CHADEMA wameshindwa kumuua nyani wameshamwangalia nyani usoni-Like the candle in the wind

Wale wabunge wa chadema waliokuwa wanalilia posho wamekwenda wapi? au wameamua kulia kimya kimya kuogopa utawala wa kimabavu wa chama hicho?
 
Vpi za masiku Wab...!
Karibu tena jamvini,
baada ya kusoma bandiko lako, na mara zote nakutana na watu wenye hoja kama zako huwa nahitimisha kwa kusema, kuwa chama cha kufanya mabadiliko chanya kwenye nchi hii ni kazi ngumu sana.
Labda nisaidie, nipe uchambuzi wako kama CDM watafanya kama unavyotamani wafanye?
Nafasi ya umma huu wa watanzania ni ipi katika uchambuzi wako? Nadhani bado umeendelea kuuchukulia kama umma wa makondoo unaobidi kuburuzwa kwenye kila kitu na ndio ukweli huo!
Mi nadhani tunakazi sana katika kuuamsha umma huu kuelekea kufanya mapinduzi wenyewe na mabadiliko maridhawa,
haya chama (cdm) yanarekebishika afu pia yamekaa kimtazamo wa mtu husika!
 
Hospitali ya Muhimbili imefungwa!

Chadema wana waza Uzini ruzuku iongezeke, kusisitiza migomo na maandamano sio rahisi kwani JK amekuwa mwenyeji wao mzuri mno....wanamuonea aibu!

kama mnaipenda nchi hii...saa ya ukombozi ni sasa, himizeni watu waingie barabarani...mkifanya hivyo support haitakuwa kwa wana CDM tu, bali na wana CCM wengi tu!!
 
wewe tunakuelewa ni nani na lengo lako linajulikana. upo chadema lakini huipendi chadema kwa sababu ya ubinafsi wako. na uenyeketi unaouota kila siku utaukosa. na kule nccr mageuzi nako kumeota mbawa. umeula wa chuya...
 
nakuambia madaktari wamegoma, jikaze hivyo hivyo..kwa bandiko hili atakuhudumia nani hospitali???
 
"Kwa sisi wenye akili ''najisifu ngaa kidogo'' kwa nini tusisifie CCM kwa siasa zake za kuharibu nguvu na bongo ya wapinzani kwa utashi wa wapinzani wenyewe? Whoever said CCM is a group of idiot and moron was wrong, Is a group of smart people who are brilliant and can play with people's mind for their own benefit! Yes chadema has been played and they are now like ‘candle in the wind"

Kwa Mtaji huu Idi Amini alifanikiwa sana katika utawala wake.
Hitler naye alifanikiwa sana.
Mobuto pia alikuwa very smart.

Hata Makaburu walifanikiwa sana katika siasa zao kwani Mandela ilibidi atoke Jela mwenyewena kwenda kuongea na wazungu kuthibitisha kwamba wazungu ni zaidi.

Akili ni nywele sasa sijui sisi wenye vipara kama Kinana akili ziko Robo????

Unaongea kishirikina.
Katika dunia yako kuingia Ikulu ni kuzinguliwa nguvu zako.
Ukitofautiana na CCM usiingie Ikulu.
Ukiingia usishikane mkono na Rais.

Naheshimu mawazo yako namwelekeo wako, lakini sioni kama unakupeleka mahali popote.
 
Waberoya,
All I can say about your perception of Chadema is that you are out of touch.

ndio majibu yako kwa hoja mzee!! angesemwa Nyerere ndio huwa una uwezo wa kaundika walau sentensi mbili!
 
"Kwa sisi wenye akili ''najisifu ngaa kidogo'' kwa nini tusisifie CCM kwa siasa zake za kuharibu nguvu na bongo ya wapinzani kwa utashi wa wapinzani wenyewe? Whoever said CCM is a group of idiot and moron was wrong, Is a group of smart people who are brilliant and can play with people's mind for their own benefit! Yes chadema has been played and they are now like ‘candle in the wind"

Kwa Mtaji huu Idi Amini alifanikiwa sana katika utawala wake.
Hitler naye alifanikiwa sana.
Mobuto pia alikuwa very smart.

Hata Makaburu walifanikiwa sana katika siasa zao kwani Mandela ilibidi atoke Jela mwenyewena kwenda kuongea na wazungu kuthibitisha kwamba wazungu ni zaidi.

Akili ni nywele sasa sijui sisi wenye vipara kama Kinana akili ziko Robo????

Unaongea kishirikina.
Katika dunia yako kuingia Ikulu ni kuzinguliwa nguvu zako.
Ukitofautiana na CCM usiingie Ikulu.
Ukiingia usishikane mkono na Rais.

Naheshimu mawazo yako namwelekeo wako, lakini sioni kama unakupeleka mahali popote.

Mkuu mpaka unaandika yote hapo juu..sina mwelekeo? you were supposed to ignore the thread...

umeandika hoja nzuri zimekuwa zako na umezifungia chumbani! kwani hujaeleweka unaandika for what? au mawazo yako hayo hapo juu yamekupeleka wapi

Nasema chadema wasaliti na walitakiwa issue ya madaktari kuingilia kati kama chama cha wananchi..AU ULITAKA NISEMEJE??
 
Wabe,

Maneno mazuri sana ila ni kwenye theory tu. Inavyokuja kwenye Practical, vyama vya Siasa au wapigania uhuru/haki inabidi wawe wamegawanyika katika sehemu mbili. Upande mmoja unaongea mezani na upande wa pili unapigana msituni.

Ungelilaumu Chadema kwa kutokuwa na wapiganaji wa msituni . Chadema kama chama cha siasa, kazi yao inatakiwa kuwa mezani na kuongea. Kuwa Ikulu na kuongea. Kuwa bungeni na kuongea.

Kwa hali tuliyonayo Tanzania, neno WAPIGANAJI WA MSITUNI sina maana watu wachukue silaha na kuingia kweli msituni kama mtani wangu kutoka Dodoma alivyosema. Chadema kama wapinzani, wanaweza kuwa wapo nyuma ya migomo mikubwa Tanzania ingawa officially hawakiri hata sehemu moja kuwa wana uhusiano wowote na migomo.

Kama Mandela angelichukua Silaha na kwenda kupigana moja kwa moja, walimlima risasi na mchezo ukaisha. Vijana wake waligawanyika huku wengine wakifanya siasa na kuishi Mazimbwe na wengine wakisomea vita na kuishi Kongwa. Msumbiji, Zimbabwe, Angola nk nako ilikuwa hivyohivyo. Wakati kulikuwa na ANC, upande mwingine kulikuwa na wale Wauwaji wa Umkhonto we sizwe au Spear of the National na kweli wameuwa sana watu weupe South Africa wakati wa ubaguzi wa rangi.

Chadema kama chama wakijipeleka mbelembele kichwakichwa kama unavyotaka wewe, wanazushiwa Vangi la kutaka kupindua nchi na hapo mechi inakuwa imekwisha. Hiyo ingelifaa tu kama nchi ingelikuwa INATAWALIWA NA NCHI/WATU WENGINE. Kwa mfano tuseme South Africa inatawala Tanzania na watu wanataka kugoma, hapo sasa Chadema wanajiingiza moja kwa moja kwani hawa jamaa wakiondoka, basi itabidi chama kingine kitawale.

Unaweza kuwa sawa kwa upande mmoja wa shilingi ila kumbuka shilingi ina pande tatu/ au zaidi? Kinachotakiwa kwa sasa ni sisi wananchi kwenda kuwasaidia Waganga katika mgomo wao na ikibidi Waalimu na taasisi nyingine ziungane kugoma na kupinga nyongeza za posho, kupanda kwa bei na maisha kwa ujumla. Chadema wawepo ila kwa siri sana.

Ahsante sana Mkuu Sikonge kwa mchango wako uliotulia na pia wenye hekima na busara za hali ya juu.
 
Ahsante sana Mkuu Sikonge kwa mchango wako uliojaa hekima na busara kubwa sana.
 
Maalim Seif ndiye atakayeimaliza CCM. Wasikilize wapambe wake akina Jussa sasa. Hata MUUNGANO huu uko mashakani sasa kuliko wakati mwingine wowote tangu kuasisiwa kwake.
CHADEMA inaandamwa na jinamizi la UCHAGGA tu. Wakiliweza hili TANZANIA ni yao.

Uchagga wa CDM uko wapi? Au kwa kuwa mwanzilishi wake ni Mchagga? kwa taarifa yenu kati ya waanzilishi ni pamoja na Mzee Bob Makani. Bado yupo na wakati fulani alikuwa Mwenyekiti wa chama. Mtazania asiyekuwa na kabilia tutampata wapi? Nina amini kila jambo lina mahali pa kuanzia na wakulianzisha! Kwani Zitto ni Mchaga? Shibuda ? Akili yetu tunatakiwa kuitoa kabisa katika maeneo ya Dini zetu na makabila yetu. Hayatufikishi popote!
 
Mhhh! Serikali ya CCM na hali yambambo ilivyo ni kwamba kwa maoni yangu binafsi,kukaa meza moja na CCM ni kuwapa faida zaidi.Chadema inazingatia maslahi ya taifa lakini wenzetu wametanguliza maslahi ya chama chao na kumaliza au kudhibiti makundi zaidi.Kwa kawaida ukiona CCM wamekubali kukaa meza moja ujue wameshikwa pabaya,wana hali ngumu kisiasa ndani ya chama chao na kuna uwezekano wa mazunguzo au muafaka na upinzani ukawa na faida kwa chama au kundi fulani ndani ya chama chao.

Kwa mazingira haya,I prefer more radical approach dhidi ya CCM.I prefer confrontation kwa kutumia legitimacy ya nguvu ya umma.Civil disobidience ingekuwa approach nzuri.CCM hawastahili kuona kwamba mapendekezo ya upinzani yakitekelezwa iwe kama vile wamefanya hisani.Inabidi wafanye hivyo kwa kulazimika ili kama ni kukaa mezani basi tukae kwa ajili ya truth and reconciliation.Iwe ni post transitional dialogue......
 
Nilikuwa nasoma hii makala kama ushairi wenye vina vya kati na mwisho.Mlianza vizuri, mlikuwa mnapiga mbio vizuri nani amewaroga? Nani kawadanganya kuwa hoja zenu nzuri ambazo mlizipeleka ikulu pasi kupata baraka za wanachama wenu..zilibarikiwa? mkafika, mkakaa kwenye makochi na kunywa gahawa na hapo ile nguvu yenu ikapotea, ikatoweka..Ila tukio hili mlilipa sifa na sababu nyingi, “siasa za kisasa, siasa za urafiki, siasa za kutokuchukiana’’ bila ya nyie kujua…...Nadhani mwandishi ana maudhui mazuri sana juu ya jambo aliloliona na kuliamini, lakini kama mwandishi ameshindwa kuficha, itikadi,attitude na emotions zake katika kufikisha ujumbe.. Kuna uwezekano mkubwa sana tukayachukua yale mawazo yake mazuri na kuyaacha yale mabaya, CDM ni chama kikuu cha upinzani, na ili kuyafikia malengo yake, lazima kijue mpinzani wake CCM anatumia silaha gani( simanishi bunduki) katika kujipatia political influence/ political power.

CCM kuwa kama wakoloni weusi, weupe, wanyonyaji kwa jina lolote lilosemwa hizo ni fikira na jinsi mwandishi alivyoichukulia, na si lazima kwa wote tuamini hivyo, tunaweza kuwa tumefocus mbele yake zaidi ya kimo alichofikia. Ni vizuri tukatambua kuwa hii Nchi ina watu zaidi ya Mil 40. Hawa ni watui wengi sana lakini hatuwezi kuwa wa aina moja wote. Na kwa kutambua hivyo basi mimi binafsi naweza kuwatenga watanzania hawa katika makundi makuu matatu.
  • Watendaji; hawa ni wale watu wenye uwezo wa kufikiria, na kuweka mawazo yao katika vitendo bila kuleta madhara kwa wengine. Kwa mara nyingi watu kama hawa ni wachache sana katika jamii na huongozwa na neno THUBUTU.
  • Washangaaji; Hili ni kundi la watu ambao hawapo kabisa katika kundi A wala hawatoi ushauri,hawakosoi wala hawapendekezi chochote kifanyike lakini hushangaa baada ya jambo fulani kutendeka.
  • Waangaliaji; Hili ni kundi la watu ambapo huangalia tu jinsi makundi mengine yanafanya, halitendi, wala halishangai kwa yaliyotendwa.Lipo tu kwa ajili ya kuangalia wale wanaoshangaa na kutenda. Mara nyingi hili kundi hufananishwa na wafuasi.
Kwa kuangalia mifano hiyo mitatu, utaweza kujua ni kundi gani haswa la kuwaweka watanzania walio wengi.
Nawasilisha...
 
mh kaka kazi nzuri.......this is the best thread in 2012....umetema facts na si majungu.....naamini ktk ww tutabluzwa na ccm mpaka basi....yaani fans wachdema viongozi wao wanawaona kama miungu,na haohao wanatumia vyombo vya habari kumchafua mwenzao zitto mwenye uelewa mpana wa siasa......cdm kama ccm tu wote wasaka tonge
 
Hatua hii ya kukutana Ikulu na JK, ilianzishwa na Chadema ambacho kilipinga muswada wa katiba mara mbili.

Chadema waliomba Appointement Ikulu, wakaruhusiwa walivyofika wakafanya mazungumzo na Rais JK, Kisha wakanywa juice,kahawa na Kashata, wakapiga picha na Rais na kuondoka.

Mie wasiwasi wangu unatokana na hii tabia ya kujifungia Ikulu kwa watu wachache na kufanya uamuzi wa watu wengi.

Hivi Chadema kwenda Ikulu, usiku kuzungumza na Rais, wananchi na wafuasi wa Chadema walihusishwa hadharani kuwa wanakwenda Ikulu kujadiliana na Rais?

ww unaona walienda kunywa juice na kashata na kahawa eeh.. hili la muswada kurudishwa bungeni hujaliona..? au wajifanya hujui wabunge wa ccm wanaweka mgomo kuupitisha marekebisho yaliofanywa na chadema..?
 
Back
Top Bottom