CHADEMA wameshindwa kumuua nyani wameshamwangalia nyani usoni-Like the candle in the wind | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wameshindwa kumuua nyani wameshamwangalia nyani usoni-Like the candle in the wind

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, Jan 31, 2012.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Mlianza vizuri, mlikuwa mnapiga mbio vizuri nani amewaroga? Nani kawadanganya kuwa hoja zenu nzuri ambazo mlizipeleka ikulu pasi kupata baraka za wanachama wenu..zilibarikiwa? mkafika, mkakaa kwenye makochi na kunywa gahawa na hapo ile nguvu yenu ikapotea, ikatoweka..Ila tukio hili mlilipa sifa na sababu nyingi, "siasa za kisasa, siasa za urafiki, siasa za kutokuchukiana'' bila ya nyie kujua…

  Bila aibu ''aliyekuwa rais wa wananchi'' ambaye akiwa msibani hamuangalii hata jirani yake!!akatamka ‘eti Mheshimiwa Rais watu wanasema mimi nakukwepa!! Nikukwepe kwa sababu gani??...ulivyosema sentensi hii Kikwete akafurahi akajibu ni maneno ya akina michuzi…saa ile roho mtakatifu wa woga na nidhamu ya kufa mtu akakushukia, ukawa mtu mpya..'coward'….Kikwete kwa mara ya kwanza tangu ameingia ikulu akalala usingizi akaota, chama kile kilichosemekana kinatisha kikawa mwisho wake saa ile!

  Ni muumini wa siasa za kukaa chini na kuelewana , ni muumini wa siasa za hoja, ni muumini wa siasa za aina ya Lema, ni muumini wa saisa za akina Zito, Ni muumini wa siasa kali na za vurugu…..Lakini uumini upi utumike wapi ndipo huwa sieleweki! CCM hii si ya siasa za kukaa chini na kuelewana, ukifanya hivyo inakula kwako! Maalim Seif anajua hivyo!

  CCM hii si chama tawala ni wakoloni weusi, kamwe hawako kwa ajili ya maslahi ya nchi hii…Sahau kuhusu Katiba,dola na kila aina ya vihonjo vinavyompa Rais mamlaka ya urais na utiisho wa urais. Rais akiwa hakubaliwi na kundi fulani dogo tena likiwa na support kubwa ya wananchi hana nguvu hizo, hana mamlaka hayo! Chadema mmeuza haki yenu na sasa mnashangaa wakati nafasi ya ukombozi ndio hii!

  Ni Chadema nyie mliojipambanua kuwa ni wakombozi, japo mnatumia slogan ya ''nguvu ya umma'' pengine ngau kwa muda mfupi mngetumia slogan ya Mtikila '' saa ya ukombozi ni sasa'' japo jamani mwee semeni jambo nchi itikisike…magazeti yauze!!

  Chadema inahitaji akili kidogo tu kuwa mgomo wa madaktari ilikuwa ni funguo yenu ya Kikwete(the chief architect wa Richmond) kujiuzulu! Ilikuwa ni nafasi ya kuhamasisha waalimu, nafasi ya kuwaleta na kuwakumbuka wazee wa afrika mashariki….ni nyakati nzuri mngewakumbuka ''wahanga wa bodi ya mikopo'' vyuo vikuu, nafasi ya kuwaunganisha vijana wa mbeya , arusha na DSM wanaojengewa masoko ambayo hawawezi kupanga.

  Wakazi wa Mabwepande na kwingineko ndio ilikuwa nafasi… Niseme nini juu ya wananchi wa sehemu mbalimbali kwa nafasi zao ambao wamekata tamaa ya kudai haki zao kwa sababu tu ya vitisho kama vya Pinda? Hivi mkazi wa Gongo la Mboto ambaye analipwa fidia ya laki tano kwa nyumba ya vyumba nane asingekuwepo kwenye maamdamano? Btw mna orodha ya wanaodhulumiwa hapo ofisini kwenu?

  Hivi wanaotoa sifa kwa chama hiki humu wanaona haya? Au mna mawazo ya kupiga kura mwaka 2015 na kushinda chini ya hao hao mnaowapa dhamana ya kubadili katiba (impossible within three years)!! Unrealistic!) kwa cizazi vingi jijavyo? Na aliyewaambia Katiba itafanikiwa kabla ya 2015 ni nani? Waizir wenu wa katiba ni nani? Anajua nchi zingine imechukua miaka mingapi?

  Hivi lile wazo la kuwa piganieni kwanza tume ya uchaguzi nani aliliua? Au hamkunisikia japo kidunyu kuwa , if you are serious then sticky on changing election committee…tunataka tume yenye kila aina ya watu na inayosimamiwa na chombo huru!

  Aliyewaroga kubadili katiba yote ni nani? 2015 ka...kuwa..waambieni wananchi CHADEMA itatoa mwanya wa CCM iendelee ili imalize mchakato wa katiba, by that time Mbowe atakuwa Tajiri kama Rostam!! Acha niseme! Maana kuna watu mnatoka povu kuitetea chadema ambayo lina wajanja fulani wanaotafuta pesa kwa nguvu zote…
  Mbowe huyu na Kikwete watoto wa Night Club ambao wamewaingiza mkenge akina Slaa na akina Warioba, huku mkitoa statement kuwa Zito ndio eti aliyefanikisha mazungumzo!

  Mkasema na kuanika uongo huu kwa watu ni dhambi!!
  Chadema haina nguvu, kwani bado inajitafuna kashata na kucheua kahawa ya ikulu! Haina nguvu kwa aibu, kwani imepoteza nuru hii na utukufu huu! Chadema hii leo inagopa kusu-pport maandamano eti Mtaambiwa chama cha vurugu!

  Chadema wanaogopa kumuua Nyani, wameishamwangalia usoni! Na kucheka naye? Na waumini wao wanawachekea na kujipa matumaini hewa kwa sababu hamna matumaini mengine…hawataki kuwaambiwa ukweli viongozi wao, eti wakisema ukweli watawaudhi na kuonekana wasaliti
  Kama ambavyo chadema inavyoogopa maandamano na migomo leo hii kwani itamuudhi ‘mwenyeji wao' kikwete ndivyo ambavyo chadema supporters wanaogopa kukosoa uongozi wao kwani watawaudhi eti wameonyesha mafanikio ya kuleta wabunge wengi sana-23!Au ni hivi….wakiandamana nani yuko tayari kwenda Jela?

  Hivi uongozi wa chadema leo hii ukaenda jela,mnajua athari zinazotokea kwa familia chache sana zinazokiunda chama hiki, Fikiria chama ambacho viongozi ni mtu, mkwe, shemeji, mpwa, mama, mtoto, mjomba, shangazi na girlfriends….halafu wakakamatwa na kuwekwa ndani!! Chama kinakufa….

  Watanzania this is just a reminder, you have to put your trust kwenye realistic! Hakuna ukombozi kwenye ballot box…..ILA nchi ingetikisika kwa migomo mingi iliyoasisiwa na chama hiki mnachokiabudu, basi leo Chadema kingeishi kama next ruling party! Sio kwa hali ya sasa ambayo wako kama hawako, huku madakatri wakirudi na na kureport makazini huku hawafanyi lolote…wamekosa support, wamekosa nguvu ya wale waliotegemewa kuwa suppport, Wale waliosema wanaweza!

  Kesho mtataka madaktari wawa support kwenye maandamano yenu yalee! Never! Madaktari hawatakuwepo! Funny! Siasa inalipa jamani,kwani wachungaji wangapi wanasema wanaponyesha na kumbe sio? Au lawyers wangapi wanasema utashinda kesi hali akijua utashindwa? Kwa nini chadema isiseme wazi kuwa ni NGO na kijiwe cha jobless na opportunist ili tutafute tumaini lingine?

  Kwa sisi wenye akili ''najisifu ngaa kidogo'' kwa nini tusisifie CCM kwa siasa zake za kuharibu nguvu na bongo ya wapinzani kwa utashi wa wapinzani wenyewe? Whoever said CCM is a group of idiot and moron was wrong, Is a group of smart people who are brilliant and can play with people's mind for their own benefit! Yes chadema has been played and they are now like ‘candle in the wind'

   
 2. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hutafanikiwa hata kidogo
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa Waberoya.
  Karibu tena Jamvini, umeanza na nondo nzito ngoja kwanza nijipange kuchangia hii thread ya ujenzi na yenye tija kwa taifa letu.
   
 4. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duu! Mkuu WABE,Ngoja nitafakari kwanza kwani ni mengi umeyaongea. Kumbe kimya chako kina mshindo mkuu. Karibu tena na tena.
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wabe,

  Maneno mazuri sana ila ni kwenye theory tu. Inavyokuja kwenye Practical, vyama vya Siasa au wapigania uhuru/haki inabidi wawe wamegawanyika katika sehemu mbili. Upande mmoja unaongea mezani na upande wa pili unapigana msituni.

  Ungelilaumu Chadema kwa kutokuwa na wapiganaji wa msituni . Chadema kama chama cha siasa, kazi yao inatakiwa kuwa mezani na kuongea. Kuwa Ikulu na kuongea. Kuwa bungeni na kuongea.

  Kwa hali tuliyonayo Tanzania, neno WAPIGANAJI WA MSITUNI sina maana watu wachukue silaha na kuingia kweli msituni kama mtani wangu kutoka Dodoma alivyosema. Chadema kama wapinzani, wanaweza kuwa wapo nyuma ya migomo mikubwa Tanzania ingawa officially hawakiri hata sehemu moja kuwa wana uhusiano wowote na migomo.

  Kama Mandela angelichukua Silaha na kwenda kupigana moja kwa moja, walimlima risasi na mchezo ukaisha. Vijana wake waligawanyika huku wengine wakifanya siasa na kuishi Mazimbwe na wengine wakisomea vita na kuishi Kongwa. Msumbiji, Zimbabwe, Angola nk nako ilikuwa hivyohivyo. Wakati kulikuwa na ANC, upande mwingine kulikuwa na wale Wauwaji wa Umkhonto we sizwe au Spear of the National na kweli wameuwa sana watu weupe South Africa wakati wa ubaguzi wa rangi.

  Chadema kama chama wakijipeleka mbelembele kichwakichwa kama unavyotaka wewe, wanazushiwa Vangi la kutaka kupindua nchi na hapo mechi inakuwa imekwisha. Hiyo ingelifaa tu kama nchi ingelikuwa INATAWALIWA NA NCHI/WATU WENGINE. Kwa mfano tuseme South Africa inatawala Tanzania na watu wanataka kugoma, hapo sasa Chadema wanajiingiza moja kwa moja kwani hawa jamaa wakiondoka, basi itabidi chama kingine kitawale.

  Unaweza kuwa sawa kwa upande mmoja wa shilingi ila kumbuka shilingi ina pande tatu/ au zaidi? Kinachotakiwa kwa sasa ni sisi wananchi kwenda kuwasaidia Waganga katika mgomo wao na ikibidi Waalimu na taasisi nyingine ziungane kugoma na kupinga nyongeza za posho, kupanda kwa bei na maisha kwa ujumla. Chadema wawepo ila kwa siri sana.
   
 6. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  CDM has to be smarter than hao unaowaita smart CCM. Na u-smart wa CDM utaonekana pale outcome yake itakapokuwa ni ile wengi wetu tunaitarajia kwa muda mrefu.
   
 7. sinapindu

  sinapindu Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Binafsi nimeipenda sana hii!..

  "Ni muumini wa siasa za kukaa chini na kuelewana , ni muumini wa siasa za hoja, ni muumini wa siasa za aina ya Lema, ni muumini wa saisa za akina Zito, Ni muumini wa siasa kali na za vuruguÂ…..Lakini uumini upi utumike wapi ndipo huwa sieleweki! CCM hii si ya siasa za kukaa chini na kuelewana, ukifanya hivyo inakula kwako! Maalim Seif anajua hivyo!
  ".

  Mkuu Sikonge:

  Nadhani mtazamo wa mkuu Webs uko hapo,CCM hawawezi kukutimizia lolote mpaka wahisi/waamini hawawezi kutawala vizuri mpaka wakutimizie!... Seif aliweza kuwaaminisha hilo.
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hawatimizi na mie nalifahamu hilo. Ndiyo maana nikaandika kuwa Chadema inabidi iwe na chombo cha siri sana cha kusaidia maandamano na migomo. Hiki kiwe ni kama chembechembe (Cell) inayojitegemea yenyewe. Chochote kikitokea, basi huwezi kukiunganisha na CHADEMA.

  Mie ni mtu ninayeamini sana kuwa HAKI HAIOMBWI ILA INADAIWA.
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Weborya,

  Nimesikitishwa na lugha uliyotumia isiyo ya kistaarabu.Lakini naomba niweke wazi na wanaJF wasikie kwamba wewe umepotosha mada yako nzima kwa lengo moja tu.Unampiga vita mwenyekiti wa CDM Freeman Mbowe.Ni majuzi tu kuna watu walileta hoja hapa kwamba Mbowe hatakiwi kupata credit yoyote kwenye mazungumzo ya Ikulu kwa sababu hakushirikishwa.Leo wewe unasema ni mpango wake.Mkuu acheni hizo!!

  Unajaribu kuleta kila aina ya fitna ili ionekane Mbowe ameshindwa uongozi kwa sababu unajua uchaguzi mkuu wa CDM umekaribia.Lakini nikuhakikishie kwamba wanachama wa CDM wako imara sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote na hawatafanya makosa katika uchaguzi ndani ya chama.

  Unapiga vita mazungumzo ya CDM na rais kuhusu mjadala wa katiba.Sasa ulitaka CDM waanzishe vita? Halafu wewe ndiye ungekuwa mtu wa kwanza kukimbilia hapa JF kuilaani.

  Niwaombe viongozi wa CDM wawe makini na watu aina ya Weborya ambao kwa sasa wanapanga kila hila kuivuruga CDM mbele ya jamii.Aina hii ya watu ndiyo jua likiwaka wanalaani na mvua ikinyesha wanalaani.Ni watu wa ajabu na hovyo kabisa.

  Weborya nikushauri tu.Tafuta kazi ya kufanya.Mambo ya kuja JF na kupiga fitna na majungu CDM hayatakusaidia,sanasana utazidi kujidhalilisha.Na ndio maana kwenye thread kama hii utashabikiwa sana na wale maadui wa CDM walioko JF.

  Nakuapia kamwe hutafanikiwa katika fitna zako hizi.

  Na tusubiri tuone!!
   
 10. s

  sebastian7 Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi sisi wana wa nchi hii atupendi kufikiri positive mtu akilalamika sana ndo anaonekana anawajibika cha msingi tukubali mabadiliko tuone mbona kenya waliweza zambia na wengine why us?
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Maalim Seif ndiye atakayeimaliza CCM. Wasikilize wapambe wake akina Jussa sasa. Hata MUUNGANO huu uko mashakani sasa kuliko wakati mwingine wowote tangu kuasisiwa kwake.
  CHADEMA inaandamwa na jinamizi la UCHAGGA tu. Wakiliweza hili TANZANIA ni yao.
   
 12. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ritz nini maana ya "TIJA KWA TAIFA"?
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wabe, hao wananchi wa kuingia mtaani kushirikiana na waganga ni wananchi wa nchi gani? Yaani una maanisha hii hii TZ; sahau!! Wananchi have a lot to themselves, sahau hili ni ndoto!! Yale maandamano ya CDM arusha ni purely wananchama na walikuwa na sababu...

  CCM being in power with everything at their disposal kushiriki kwa maandamano ingekuwa suicidal kwa CDM!! Binafsi siamani kutakuwa na mabdiliko ya ki-utawala kwa ballot box! Never!! CVhanges will be possible pale CCM itakapogawanyika mara mbili au hata mara tatu!!
   
 14. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  huu ni ushauri wa kuimaliza chadema, that's the most crap post i ever seen from you
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Waberoya this is 2012, bado tu umekomaa na CDM ulishashauriwa huko nyuma "leave them alone"
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Hatua hii ya kukutana Ikulu na JK, ilianzishwa na Chadema ambacho kilipinga muswada wa katiba mara mbili.

  Chadema waliomba Appointement Ikulu, wakaruhusiwa walivyofika wakafanya mazungumzo na Rais JK, Kisha wakanywa juice,kahawa na Kashata, wakapiga picha na Rais na kuondoka.

  Mie wasiwasi wangu unatokana na hii tabia ya kujifungia Ikulu kwa watu wachache na kufanya uamuzi wa watu wengi.

  Hivi Chadema kwenda Ikulu, usiku kuzungumza na Rais, wananchi na wafuasi wa Chadema walihusishwa hadharani kuwa wanakwenda Ikulu kujadiliana na Rais?
   
 17. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  chadema walicholenga kwenye suala la katiba ni kuhakikisha alternative yao ya rais kurudisha muswada kusomwa mara ya 2 inakamilika subiri mambo ya kustrike dhidi ya maisha magumu yanakuja kama kawaida plan za chadema ni nzuri mkuu wakiyumba watu wote tutageuka ila kwa sasa wako sawa bado
   
 18. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kaka kuna kamati kuu ya baraza kuu la mkutano mkuu taifa wa mikutano yote mikuu ya wilaya hivi ndivyo maamuzi yanavyofanyika kwa kuhusisha watu wachache
   
 19. d

  davidie JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  smart ya kuvaa koti wakati chini hauna hata kifunika maungo yaani upo na suti ya kuzaliwa nayo huo nao waweza kuwa u smart? ebu wafanye jambo ambalo umma wa watanzania watakubali kuwa hawa jamaa ni smart sio kujifaraghua tu
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  CHADEMA wana akili mara mia zaidi ya unavyofikiri.......

  given hali ngumu ya uchumi, na hali mbaya ya wananchi...... upepo wa uchumi wa dunia...na mengineyo wangelianzuisha ingekuwaje??

  labda hauko tanzania.....serekali haijaweza kurecover majeraha ya kifedha yaliyotokana na uchaguzi mdogo wa igunga..... taasisi za serekali zimekosa fedha na hata halmashauri nyingi zinashindwa kujiendesha vyema.......

  ndio maana kila mtu asingependa kusikia fujo za kitoto za wawi na kigoma kusini...kumfukuza hamad na kafulila....

  ndio maana unaona umma hautaki, mahakama haitaki, bunge halitaki......e.t.c.....

  chadema pia inahitaji njia za kidiplomasia na zinazokubalika na wengi kushika dola....

  MMESHINDWA NA MMLEGE.....hii singo yenu ya CHAMA CHA FUJO imeshindwa kuingia sokoni na kutamba baada ya ile ya udinio iliyozikwa igunga!!!

  system@work
   
Loading...