Mkuu Mungi mbona Chadema mnatoka povu? umaarufu wa Zitto upo na utakuwepo kwani michango yake kisiasa imegusa mioyo ya watanzania na itabaki kuwa hivyo katika historia yetu.Kwahiyo hata Dr Slaa anaposema kuna ufisadi sehemu tuanze kuamini anafanya vile kutafuta umaarufu?
Wakati wowote ule, sijapata kuelewa Wanasiasa humaanisha nini kwa maneno "Masilahi ya Umma"? Kuna kila haja ya kupata tafsiri ya Kikatiba ya maneno haya ili kuepusha mkanganyiko katika matumizi yake.
Maswali:
- Iwapo siku ya PAC kuwahoji Makatibu Wakuu Dr.W.Slaa atakuwa na udhuru wa kushindwa kuhudhuria, ni nani ndani ya CHADEMA anapaswa kumwakilisha?
- Na, Je kwenye Jopo la kumuhoji mwakilishi wa CHADEMA Zitto atasimama kwa kofia ipi? Hakuna mgongano au mgogoro katika vyeo vyake dhidi ya azma iliyo mbele yake?
Mpango mfu wa ccm na kibaraka wao unapikufa huku wakiona
Nitakujibu swali No.1
Mara zote Dr.anaposafiri au kuwa nje ya Ofisi John Mnyika ndiye hua anakaimishwa, ingawa kiprotokali Zitto ndiye anayepaswa kukaimu nafasi ile Hapo usiniulize kwanini maana mi pia sijui ila kuna uzi flani hivi wa @Election Observer una kichwa habari "Ugaidi ndani ya Vyama vya siasa " unaweza kuunganisha dots
Kakuambia tayari yeye ni maarufu hiyo attention itamsaidia nini? Sema kijana anatishia ulaji wa wanasaccoss wenu wa chadema.
Mpango mfu wa ccm na kibaraka wao unapikufa huku wakiona
Facts should be kept at a public disposal son,it is not for Zitto to know,it is for the public to get rid of the suspi cion at this particular moment and for the party to comply!!!!!!
Kamati ndio inataka mkuu sio ZZK jamani kwa nini analaumiwa yeye binafsi,vipi kama aliwaambia kamati kuwa cdm imekaguliwa na kamati ikasema wana mashaka na ukaguzi hivyo zoezi lirudiwe kwa vyama husika sasa hapo yeye asemaje?????!!!
Hivi kama wewe ni mfanyabiashara na TRA wanadai haukupeleka estimates za kodi kwa mwaka huo,nini unafanya???!!! Si unaambatanisha barua,makadirio na barua waliyokuandikia inayotamka makadirio kutka kwao,au unaitisha mkutano na wanahabari?????!!!!!
Au point yako ni kuwa alitakiwa awatonye kuwa kamati itakisanua,au alitakiwa afanyaje sasa????!!!
Mpango mfu wa ccm na kibaraka wao unapikufa huku wakiona
Acha kuota wewe bwana mkubwa. Nape hana ubavu wa kuniajili mimi wacha kujishtukia kwasababu ya viloba unavyohongwa.
Huyo ZZK mwenyewe maneno mengi, ninachojua huwa kuna utaratibu wa kutoa notification kwa jambo au limecheleweshwa au halikufanywa kabisa, sasa unataka kusema POAC wametoa notification yoyote ikashindikana hadi wakaamua kuibroadcast hii habari? Mbona kuna dalili kuwa kuna jambo! Na itakuwa ana maana gani kusema 4yrs wakati ni mwaka mmoja tu tena ambao bado haujaisha? Pamoja na kuwa mwaka wa serikali unaishia July, angeuliza si angepewa maelezo kwa nini imechelewa? Hapa mchezo unaweza kuwa wa kuchuja hadi anabaki yule uliyekuwa unamtafuta. Kumbe kuna ambao hawajawahi kupeleka
na wala hawatajwi sana, ZZK anataka kusema ameilenga CCM au CDM? Ngoja tuone mwisho wa mziki utakuwaje
Nikweli mkuu facts should be kept at public disposal, lakini kwa mtazamo wangu PAC ingekutana na vyama vya siasa, msajili wa vyama vya siasa pamoja na CAG, baada ya hapo kama ingegundulika hawajafanya kama sheria inavyo wataka basi PAC inge utaarifu Umma, lakini kwanini haikuwa hivyo?
Zito anakoelekea atasababisha sheria ibadilishwe ili kiongozi wa kamati ya hesabu za serikali isiwe lazima atoke upinzani. Nahisi hapa kuna watu wamemtuma ili aanze kuropoka baadae ionekane hii kamati ipo kimajungu na sheria ibadilishwe.
Mtaniambia mbele ya safari.
Nafikiri hujamuelewa; ameuliza swali la msingi.. Jukumu la kukagua au kuhakikisha zimekaguliwa ni la CAG au Chama husika (in this case CDM)..? Kama ni la CAG, je, walifanya kazi yao ya kwenda kukagua au walienda kukagua wakanyimwa access to the required information (i.e. limitation of scope).? Kama ni jukumu la chama, je, walimu-engage independent auditor kukagua hesabu zao na wao kuziwasilisha kwa msajili.? If chama walikaguliwa kwa madai ya Komu na hesabu kaguliwa (audited accounts) zikawa submitted to the right authorities as required; then hakuna cha ku-discuss here..!!