CHADEMA wanaingilia Ngome ya CUF - Mtatiro

CHADEMA wanaingilia Ngome ya CUF - Mtatiro

Dr Slaa amekuwa mbunge wa Karatu 1995 to 2005: ni sawa na miaka 15 na 2010 akagombea urais, vile vile 2015 ndiye mgomea wenu! Inakua miaka mingapi kwenye uongozi? 25 years, is it too much for him? Au CHADEMA haina hazina ya wsomi kushika hizo nafasi kwa vipindi vyote hivyo? Au DR ni mgombea wa kudumu na yeye?

Maalim Seif amekuwa waziri Kiongozi kwa muda gani?? pamoja na kuwa Waziri kiongozi mhaini kwa muda mrefu bado amekuwa ndo mgombea pekee wa urais kupitia CUF tokea 1995 hadi mlipoamua kufunga ndoa na maccm ili tu apate ving'ora vya kumsindikiza kama enzi zile za uwaziri kiongozi Hachokiiii?? ina maana CUF huko Zenji ni Maalim peke yake??? Hivi bado anaamini atakuja kuwa Rais wa zenji, kama bado namshauri afute kabisa mawazo hayo, awaachie na wengine wajaribu, 20 yrs ya ugombea + >15 yrs ya uwaziri kiongozi inamtosha, ameshachuja. Lipumba naye kujiita mlima K'njaro wakati hata urefu wa kichuguu hajaufikia ni pumba tu, yule hata akigombea udiwani kule kwao TB hataambulia kitu, arudi chuo akafundishe, huko ndo kunamfaa, siasa zimeshamuweka kando.
 
Msameeni bure,nadhani alitaka kusema makunduchi,simnaelewa hawa jamaa wanadhani huku ni zanziba,kwahiyo waacheni tu,unajua mara nyingi ukibishana na chiz............
 
Siku hizi nimekuwa mvivu wa kufuatilia vyombo vya habari mambo mengi yananipita, kumbe MTEMVU amehamia CUF na akagombea ubunge?
 
Kama kuna utaratibu wa upinzani kushirikiana utangazwe hadharani, haiwezekani chadema iibuke ghafla na kujaribu kutudanganya ATI Leo wanaitaka CUF, si jambo jepesi, linahitaji mchakato, miezi kadhaa iliyopita nilimsikiliza Mbowe na SLAA wakihutubia mikutano kadhaa Mtwara, kila mmoja kwa wakati wake aliwataka wananchi waachane na CUF kwa sababu siyo chama cha upinzani na ni wasaliti. Katika Hali kama hiyo Leo wanatakaje kuandamana na wasaliti. I think CUF wana "aseti" ya muda mrefu. Mtatiro atawasaidia sana, ana msimamo na hayumbishwi, ndiyo maana chadema kila siku mnapambana eti atoke CUF aje kwenu. Akiendelea na msimamo wake atakuja kuwa kiongozi mkubwa zaidi ya halo, and infact in CUF, he is the only vibrant and consistent youth. Mtatiro usiyumbe, usifanye kazi kwa matakwa ya chadema, songs mbele.

Kweli upofu sio wa macho tu,.. ni pamoja na akili nimejaribu kusoma post yako taratiiiiibu na kwa umakini mkubwa lakini ninachokiona hapa ni chuki, hofu, hila,njama chafu za kuichafua chadema isiyoweza chafuka na majungu na mipasho vile,....sasa ninachokiona hapa wewe huenda unalindugu au kandugu kapo kwenye mfumo na wewe ni kiwete nadhani huwezi endesha maisha bila huyo mtu ambaye ananufaika na mfumo wa kuwa mporaji wa rasirimali za watanzania kwa kuwa CCM A au CCM B,....pole naomba usubiri kesho utaona uungwaji mkono kwa CHADEMA kama utakuwa hai urudi jamvini uniambie,...wewe Gamba dogo au Gamba B dogo a.k.a KIWETE
 
Temeke ngome ya CUF? Kama TEMEKE ni ngome ya CUF basi wanajaribu kutuonyesha namna chama hicho kilivyojichokea na kubaki skeleton tu.
Point ya mtatiro ninayoiunga mkono ni hiyo "tangu lini CDM wameacha kuwaona wao CUF kuwa ni CCM B?".
Hapo CDM walichemka na mtatiro yupo sahihi.
 
Wala simsafishi Mtatiro, na mara nyingi nimewahi kumkosoa kama navyowakosoa viongozi wengine wa vyama vya siasa. Katika hili chadema wamechemka, wamezoea vya kunyonga, hebu chadema ijipange zaidi, jana ninasikia kwenye maspika yao ya matangazo wakinadi eti Lipumba atakuwepo....mbatia atakuwepo....SLAA atakuwepo....mbowe atakuwepo....zitto atakuwepo...Mtatiro atakuwepo....mnyika atakuwepo.....kumbe hawajawashirikisha wenzao. Huu ni unafiki mkubwa sana. Narudia tena, chadema watengeneze upinzani imara kwa njia sahihi, siyo kama vibaka.


Blaza naona unatumia nguvu nyingi kuongea pumba, cdm imewashika pabaya.

Umeniboa ulipoingiza mambo ya kuuwa watu, we wauwaji huwajui? Ngoja nikuache usiniharibie siku.
 
Kama kufanya siasa kungekuwa na mipaka basi kusingekuwa na chama tawala na vya upinzani kwani wapinzani wangekosa pa kuanzia hapa Tz maana enzi za chama kimoja kingedai nchi nzima ni ngome yake. Afadhali Ntatiro aliposhauriwa kwenda CHADEMA alikataa maana angekuwa MZIGO kwa CDM.
 
Ngome kivipi?hivi cuf wana madiwani wangapi huko temeke?hivi ana wabunge wangapi?ni kipimo gani cha uungwaji mkono kama sio kuwa na wabungena madiwani?kama huna nini kinakusukuma kuwaza kuwa temeke ni ngome yako?huo ni ushirikina.
 
Katika hali ya kushangaza Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro amesema CHADEMA kufanya maandamano na Mkutano Temeke Mwisho ni kuingilia ngome yao.

Akizungumzia mwaliko wa CHADEMA kuitaka CUF kushiriki mapokezi ya wabunge wa upinzani kesho na hatimaye kushiriki mkutano wa pamoja Mtatiro amesema kamwe CUF haiwezi kushirikiana na CHADEMA.



Mtatiro amesema mwaliko wa CHADEMA ni wa kisanii na wamegundua Temeke ni ngome kuu ya CUF kwa hiyo CHADEMA haiwezi kupata watu mkutanoni bila kuishirikisha CUF.Mtatiro ameuliza tangu lini Chadema imegundua CUF siyo CCM B? Mtatiro amelalamika CHADEMA inatafuta umaarufu Temeke kupitia mgongo wa CUF.

Kwa upande wake Chama cha NCCR Mageuzi kupitia Katibu Mkuu Sam Ruhuza kimesema kitashiriki kikamilifu mapokezi hayo kwani CHADEMA siyo adui yao bali adui yao ni CCM tu.

Wabunge wa CHADEMA na NCCR waliungana pamoja bungeni kupinga uonevu,ukandamizaji na udhalilishaji wa Spika wa bunge Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai dhidi ya Upinzani bungeni.Hata hivyo mara zote CUF wamekuwa wakiungana na wabunge wa CCM kuwapinga wapinzani wenzao.

Kesho Jumapili CHADEMA imepanga mapokezi makubwa na maandamano kisha mkutano mkubwa wa hadhara Temeke Mwisho kwa lengo la kulaani ukandamizaji wa Spika na Naibu wake.

Source:Tanzania daima/Nipashe.

Hapa ndipo CUF wamedhihirisha kuwa wao ni CCM B.
 
hayaaa Mtatiro hayawi hayawi yamekuwa Temeke ni ya watu wote, hata CCM imejijenga sana kinondoni mali nyingi ziko kinondoni lakini CHADEMA iko mita mia tatu kutoka ofisi zao.
 
Bila shaka mtatiro atakuwepo kwenye mkutano temeke hana jinsi maana alitegemea polisi watazuia hiyo shughuli
 
Mtatiro acha siasa huiwezi unalazimisha kachunge ngombe tu Tarime,kama ndio imekuweka Dar basi si muda mrefu utaumbuka ndugu
 
Naona imekuchanganya! Tunazungumzia uongozi, kwani uwakilishi sio uongozi? Kwa kifupi Mwita Maranya anataka kutwambia kutwambia kwamba CHADEMA kuna ukomo wa kugombea uongozi. Kama unajua tuambie ni vipindi vingapi maana Dr Slaa isingekuwa kukubaliwa matakwa yake ya kulipwa milioni saba kwa mwezi bado angeendelea kuwa mbunge wa Karatu. Huyu kwa ulafi wa madaraka anaonekana kiboko, hana uzalendo anawakilisha wananchi kwa pesa.
naona mnahama kwenye mjadala.
 
Mtatiro anapoteza nafasi nzuri sana ya wapinzani kuungana
 
Teh teh sehemu hauna hata mbunge unaita ngome yako....nimeamini CUF ni CCM B kwa sababu mbunge wa Temeke ni CCM halafu CUF wanasema ni ngome yao....Think big!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom