kweli pesa hizi zitatupeleka pabaya.
Chadema mmewashirikisha familia ya Mwangosi (R.I.P) kwenye kutengeza hiyo CD Chadema wametengeza Copy 30,000 na wanauza CD moja Sh 5000 hizo pesa wanazoingiza kutokana na hayo mauzo kiasi gani kinakwenda kwenye familia ya Mwangosi kumsaidia mjane wa marehemu.
Mkuu Ritz heshima mbeeele kwanza japo ni mtani wangu wa kule Magambani,
Kwa mujibu wa swali uliloliuliza hapo juu bana hebu tufahamishe japo kidogo ya kwamba siku hizi haki kama hiyo huuzwa katika duka gani siku hizi mkuu?? Bwana Ritz, hapa katikati kidogo naona kam vile umepwaya sana kwenye aina ya maswali unayoyauliza.
Hakika, nielewavyo mimi, CHADEMA kama chama kina haki zote za kuelimisha umma juu yaa jambo lolote lenye maslahi kwao kwa kutumia msaada wa njia mbalimbali halali za kuwawezesha kufikisha vema zaidi ujumbe wowote watakaokua nao wakati wowote na mahali popote pale ilmradi taarifa wanazozitumia ni sahihi za zenye kuthibitika.
Kwa mfano, niliposoma pale ulipokua ukihoji juu ya uwezekano wa Mhe Lema kwepo katika jimbo la Simanjiro naa vile vile kuripotiwa kuongoza mkutano mwingine wa kukata na shoka pale Daraja Mbili mjini Arusha kidogo uliniacha hoi na mbavu kuniuma sana kwa kicheko huku nikijiuliza kwamba huyu rafiki yangu hapa JF na Mtani wa kisiasa kule Magambani kapatwa na nini tena au kaibiwa ufunguo wa kufungulia ukurasa wake mtandaoni?
Kimsingi, nakubali kwamba siku zote umekua ukionyesha viwango vya juu sana ya CRITICAL THINKING CAPACITIES hivyo kunifanya wakati mwingine niwe nikivutiwa na baadhi ya hoja zako japo KIMTAZAMO wewe na mimi ni kama bingu na ardhi - wewe ukivutiwa zaidi na hii CCM nyakua nyakua ya siku hizi na mimi nikitetea chama chochote chenye msimamo kama wa CCM ya enzi za Mwalimu Nyerere (ambacho kwa sasa ni CHADEMA pekee).
Hadi hapo mkuu sasa hebu nielimishe kidogo; kulikoni, kumekupata nini tena hadi kuhoji utitiri wa maswali chini ya kiwango hivi??
Wanabodi.
Imepita mwezi na siku kadhaa toka yafanyike mauji ya Mwandisi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Daudi Mwangosi, baada ya kuuliwa na polisi kwa kuripuliwa na bomu.
Chama Cha Demokrasia na Maendeo Chadema wamezindua CD ya mauaji ya Davidi Mwangosi (R.I.P) na kuisambaza mitaani na kuanza kuiuza. Chadema wamepata wapi haki ya kutengeneza hiyo CD na kuiingiza sokoni kwa mauzo.
Familia ya Mwangosi (R.I.P) pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania wanapata mgao wowote wa mauzo ya hiyo CD kama hawapati jambo ili kisheria linakuaje.
Watoto wa Marehemu ambao ni wadogo kiumri wanajua chochote kuhusu mauzo ya CD ya baba yao kipenzi.
Chadema mmewashirikisha familia ya Mwangosi (R.I.P) kwenye kutengeza hiyo CD Chadema wametengeza Copy 30,000 na wanauza CD moja Sh 5000 hizo pesa wanazoingiza kutokana na hayo mauzo kiasi gani kinakwenda kwenye familia ya Mwangosi kumsaidia mjane wa marehemu.
Hakuna sehemu niliotetea Jeshi la Polisi kwa unyama waliofanya, mie naulizia mapato ya CD ya mauji ya Mwangosi mjane anapata kiasi gani?
Mwangozi alikuwa Raia au "Kamanda"?
Kwenye red hapo Gamba!