Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
"Waziri Lugola anasema eneo analokaa Tundu Lissu halina ulinzi wa askari polisi, ni wa kampuni binafsi, sasa Waziri Lugola kama anataka aaminike kwa kauli zake, atuambie wamechukua hatua gani kwa hiyo kampuni?" Benson Kigaila.
"Kama Serikali haijui aliyefanya tukio la kumshambulia Lissu na Spika anawaambia wabunge Dodoma iko salama anajuaje Dodoma iko salama kama hawamjui aliyemshambulia Lissu?" Benson Kigaila - Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema.
"Anachotaka kutuambia Waziri Lugola ni kwamba uchunguzi wa matukio kama haya haufanyiki mpaka waathirika wa matukio hayo warudi, mbona kuna waliorudi na hatujaambiwa majibu ya uchunguzi wao" Benson Kigaila - Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema.
"Kama msimamo wa jeshi la polisi ni hadi waathirika warudi ndio wachunguze, wapo waliorudi mfano MO Dewji na Roma Mkatoliki, je wameshachunguza na kujua waliowateka? Kangi Lugola anatuaminisha kuwa Ben Saa nane na Azory kesi zao haziwezi kupelelezwa kwa kuwa hawapo"Benson Kigaila
"Kazi ya kuchunguza, kukamata na kupeleka mahakamani ni kazi ya Jamhuri kupitia jeshi la polisi, muathirika yeye atakwenda mahakamani kama shahidi namba moja, wao wanatuambia Lisu aje ndio uchunguzi ufanyike" Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA
"Ni kazi ya jeshi la polisi kuchunguza tukio la uhalifu bila kujali waathirika wa tukio wapo ama hawapo, Lissu hawezi kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi kwenye kesi yake" Benson Kigaila, Mkurugenzi wa mafunzo na Oganaizesheni wa CHADEMA
"RPC wa Dodoma alisema wamekamata Nissan nyeupe 8, lakini hawakutaja majina ya wamiliki wa magari hayo na hatimaye yakatokomea gizani. Kwanini hili swala na uchunguzi wake linakuwa na kinga ya serikali? Kwanini serikali inatoa majibu badala ya watuhumiwa?" Benson Kigaila
"Abdallah Zombe na wenzake walikamatwa kwa kutuhumiwa kuwua wafanyabiashara wa madini wa Morogoro, watuhumiwa wenzake na Zombe walihukumiwa bila ya wafanyabiashara hao kufufuliwa, Kangi Lugola anataka kutuaminisha kuwa Lisu angekufa na upelelezi usingefanyika?" Benson Kigaila
"Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba alisema Toyota Premio iliyokuwa ikimfatilia Tundu Lisu walichunguza na kugundua iko Arusha na haikuwahi kufika Dar, sisi tunahoji polisi wana kifaa gani cha kugundua kuwa gari hii haijawahi kufika Dodoma au Mbeya"Benson Kigaila
"Swala la Tundu Lisu lipo mikononi mwa serikali, wanatakiwa wachunguze na watupe majibu, serikali inatakiwa kuchunguza suala hili na si kujivua, serikali ichunguze na uwezo huo wanao kama hawana waombe usaidizi kwa vyombo vya uchunguzi vya kimataifa, tushasema hilo"Benson Kigaila
"Tundu Lissu anasema mambo ya kweli ambayo yametokea Tanzania, sasa hayo mambo ya kweli kama yanachafua mtu, nchi au serikali basi ni wao wanayoyatenda ndio wanachafua nchi na si Lissu" Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni- CHADEMA
"Kama Serikali ingetaka kufanya uchunguzi,kuna kitu kinaitwa ballistic analysis,polisi walichukua maganda ya risasi,unaweza kujua ni aina gani ya silaha iliyotumika utajua batch no. imetengenezwa nchi gani na iliingia mwaka gani nchini,ililetwa na serikali au mtu binafsi" Kigaila