawala yeyote awe CCM au Chadema hawezi kuzuia kufikia malengo yangu. lakini kama vyama vya upinzani au CCM wasipojifunza mabishano ya hoja na si matusi hakuna maana ya kuwa na vyama bali wagombea binafsi ndio wawe kimbilio la wananchi.
 
Panapowasha utajikuna tu, naona Magamba wananyimwa usingizi na "chama cha msimu", hatimae "kelele za mlango" zimeanza kumuamsha "mwenye nyumba".
 
Mkuu,kwanza nikukumbushe kwamba mikakati(strategies) ya chama inabadilika kila leo, labda tu wewe ndiye hufahamu hilo kwakuwa mikakati ya chama haitangazwi hadharani, inajadiliwa kwenye vikao na kuwekewa mpango wa utekelezaji.

Pili naomba utambue kwamba Chama ni wanachama. Wanachama wenyewe huko waliko wanatakiwa waji organise kulingana na mazingira yao. Wananchi wanatakiwa wajiunge na chama ili wanachama hao waweze kutekeleza majukumu ya ustawi wa chama katika eneo na ngazi husika.

Makao makuu kazi yao ni kuweka mikakati ya jumla na ya kitaifa, then ngazi husika za uongozi za chini zina tafsiri mikakati hiyo kulingana na mazingira yao.

Mazingira ya dsm ni tofauti na Mbeya na ni tofauti na Mara ama Arusha. Na wewe kama ni mwanachama una haki ya kutoa mawazo yako katika vikao husika, iwe kwenye tawi, kata, jimbo, mkoa na hata taifa. Then yatafanyiwa kazi kadri uuongozi utakavyo ona inafaa.

Tatizo moja na la msingi tulilonalo watu wengi, hasa hapa JF ni wazuri sana kwa kuandika, lakini inapofika kwenye utekelezaji wanakuwa wagumu. Sisi wengine tumejitolea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba chama kinawafikia wananchi kadri iwezekanavyo.
Mathalani mim i binafsi pamoja na kuwa kiongozi katika ngazi ya jimbo lakini nimeamua kuelekeza nguvu zangu kwa kushirikiana na wanachama wenzangu kuanzisha matawi mapya na kuimarisha yale yaliyopo. Tumefanikiwa kufungua matawi katika mitaa yote iliyopo ndani ya kata yetu ya ukonga na juhudi zinaendelea kuona kwamba jimbo zima linakuwa na tawi kila mtaa.

Kwahiyo inatakiwa kila mmoja kwa nafasi yake awajibike, hatuwezi kukaa na kusubiri dr.slaa ama mbowe wafanye kazi ya kuanzisha na kufungua matawi kila kona, hiyo ni kazi yetu wananchi wenyewe.

Mkuu nashukuru sana kwa mawazo na majibu yako,naheshimu sana sana mawazo hayo,lakini naomba nipishane nawewe katika mambo haya.Mkuu mtazamo ulioutumia kujibu ndio mtazamo wa viongozi wetu wa juu karibu wote,amabo kimsingi wanakosea sana,wewe umejibu kama mwanasiasa(Politician),na uko sahihi kabisa kwa mtazamo wa kisiasa,lakini kwa mtazamo wa kitaaluma ya kisiasa umekosea sana sana tena sana,na nikili viongozi wetu wengi sana wanalizalau hili na hawaoni umuhimu wake.

nikianza kunukuu huja hii,"kwanza nikukumbushe kwamba mikakati(strategies) ya chama inabadilika kila leo, labda tu wewe ndiye hufahamu hilo kwakuwa mikakati ya chama haitangazwi hadharani, inajadiliwa kwenye vikao na kuwekewa mpango wa utekelezaj".

Katika maelezo yako mwenyewe kama mtaalamu wa siasa umekili wazi kwamba kuna tatizo nalilolisema mwanzao,kusema kwamba startegies za chama zinabadilika kila siku labda mimi sijui,inaonesha wazi kunatatizo nalolisema kwamba bado tunajiweka kama chama pinzania na badala ya chama Dola tarajiwa.kama strategies hazijulikani kwa wanachama na hata ambao sio wanachama zaitakifaa nini sasa chama?? tutachukuwaje madaraka na kupata wanachama wengi kama wananachi hawajui nini mikakatai yetu?,

Na pili mkuu wewe na viongozi wetu wengi wanachanganya Strategies (Mikakati) na Tactics(miundo tekelezi),hivi ni vitu viwili tofauti kabisa,startegies zenu zote lazima zijulikane kwa watu wote,ila tactics ambazo mtatumia kufikia mikakati yenu hiyo mliopanga ndio haitakiwi kujulikana kwa watu wote-sasa wengi wa viongozi wetu wanachanganya hili ndio hapo naposema utaalamu unaitajika.

Naomba kukunukuu tena mkuu "Makao makuu kazi yao ni kuweka mikakati ya jumla na ya kitaifa, then ngazi husika za uongozi za chini zina tafsiri mikakati hiyo kulingana na mazingira yao.

Mazingira ya dsm ni tofauti na Mbeya na ni tofauti na Mara ama Arusha. Na wewe kama ni mwanachama una haki ya kutoa mawazo yako katika vikao husika, iwe kwenye tawi, kata, jimbo, mkoa na hata taifa. Then yatafanyiwa kazi kadri uuongozi utakavyo ona inafaa.

Mkuu nukuu yako hapo juu ni tatizo lingine la msingi sana viongozi wetu wanalolifanya sasa,kusema viongozi wa juu wanakazi ya kuweka mikakati ya jumla ya kitaifa,na viongozi wa chini watekeleze kutokana na mazingira yao na hali halisi ya mahalia,ni kosa kubwa sasa,kwa chama kama chetu amabacho kinaitaji kuchukua dola ni lazima viongozi wa juu wawe seehemu kabisa ya utekelezaji wa mikakati ya chini kabisa na pia katika kufikisha ujumbe na malengo ya chama moja kwa moja kwa wananchi,hili linasaidia sana kwanza kuhakikisha chama kinakua na agenda kuu chache na zinazowafikia wananchi wote moja kwa mmoja na bila kupotosha maana halisi,kwani kumbuka watu wengi sana wanaogopa kuchagua chama pinzania kwa kuogopa mabadilioko hii ndio hofu kubwa kabisa ya kwanza.

Kwani kwa uzoefu na utaalamu chama tawala hutumia njia zote kupotosha maana na nia halisi ya agenda za chama pinzania,mfano vita zidi Ufisadi,imepotoshwa sana sana,na hata sasa watu wengi wanazani mtu yoyote mwenye mali ni fisadi,sasa ukienda kijijini kwa bibi yangu mtu mwenye ngomb'e wa 5 na nyumba mbili anaonekana tajiri na hata kuitwa fisadi kwa madhingira ya pale kijijinini.

Halii kama hii inatokea kwa kukosa muunganiko naousema wa kwenda kwa watu sasa na nguvu yote kupelekwa huko ili kutoa tafasiri halisi ya agenda na sera za chama kwa watu.

Kitaalamu chama kinachojiaanda kuchukua dola lazima kiwe na agenda chache za kitaifa bila kujali umahalia,kwanu ukiacha kila mahali wachague nini cha kufanya kwa mujibu wa mazingira yao kamwe hautafikia lengo la kuchukua dola.

Ushauri wangu mkuu ni mmoja tu hakuna chama chochote duniani kilichofanikiwa kuchukua uongozi kwa kutegemea nguvu ya siasa tu au uwezo wa viongozi fulani kutawala majukwaa vizuri,chama kama chadema katika hatua hii ni lazima kitoe nguvu kubwa kwa wataalamu wa siasa(sio wasomi wowowte tu).

Nitakupa mfano katika siasa za chama kinachoelekea kuchukua dola kuna miiko 180,mmoja kati ya miiko mikubwa kabia ni huu "Never personalize Party Agenda",ikiwa na maana usifanye agenda ya chama ikawa agenda ya mtu,hili ndio linatokea sana sasa Chadema kwani agenda nyingi zikitolewa mtu amaitoa kama yake na sio ya chama na inaenda mabli hata baadhi ya viongozi kuipinga agenda ile au msimamo ule.ukiacha agenda za chama zitawaliwe na watu au awatu wafanye agenda za cha ziwe zao binafsi utachochea mgawanyiko ndani ya chama na kuanzisha vita ndani ya chama vya kujitakia umaarufu binfsi au wengine kukaataa hoja za wengine kwa kuzani watawazidi umaarufu hata kama hoja hizo zina tija kwa chama.
Nawasilisha.

Daima sina upande wa kushambulia au kusifia daima bali niko katika sehemu ya kutaka taifa lipambane kwa hoja na si ushabiki na matusi kwani kwangu mimi mtawala yeyote awe CCM au Chadema hawezi kuzuia kufikia malengo yangu. lakini kama vyama vya upinzani au CCM wasipojifunza mabishano ya hoja na si matusi hakuna maana ya kuwa na vyama bali wagombea binafsi ndio wawe kimbilio la wananchi.
Mdau unalosema ni kweli kabisa ndani ya Chadema sasa kunajengeka tabaka la kutokubali hoja mbadala na pia kuona yoyote anaetoa mawazo mbadala ni mpinzania na anainia ovu,lakini ukweli ni kwamaba wengi wetu hatutaki chama kwa sababu tunawapenda watu fulani au mitazamo yao fulani,tunataka chama kitachokomboa watanzania,chama kitakachookoa wanyonge,na chama cha kuokombowa wanyone na lazima kijenwge katika misingi ya watu na watu waone ni mali yao,kitokane na nia halisi ya watu walioamua chama chao kiweje,sasa ukiwanyima hao nafasi na kuamini mawazo ya viongozi tu ndio sasa,unanyima watu nafasi ya kuona hiki ni chama chetumhaya ni mawzo yetu hawa viongozi ni wenzetu!Hii tu ndio misingi inayokipa chama madaraka na kukifanya kidumu madarakani,ccm walisahau hayo na leo wapo hapo walipo.
 
​lakini katika kila jambo linalojadiliwa humu lazima kuna mambo ya ukweli yanawasilishwa kupitia utani utani hivi
 
Wakuu nawaunga mkono kwani hata mimi hilo mlilodokeza kuwa baazi ya wafuasi wa chadema hususani humu JF wanarusha sana matusi.Ila lazima tujiulize kwa nini wanarusha matusi na ni kwenye hoja gani haswa wanarusha matusi.Mimi nilichogundua ni kuwa baazi ya watu wanaorusha matusi wengi wao ni waadhirika direct na utawala mbovu wa Chama Cha Magamba, mfano wanafunzi watoto wa masikini wanaoadhirika kwa kukosa mikopo katika elimu ya juu ili hali kuna watu wenye uwezo wa viongozi wanapata hizo fedha.Watu kama hawa wanakuwa na hasira coz hawana jinsi na wanaona udhalimu unaofanywa na serikali yao. Pia ikumbukwe kuwa kuna watu wanaanzisha mada humu wakisifia utawala wa Chama cha Magamba kutokana na wao wanavyofaidika na ufisadi wa hao wanaotuongoza.Kwa hiyo ni lazim tuwe tunajua ni kwa nini ndugu zetu wanachangia kwa jazba ,wakati mwingine yanazidi ila kuna sababu sio kuwa watu hawana upeo wa kuchambua na kutabainisha mambo
 
Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA

Dah,JF raha,kuna watu wanakurupuka hadi wanafurahisha.Hongera kwa hoja yako
 
Back
Top Bottom