CHADEMA wamjibu Waziri Kangi Lugola kuhusu shambulio la Tundu Lissu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,251
2,000

"Waziri Lugola anasema eneo analokaa Tundu Lissu halina ulinzi wa askari polisi, ni wa kampuni binafsi, sasa Waziri Lugola kama anataka aaminike kwa kauli zake, atuambie wamechukua hatua gani kwa hiyo kampuni?" Benson Kigaila.

"Kama Serikali haijui aliyefanya tukio la kumshambulia Lissu na Spika anawaambia wabunge Dodoma iko salama anajuaje Dodoma iko salama kama hawamjui aliyemshambulia Lissu?" Benson Kigaila - Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema.

"Anachotaka kutuambia Waziri Lugola ni kwamba uchunguzi wa matukio kama haya haufanyiki mpaka waathirika wa matukio hayo warudi, mbona kuna waliorudi na hatujaambiwa majibu ya uchunguzi wao" Benson Kigaila - Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema.

"Kama msimamo wa jeshi la polisi ni hadi waathirika warudi ndio wachunguze, wapo waliorudi mfano MO Dewji na Roma Mkatoliki, je wameshachunguza na kujua waliowateka? Kangi Lugola anatuaminisha kuwa Ben Saa nane na Azory kesi zao haziwezi kupelelezwa kwa kuwa hawapo"Benson Kigaila

"Kazi ya kuchunguza, kukamata na kupeleka mahakamani ni kazi ya Jamhuri kupitia jeshi la polisi, muathirika yeye atakwenda mahakamani kama shahidi namba moja, wao wanatuambia Lisu aje ndio uchunguzi ufanyike" Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA

"Ni kazi ya jeshi la polisi kuchunguza tukio la uhalifu bila kujali waathirika wa tukio wapo ama hawapo, Lissu hawezi kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi kwenye kesi yake" Benson Kigaila, Mkurugenzi wa mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA

"RPC wa Dodoma alisema wamekamata Nissan nyeupe 8, lakini hawakutaja majina ya wamiliki wa magari hayo na hatimaye yakatokomea gizani. Kwanini hili swala na uchunguzi wake linakuwa na kinga ya serikali? Kwanini serikali inatoa majibu badala ya watuhumiwa?" Benson Kigaila

"Abdallah Zombe na wenzake walikamatwa kwa kutuhumiwa kuwua wafanyabiashara wa madini wa Morogoro, watuhumiwa wenzake na Zombe walihukumiwa bila ya wafanyabiashara hao kufufuliwa, Kangi Lugola anataka kutuaminisha kuwa Lisu angekufa na upelelezi usingefanyika?" Benson Kigaila

"Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba alisema Toyota Premio iliyokuwa ikimfatilia Tundu Lisu walichunguza na kugundua iko Arusha na haikuwahi kufika Dar, sisi tunahoji polisi wana kifaa gani cha kugundua kuwa gari hii haijawahi kufika Dodoma au Mbeya"Benson Kigaila

"Swala la Tundu Lisu lipo mikononi mwa serikali, wanatakiwa wachunguze na watupe majibu, serikali inatakiwa kuchunguza suala hili na si kujivua, serikali ichunguze na uwezo huo wanao kama hawana waombe usaidizi kwa vyombo vya uchunguzi vya kimataifa, tushasema hilo"Benson Kigaila

"Tundu Lissu anasema mambo ya kweli ambayo yametokea Tanzania, sasa hayo mambo ya kweli kama yanachafua mtu, nchi au serikali basi ni wao wanayoyatenda ndio wanachafua nchi na si Lissu" Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni- CHADEMA

"Kama Serikali ingetaka kufanya uchunguzi,kuna kitu kinaitwa ballistic analysis,polisi walichukua maganda ya risasi,unaweza kujua ni aina gani ya silaha iliyotumika utajua batch no. imetengenezwa nchi gani na iliingia mwaka gani nchini,ililetwa na serikali au mtu binafsi" Kigaila
 
MSN TZ

Member
Feb 13, 2019
10
45
Mimi nadhani sio sahihi kwa kila jambo Chadema kukurupuka na kuijibu CCM......Lugola ni CCM....na hawezi isaliti kambi yake na serikali anayoiongoza!

Lengo la Chadema kama chama pinzani wawe na sera madhubuti za kuweza kuishawisha jumuiya ya watanzania na hatimae kuwapa ridhaa ya kushika dola.

Kujipanga kimikakati ni muhimu zaidi kuliko kelele zisizo na mashiko.

Nichelee tu kusema..endapo CDM hawatobadilika basi itakuwa ni ndoto kwa wao kuweza kuiongoza nchi hii ya Tanzania.

NB: Siasa ni mikakati na sio kubwabwaja pasipo kuwa na malengo mahususi.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,124
2,000
Ukitaka kuwavuruga chadema waambie wamtoe dereva wa Lissu
Wasanii hawa,huyo mkuu wa kikosi cha utesaji viongozi kigaila,angefanya la maana sana kama angetangaza kumtoa dereva ili ahojiwe
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,280
2,000
Mimi nadhani sio sahihi kwa kila jambo Chadema kukurupuka na kuijibu CCM......Lugola ni CCM....na hawezi isaliti kambi yake na serikali anayoiongoza!

Lengo la Chadema kama chama pinzani wawe na sera madhubuti za kuweza kuishawisha jumuiya ya watanzania na hatimae kuwapa ridhaa ya kushika dola.

Kujipanga kimikakati ni muhimu zaidi kuliko kelele zisizo na mashiko.

Nichelee tu kusema..endapo CDM hawatobadilika basi itakuwa ni ndoto kwa wao kuweza kuiongoza nchi hii ya Tanzania.
Hivi Kuna watanzania bado wana akili Kama za huyu jamaa

NB: Siasa ni mikakati na sio kubwabwaja pasipo kuwa na malengo mahususi.
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,280
2,000
Hivi Kuna watanzania bado wana akili Kama za huyu jamaa
Mimi nadhani sio sahihi kwa kila jambo Chadema kukurupuka na kuijibu CCM......Lugola ni CCM....na hawezi isaliti kambi yake na serikali anayoiongoza!

Lengo la Chadema kama chama pinzani wawe na sera madhubuti za kuweza kuishawisha jumuiya ya watanzania na hatimae kuwapa ridhaa ya kushika dola.

Kujipanga kimikakati ni muhimu zaidi kuliko kelele zisizo na mashiko.

Nichelee tu kusema..endapo CDM hawatobadilika basi itakuwa ni ndoto kwa wao kuweza kuiongoza nchi hii ya Tanzania.

NB: Siasa ni mikakati na sio kubwabwaja pasipo kuwa na malengo mahususi.
 
MSN TZ

Member
Feb 13, 2019
10
45
Kwani ni chadema wamejibu au ni Lugola aliwajibu kuhusu tuhuma za mpango wa mauwaji ya Lissu?
sasa kama amewajibu si wakae kimyaa....waridhike na hilo jibu sio kila kitu unabisha.

unajua karibu watanzania wote wenye akili wanajua ni nani mhusika mkuu wa issue ya Lisu.....hata wewe na mimi, na hata Lugola mwenyewe anajua ukweli. Lakini cha msingi cha kufahamu ni kuwa hata siku moja serikali haitokuja kukiri kuwa ile kitu ilikuwa ni maagizo ya mzee baba.

Hivyo kuepusha mijadala isiyo na tija, ni vema tu tukamuachia Mungu awajibu wanafiki....kama alivyoamua ku-mbeeep jana...ndugu yetu lameck madelu wa kwa Nchemba.

ni hayo tu ndugu yangu, but tupo pamoja .
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,280
2,000
Pima IQ yako kwanza kabla ya kuwa unaleta mijadala humu...haya mambo nenda simuliana na babu yako koridoni sio kwa watu waelevu unatuletea pumba hizi
sasa kama amewajibu si wakae kimyaa....waridhike na hilo jibu sio kila kitu unabisha.

unajua karibu watanzania wote wenye akili wanajua ni nani mhusika mkuu wa issue ya Lisu.....hata wewe na mimi, na hata Lugola mwenyewe anajua ukweli. Lakini cha msingi cha kufahamu ni kuwa hata siku moja serikali haitokuja kukiri kuwa ile kitu ilikuwa ni maagizo ya mzee baba.

Hivyo kuepusha mijadala isiyo na tija, ni vema tu tukamuachia Mungu awajibu wanafiki....kama alivyoamua ku-mbeeep jana...ndugu yetu lameck madelu wa kwa Nchemba.

ni hayo tu ndugu yangu, but tupo pamoja .
 
MSN TZ

Member
Feb 13, 2019
10
45
Hivi Kuna watanzania bado wana akili Kama za huyu jamaa
Ni kheri ya wewe mwenzangu mwenye akili nyingi kuliko wengine wote.

Ndugu yangu naomba unisome between the lines......Ni hivi, ishu ya TL kupigwa risasi umma wote wa watanzania na mataifa ya nje wanajua mhusika mkuu ...or suspect no.1 ni Mzee baba......FULl STOP!

lakini pamoja na ukweli huo hapo juu kutokuwa disclosed na kamwe hautokuwa disclosed......hasa kwa uongozi wa huyu mzee baba, ni vema sasa Chadema wakachukua muda kujipanga kimikakati ili kujiimairisha na hatimaye wananchi kuwaelewa ili waweze kushika dola.

Ukijua weakness ya adui yako ni vema kutumia hiyo nafasi kuandaa strategy ili kummaliza. hivyo nilichomaanisha ni kuwa CDM watumie hii nafasi vizuri na sio kupiga kelele zisizo na tija.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,745
2,000
Mimi nadhani sio sahihi kwa kila jambo Chadema kukurupuka na kuijibu CCM......Lugola ni CCM....na hawezi isaliti kambi yake na serikali anayoiongoza!

Lengo la Chadema kama chama pinzani wawe na sera madhubuti za kuweza kuishawisha jumuiya ya watanzania na hatimae kuwapa ridhaa ya kushika dola.

Kujipanga kimikakati ni muhimu zaidi kuliko kelele zisizo na mashiko.

Nichelee tu kusema..endapo CDM hawatobadilika basi itakuwa ni ndoto kwa wao kuweza kuiongoza nchi hii ya Tanzania.

NB: Siasa ni mikakati na sio kubwabwaja pasipo kuwa na malengo mahususi.
Kama wanachofanya cdm kuijibu ccm ni kubwabwaja na hawawezi kupata nafasi ya kuongoza nchi, iweje ccm inayobwabwaja iwe madarakani? Hayo majibu ni sahihi na kuweka rekodi sawa. Ni wendawazimu kukaa kimya upotoshaji ukifanyika kisha utegemee kwenda kuongea na wananchi ambao madaraka ya rais yanatumika kuzuia wananchi kusogelewa na cdm.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom