CHADEMA wanapata ruzuku kubwa kila mwezi nini kinachosababisha wasifungue matawi kila kijiji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wanapata ruzuku kubwa kila mwezi nini kinachosababisha wasifungue matawi kila kijiji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Godwine, Dec 28, 2011.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mimi bado nakuja kwenye hoja ya matawi nchi nzima , kwanini chama hiki kimeshindwa kufanya hivyo wakati kimeweza kufanya maandamano karibu nchi nzima. au katika maandamano hayo kuna maslahi kiasi kikubwa kwa viongozi wake wa ngazi ya juu.

  NAOMBA CHADEMA KIFUTWE TOKA KWENYE ORODHA YA VYAMA VYA SIASA KWASABABU WAMESHINDWA KUFUNGUA MATAWI MPAKA NGAZI YA KIJIJI . TENDWA FANYA KAZI YAKO MARA MOJA

   
 2. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tupatie data ya matawi ya CDM kabla ya kukilaumu kushindwa. By the way serkali imefisilika ruzuruku za vyama haitoki kabisa!
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Godwine, leo umeamkia huku tena? habari ya sikukuu ya krismasi na kufungua vifurushi.

  Je unafahamu chadema wanapata shilingi ngapi kwa mwezi kama ruzuku? Manake usiseme tu kubwa bila kujua ni kubwa kiasi gani.

  Kabla hujatoa ushauri mbovu kama huu, ungejitahidi kupitia sheria ya usajili wa vyama vya siasa pamoja na majukumu/wajibu wa msajili kwa vyama vya siasa ujiridhishe kama chama cha siasa kutokuwa na ofisi za matawi kila kijiji inaweza kuwa sababu ya msajili kukipa karipio/onyo achilia mbali kukifuta.

  Labda nikusaidie tu kwamba kazi ya kufungua ofisi za matawi ni majukumu ya wanachama na viongozi wa maeneo husika. Wanachama wenyewe wanajikusanya na kuanzisha misingi, kisha matawi, baadae kata na hatimaye jimbo. Viongozi wa kitaifa wanahusika kusimamia chaguzi za kuanzia ngazi ya jimbo/wilaya. Viongozi wa kitaifa hawawezi kuwa na jukumu la kufungua matawi, hadi wamepata mwaliko kutoka jimbo/wilaya husika. Na wanapopata mwaliko wanakwenda kuzindua tawi ambalo tayari limekamilisha taratibu za kichama na lina viongozi, si kazi yao kuanzisha matawi.
   
 4. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mada nyingine Jamani...,Upuuzi Mtupu! Kwanza Kama Ungekuwa Msomi Ungehoji kwanza taarifa ya Mapato na Matumizi Ujue kwanini Pesa hazifiki Kijijini,,...Na Pili Kila Chama Kina Mipango na Taratibu zake...,Chadema Hakiwezi Kukiiga CCM Ambao Wanafunua Matawi na Kugawa Fulana,Na Khanga,Sukari Na Chumvi!
  Na Mwisho Hufuatilii Mambo ya Chadema Unaropoka tu Hovyo! Kwani sasa hivi chama kimeagiza magari si zaidi ya Hamsini Kwaajili ya Kuweza kufika huko kwanza vijijini...na Tendwa hawezi kufuta chama kwani kila siku wanapelekewa taarifa ya matumizi ya ruzuku ndio maana hujawi kusikia hajawi kukilalamikia chama kuhusu ruzuku! Tafadhali kajipange upya...JF sio Forum ya Wajinga Kuandika Upuuzi wako Huku
   
 5. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  nitaleta uchumi unao paa by jk 2005
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mnapata zaidi ya shs mil 200 kwa mwezi
   
 7. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135


  nimekuelewa, unataman sana CHADEMA ikue haraka. Asante kwa wazo lako japo umelileta kwa jazba au umekulupuka. Ila meseji imefika

   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  tafadhali tuletee idadi yamatawi ya kila chama kinachopokea ruzuku, anza na chadema, ccm,cuf,nccr,tlp na udp
   
 9. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona hujaisema PONA,TADEA,SAU, NA TLP kuwa vifutwe kwa sababu vyote hivyo vina tawi mojamoja ambalo ni familia ya mwenyekiti wa chama
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hizi ni zama za science & Technology. Huitaji physical building ili uimarishe chama. Na CHADEMA wamethibisha hilo. Wanafanya kazi kwa mfumo wa i-office na sio P.O.BOX. Binafsi mtindo wa ccm wa kuwa na office kila mtaa ni sawa na UKUPE. Watu wazima wananshinda kwenye office wanafanya nini?
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Godwine ana hoja aidha haelewi ni kwa nini CDM hawafungui matawi vijijini wakati wanapata ruzuku ambayo ana haki ya kuihoji au inawezeka CDM hawatoi taarifa wapi wamefungua na Godwine akazipata.
   
 12. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na huko kijijini? Au cdm ipo mjini? Ni lazima iwe na ofisi za matawi ili iwe karibu na wananchi na kusikiliza matatizo yao kutoa mbinu za kupambana na maisha. Kumbukeni vijijini hakuna umeme, tv na vyombo vingine vya mawasiliano zaidi ya radio, hvy ni muhimu sana kuwa na matawi
   
 13. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  huyu mtoa mada naye hana tofauti na popo! yeye ni mtu asiyependa mafanikio ya chadema na wakati huo huo anailaumu chadema kwa kutofungua matawi mpaka vijijini.sasa badala ya kufurahia hali hiyo kwani ni ya manufaa kwa chama chake ccm yeye anajifanya kuchukia.Huo sasa ndo tunaita unafki wa kisiasa!
   
 14. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ofisi ndo kama club mkuu ndo mnapokutana na kupanga/kuibua mikakati,besides watu wetu wa vjjn still hawana "i"- i-office hawana acces nayo,so matawi bado muhimu
   
 15. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hata demu wangu wa kwanza aliyeishia std 7 hana mawazo kama haya. Hivi kumbe CDM inawanyima kulala eeh?!! Jana umetaka Dr.Slaa na Mbowe wafutwe uraia (ndoto za mchana) leo unataka ifutwe CHADEMA, ndugu yetu unajifunza uchawi au umetumwa?

  Hizi conclusion za fulani afutwe uraia, chama fulani kifutwe ni malezi mabaya ya utotoni. Inaelekea mzazi wako alikuwa akikerwa na taarifa fulani redioni anavunja redio.

  CCM ina matawi mpk kwenye malago ya wapika gongo, nini kipya zaidi ya kuona watu wazima na akili zao wanaacha kufanya kazi wanacheza bao mchana kutwa wakisubiri kuitwa na dokta kwa kofia ya Wazee wa DSM?

  Mimi nachoona mtoa mada anaishauri CDM ianzishe vituo vya kuchezea bao kama CCM.
   
 16. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
   
 17. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sheria ya kuandikisha vyama vya siasa haisemi kuwa chama ilikisajiliwe kiwe na matawi nchi nzima! Pia si lazima kufuata mfumo wa uendeshaji chama wa CCM, kila chama kina taratibu zake. Unaweza kuwafikia wananchi kwa mitandao ya simu ndio maana Chadema wanasajili na kupokea ada za wanachama kwa kupitia mitandao ya simu. Kujenga majengo kila kijiji na kuweka watu wa kupiga porojo na kuanzisha majungu ndio vitu vinavyoiua CCM kwa sasa. Mashina na matawi ya CCM hayana kazi zaidi ya kugombea pesa za "kupark" magari ("open spaces" zenyewe vya kupark magari vinatakiwa virudishwe halmashauri) na fremu za kukodi.
   
 18. G

  Godwine JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145

  Nadhani chadema na CCM ndio vyama vinavyopata ruzuku kubwa ambayo inaweza kufanya kazi mpaka ngazi za chini, lakini CCM wao wameshuka mpaka chini kwa wajumbe wa nyumba kumi toka enzi za nyerere, lakini Chadema wao wameamua kubaki juu toka wachukue mamilioni ya ruzuku zako . kuna nini kinaendelea mpaka washindwe kushuka chini? hayo ndiyo matumizi mabaya ya ruzuku wanayopewa ndio maana namshauri bwana Tendwa wakifute chama hiki au wakifungie mpaka kitekeleze jambo hili
   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwani mpaka sasa wamefungua matawi mangapi na ilipaswa wawe wamefungua mangapi? hebu tupe takwimu ili tujue udhaifu wa hiki chama na ikiwezekana tukuunge mkono Tendwa "akifute". Hata hivyo pia ungefanya vizuri kutuambia ni kiasi gani cdm wanapata cha ruzuku kwa mwezi/mwaka pia matumizi ya ofisi kuu ili tujiulize kinachosalia kinatumika wapi..!
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Feedback,

  Kwa taarifa yako na wengine ni kwamba mwaka kesho tunaanza mchakato wa uchaguzi ndani ya chama. Tutaanza na ngazi ya chini kabisa ya msingi, tawi, kata, jimbo/wilaya, mkoa na hatimaye taifa.

  Maelekezo ya ofisi ya katibu mkuu ni kwamba hakutakuwa na uchaguzi wa tawi bila chaguzi za misingi kukamilika, hakutakuwa na uchaguzi wa kata bila uchaguzi wa matawi kukamilika, hakutakuwa na uchaguzi wa jimbo/wilaya bila chaguzi za kata kukamilika, na utaratubu utakwenda hivyo hivyo hadi ngazi ya taifa, kwa mujibu wa katiba ya chama.

  Na kwakuwa ni lazima chaguzi ngazi zote zifanyike, na kwa kuzingatia mwitikio wa wananchi katika kujiunga na chadema, hatuna shaka kwamba kabla ya kuwa na uchaguzi wa ngazi za majimbo/wilaya, kila kijiji na mtaa kutakuwa na ofisi ya chadema. Jambo la msingi ni kuunganisha nguvu na wanaharakati wote kujiunga na chadema ili tupate viongozi wazalendo na watakao kuwa commited ili hatimaye chama kiwe na uongozi imara toka ngazi za chini kabisa kama ilivyo kwenye level ya kitaifa.
   
Loading...