CHADEMA wanakosea kwenye mpangilio wa kuomba Katiba Mpya

Mimi ni mdau ambaye naunga mkono sana mabadiliko ya katiba lakini mpangilio wa sasa ambao unaongozwa na Chadema sijaupenda na hautasaidia mafanikio haya kwasababu zifuatazo

1. Raisi mpya Samia hawezi kukubali kufanya katiba wakati mapema kwa kuzingatia ameingia majuzi tu na kachukuwa madaraka kwenye wakati mgumu kwa mtangulizi wake kupoteza maisha. Hii kwa nchi nyingine ambazo hazina usalama wangeweka " state of emergency" ingawa hatukufika huko Raisi anahitaji muda kwanza kupata nguvu na kuungwa mkono kabla ya kudandia swala nyeti na lenye kugawanya watu kama katiba mpya.
2. Corona ni ugojwa ni sio kitu cha kisiasa. Huu ni ugojwa na kuna Watanzania wengi wamepoteza ndugu wengi kuanzia mwaka 2019. Tuliulize ni kitu gani kimetokea kusababisha haya? jibu ni Corona. Corona imeondoa watu wengine ambao hata familia hazijui wamekufa kwa nini. Kuna watu wawili ambao nina mfano mmoja ni rafiki yangu wa Ilboru ambaye alikuwa anamiliki mgodi kule Mererani kwenye wimbi la pili alikufa ghafla wakidai alikosa pumzi na kafariki wa kisukari. Familia ikadai apimwe Corona maana alikuwa na miaka 44 tu na sukari yake haikuwa mbaya hivyo! walivyopima zaidi ya mara moja wakakuta ana Corona. Juzi pia mzazi wa rafiki yangu naye sukari imepanda akafariki Musoma baada ya familia kulazimisha apimwe wamekuta naye alikufa kwa Corona ingawa kabla ya kupima walisema sukari imepanda. Kwa ufupi huu sio wakati mzuri wa kufanya makusanyiko yeyote yasiyo ya lazima. Kwa msingi huu naunga mkono Raisi samia kwamba huu sio wakati mzuri wa kuanzisha mikutano ambayo inaweza kuongeza na sio kuzuia Corona.
3. Mkutano na Raisi: Chadema wanakosea kufanya huu mkutano mkubwa kuliko ulivyo. Chadema kukuza huu mkutano na Raisi Samia unamfanya Raisi aone kwamba anatakiwa kujiandaa sana badala ya Chadema kuuchukulia mkutano wa kawaida wa kujua. Chadema kwa faida za nchi na kisiasa wanatakiwa kuweka urafiki na Raisi na sio kufanya mkutano kama unaenda kukutana na watekaji wako. Mama anapenda sana umoja, yeye pekee ndiye alienda kumwangalia Lissu Kenya makusudi bila hata kumwambia kiongozi wake Magu. Hata safari ya Kenya inawezekana alilazimisha kwenda Kenya ili akamuone Lissu bila kuwaambia nia yake Chama. Haya yote kafanya ili Chadema wajue na yeye binafsi aweke rekodi kwamba yeye kama Samia hajahusika kwenye njama zozote za kumuumiza Lissu. Cha ajabu chadema pamoja na kuwa na mtu ambaye ataweza kufanya nao kazi wanataka wampime kijinga kwa kuweka maandamano ambayo yatawasaidia wale ndani ya CCM wanaotafuta sababu za kuwapiga upinzani kwa faida zao. Chadema ni lazima wajue kule CCM kuna wengi walikuwa wananufaika na biashara za upinzani ilikwa ni pamoja na kutumia pesa za kununua wapinzani nje ya utaratibu, kuunda vikundi vya ajabu, kuomba pesa za teknologia za kurekodi watu..... hizo zote ni biashara za mabilioni ambazo Chadema kwa kuleta mikutano ya ajabu itawapa sababu hawa walaji kwenda kwenye chama na kuanza tena kuchukua pesa baada ya kumuogopesha Raisi
Umeeleza vizuri hasa kuhusu wakati kuwa bado ni mapema na pia janga la corona. Tusiharakishe.
 
Ww ni mfaidika wa uchaguzi ule wa kishenzi, hivyo huwezi kuona tatizo lake. Ccm kilikuwa chama cha kijamaa enzi za Nyerere, sasa hivi hawana itikadi yoyote bali kinacheza na upepo. Nguvu pekee ya ccm sio ushawishi kwa wananchi, bali ni kwa jinsi kilivyoshikamana na vyombo vya dola. Ila kwa hii agenda ya katiba mpya lazima tuwavuruge vibaya. Haya ni madai halali, mabavu hayawatoi kwenye hili, na vile hamkushinda uchaguzi kihalali lazima mpanic.
Huyo mpuuze kwani ni mpuuzi, atakupotezea muda.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
..uongozi wa cdm ulishaomba kukutana na raisi.

..je, ni sahihi kudai watu wanaoomba na wakati mwingine kubembeleza kukutana na raisi kuwa wanataka kuleta chokochoko au vurugu?

..mimi nadhani Rais SSH hana nia ya dhati kukutana na wapinzani na ndio maana ameanza kuwapakazia na kuwapa sifa mbaya kwa wananchi.

..kama Rais SSH angekuwa na nia njema na wapinzani, asingeruhusu mbunge aliyefukuzwa chadema ashiriki ktk mkutano wake na ajitambulishe kama muwakilishi wa cdm.

..pia kama angekuwa anataka kufungua ukurasa mpya ktk mahusiano baina ya serikali / ccm na wapinzani asingeteua wahuni waliopata kujiapiza kutaka kuwauwa viongozi wa upinzani.

..Katibu Mkuu mpya wa UV-CCM ni kijana aliyetamka hadharani kwamba Zitto Kabwe anastahili kuuwawa. Sasa Rais Samia anawezaje kubariki uteuzi huo, halafu akadai ana nia njema na wapinzani?

..Suala la kuinua uchumi na kurejesha wawekezaji kabla ya kukutana na wapinzani ni kisingizio tu. Rais Dr.Hussein Mwinyi amekutana na wapinzani bila kuchelewa. Je, Znz wao hawataki kuinua uchumi au kuvutia wawekezaji?

..Vilevile siyo lazima Raisi akutane yeye binafsi na wapinzani. Ungeweza kutengenezwa utaratibu wa wapinzani kukutana kwanza na Waziri wa Sheria, au Waziri asiye na wizara maalum, kama utangulizi wa kikao cha Raisi na wapinzani.

..Binafsi naamini tatizo liko upande wa Rais SSH. Sidhani kama ana mpango wowote ule wa kurekebisha mazingira ya kisiasa ili vyama vyote viwe na HAKI na UHURU wa kufanya siasa hapa nchini.
Mimi nashauri namna ya kudai katiba , sijasema ssh hana makosa.
Angalau anaachia mwanya watu wapumue. Ni muhimu kutumia huu mwanya kwa hesabu makini la sivyo kuna uwezekano tukapata kiongozi wa kwanza wa kiislam katili(Mwinyi na Kikwete walikuwa waungwana sana) . Na sababu zipo wazi - amefanya kazi bega kwa bega na dikteta hivyo kumuiga ni swala la kubonyeza batan tu. Si umeona ameanza hotuba za kwenye magari! Kinachofata ataanza kugawa hela barabarani kwani nyuma yake kuna nguvu kubwa ya genge linalofurahia udikteta.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Udikteta kwao genge ni kumuenzi bwana wao, muungu wao. Si ajabu wameanza angalau kutabasamu. Ila bado wanataka kuona ukatili zaidi kama wa zamani hivyo wataendelea kushinikiza na kumzunguka ili angalau matendo ya bwana wao yaenziwe. Kazi ipo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Nani anaomba katiba Tunataka katiba sio ombi

Yaani mnatupangia jinsi ya kupata katiba

Ccm toka lin wakataka ustarabu?
Bro kama unataka si andika tu hata leo. Hahahhhahaa..! Acheni kujidanganya Chama Tawala pekee ndio chenye ridhaa ya kuleta katiba mpya msijifanganye
 
Mimi ni mdau ambaye naunga mkono sana mabadiliko ya katiba lakini mpangilio wa sasa ambao unaongozwa na Chadema sijaupenda na hautasaidia mafanikio haya kwasababu zifuatazo

1. Raisi mpya Samia hawezi kukubali kufanya katiba wakati mapema kwa kuzingatia ameingia majuzi tu na kachukuwa madaraka kwenye wakati mgumu kwa mtangulizi wake kupoteza maisha. Hii kwa nchi nyingine ambazo hazina usalama wangeweka " state of emergency" ingawa hatukufika huko Raisi anahitaji muda kwanza kupata nguvu na kuungwa mkono kabla ya kudandia swala nyeti na lenye kugawanya watu kama katiba mpya.
2. Corona ni ugojwa ni sio kitu cha kisiasa. Huu ni ugojwa na kuna Watanzania wengi wamepoteza ndugu wengi kuanzia mwaka 2019. Tuliulize ni kitu gani kimetokea kusababisha haya? jibu ni Corona. Corona imeondoa watu wengine ambao hata familia hazijui wamekufa kwa nini. Kuna watu wawili ambao nina mfano mmoja ni rafiki yangu wa Ilboru ambaye alikuwa anamiliki mgodi kule Mererani kwenye wimbi la pili alikufa ghafla wakidai alikosa pumzi na kafariki wa kisukari. Familia ikadai apimwe Corona maana alikuwa na miaka 44 tu na sukari yake haikuwa mbaya hivyo! walivyopima zaidi ya mara moja wakakuta ana Corona. Juzi pia mzazi wa rafiki yangu naye sukari imepanda akafariki Musoma baada ya familia kulazimisha apimwe wamekuta naye alikufa kwa Corona ingawa kabla ya kupima walisema sukari imepanda. Kwa ufupi huu sio wakati mzuri wa kufanya makusanyiko yeyote yasiyo ya lazima. Kwa msingi huu naunga mkono Raisi samia kwamba huu sio wakati mzuri wa kuanzisha mikutano ambayo inaweza kuongeza na sio kuzuia Corona.
3. Mkutano na Raisi: Chadema wanakosea kufanya huu mkutano mkubwa kuliko ulivyo. Chadema kukuza huu mkutano na Raisi Samia unamfanya Raisi aone kwamba anatakiwa kujiandaa sana badala ya Chadema kuuchukulia mkutano wa kawaida wa kujua. Chadema kwa faida za nchi na kisiasa wanatakiwa kuweka urafiki na Raisi na sio kufanya mkutano kama unaenda kukutana na watekaji wako. Mama anapenda sana umoja, yeye pekee ndiye alienda kumwangalia Lissu Kenya makusudi bila hata kumwambia kiongozi wake Magu. Hata safari ya Kenya inawezekana alilazimisha kwenda Kenya ili akamuone Lissu bila kuwaambia nia yake Chama. Haya yote kafanya ili Chadema wajue na yeye binafsi aweke rekodi kwamba yeye kama Samia hajahusika kwenye njama zozote za kumuumiza Lissu. Cha ajabu chadema pamoja na kuwa na mtu ambaye ataweza kufanya nao kazi wanataka wampime kijinga kwa kuweka maandamano ambayo yatawasaidia wale ndani ya CCM wanaotafuta sababu za kuwapiga upinzani kwa faida zao. Chadema ni lazima wajue kule CCM kuna wengi walikuwa wananufaika na biashara za upinzani ilikwa ni pamoja na kutumia pesa za kununua wapinzani nje ya utaratibu, kuunda vikundi vya ajabu, kuomba pesa za teknologia za kurekodi watu..... hizo zote ni biashara za mabilioni ambazo Chadema kwa kuleta mikutano ya ajabu itawapa sababu hawa walaji kwenda kwenye chama na kuanza tena kuchukua pesa baada ya kumuogopesha Raisi
CHADEMA wamebeba malengo mazuri lakini wanapita njia chafu kufikia malengo. Hawatoweza kufika. Malengo mazuri hufikiwa kwa njia nzuri kwani baraka za Mungu huwa ndani yake
 
Kwa ujinga wenu wa kudai katiba mpya, Kwa unafki wa kuvutia kamba kwenu,,,, sidhani kama mtapata hyo mnayoiita " katiba mpya" na watanzania tulivyo wanafki,, Twitter na Jf tunapiga kelele kama mbwa koko ,, ifike muda wa implementation . Hata mkitaka kuandamana hampati kamwee
 
Hivi ni katiba nzima from page ya 1 had ya 221 au ndo mnataka kuondoa vle vipengele vinanyowakera kwenye sura ya 2-5

Wanasiasa ni mashetani sio CCM wala CDM
 
Mama alikosea Sana siku amekaa na wahariri wa habari akatoa kauli ya kuendeleza amri haramu ya mwendazake ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kupiga danadana suala la katiba mpya

Haya yalikuwa ndiyo ajenda kuu za chadema kwenda kukutana na Samia. Sasa kama amezipiga teke hadharani mkutano wa chadema na Samia ni wa nini?
Mama hakukosea alisema ukweriii, namsema kweli ni mpenzi wa Mungu,au nasema uongo ndugu zangu.
 
Pia agenda ya katiba iwe jumuishi.Kwa Sasa hivi Ni kama CHADEMA wanataka katiba mpya itakayowezesha upinzani kuingia Ikulu basi au kushiriki uchaguzi bila makandokando.Hii kitu inawafanya CCM waone kama Katiba mpya kwao haina umuhimu.CHADEMA waweke mpango utakaowashawishi Wapenzi wa CCM nao kuona Kuna umuhimu wa Katiba mpya.
Mambo mengi huwa yanafanikiwa kama huwa kunakuwa na uungwaji mkono na watu kutoka CCM.
 
Katiba idaiwe kwa kwa hesbau nzuri, maneno ya kusema tunataka bila kujua mnatakeje ,,eti kwa kuandika hapa jf na twitter,, hii itatuchelewesha.
Mama pia ni binadamu mwenye madhaifu yake, naye anaweza kuchukia kama ambavyo mtu yeyote humu anaweza kuchukia. Lakini yeye akichukia tusisahau kuwa ndiye mwenye amri ya mwisho kuhusu vyombo vyetu vyenye silaha za moto (kwa mujibu wa katiba JMT)

Wananchi tunataka katiba lakini wenye vyama mnaweza mkaichelewesha au mkaiwaisha katiba ya hovyo .

HESABU ZIPANGWE VYEMA
la sivyo haya maneno ambayo ni maneno tu hakika ya ,,tunataka katiba,, yatabaki kwenye mitandao.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hili jambo linahitaji akili kubwa ambayo chadema wanaitumia mpaka sasa, sema ww hujagundua

Kumbuka chadema hawahitaji huruma, alafu ujue pia, chadema watampinga kwenye uchaguzi mkuu ujao

Wakianza kubembeleza leo, kwenye kampen watateseka sana, yaani leo chadema itumie rasimali zake kumbembeleza rais alafu rais atende kutokana na kuwaonea chadema huruma, unajua madhara yake? Hata chadema itapoteza wanachama wake maana wapo watakaosema Samia aendelee maana akiombwa anasikiliza

Inanidi chadema watumie mtindo kama wa kulazimisha lakin huku chini wana njia nyingine za kubembeleza ili jamii ione kama sio nguvu ya chadema, jambo flan lisingewezekana, hapo watakuwa wana win kote kote, kwa jamii na kile wanachokitaka

Kesho chadema ikiomba kura, itaonekana inaweza na ina dhamira ya dhat

**** hujaelewa, mwanagile makamu wa kwanza wa rais kule Zanzibar anavyoenda na rais, yy amejua Wazanzibar wanataka nini, moja ni Zanzibar kujitegemea kila kitu, ndo mana pamoja na kushiriki vikao na rais, bado akitoka nje anaisema Zanzibar, mfano ni kusema code ya Zanzibar +259 na sio +255, vitu ambavyo CCM na rais Mwinyi hawawez kusema kwa kuigopa CCM bara
 
Kwa ujinga wenu wa kudai katiba mpya, Kwa unafki wa kuvutia kamba kwenu,,,, sidhani kama mtapata hyo mnayoiita " katiba mpya" na watanzania tulivyo wanafki,, Twitter na Jf tunapiga kelele kama mbwa koko ,, ifike muda wa implementation . Hata mkitaka kuandamana hampati kamwee
Kwa hiyo uvccm mnataka wapinzani wenu waende kuiomba katiba mpya kanisani au misikitini ?!. Katiba mpya ni jambo la wananchi . Kwingine huko watu huitaka kivita, maandamano na vurugu. Lakini WaTz mbona waungwana ?!. Wanaudai kwa maneno tu !!. Tena kwa kumuomba Rais akubali kurejesha mchakato uliosimama .

Tatizo WaTz humfanya Rais kuwa mungumutu asiyehojiwa chochote. Eti afanye kwa hisani !!!
 
Ww ni mfaidika wa uchaguzi ule wa kishenzi, hivyo huwezi kuona tatizo lake. Ccm kilikuwa chama cha kijamaa enzi za Nyerere, sasa hivi hawana itikadi yoyote bali kinacheza na upepo. Nguvu pekee ya ccm sio ushawishi kwa wananchi, bali ni kwa jinsi kilivyoshikamana na vyombo vya dola. Ila kwa hii agenda ya katiba mpya lazima tuwavuruge vibaya. Haya ni madai halali, mabavu hayawatoi kwenye hili, na vile hamkushinda uchaguzi kihalali lazima mpanic.
CCM siyo chama tena ni genge la wahuni tu
 
Mimi ni mdau ambaye naunga mkono sana mabadiliko ya Katiba lakini mpangilio wa sasa ambao unaongozwa na CHADEMA sijaupenda na hautasaidia mafanikio haya kwasababu zifuatazo

1. Rais mpya Samia hawezi kukubali kufanya katiba wakati mapema kwa kuzingatia ameingia majuzi tu na kachukuwa madaraka kwenye wakati mgumu kwa mtangulizi wake kupoteza maisha. Hii kwa nchi nyingine ambazo hazina usalama wangeweka " state of emergency" ingawa hatukufika huko Rais anahitaji muda kwanza kupata nguvu na kuungwa mkono kabla ya kudandia suala nyeti na lenye kugawanya watu kama katiba mpya.

2. Corona ni ugojwa ni sio kitu cha kisiasa. Huu ni ugojwa na kuna Watanzania wengi wamepoteza ndugu wengi kuanzia mwaka 2019. Tuliulize ni kitu gani kimetokea kusababisha haya? jibu ni Corona. Corona imeondoa watu wengine ambao hata familia hazijui wamekufa kwanini. Kuna watu wawili ambao nina mfano mmoja ni rafiki yangu wa Ilboru ambaye alikuwa anamiliki mgodi kule Mererani kwenye wimbi la pili alikufa ghafla wakidai alikosa pumzi na kafariki wa kisukari. Familia ikadai apimwe Corona maana alikuwa na miaka 44 tu na sukari yake haikuwa mbaya hivyo! Walivyopima zaidi ya mara moja wakakuta ana Corona. Juzi pia mzazi wa rafiki yangu naye sukari imepanda akafariki Musoma baada ya familia kulazimisha apimwe wamekuta naye alikufa kwa Corona ingawa kabla ya kupima walisema sukari imepanda. Kwa ufupi huu sio wakati mzuri wa kufanya makusanyiko yoyote yasiyo ya lazima. Kwa msingi huu naunga mkono Rais Samia kwamba huu sio wakati mzuri wa kuanzisha mikutano ambayo inaweza kuongeza na sio kuzuia Corona.
3. Mkutano na Rais: Chadema wanakosea kufanya huu mkutano mkubwa kuliko ulivyo. Chadema kukuza huu mkutano na Rais Samia unamfanya Rais aone kwamba anatakiwa kujiandaa sana badala ya Chadema kuuchukulia mkutano wa kawaida wa kujua. Chadema kwa faida za nchi na kisiasa wanatakiwa kuweka urafiki na Rais na sio kufanya mkutano kama unaenda kukutana na watekaji wako. Mama anapenda sana umoja, yeye pekee ndiye alienda kumwangalia Lissu Kenya makusudi bila hata kumwambia kiongozi wake Magu. Hata safari ya Kenya inawezekana alilazimisha kwenda Kenya ili akamuone Lissu bila kuwaambia nia yake Chama. Haya yote kafanya ili Chadema wajue na yeye binafsi aweke rekodi kwamba yeye kama Samia hajahusika kwenye njama zozote za kumuumiza Lissu. Cha ajabu chadema pamoja na kuwa na mtu ambaye ataweza kufanya nao kazi wanataka wampime kijinga kwa kuweka maandamano ambayo yatawasaidia wale ndani ya CCM wanaotafuta sababu za kuwapiga upinzani kwa faida zao. Chadema ni lazima wajue kule CCM kuna wengi walikuwa wananufaika na biashara za upinzani ilikwa ni pamoja na kutumia pesa za kununua wapinzani nje ya utaratibu, kuunda vikundi vya ajabu, kuomba pesa za teknologia za kurekodi watu..... hizo zote ni biashara za mabilioni ambazo Chadema kwa kuleta mikutano ya ajabu itawapa sababu hawa walaji kwenda kwenye chama na kuanza tena kuchukua pesa baada ya kumuogopesha Rais
unataka watembee kwa magoti,kwanza nani anaomba katiba,ni kwamba wananchi tunataka katiba mpya
 
Back
Top Bottom