CHADEMA wamfungulia kesi Nape

CHADEMA wamfungulia kesi Nape

Kutokana na vyanzo vyangu vilivyopo Mahakama kuu ya Tanzania Leo Nape amefunguliwa kesi ya madai na imepewa namba 186 ya mwaka 2012.

Kesi hii ni kuhusiana na madai ya nnape kuwa CDM wana pokea pesa kutoka nje ya nchi.

Tuendelee kufuatilia


Updates.

Inaitwa civil case no.186 of 2012 ,board of registered trustees of chadema ... Plaintiff versus nnape nnauye defendant .

Tusubiri kupata ukweli..kimsingi tu mahakama za mtaani zisitumike ku-justify!
 
Hii kesi ni ngumu sana make CCM wakijaribu kuchakachua wamekwisha HIZO NCHI ZITAKAZO TAJWA ZITAKUJA JUU NA KUKATA MISAADA NA HAPO NDO UTAKUWA MWISHO WA CCM, MAtaifa kama Ujerumani,Norway, Na mengineyo hayataki. Porojo
NA hii kesi Serikali itaomba imalizwe nie nie ya mahakama
 
Anasimama na Lissu Mahakamani pembeni kuna Prof.Safari au kuna kitu gani kwa upande wa Chadema ? Na hii ndiyo watanzania watajua kwamba Chadema wako serious sasa .Komesha kuropoka bila ushahidi .Marando am sure hatakosa hapa kuongoza kuutafuta ukweli .

Nadhani sasa uropokaji karibu utafikia mwisho. Huyu (Nape) anapendezea sana kuimba taarabu lakini magamba wameona anawafaa. Sasa kazi kwao, akaropoke mahakamani. Natamani pia nimjue wakili wake.
 
Kama kuna wasomi nyinyiem wangemtetea kafumua ndo tungejua wana uwezo, chezea chadema weyeeee
 
Ni wakati wa Chadema kuumbuka. Nape atakuja na ushahidi wa kutosha.

Usiwe mjinga kiasi hicho, CHADEMA wasingethubutu kufungua kesi bila ya kuwa na uhakika kama Nape ana ushahidi au la!! Ukiona kesi imefunguliwa, ujue TISS wa CHADEMA wameshafanya kazi yao na kuhakikisha kuwa Nape ni mweupe, hana ushahidi wala nini! Unafikiri kuwa tunaweza kwenda mahakamani bila ya kujihakikishia ushindi? Nape hana kitu, aliropoka tu. Tundu Lissu atakuwa kando ya Prof Safari na Mabere Marando, Nape ataponyokea wapi? Kazi kwisha, ndio magamba yakome kuropoka bila ya kuwa na LOGICAL and CRITICA EVIDENCE.
 
Chadema naona nao wameanza kufilisika.

Sasa mimi najua siku zote hamna imani na mahakama na mnasema hao majaji wote vimeo sasa inakuwaje tena mnafungua kesi huko huko?
 
Nape kasema Chadema wanapokea pesa kutoka nje au wampokea. Sasa pesa kutoka nje zinaweza kuwa na maana pana.

Hata kama ni USD 500 walipokea kutoka kwa watanzania waishio USA Nape akitoa ushahidi wa kutosha basi kesi kwishnei.
 
Mimi sioni umuhimu wa hii kesi, ni kuendekeza uhasama wa kijinga. CDM walipaswa wampuuze Nape baas! Huku ni kupotezeana Muda na raslimali fedha
 
Ngoja mkapambane na vichwa vya sheria,kuna mtu kama Lussu hadi JK anamuogopa,waaulize majaji alivyo wachachavya huko arusha kwenye kikao cha majaji na mawakili,hii ngoma ni lazima CCM wakimbie na kumtelekeza Nape mtaniambia
 
Mimi sioni umuhimu wa hii kesi, ni kuendekeza uhasama wa kijinga. CDM walipaswa wampuuze Nape baas! Huku ni kupotezeana Muda na raslimali fedha

kwa uwezo wa akili yako finyu kama kiuno cha sisimizi ndio utaona hili jambo huoni umuhimu,tulia mnyolewe.CDM kuna wanasheria walio bobea hawana kazi,ndio mtawatambua sasa kama hawana utani
 
Amezoea kwao mtu mkubwa kuropoka ni busara ya pekee.
 
Nape kasema Chadema wanapokea pesa kutoka nje au wampokea. Sasa pesa kutoka nje zinaweza kuwa na maana pana.

Hata kama ni USD 500 walipokea kutoka kwa watanzania waishio USA Nape akitoa ushahidi wa kutosha basi kesi kwishnei.

umeona ulivyo mpuuzi?emu nenda ulejee hatua kwa hatu kauli ya nape alafu ndio utajiona we ni pumbaman kias gan
 
Hivi, ameshitakiwa yeye kama nape Nnauye au kama KATIBU MWENEZI WA CCM?
 
kwa uwezo wa akili yako finyu kama kiuno cha sisimizi ndio utaona hili jambo huoni umuhimu,tulia mnyolewe.CDM kuna wanasheria walio bobea hawana kazi,ndio mtawatambua sasa kama hawana utani
Hivi kwenye uwanja wa kisiasa tukisema kila jambo lipelekwe mahakamani mahakama si zitajaa kesi za kipuuzi?? Hii ni kesi isiyo na maslahi kwa taifa na haimsaidii mtanzania maskini. Ni kutunishiana misuli kusiko na tija. Kukanusha kauli ya Nape kulitosha kuliko kukimbizana mahakamani.
 
Huu ni uchanga katika siasa. mambo ya siasa, hukumu yake ni jukwaani, ambapo wananchi ndiyo huhukumu. Kama kesi ni kupokea pesa kutoka nje ya nchi, hapo hakuna shaka, inathibitishika. kwani mchango wa London pesa si zilipokelewa?????
 
Back
Top Bottom