CHADEMA wameshindwa kumuua nyani wameshamwangalia nyani usoni-Like the candle in the wind

Hospitali ya Muhimbili imefungwa!

Chadema wana waza Uzini ruzuku iongezeke, kusisitiza migomo na maandamano sio rahisi kwani JK amekuwa mwenyeji wao mzuri mno....wanamuonea aibu!

kama mnaipenda nchi hii...saa ya ukombozi ni sasa, himizeni watu waingie barabarani...mkifanya hivyo support haitakuwa kwa wana CDM tu, bali na wana CCM wengi tu!!

Tuseme kweli unaiamini kauli hii au ni bezo kwa CHADEMA?
 
Kiukweli nami naona kama panga la CDM limeanza kuwa butu,yawezekana limekata jiwe lina hitaji kunolewa.
 
Nilikuwa nasoma hii makala kama ushairi wenye vina vya kati na mwisho.Mlianza vizuri, mlikuwa mnapiga mbio vizuri nani amewaroga? Nani kawadanganya kuwa hoja zenu nzuri ambazo mlizipeleka ikulu pasi kupata baraka za wanachama wenu..zilibarikiwa? mkafika, mkakaa kwenye makochi na kunywa gahawa na hapo ile nguvu yenu ikapotea, ikatoweka..Ila tukio hili mlilipa sifa na sababu nyingi, "siasa za kisasa, siasa za urafiki, siasa za kutokuchukiana'' bila ya nyie kujua…...Nadhani mwandishi ana maudhui mazuri sana juu ya jambo aliloliona na kuliamini, lakini kama mwandishi ameshindwa kuficha, itikadi,attitude na emotions zake katika kufikisha ujumbe.. Kuna uwezekano mkubwa sana tukayachukua yale mawazo yake mazuri na kuyaacha yale mabaya, CDM ni chama kikuu cha upinzani, na ili kuyafikia malengo yake, lazima kijue mpinzani wake CCM anatumia silaha gani( simanishi bunduki) katika kujipatia political influence/ political power.

CCM kuwa kama wakoloni weusi, weupe, wanyonyaji kwa jina lolote lilosemwa hizo ni fikira na jinsi mwandishi alivyoichukulia, na si lazima kwa wote tuamini hivyo, tunaweza kuwa tumefocus mbele yake zaidi ya kimo alichofikia. Ni vizuri tukatambua kuwa hii Nchi ina watu zaidi ya Mil 40. Hawa ni watui wengi sana lakini hatuwezi kuwa wa aina moja wote. Na kwa kutambua hivyo basi mimi binafsi naweza kuwatenga watanzania hawa katika makundi makuu matatu.
  • Watendaji; hawa ni wale watu wenye uwezo wa kufikiria, na kuweka mawazo yao katika vitendo bila kuleta madhara kwa wengine. Kwa mara nyingi watu kama hawa ni wachache sana katika jamii na huongozwa na neno THUBUTU.
  • Washangaaji; Hili ni kundi la watu ambao hawapo kabisa katika kundi A wala hawatoi ushauri,hawakosoi wala hawapendekezi chochote kifanyike lakini hushangaa baada ya jambo fulani kutendeka.
  • Waangaliaji; Hili ni kundi la watu ambapo huangalia tu jinsi makundi mengine yanafanya, halitendi, wala halishangai kwa yaliyotendwa.Lipo tu kwa ajili ya kuangalia wale wanaoshangaa na kutenda. Mara nyingi hili kundi hufananishwa na wafuasi.
Kwa kuangalia mifano hiyo mitatu, utaweza kujua ni kundi gani haswa la kuwaweka watanzania walio wengi.
Nawasilisha...

Asante kaka, you make JF proud....hata kama unanipinga sina tatizo, nimefurahi ulivyoeleza..

Good work!
 
Back
Top Bottom