sixgates
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 3,979
- 1,667
Kapiga marufuku maandamano lakini karuhusu mkutano.
Sasa utaratibu ukoje?? Jee tumsikilize ama tupige andamano..?
Kapiga marufuku maandamano lakini karuhusu mkutano.
na CHADEMA waliwaarika wa nini?
Hata makamu mwenyekiti Arfi hajui CDM ilipotoka,ilipo na inapoelekea1Tatizo la Mtatiro hajui CUF ilipotoka,ilipo na inapoelekea!
umeiweka siku yangu sawa
Ni katika hali ya kutafuta uungwaji mkono wa vyama vingine, ili siku nyingine nao tuwashitaki kwa wananchi kuwa wanaungana na CCM kuwakandamiza watz kama wanashindwa kuungana nasi kuwatetea.
Hili gazeti ni sawa na gazeti la uhuru. Yanaandika habari za upande mmoja hayana maana yeyote.
CUF hiki chama kina gubu sana..kama mwanamke wa kizaramo!
Katika hali ya kushangaza Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro amesema CHADEMA kufanya maandamano na Mkutano Temeke Mwisho ni kuingilia ngome yao.
Akizungumzia mwaliko wa CHADEMA kuitaka CUF kushiriki mapokezi ya wabunge wa upinzani kesho na hatimaye kushiriki mkutano wa pamoja Mtatiro amesema kamwe CUF haiwezi kushirikiana na CHADEMA.
Mtatiro amesema mwaliko wa CHADEMA ni wa kisanii na wamegundua Temeke ni ngome kuu ya CUF kwa hiyo CHADEMA haiwezi kupata watu mkutanoni bila kuishirikisha CUF.Mtatiro ameuliza tangu lini Chadema imegundua CUF siyo CCM B? Mtatiro amelalamika CHADEMA inatafuta umaarufu Temeke kupitia mgongo wa CUF.
Kwa upande wake Chama cha NCCR Mageuzi kupitia Katibu Mkuu Sam Ruhuza kimesema kitashiriki kikamilifu mapokezi hayo kwani CHADEMA siyo adui yao bali adui yao ni CCM tu.
Wabunge wa CHADEMA na NCCR waliungana pamoja bungeni kupinga uonevu,ukandamizaji na udhalilishaji wa Spika wa bunge Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai dhidi ya Upinzani bungeni.Hata hivyo mara zote CUF wamekuwa wakiungana na wabunge wa CCM kuwapinga wapinzani wenzao.
Kesho Jumapili CHADEMA imepanga mapokezi makubwa na maandamano kisha mkutano mkubwa wa hadhara Temeke Mwisho kwa lengo la kulaani ukandamizaji wa Spika na Naibu wake.
Source:Tanzania daima/Nipashe.
Mbona kule bungeni haya mlikuwa hamyaoni uwaziri kivuli shida kwa CUF wakati wao wanaongoza pale bungeni waliwapa unaibu wacheni unafiki
Ni katika hali ya kutafuta uungwaji mkono wa vyama vingine, ili siku nyingine nao tuwashitaki kwa wananchi kuwa wanaungana na CCM kuwakandamiza watz kama wanashindwa kuungana nasi kuwatetea.
For what, msimamo wa CUF siunaeleweka jamani?
Imenikumbusha kuwa mwanzoni Sir Elton John alikuwa anakana yeye siyo shoga, hadi baadae sana.Hongera Mtatiro kwa kukiri hili...
Mkuu kwanini unasema hivyo ?Hata makamu mwenyekiti Arfi hajui CDM ilipotoka,ilipo na inapoelekea1
Ni kweli mkuu, lakini wananch wa CUF ni watz kama tulivyo sisi, na kumbuka, kilichoungana na ccm zanzibar ni chama na siyo wanachama, kuna wanaCUF hawapendi kabisa kilichotokea Zenji, ndio maana tunajaribu kuwatafuta na kuwarudisha kwenye mstari. Watarudi tu, we utaona kama wanaCUF hawahudhuria huo mkutano.
Tuko unapindisha maana ya maneno ya Mtatiro kwa makusudi. Walichotaka kufanya CDM ni kuitumia CUF kwa maslahi yake. Ni marangapi tumesikia wafuasi wa CDM na viongozi wao wakiita CUF CCM B bila ya justification yoyote?
Justification ipi zaidi ya hii ya kupinga kupingwa kwa CCM?
Kwa ushahidi upi?
Hivi CCM inaelekea wapi??Hata makamu mwenyekiti Arfi hajui CDM ilipotoka,ilipo na inapoelekea1
Wa matamshi ya Mtatiro...
Chadema waitumie CUF? huijui Chadema nini!!Tuko Walichotaka kufanya CDM ni kuitumia CUF kwa maslahi yake. Ni marangapi tumesikia wafuasi wa CDM na viongozi wao wakiita CUF CCM B bila ya justification yoyote?