CHADEMA wanakosea kwenye mpangilio wa kuomba Katiba Mpya

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,619
8,770
Mimi ni mdau ambaye naunga mkono sana mabadiliko ya Katiba lakini mpangilio wa sasa ambao unaongozwa na CHADEMA sijaupenda na hautasaidia mafanikio haya kwasababu zifuatazo

1. Rais mpya Samia hawezi kukubali kufanya katiba wakati mapema kwa kuzingatia ameingia majuzi tu na kachukuwa madaraka kwenye wakati mgumu kwa mtangulizi wake kupoteza maisha. Hii kwa nchi nyingine ambazo hazina usalama wangeweka " state of emergency" ingawa hatukufika huko Rais anahitaji muda kwanza kupata nguvu na kuungwa mkono kabla ya kudandia suala nyeti na lenye kugawanya watu kama katiba mpya.

2. Corona ni ugojwa ni sio kitu cha kisiasa. Huu ni ugojwa na kuna Watanzania wengi wamepoteza ndugu wengi kuanzia mwaka 2019. Tuliulize ni kitu gani kimetokea kusababisha haya? jibu ni Corona. Corona imeondoa watu wengine ambao hata familia hazijui wamekufa kwanini. Kuna watu wawili ambao nina mfano mmoja ni rafiki yangu wa Ilboru ambaye alikuwa anamiliki mgodi kule Mererani kwenye wimbi la pili alikufa ghafla wakidai alikosa pumzi na kafariki wa kisukari. Familia ikadai apimwe Corona maana alikuwa na miaka 44 tu na sukari yake haikuwa mbaya hivyo! Walivyopima zaidi ya mara moja wakakuta ana Corona.

Juzi pia mzazi wa rafiki yangu naye sukari imepanda akafariki Musoma baada ya familia kulazimisha apimwe wamekuta naye alikufa kwa Corona ingawa kabla ya kupima walisema sukari imepanda. Kwa ufupi huu sio wakati mzuri wa kufanya makusanyiko yoyote yasiyo ya lazima. Kwa msingi huu naunga mkono Rais Samia kwamba huu sio wakati mzuri wa kuanzisha mikutano ambayo inaweza kuongeza na sio kuzuia Corona.

3. Mkutano na Rais: Chadema wanakosea kufanya huu mkutano mkubwa kuliko ulivyo. Chadema kukuza huu mkutano na Rais Samia unamfanya Rais aone kwamba anatakiwa kujiandaa sana badala ya Chadema kuuchukulia mkutano wa kawaida wa kujua. Chadema kwa faida za nchi na kisiasa wanatakiwa kuweka urafiki na Rais na sio kufanya mkutano kama unaenda kukutana na watekaji wako.

Mama anapenda sana umoja, yeye pekee ndiye alienda kumwangalia Lissu Kenya makusudi bila hata kumwambia kiongozi wake Magu. Hata safari ya Kenya inawezekana alilazimisha kwenda Kenya ili akamuone Lissu bila kuwaambia nia yake Chama.

Haya yote kafanya ili Chadema wajue na yeye binafsi aweke rekodi kwamba yeye kama Samia hajahusika kwenye njama zozote za kumuumiza Lissu. Cha ajabu chadema pamoja na kuwa na mtu ambaye ataweza kufanya nao kazi wanataka wampime kijinga kwa kuweka maandamano ambayo yatawasaidia wale ndani ya CCM wanaotafuta sababu za kuwapiga upinzani kwa faida zao.

Chadema ni lazima wajue kule CCM kuna wengi walikuwa wananufaika na biashara za upinzani ilikwa ni pamoja na kutumia pesa za kununua wapinzani nje ya utaratibu, kuunda vikundi vya ajabu, kuomba pesa za teknologia za kurekodi watu, hizo zote ni biashara za mabilioni ambazo Chadema kwa kuleta mikutano ya ajabu itawapa sababu hawa walaji kwenda kwenye chama na kuanza tena kuchukua pesa baada ya kumuogopesha Rais
 
Katiba idaiwe kwa kwa hesbau nzuri, maneno ya kusema tunataka bila kujua mnatakeje ,,eti kwa kuandika hapa jf na twitter,, hii itatuchelewesha.

Mama pia ni binadamu mwenye madhaifu yake, naye anaweza kuchukia kama ambavyo mtu yeyote humu anaweza kuchukia. Lakini yeye akichukia tusisahau kuwa ndiye mwenye amri ya mwisho kuhusu vyombo vyetu vyenye silaha za moto (kwa mujibu wa katiba JMT)

Wananchi tunataka katiba lakini wenye vyama mnaweza mkaichelewesha au mkaiwaisha katiba ya hovyo .

HESABU ZIPANGWE VYEMA
la sivyo haya maneno ambayo ni maneno tu hakika ya ,,tunataka katiba,, yatabaki kwenye mitandao.
 
Kamundu,

..tatizo ni " mama " kutumia sababu za UONGO kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani.

..kama kuna tatizo la corona mbona " mama " ameruhusu mikutano ya wabunge wa ccm, mbio za mwenge, mashabiki kuhudhuria mechi za mpira, na mihadhara ya kidini?
Hapa mngeweka mkazo kwenye mikutano kwanza ,, halfu huko kwenye mikutano ndiko mngeanza kufundisha watu kuhusu katiba,, watu wakielewa maana ya katiba bora wataanza kudai wenyewe bila nyie kuwashawishi tena. Lakini hii mnafanya kama mnataka kupambana na rais, nayeye ni lazima atajiandaa kwa mapambano,, kitakachofuata ni dikteta mwingine kutawala Tanzania.
Uhujumu uchumi utarudi
Kutakatisha fedha
Uchochezi
Wasiojulikana nk.nchi itaanza tena kuwayawaya

Ushauri wangu tu.
 
Hapa mngeweka mkazo kwenye mikutano kwanza ,, halfu huko kwenye mikutano ndiko mngeanza kufundisha watu kuhusu katiba,, watu wakielewa maana ya katiba bora wataanza kudai wenyewe bila nyie kuwashawishi tena. Lakini hii mnafanya kama mnataka kupambana na rais, nayeye ni lazima atajiandaa kwa mapambano,, kitakachofuata ni dikteta mwingine kutawala Tanzania.
Uhujumu uchumi utarudi
Kutakatisha fedha
Uchochezi
Wasiojulikana nk.nchi itaanza tena kuwayawaya

Ushauri wangu tu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Uongozi wa CHADEMA ulishaomba kukutana na rais.

Je, ni sahihi kudai watu wanaoomba na wakati mwingine kubembeleza kukutana na raisi kuwa wanataka kuleta chokochoko au vurugu?

Mimi nadhani Rais SSH hana nia ya dhati kukutana na wapinzani na ndio maana ameanza kuwapakazia na kuwapa sifa mbaya kwa wananchi.

Kama Rais SSH angekuwa na nia njema na wapinzani, asingeruhusu mbunge aliyefukuzwa chadema ashiriki ktk mkutano wake na ajitambulishe kama muwakilishi wa cdm.

Pia kama angekuwa anataka kufungua ukurasa mpya ktk mahusiano baina ya serikali / ccm na wapinzani asingeteua wahuni waliopata kujiapiza kutaka kuwauwa viongozi wa upinzani.

Katibu Mkuu mpya wa UV-CCM ni kijana aliyetamka hadharani kwamba Zitto Kabwe anastahili kuuwawa. Sasa Rais Samia anawezaje kubariki uteuzi huo, halafu akadai ana nia njema na wapinzani?

Suala la kuinua uchumi na kurejesha wawekezaji kabla ya kukutana na wapinzani ni kisingizio tu. Rais Dr.Hussein Mwinyi amekutana na wapinzani bila kuchelewa. Je, Znz wao hawataki kuinua uchumi au kuvutia wawekezaji?

Vilevile siyo lazima Raisi akutane yeye binafsi na wapinzani. Ungeweza kutengenezwa utaratibu wa wapinzani kukutana kwanza na Waziri wa Sheria, au Waziri asiye na wizara maalum, kama utangulizi wa kikao cha Raisi na wapinzani.

Binafsi naamini tatizo liko upande wa Rais SSH. Sidhani kama ana mpango wowote ule wa kurekebisha mazingira ya kisiasa ili vyama vyote viwe na HAKI na UHURU wa kufanya siasa hapa nchini.
 
..uongozi wa cdm ulishaomba kukutana na raisi.

..je, ni sahihi kudai watu wanaoomba na wakati mwingine kubembeleza kukutana na raisi kuwa wanataka kuleta chokochoko au vurugu?

..mimi nadhani Rais SSH hana nia ya dhati kukutana na wapinzani na ndio maana ameanza kuwapakazia na kuwapa sifa mbaya kwa wananchi.

..kama Rais SSH angekuwa na nia njema na wapinzani, asingeruhusu mbunge aliyefukuzwa chadema ashiriki ktk mkutano wake na ajitambulishe kama muwakilishi wa cdm.

..pia kama angekuwa anataka kufungua ukurasa mpya ktk mahusiano baina ya serikali / ccm na wapinzani asingeteua wahuni waliopata kujiapiza kutaka kuwauwa viongozi wa upinzani.

..Katibu Mkuu mpya wa UV-CCM ni kijana aliyetamka hadharani kwamba Zitto Kabwe anastahili kuuwawa. Sasa Rais Samia anawezaje kubariki uteuzi huo, halafu akadai ana nia njema na wapinzani?

..Suala la kuinua uchumi na kurejesha wawekezaji kabla ya kukutana na wapinzani ni kisingizio tu. Rais Dr.Hussein Mwinyi amekutana na wapinzani bila kuchelewa. Je, Znz wao hawataki kuinua uchumi au kuvutia wawekezaji?

..Vilevile siyo lazima Raisi akutane yeye binafsi na wapinzani. Ungeweza kutengenezwa utaratibu wa wapinzani kukutana kwanza na Waziri wa Sheria, au Waziri asiye na wizara maalum, kama utangulizi wa kikao cha Raisi na wapinzani.

..Binafsi naamini tatizo liko upande wa Rais SSH. Sidhani kama ana mpango wowote ule wa kurekebisha mazingira ya kisiasa ili vyama vyote viwe na HAKI na UHURU wa kufanya siasa hapa nchini.

Mama ana urais wa kurithi, kundi linalomzunguka ni lililokuwa la Magufuli, hivyo wanamtisha na kumvika kivuli cha marehemu. Huyo mama hana jinsi zaidi ya kutaka kuwafurahisha chama chake, na agenda ya katiba mpya anataka chama chake ndio kiridhie. Hili inapelekea mama kucheza delaying tactic ambazo hajui hata hatima yake ndio maana anatoa sababu zisizo ma mashiko.
 
Saccos ya CHADEMA ni sikio la kufa.....

Hiki chama cha VICOBA kinamlazimishaje Rais wa Kiafrika?!!!

Tanzania si nchi ya KILIBERALI....

#KaziIendelee
 
Rais aliyepatikana kwa uchaguzi wa kishenzi kama ule naye ni wa kusifia?
Uchaguzi wa kishenzi kwako....si kwangu....

Tindo utaendelea kulalamika mpaka uzee wako.....

CCM ni chama cha KIJAMAA....na wajamaa tunaposhika hatamu basi "tutalaumiwa nanyi kila uchao".....

#KaziIendelee
#KatibaYetuNiBora
 
Uchaguzi wa kishenzi kwako....si kwangu....

Tindo utaendelea kulalamika mpaka uzee wako.....

CCM ni chama cha KIJAMAA....na wajamaa tunaposhika hatamu basi "tutalaumiwa nanyi kila uchao".....

#KaziIendelee
#KatibaYetuNiBora

Ww ni mfaidika wa uchaguzi ule wa kishenzi, hivyo huwezi kuona tatizo lake. Ccm kilikuwa chama cha kijamaa enzi za Nyerere, sasa hivi hawana itikadi yoyote bali kinacheza na upepo. Nguvu pekee ya ccm sio ushawishi kwa wananchi, bali ni kwa jinsi kilivyoshikamana na vyombo vya dola. Ila kwa hii agenda ya katiba mpya lazima tuwavuruge vibaya. Haya ni madai halali, mabavu hayawatoi kwenye hili, na vile hamkushinda uchaguzi kihalali lazima mpanic.
 
Ww ni mfaidika wa uchaguzi ule wa kishenzi, hivyo huwezi kuona tatizo lake. Ccm kilikuwa chama cha kijamaa enzi za Nyerere, sasa hivi hawana itikadi yoyote bali kinacheza na upepo. Nguvu pekee ya ccm sio ushawishi kwa wananchi, bali ni kwa jinsi kilivyoshikamana na vyombo vya dola. Ila kwa hii agenda ya katiba mpya lazima tuwavuruge vibaya. Haya ni madai halali, mabavu hayawatoi kwenye hili, na vile hamkushinda uchaguzi kihalali lazima mpanic.
Tindo endelea kuukimbiza UPEPO....

Suala la KATIBA mpya SI JIPYA....

Mbona hamkuvuruga baada ya mchakato ule kujifia mikononi mwa hayati mzee SITA?!!!

Hamkuwepo?!!!!

Mkuu endelea kuota njozi.....

Uchaguzi uliopita mliutengenezea "movies" za kura FEKI na ikathibitika JANJA YENU....
 
Mkutano na Raisi: Chadema wanakosea kufanya huu mkutano mkubwa kuliko ulivyo. Chadema kukuza huu mkutano na Raisi Samia unamfanya Raisi aone kwamba anatakiwa kujiandaa sana badala ya Chadema kuuchukulia mkutano wa kawaida wa kujua
Mama alikosea Sana siku amekaa na wahariri wa habari akatoa kauli ya kuendeleza amri haramu ya mwendazake ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kupiga danadana suala la katiba mpya

Haya yalikuwa ndiyo ajenda kuu za chadema kwenda kukutana na Samia. Sasa kama amezipiga teke hadharani mkutano wa chadema na Samia ni wa nini?
 
Mama alikosea Sana siku amekaa na wahariri wa habari akatoa kauli ya kuendeleza amri haramu ya mwendazake ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na kupiga danadana suala la katiba mpya

Haya yalikuwa ndiyo ajenda kuu za chadema kwenda kukutana na Samia. Sasa kama amezipiga teke hadharani mkutano wa chadema na Samia ni wa nini?
Kwani CHADEMA walidhani watakwenda "kuropoka" huko mkutanoni na kutekelezewa MATAKWA YAO YOTE?!!!

Kwa hiyo CHADEMA wana AJENDA MOJA TU katika mkutano wao na mh.Rais SSH?!!!!
 
Ajenda ni mbili tu.
-haki kwa mujibu wa Katiba iliyopo itamalaki
-katiba iliyopo ina mapungu, hivyo ibadilishwe.
Sawa.....

Mh.Rais akiwajibu AMEWASIKIA na KUWAELEWA VYEMA tu..

Mtamuuliza amewaelewa KIVIPI ?!!! 🤣🤣
 
Tindo endelea kuukimbiza UPEPO....

Suala la KATIBA mpya SI JIPYA....

Mbona hamkuvuruga baada ya mchakato ule kujifia mikononi mwa hayati mzee SITA?!!!

Hamkuwepo?!!!!

Mkuu endelea kuota njozi.....

Uchaguzi uliopita mliutengenezea "movies" za kura FEKI na ikathibitika JANJA YENU....
Ccm mbona mnafurahia katiba inayobana haki za baadhi ya wananchi ?!. Nyinyi ni chama kikongwe uoga wa katiba nzuri ya nini ?! Kwanini muishi kwa mbeleko ?!
 
Ccm mbona mnafurahia katiba inayobana haki za baadhi ya wananchi ?!. Nyinyi ni chama kikongwe uoga wa katiba nzuri ya nini ?! Kwanini muishi kwa mbeleko ?!
Hata tuliyonayo ni nzuri....

Katiba iliyopo kweli inawabana wanaotaka TANGANYIKA irudi.....
 
Hata tuliyonayo ni nzuri....

Katiba iliyopo kweli inawabana wanaotaka TANGANYIKA irudi.....
Uzuri wake nini, kama viongozi unaowachagua hawana nguvu dhidi ya wateule wa mtu mmoja (Rais) !!. Uzuri wake nini kama kina Ndugai wanajitungia sheria za kutokushtakiwa ?!
 
Uzuri wake nini, kama viongozi unaowachagua hawana nguvu dhidi ya wateule wa mtu mmoja (Rais) !!. Uzuri wake nini kama kina Ndugai wanajitungia sheria za kutokushtakiwa ?!
Ninajaribu KUWAELEWA akina mh.Ndugai.

Uhalisia ni kuwa humu AFRIKA ,tunapenda sana kukomoana....unaweza ukakataa tu kwa kuongozwa na "hisia".

Tumekuwa na mifano tele ambako VIONGOZI WA SERIKALI walitolewa kafara pale bungeni kwa KUCHANGIWA KUSHAMBULIWA na wanasiasa wa VYAMA VYOTE(mifano ipo).

Humu Afrika ukiweka vipengele vya KATIBA YA KILIBERALI basi ujue hakuna SERIKALI itakayotawala....kila uchao kutakuwa na CHOKOCHOKO na hata mapinduzi.

Yote hayo yanatokana na historia ya MWAFRIKA....kuishi katika UCHIFU....TUNU za kuheshimu na kutukuza WAZEE NA WENYE MAMLAKA.
 
Back
Top Bottom