CHADEMA wanakaribia kukamata Dola-Balozi Lusinde

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Nguli wa siasa nchini na kada mashuhuri wa CCM Balozi Job Lusinde amevunja ukimya na kusema kuna kila dalili kwamba CDM inakaribia kuchaguliwa na wananchi kuongoza dola ya Tanzania.

Mkongwe huyo wa siasa amesema CDM imejipanga vyema na ina uongozi madhubuti unaopanga vyema harakati zake za kisiasa nchini.Balozi Lusinde amesema amekuwa akifurahishwa jinsi CDM inavyotangaza sera zake kwa wananchi kwa kutumia maandamano na mikutano ya hadhara.Amesema CCM inapaswa kukubali kwamba lolote linaweza kutokea katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Kuhusu chama chake cha CCM Balozi huyo ameeleza kusikitishwa na hali ya uhasama ilivyofikia ndani ya chama hicho kufikia wanachama kutaka kuuana kwa bastola kwa uroho wa madaraka akirejea tukio lililotokea hivi karibuni huko Nzega kati ya Hamis Kigwangala na Hussein Bashe.Amesema kiuhalisia sasa CCM imekosa mwelekeo.

Source:Tanzania Daima Uk 6
 
Huo ndio ukweli na wasichojua CCM ni kwamba wanavyotumia vyombo vya usalama especially polisi kuzuia maandamano ya amani kuelekea kwenye mikutano ya CDM ndivyo wanavyowafanya wananchi wazidi kuipenda na kuiweka CDM moyoni kama chama mbadala wa CCM katika chaguzi zijazo.

Chama kitakachowakomboa kutoka katika mikono dharimu ya viongozi wa serikali hii.
 
Huyu Lusinde si ndiye juzi alikuwa anasema chadema bado, leo ndo ameongea hayo???? Au hiyo source yako mkuu Molemo imeongeza munyu?
 
Alichosema ndio ukweli,ila aangalie yule mwanae Livingstone ambaye hakumlea kwa maadili mema asije mshushia mitusi kama kawaida yake akaishia kumlaani akatembea uchi bure Mheshimiwa wa Mtera.
 
Nina imani kuwa serikali yetu SIKIVU ya CCM inayasikia haya yote na kuyafanyia kazi na ndiyo maana wanazidi kuweka uhasama kati yao na wapiga kura kwa kuwaua bila huruma!.
 
Huo ndio ukweli na wasichojua CCM ni kwamba wanavyotumia vyombo vya usalama especially polisi kuzuia maandamano ya amani kuelekea kwenye mikutano ya CDM ndivyo wanavyowafanya wananchi wazidi kuipenda na kuiweka CDM moyoni kama chama mbadala wa CCM katika chaguzi zijazo. Chama kitakachowakomboa kutoka katika mikono dharimu ya viongozi wa serikali hii.

Cdm muache udini na ukaskazini
 
Hata wasiposema wao,kwa hali ilivyo sasa basi mawe yatasema. Hakuna kuraraaa!!!!!
 
Huyu ana uhusiano gani na huyu jamaa (Kilaza)?

images
 
Nguli wa siasa nchini na kada mashuhuri wa CCM Balozi Job Lusinde amevunja ukimya na kusema kuna kila dalili kwamba CDM inakaribia kuchaguliwa na wananchi kuongoza dola ya Tanzania.
Mkongwe huyo wa siasa amesema CDM imejipanga vyema na ina uongozi madhubuti unaopanga vyema harakati zake za kisiasa nchini.Balozi Lusinde amesema amekuwa akifurahishwa jinsi CDM inavyotangaza sera zake kwa wananchi kwa kutumia maandamano na mikutano ya hadhara.Amesema CCM inapaswa kukubali kwamba lolote linaweza kutokea katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Kuhusu chama chake cha CCM Balozi huyo ameeleza kusikitishwa na hali ya uhasama ilivyofikia ndani ya chama hicho kufikia wanachama kutaka kuuana kwa bastola kwa uroho wa madaraka akirejea tukio lililotokea hivi karibuni huko Nzega kati ya Hamis Kigwangala na Hussein Bashe.Amesema kiuhalisia sasa CCM imekosa mwelekeo.

Source:Tanzania Daima Uk 6

Inafurahisha,inatia moyo na nguvu kusikia habari kama hizi zikitoka kinywani mwa kada wa CCM tena wa siku nyingi.Ambassador Job Lusinde amezungumza ukweli ule wa kutoka moyoni.

Ndiyo hali halisi kwamba CDM wamejipanga kushika Dola mwaka 2015 na ndiyo maana CCM mpaka sasa inaweweseka kwa kufuatilia mikutano ya CDM(sangara na M4C) kwa kuipiga mabomu na kuua ili kujaribu kuwatisha Watanzania na kuwashawishi kuwa CDM ni chama chenye vurugu na kisicho na uwezo wa kuongoza nchi jambo ambalo halikubaliki kabisa ndani ya mioyo ya mamilioni ya Watanzania.

CCM hata wangekesha wanatunga mipango ya kuihujumu CDM wajue kuwa wanapoteza nguvu zao bure. Kwa hali ilipofikia sas tayari Watanzania walisha fanya maamuzi ya kuipa CDM ridhaa ya kuwaongoza!
 
Cdm muache udini na ukaskazini

huyu Mzee Balozi Mstaafu ni mtu muhimu sana ndani ya ccm ni trustee wa chama, ni mtu mwenye sauti. Lusinde huyu hana undugu na Lusinde wa matusi aka Kibajaji cha mchina. Lusinde alioona nimehama ccm kwenda CDM aliduwaa sana nadhani sasa ameanzxa kuona kwamba uamuzi wangu ulikuwa sahihi kuja CDM.
Mnaosema chadema ina udini na ukasikazini mna udhaifu mkubwa sana mimi ni wa Dodoma ni CHADEMA, wapo waislam kibao ni CDM wapo wapagani CDM unataka udini na ukabila ili iweje? DHAIFU SIKU ZOTE NI DHAIFU
 
Mzee Lusinde waambie ukweli hao magamba/mabwepande hawakubaliki tena! Hawana ridhaa tena ya wananchi! wana udhaifu kuanzia mbele mpaka nyuma! Nyani haoni kundule! waambie hao magamba!
Achana nao! Amia CDM.
 
Cdm muache udini na ukaskazini

Walioasisi uchochezi huu wameshindwa kwani watanzania siyo wajinga na sasa wameona watumie polisi muuaji na kuendeleza uzalimu

wewe kikaragosi ambaye ujinga na njaa ndivyo vinavyokusumbua naona bado unatunza ujinga katika akili zako ulizopewa na mungu uzitumie madhubuti hapa duniani lakini umeshindwa .... unasikitisha sana ....

this isn't a political trick ..... but it is an old fashioned stupidity
 
Cdm muache udini na ukaskazini

CCM wapingacho ndicho wafanyacho
1. Mawaziri wakuu wa CCM (Mara) - J.k. Nyerere - Kaskazini;
2. Joseph Sinde Warioba (Mara) - Kaskazini;
3. Cleopa Msuya - Kaskazini;
4. Edward Moringe Sokoine (Arusha) - Kaskazini;
5. Fredrick Sumaye (Arusha) - Kaskazini;
6. Edward Lowasa (Arusha) - Kaskazini.

Back
Top Bottom