Chadema wamepata wapi haki ya kutengeneza CD mauaji ya Mwangosi (R.I.P) na kuiuza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema wamepata wapi haki ya kutengeneza CD mauaji ya Mwangosi (R.I.P) na kuiuza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Oct 7, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Imepita mwezi na siku kadhaa toka yafanyike mauji ya Mwandisi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Daudi Mwangosi, baada ya kuuliwa na polisi kwa kuripuliwa na bomu.

  Chama Cha Demokrasia na Maendeo Chadema wamezindua CD ya mauaji ya Davidi Mwangosi (R.I.P) na kuisambaza mitaani na kuanza kuiuza. Chadema wamepata wapi haki ya kutengeneza hiyo CD na kuiingiza sokoni kwa mauzo.

  Familia ya Mwangosi (R.I.P) pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania wanapata mgao wowote wa mauzo ya hiyo CD kama hawapati jambo ili kisheria linakuaje.

  Watoto wa Marehemu ambao ni wadogo kiumri wanajua chochote kuhusu mauzo ya CD ya baba yao kipenzi.

  MAJIBU YA CHADEMA:
   
 2. s

  salomoe JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 708
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 80
  mwongo mkubwa wewe. mbona hatuioni sokoni?
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Je, umejiuliza kwanza source ya mauaji hayo ni kutokana na Chadema kufungua tawi lake la Chama? Polisi walifuata nini Nyororo? Walimfuata Mwangosi au Chadema?
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu unabisha au hutaki kuamini?
   
 5. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Nanyie mmepata wapi haki ya kuua raia kila mkutano wa chadema
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo cd ilikuwa ni mtiririko wa ufunguzi wa Tawi la CDM huko nyororo sasa Kama kifo kilitokea wakati wa ufunguzi unataka isiwe ni sehemu ya tukio kwenye video Yao? Mbona hamhoji video za zinazouzwa za ufunguzi wa matawi mengine ambavyo Vifo havikutokea?
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Weka picha ya cover yake hapa jamvin
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ritz heshima mbeeele kwanza japo ni mtani wangu wa kule Magambani,

  Kwa mujibu wa swali uliloliuliza hapo juu bana hebu tufahamishe japo kidogo ya kwamba siku hizi haki kama hiyo huuzwa katika duka gani siku hizi mkuu?? Bwana Ritz, hapa katikati kidogo naona kam vile umepwaya sana kwenye aina ya maswali unayoyauliza.

  Hakika, nielewavyo mimi, CHADEMA kama chama kina haki zote za kuelimisha umma juu yaa jambo lolote lenye maslahi kwao kwa kutumia msaada wa njia mbalimbali halali za kuwawezesha kufikisha vema zaidi ujumbe wowote watakaokua nao wakati wowote na mahali popote pale ilmradi taarifa wanazozitumia ni sahihi za zenye kuthibitika.

  Kwa mfano, niliposoma pale ulipokua ukihoji juu ya uwezekano wa Mhe Lema kwepo katika jimbo la Simanjiro naa vile vile kuripotiwa kuongoza mkutano mwingine wa kukata na shoka pale Daraja Mbili mjini Arusha kidogo uliniacha hoi na mbavu kuniuma sana kwa kicheko huku nikijiuliza kwamba huyu rafiki yangu hapa JF na Mtani wa kisiasa kule Magambani kapatwa na nini tena au kaibiwa ufunguo wa kufungulia ukurasa wake mtandaoni?

  Kimsingi, nakubali kwamba siku zote umekua ukionyesha viwango vya juu sana ya CRITICAL THINKING CAPACITIES hivyo kunifanya wakati mwingine niwe nikivutiwa na baadhi ya hoja zako japo KIMTAZAMO wewe na mimi ni kama bingu na ardhi - wewe ukivutiwa zaidi na hii CCM nyakua nyakua ya siku hizi na mimi nikitetea chama chochote chenye msimamo kama wa CCM ya enzi za Mwalimu Nyerere (ambacho kwa sasa ni CHADEMA pekee).

  Hadi hapo mkuu sasa hebu nielimishe kidogo; kulikoni, kumekupata nini tena hadi kuhoji utitiri wa maswali chini ya kiwango hivi??
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,781
  Trophy Points: 280
  Cd ni ya mkutano wa ufunguzi wa tawi la Chadema Nyalolo.
  Sasa kama moja ya matukio yaliyojiri kwenye ufunguzi uwo ni kifo cha mwagosi basi tukio ilo linapaswa kuwa ktk sehemu ya cd hiyo.
  Tunazo nyingi tu
  1.Ujasiri wa Kidemokrasia Tarime.
  2. Ukiukwaji wa demokrasia Arusha.
  Na nyingine nyingi.

  Na nyie tengenezeni ya kwenu ile ambayo makada wa ccm waliochapana makofi kwenye uchaguzi wa jana hapo karemjee hall.
  Jina liwe 'UTANDIKANAJI WA MAKOFI KTK CHAGUZI ZA NDANI ZA CCM.'

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hoja dhaifu toka kwa dhaifu
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu Uwezo Tunao,
  Sijui kama una ufahamu wowote wa neno hati miliki...ukinunua DVD yeyote lazima utaona maneno hairuhusiwi kunakili haki zote zimeifadhiwa...DVD za Marekani kuna onyo kabisa kutoka FBI.

  Naomba unipe jibu sahihi mauzo ya hizo CD pesa zake ni mali ya nani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,819
  Likes Received: 10,108
  Trophy Points: 280
  Nimetoka soko la Kariakoo nikapitia na soko lManzese mbona nimekuta nyanya tu?
   
 13. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu hawa jamaa ni dhaifu kama baba yao... hawana uwezo wa kujibu hoja nzito kama hizi.
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mwangozi alikuwa raia au "kamanda"?
   
 15. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mkuu! mambo hayo ni makubwa, sidhani kama watoto wa marehemu watapenda kuona hizo movie. Siungi mkono kuuzwa kwa hiyo mikanda, lakini ni ushahidi tosha kuishitaki serikali ya Kikwete
   
 16. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Na mamlaka ya kuandika ya hii post umeitoa wapi fuatilia yanakuhusu kama umetumwa kuwatetea hawa wahuni waliohusika na mauaji wanajulikana unataka kujua kibali ili ufanyaje ??:-|
   
 17. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Na wewe mamlaka ya kuandika ya hii post umeitoa wapi fuatilia yanakuhusu kama umetumwa kuwatetea hawa wahuni waliohusika na mauaji wanajulikana unataka kujua kibali ili ufanyaje ??:-|
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Chadema mmewashirikisha familia ya Mwangosi (R.I.P) kwenye kutengeza hiyo CD Chadema wametengeza Copy 30,000 na wanauza CD moja Sh 5000 hizo pesa wanazoingiza kutokana na hayo mauzo kiasi gani kinakwenda kwenye familia ya Mwangosi kumsaidia mjane wa marehemu.
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,528
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  Kwani huo mkutano aliandaa marehemu Mwangosi (RIP).?
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hakuna sehemu niliotetea Jeshi la Polisi kwa unyama waliofanya, mie naulizia mapato ya CD ya mauji ya Mwangosi mjane anapata kiasi gani?
   
Loading...