CHADEMA wamhujumu Lowassa rasmi, wavunja UKAWA kusini, CUF kumwaga mboga

chadema wanamtaka lowasa awe rais,tatizo lao ni tamaa.
wao wanataka kuwatumia caf na wengine ili wafanikiwe,kish watawadump.
cuf walivyo wajinga wameingia kichwakichwa ukawa licha ya watu kuonya kuwa itakula kwao.

Watasutwa Na Dhamira Zao Hao.
 
Propaganda za jk, alisema anahakikisha media zote zinauwa upinzan, nadhani usanii wenyewe huu.. Ngoja tutaendelea kuyaskia
 
Habari wadau,
Kuna uzi umepandishwa hapa jamvini kuhusu UKAWA kuvunjika rasmi kanda ya kusini(Lindi &Mtwara) kama mdau nililazimika kupata ukweli wa taarifa hizo, zifuatazo ndio taarifa rasmi kutoka majimbo mbalimbali ya kusini

Itakumbukwa kwamba katika mgawanyo wa majimbo uliotangazwa hivi karibuni na kwa kuzingatia vigezo vya msingi vya ugawanaji wa majimbo kama vilivyotangazwa,majimbo yote ya mkoa wa Lindi na majimbo karibia yote ya mkoa wa mtwara yamekabidhiwa kwa chama cha wanainchi CUF,na majimbo matatu yakikabidhiwa kwa chama cha NLD

Tayari maandilizi ya kutosha yamefanyika kwa wagombea wa chama cha wanainchi CUF, wa Ubunge na wale wa udiwani wameshachukua form za serikali wameshazijaza tayari kwa kuzirejesha.

Kwa mshangao mkubwa mapema juzi na jana tena kwa mshangao mkubwa wagombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA majimbo yote ya Mkoa wa Lindi na Mtwara nao wameenda kuchukua form za serikali wamezijaza na kuzirudisha.

Wanainchi wapenda mabadiliko,wanachama wa CUF na NLD wanahoji hayo ndio mashirikiano yaliokuwa yanahubiriwa na UKAWA!?
Na kwa nini CHADEMA wameamua kuchukua hatua hiyo kwenye majimbo ya CUF vipi nao wangefanyiwa Uhuni kama huo kwenye majimbo yao wanayokubalika hali Ingekuwaje?

Tayari kutokana na sintofahamu hiyo wanainchi, wanachama na viongozi
waandamizi wa CUF wa majimbo wamehaidi kutokumuunga mkono Mgombea Urais wa CHADEMA Ndugu lowassa kama viongozi wa CHADEMA hawatasawazisha hali hiyo .

Niandikapo uzi huu vurugu za wanachama zinaendelea kutanda karibu kila kwenye Ofisi ya CUF majimbo ya kusini wakitaka kujua hatima ya UKAWA.
Kutokana na sintofahamu hiyo ni dhahiri kama itaendelea Lowassa hataokota kura hata moja kusini.
Ni dhahiri pia
Kwa ubinafsi huo unaoneshwa na CHADEMA hakika sioni kama UKAWA unaweza ukaingia Ikulu

Swali ambalo najiuliza na hakika ningefurahi kama ningepatiwa majibu,

Hivi ni kweli CHADEMA wanamtaka lowassa haingie ikulu au wao wana ajenda yao nyingine tu?

Propaganda
 
Nilisema Muda Ukifika Mtaijua Na Kuitambua CCM Na Labda Nikuambie Na Nikuhakikishie Tu Wewe Mleta Uzi Kuwa Hilo Uliloliona au Kulisikia Huko Kusini Ni Cha Mtoto Na Badala Yake Nakuomba Sana Tegea Sikio Kati Ya Jumanne na Alhamisi Wiki Ijayo Kuna KITU Kingine Cha Kutikisa Nchi Na Cha Kuisambaratisha Rasmi CHADEMA / UKAWA Huku Wakikwaruzana Na Hamtaamini Macho Na Masikio Yenu. Nilisema Kuwa CHADEMA / UKAWA Walijamba Na Sasa CCM Inakwenda Kunya Na Wataomba PO Wenyewe Na Mtajuta Kupokea Pesa / Hela Za Lowassa Na Kumuuzia Chama Na Kuwadhihaki Dr. Slaa Na Professor Lipumba.
 
cuf walionywa toka zamani, kweli sikio la kufa haliskii dawa! cdm hawajaanza leo ukigeugeu na cuf walijua hilo.
 
Mleta mada ni muongo sana kilichofanyika wagombea wa CUF wa ubunge na udiwani wengi wao hawakuoneka muda wa kurudisha form wengine mpaka sasa hawaonekani kuna hujuma imefanywa na magamba ya kuwahonga wagombea wasirudishe form au wazikosee kuzijaza makusudi sasa dawa yao wamerudisha wa vyama vyote ili CCM wasipite bila upingwa maeneo wamefaulu mfano Sengerema walipozubaa.
 
Nilisema Muda Ukifika Mtaijua Na Kuitambua CCM Na Labda Nikuambie Na Nikuhakikishie Tu Wewe Mleta Uzi Kuwa Hilo Uliloliona au Kulisikia Huko Kusini Ni Cha Mtoto Na Badala Yake Nakuomba Sana Tegea Sikio Kati Ya Jumanne na Alhamisi Wiki Ijayo Kuna KITU Kingine Cha Kutikisa Nchi Na Cha Kuisambaratisha Rasmi CHADEMA / UKAWA Huku Wakikwaruzana Na Hamtaamini Macho Na Masikio Yenu. Nilisema Kuwa CHADEMA / UKAWA Walijamba Na Sasa CCM Inakwenda Kunya Na Wataomba PO Wenyewe Na Mtajuta Kupokea Pesa / Hela Za Lowassa Na Kumuuzia Chama Na Kuwadhihaki Dr. Slaa Na Professor Lipumba.

uoga+propapanda = #hatari
 
Hao ni reserves. Hawatapiga kampeni ila ikitokea hujuma yeyote, watu-take over

Nashukuru kuwapa jibu zuri, kuna uzi humu unaendelea kuwa mgombea wa Nanyamba ashindwa kurejesha fomu. Hapo alikaa CUF peke yake, intelijensia ya chadema ililiona hilo so lazima bao la mkono lizuilike.
 
----- wewe umetumwa na unatumika na ccm
chadema ilishatangaza majimbo yake
hao mapandikizi ya ccm hayatambuliki
umetumwa kuleta uchonganishi mbona CCM NA ACT mmeshindwa kuachiana majimbo ccm hatulalamiki
 
Nafikiri mleta mada haulewi au umekurupuka, kila kitu kiko sawa. UKAWA wako makini sana. Hiyo ni mbinu ya UKAWA kuwachanganya CCM.
CCM walikuwa wamepanga kutumia goli la mkono dakika za mwanzo sana ili kupata ushindi kwa kuweka mapingamizi ili mgombea wa UKAWA akatwe na wao kupita bila kupingwa. Sasa mchezo ukapangwa kuwa kila mahali ambapo CCM ilizoea kupita bila kupingwa basi wagombea wa UKAWA wengi wachukue fomu.

Narudia kusema majimbo yote ya Lindi na Mtwara ni wagombea wa CUF na NLD. Baada ya kuteuliwa tu, wagombea wa CHADEMA watapaswa kujitoa. Tofauti na hapo, mtu yoyote anayefanya hayo anafanya kwa maslahi yake, CHADEMA hakijamtuma na atafukuzwa hata uanachama.

Mbona kwenye majimbo ya CHADEMA CUF hawajaweka wagombea wa ziada?
Hoja ninayoiona hapa ni kuwa CHADEMA hawaamini CUF. Hii si sawa na inavunja imani ya ushikiano thabiti.
Hapa kuna harufu ya mchezo mchafu. Mbona hamkuwataarifu wanachama wa CUF wao wametaharuki tu kushtukia kuna watu wa CHADEMA washachukua fomu ndo maana unaona taharuki
 
Mleta Mada kama wadau wengi walivyoongea, hatutaki ccm ipite bila kupingwa, subiri uone nini tamko la Ukawa. Kuwa mvumilivu acha hasira, viongozi wetu wako makini sana kuliko unavyodhani. Na kinachoendelea kusini kiko planned.
 
ma ccm bana kazi kukurupuka tu ukawa tuna plan B kama yule jamaa wa Nanyamba kaingia mitini wa cdm ata take over no room for ACt and CCM
 
Hizo ni tahadhari mwisho wa cku wa chadema atajitoa,siunajua wagombea cuf washaanza kuingia mitini na fomu?
 
Back
Top Bottom