CHADEMA wamlipua Kikwete Bungeni

Hawa watu Nape anawatoa wapi ?? milembe au??

Yaaan watu hajui hata taratibu za kutunga sheria! hata elimu ya urai ya dalasa la tano hawajapata?

Ulishaona wapi mada ikapelekwa bungeni kujadiliwa imsha sihinwa na Rais, hiyo inakuwa sio mada/rasimu tena inakuwa ni sheria.

Kiutaratibu inatakiwa ijadiriwe bungeni, ikishapitishwa na bunge ndio inahisiniwa na rais kuwa sheria/kanuni.

Lkn...Rais na wasaidiz wake ...mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh!

Tutafika kweli..? kwa mwendo huu wa kuvunja vunja kanuni na taratibu??

This is shame!
 
Hii inadhihilisha ya kua Jk na serikali yake wanafanya mambo kwa mazoea na kwa masilahi Yao binafsi.Huo mpango hauna lengo la mumsahidia mlalahoi Bali ni mlango mwingine wa kupitishia pesa kwa manufaa ya Mafisadi (Jk na Viongozi wa serikali yake na CCM .Jambo la pili mango huu ni chambo ya kutega misaada ya wafadhili ndiomaana umeandikwa kiingereza.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mlitaka alete bungeni bila kusaini hoja yake? Mnanshangaza!
Unashangaa nini hapa ndugu Mtanzania mwenzangu, hivi kweli kwa uelewa wako Rais azindue mpango kukiwa na timu yake ya wataalamu waliobobea halafu mpango huo ndiyo utolewe maoni?

Nilifikiri kiustaarabu ni kwanza ujadiliwe, uboreshwe na hatimaye mkuu wa nchi asaini ili kuanzisha rasmi kutumika kwake. Lakini nikupongeze yawezekana utaratibu huu ndiyo uliozoeleka kwako. Tuchukulie mfano wa utungaji wa sheria kwamba Bunge letu likishapitisha ndipo Rais husaini ikiwezekana kwa mbwembwe na sherehe, labda kama ni rasimu ya mpango ndiyo aliyoizindua hiyo haina shaka.
 
Bora aliisha saini kwani alijua CDM hawana jipya na ni wachache bungeni hawana lakufanya. Andaeni basi maandamano juu ya hilo

Alisaini kwa sababu hajui katiba inasema nini, mkulu asiyesoma anaumbuka mbele ya wabunge alert. Mwaka huu CCM kazi mnayo!
 
Welevu si kusikika au kuonekana unafanya juhudi bali ni kufanikisha na kuepuka kufanya mambo ambayo mchango wako unakutenga na uelevu. Mpango huu bungeni umewasilishwa ili ukafanyiwe nini?

Tunajua anayewasilisha ni serikali ambaye mkuu wake ni Rais. Lakini inapotokea ameshukuru wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bunge kwa mchango wake nini kusudio lake? Kuwaziba midomo ili wapitishe bila kujadili, na kama anawashukuru kwa mchango wao anawapelekea wakafanye kitu gani. Na ikitokea wakarudisha serikalini kwa marekebisho. Mapenzi ya kisiasa yanakuziba jicho moja na uelevu.

Tunakupenda na tunapenda kuendelea kuwa na wewe jamii forums lakini tunakuomba uitendee haki jamii forum.


Thanks Mkuu. Busara ulizomwaga hapa ni za kiwango cha juu. Natumaini kwamba dada ana upeo wa kutosha kukuelewa- labda aamue tu kufanya makusudi!
 
Uwa naamini tunaongozwa na wajinga na bado nitaendelea kuamini hivyo mpaka watakapo onyesha kwa vitendo kuwa wao si wajinga hata kidogo, kuanzia watendaji wetu, watawala na wabunge wa kupiga makofi na kusinzia Bungeni.

Huwezi kutengeneza mpango bila kushirikisha wananchni ikatekelezeka hata siku moja haijawai kutokea Duniani na haitawai kutokea hata siku moja maana huo ndio msingi mkuu wa elimu ya mipango ya maendeleo labda kama ni mipango ya kivita na kijasusi.

Mipango yote iliyowai kupangwa huko nyuma hapa Tanzania ili shindwa kwasababu kuu ya kuto kushirikisha wananchni wakati wa kuandaa mipango na mikakati yake. Sasa kama hata Bunge haikushirikishwa hiyo mipango itatekelezwa wapi na itatekerezwa na nani?!
 
Rais Kikwete ni Rais makini sana hivyo hawezi kulishukuru Bunge na wadau wengine bila Bunge na wadau hao kushiriki kwenye mchakato.

Kwanini mnataka kuturudisha nyuma? Evi mmesahau kuwa wakati bunge letu likishiriki kwenye mchakato nyie mlikuwa kwenmye maandamano? au mlifikiri kuwa Bunge litawasubiri mrudi kwenye maandano yenu ya kiuchochezi? si hivyo kaka, bunge lina taratibu zake.Msianze kumlaumu Rais wakati huo nyie ndie wenye makosa.

Tekeleza wajibu, dai haki yako na huo ndio utaratibu kaka.
 
magamba jibuni hoja, msiwe vilaza kama... anasaini asichokifahamu
 
islam12.jpg

Hivi ni mahakama ipi tukianzisha ndo tutakua na huu mtindo? Nimesahau ...
 
Atachapwa hamsa ishirini and then .................. atawajibu wabongo swali moja baada ya lingine
islam12.jpg
 
sasa rais alilishukuru bunge lipi kwa mchango wao katika huo mpango wa 5yr kama kitu hakikua kimeshapita kupata inputs za hao wabunge, jamani hivi tunapelekana wapi? ndio maana mambo ni hovyo hovyo.
 
Mlitaka alete bungeni bila kusaini hoja yake? Mnanshangaza!
Watu kama hawa wa CCM wakiongozwa na Nape wananipa burudani sana kwani kwa mtindo waliouanzisha wanarahisisha sana kazi ya nguvu ya uma kuwang'oa mapema sana.

Wazalendo wanaongelea mambo makubwa ya msingi kwa maslahi ya Taifa, ambayo bila hivyo ndio imetufikisha hapa tulipo, nchi inaendeshwa hovyo hovyo bila kufuata sheria wala taratibu zilizowekwa, halafu wanakuja watu waliofilisika kifikra na uchovu wa akili na siasa zilizopitwa na wakati za kutetea chochote kinachopitia kwenye chama chao kichovu cha ccm.

Hakika CCM imefikia ukingoni, mkubali msikubali, hoja zenu zinadhihirisha, mnaweweseka tu hata kwa mambo ambayo yako wazi.

Hivi sasa slogan yenu ndio inatambulika vizuri - 'MAISHA BORA KWA KILA FISADI'.
 
Hapa hakuna mpango wowote, hizi ni dalili za kukurupuka, yaani mkuu amejifungia na wataalam wake sasa kaja na mpango wa miaka 5, ameshasign yaani tayari kwa kutekelezwa then analeta bunge lijadili nini!? utekelezaji!? ama.

Haya ndiyo mambo yanayorudisha nyuma taifa hili watu wanakurupuka wanakuja na mipango ya kuwarubuni wananchi ili wawape tena Dolla katika chaguzi zinazofuata, lakini safari hii wamekwama maana wana wa nchi sasa hawadanganyiki na wamesha fumbua macho, maana tulisikia oo mkurabuta, mara Mkukuta lakini yote kiini macho tu sasa inakuja Mpango wa kuinua uchumi, uchumi gani wewe wakati raslimali za nchi mnagawia watu!? Wizi tu!

Jama Ndugu zangu watanzania tuamke hapa hakuna mpango wala nini, mpango ni kuiondoa ccm kwenye madaraka tu, huo ndio mpango utakaoinua uchumi wa nchi yetu.
 
Mlitaka alete bungeni bila kusaini hoja yake? Mnanshangaza!
Kumbe Kweeli Bunge ni rubber stamp tu???!!!
Shame on you and the Government of Magamba!!!
Shame upon anybody marginalizing the poor Tanzanians at the expense of stupid rulers!
Now Tanzanians we are getting marginalized! what do we do?! Do we need the MPs anyway ?If this is the practice!!
Shaaammmmmmeeeeeeeeeeee!!!
 
Back
Top Bottom