CHADEMA wamhujumu Lowassa rasmi, wavunja UKAWA kusini, CUF kumwaga mboga

Habari wadau,
Kuna uzi umepandishwa hapa jamvini kuhusu UKAWA kuvunjika rasmi kanda ya kusini(Lindi &Mtwara) kama mdau nililazimika kupata ukweli wa taarifa hizo, zifuatazo ndio taarifa rasmi kutoka majimbo mbalimbali ya kusini

Itakumbukwa kwamba katika mgawanyo wa majimbo uliotangazwa hivi karibuni na kwa kuzingatia vigezo vya msingi vya ugawanaji wa majimbo kama vilivyotangazwa,majimbo yote ya mkoa wa Lindi na majimbo karibia yote ya mkoa wa mtwara yamekabidhiwa kwa chama cha wanainchi CUF,na majimbo matatu yakikabidhiwa kwa chama cha NLD

Tayari maandilizi ya kutosha yamefanyika kwa wagombea wa chama cha wanainchi CUF, wa Ubunge na wale wa udiwani wameshachukua form za serikali wameshazijaza tayari kwa kuzirejesha.

Kwa mshangao mkubwa mapema juzi na jana tena kwa mshangao mkubwa wagombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA majimbo yote ya Mkoa wa Lindi na Mtwara nao wameenda kuchukua form za serikali wamezijaza na kuzirudisha.

Wanainchi wapenda mabadiliko,wanachama wa CUF na NLD wanahoji hayo ndio mashirikiano yaliokuwa yanahubiriwa na UKAWA!?
Na kwa nini CHADEMA wameamua kuchukua hatua hiyo kwenye majimbo ya CUF vipi nao wangefanyiwa Uhuni kama huo kwenye majimbo yao wanayokubalika hali Ingekuwaje?

Tayari kutokana na sintofahamu hiyo wanainchi, wanachama na viongozi
waandamizi wa CUF wa majimbo wamehaidi kutokumuunga mkono Mgombea Urais wa CHADEMA Ndugu lowassa kama viongozi wa CHADEMA hawatasawazisha hali hiyo .

Niandikapo uzi huu vurugu za wanachama zinaendelea kutanda karibu kila kwenye Ofisi ya CUF majimbo ya kusini wakitaka kujua hatima ya UKAWA.
Kutokana na sintofahamu hiyo ni dhahiri kama itaendelea Lowassa hataokota kura hata moja kusini.
Ni dhahiri pia
Kwa ubinafsi huo unaoneshwa na CHADEMA hakika sioni kama UKAWA unaweza ukaingia Ikulu

Swali ambalo najiuliza na hakika ningefurahi kama ningepatiwa majibu,

Hivi ni kweli CHADEMA wanamtaka lowassa haingie ikulu au wao wana ajenda yao nyingine tu?

ndugu yangu katika wakati kama huu,, kuna wanaukawa na wanaukawa njaa( mamluki waliopewa pesa na ccm kuangusha nguvu ya ukawa ) hivyo watu kama hao wapo maana ccm wanatumia kila namna kujiokoa
 
"Hivi ni kweli CHADEMA wanamtaka lowassa haingie ikulu au wao wana ajenda yao nyingine tu?"

Biashara imeshaisha zamani Mbowe keshapata za kwakwe sa hivi anabadili santuri kila dakika ili nyumbu waendelee kucheza uwanjani, Muziki ukiisha tarehe 25/10 nyumbu watakosa pa kwenda kwani tayari DJ atakuwa hayupo ukumbini!

[/COLOR][/I][/B]
Hatuwaamini kwa propaganda hizi za kitoto.
 
wamesaidia coz ccm iliandaa hela kuwahonga watu wajitoe kwenye kinyanga'anyiro...sasa jamaa wakazinyaka..wakaruhusu watu wachukue forms wa kutosha...haya sasa ccm iwahonge wooote wajitoe....jaman siasa ni zaidi muionavyo
 
ndugu yangu katika wakati kama huu,, kuna wanaukawa na wanaukawa njaa( mamluki waliopewa pesa na ccm kuangusha nguvu ya ukawa ) hivyo watu kama hao wapo maana ccm wanatumia kila namna kujiokoa
Nimekupata mkuu.
 
wamesaidia coz ccm iliandaa hela kuwahonga watu wajitoe kwenye kinyanga'anyiro...sasa jamaa wakazinyaka..wakaruhusu watu wachukue forms wa kutosha...haya sasa ccm iwahonge wooote wajitoe....jaman siasa ni zaidi muionavyo
Wamevurugwa wakavurugika. UKAWA NI NOMA.
 
nao chadema wasichojua lowasa anawatumia tu,ikitokea amepata urais,lazima atawadump tu.
msije shangaa mbowe akaenda kuwa mkuu wa wilaya ya rufiji.
huku kina chenge ndo wanakamata nyadhifa.....

Ishu sio mdaraka ishu we dont want CCM
 
Napata hisia muungano wa hivi vyama hauko sawa na hauna uwiano, hawaaminiani na kuna harufu kuwa kuna kuburuzana hivyo wengine wanakubali maazimio kwa maneno tu wakija katika utekelezaji kutakuwa na shida kubwa kwani malengo yao hayako sawa. Naanza kuona uwezekano wa watanzania kuhuzunishwa mpaka wataacha kabisa kushiriki katika mambo yote ya siasa za upinzani huko mbele
Unakubali kushindwa kabla mkuu. Acha kuhisi na kupiga ramli.
 
Nafikiri katika kila plan A kunatakiwa kuwe na plan B...

Bila shaka ni maandalizi ya kukwepa hujuma kama kweli hali unayoielezea ndiyo iliyotokea...
 
Kukaa Kwako Kijijini Huku Ukila Nzige Na Mizizi Kusikufanye Utuchukie Tunaojitambua Na Tunaishi Mjini. Endelea Kutulimia Mazao kisha Tuje Tuyanunue Huko Kwenu Ulipo Kwa Bei Ya Kuwalalieni. UPOPOMA Wenu Watu Wa Vijijini Ndiyo Unawaponza Ila Nafurahi Tu Kuwa Wengi Wenu Ni Wapiga Kura Wetu WAAMINIFU Sana Na Mno Na Naamini Hata Mwaka Huu Kura Zetu Mnazo Tena. Nisalimie Wana Vijiji Wenzako Wote Huko KYAKA NKUNDE Na IKUPILIPA NKOBA.

Kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi!!
Mkuu nimesalimu amri,hata Nape cha mtoto:eek: kweli CCM ina hazina ya machz. Tawasalimia mkuu ila sina mbavu.........
 
Unakubali kushindwa kabla mkuu. Acha kuhisi na kupiga ramli.

Pita kila sehemu, sikia imani ya watanzania kwa UKAWA, sikia hamu yao ya kupata mabadiliko. Kama kweli kuna wanaofanya makusudi kutorudisha fomu mpaka wasimamiwe wakati walishakubaliana. Kama inabidi chama kingine kisimamishe wagombea kinyume cha makubaliano ili kulinda jimbo au kata isuchukuliwe bila kupingwa kuna nini? Kuna kuaminiana hapo? Wasipoaminiana wakaanza kulumbana hadharani nini kitatokea? Imani ya wananchi kwao itakuwaje?
 
Habari wadau,
Kuna uzi umepandishwa hapa jamvini kuhusu UKAWA kuvunjika rasmi kanda ya kusini(Lindi &Mtwara) kama mdau nililazimika kupata ukweli wa taarifa hizo, zifuatazo ndio taarifa rasmi kutoka majimbo mbalimbali ya kusini

Itakumbukwa kwamba katika mgawanyo wa majimbo uliotangazwa hivi karibuni na kwa kuzingatia vigezo vya msingi vya ugawanaji wa majimbo kama vilivyotangazwa,majimbo yote ya mkoa wa Lindi na majimbo karibia yote ya mkoa wa mtwara yamekabidhiwa kwa chama cha wanainchi CUF,na majimbo matatu yakikabidhiwa kwa chama cha NLD

Tayari maandilizi ya kutosha yamefanyika kwa wagombea wa chama cha wanainchi CUF, wa Ubunge na wale wa udiwani wameshachukua form za serikali wameshazijaza tayari kwa kuzirejesha.

Kwa mshangao mkubwa mapema juzi na jana tena kwa mshangao mkubwa wagombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA majimbo yote ya Mkoa wa Lindi na Mtwara nao wameenda kuchukua form za serikali wamezijaza na kuzirudisha.

Wanainchi wapenda mabadiliko,wanachama wa CUF na NLD wanahoji hayo ndio mashirikiano yaliokuwa yanahubiriwa na UKAWA!?
Na kwa nini CHADEMA wameamua kuchukua hatua hiyo kwenye majimbo ya CUF vipi nao wangefanyiwa Uhuni kama huo kwenye majimbo yao wanayokubalika hali Ingekuwaje?

Tayari kutokana na sintofahamu hiyo wanainchi, wanachama na viongozi
waandamizi wa CUF wa majimbo wamehaidi kutokumuunga mkono Mgombea Urais wa CHADEMA Ndugu lowassa kama viongozi wa CHADEMA hawatasawazisha hali hiyo .

Niandikapo uzi huu vurugu za wanachama zinaendelea kutanda karibu kila kwenye Ofisi ya CUF majimbo ya kusini wakitaka kujua hatima ya UKAWA.
Kutokana na sintofahamu hiyo ni dhahiri kama itaendelea Lowassa hataokota kura hata moja kusini.
Ni dhahiri pia
Kwa ubinafsi huo unaoneshwa na CHADEMA hakika sioni kama UKAWA unaweza ukaingia Ikulu

Swali ambalo najiuliza na hakika ningefurahi kama ningepatiwa majibu,

Hivi ni kweli CHADEMA wanamtaka lowassa haingie ikulu au wao wana ajenda yao nyingine tu?

Huu uzi ni wa upotoshaji wa hali ya juu. Jana nilipata nafasi ya kumsindikiza Mh Baruwani kurudisha fomu za ubunge Jimbo la Lindi mjini, hali ilikuwa ni shwari hakukuwa na taharifa wala manung'uniko yoyote kuhusu ukawa, isipokuwa tu Mh Baruwani alilaani sana mgombea wa ubunge jimbo la Nanyamba kwa tiketi ya CUF kutokomea na fomu. kuhusu wananchi bado wanamatumaini tele na Mh Lowassa. siku nyingine uache kuandika kwa kufwata mihemko
 
Kukaa Kwako Kijijini Huku Ukila Nzige Na Mizizi Kusikufanye Utuchukie Tunaojitambua Na Tunaishi Mjini. Endelea Kutulimia Mazao kisha Tuje Tuyanunue Huko Kwenu Ulipo Kwa Bei Ya Kuwalalieni. UPOPOMA Wenu Watu Wa Vijijini Ndiyo Unawaponza Ila Nafurahi Tu Kuwa Wengi Wenu Ni Wapiga Kura Wetu WAAMINIFU Sana Na Mno Na Naamini Hata Mwaka Huu Kura Zetu Mnazo Tena. Nisalimie Wana Vijiji Wenzako Wote Huko KYAKA NKUNDE Na IKUPILIPA NKOBA.

"Tuje 2nunue mazao yenu kwa kuwalalieni"mungu cyo mjinga kawa huyu ngedere 2015 hakuna ---- mkatawale vichaa milembe mwaka huu mnakaa
 
Mambo ya kimkakati walijua kuna watu hawatarudisha fomu na kweli kuna mgombea wa CUF hajarudisha fomu na had leo hapokei simu. Sasa mlitaka jimbo liende CCM bila kupingwa?
 
Hiyo issue CHADEMA wako vzr kichwani.

Hawa CUF wanaweza jitoa anytime na kumuachia mgombea wa CCM, ni bora wakabe kwanza hadi Sept 25.
 
Mimi nadhani nyie Cuf hamuwajui chadema kama walikuwa wanawatumia kama ngazi na kwavile hamna akili mkapandwa kama ngazi kirahisi kabisa pole hao ndiyo wachaga bana.
 
Tatizo la wa kijani uongo wao hawaupimi hivi mtu mwenye akili timamu unaamka kuzusha uongo unakuwa unamdanganya nani au ndiyo ndiyo hofu poleni sana lakini chama washirika kitawasaidia kuwalinda ingawaje nao zamu hii sijui kama wataweza kuwasaidia kuiba kura
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom