CHADEMA wamejiandaa vipi KUENDESHA NCHI?

Nchi gani hiyo unayo ongelea hapa? Jifunzeni ustarabu kwanza halafu acheni udini. Hii nchi itaongozwa na watu wenye akili timamu na sio wavuta bangi.

wavuta bangi kama wewe? Mi mvuta kamba nikibadili sana sana manati.
 
nilisikia mahojiano jana ya nelson mandela na mwanaharakati mmoja kijana yule kijana alimwuuliza mandela wakati anapigania uhuru hali ilikuwa tete je haikufika wakati alijisikia kukata tamaa? mandela alijibu anayekata tamaa si mpiganaji .kwa matokeo ya nepi tu japokuwa kayakana yameonyesha wazi ccm iko dakika za mwisho mwisho kusema ukweli nilikuwa nafuatilia picha za wapiga kura hasa wakina mama huko igunga wako hoi sana ule ni umaskini uliokithiri .
 
 
Mandela alikuwa anapigania haki, CDM inapigani tumbo.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mwenendo wa uchaguzi wa Igunga tangu kampeni hadi uchanguzi na mtiririko wa matokeo yanavyotolewa.

Binafsi nimeshangazwa sana na pia kutiwa moyo na jinsi CHADEMA ilivyojipatia idadi kubwa ya kura katika jimbo lenye madiwani wote wa CCM, hii inaashiria kuwa kiwango cha kukubalika kwa CHADEMA kinakua kwa kasi kubwa mno, nionavyo mimi katika uchaguzi wa serikali za mitaa ujao kuna uwezekeno mkubwa maeneo mengi nchini yakawa chini ya CHADEMA kitu ambacho kitaweka msingi wa ushindi 2015.

Pia Igunga imeniacha mdomo wazi kwa kushuhudia kuporomoka vibaya kwa CUF ambayo awali ilidai kuwa ndiyo yenye mtaji mkubwa na inaweza kushinda.

Niombe tu viongozi wa CHADEMA kukubaliana na matokeo kistaarabu (kama hakuna utata wa uchakachuaji) na kujipanga kujieneza zaidi vijijini ambako ndiko bado wananchi hawajitambua vizuri.Mwendo wa Chadema unaridhisha mno.

CHADEMA endeleeni kuchapa kazi vizuri hasa mlipo na dhamana tayari, dalili za mageuzi TZ zinaonekana.

Hongereni wana Igunga kwa kupiga kura kwa amani na utulivu,huu ndio ukomavu wa kisiasa.

Mungu ibariki Tanzania
 
Tuwasaidie Chadema let everyone become Chadema hubiri Uchadema popote utakapokuwa tusiwanyosheee wao kidole pekee maana wako wachache na Nchi ni kubwa na sisi tunaishi na hawa vichwa ngumu kwenye maisha yetu ya kila siku .Tuanze sisi wenyewe na Chadema wakifika wanamalizia kwa maana ya vingoozi.Kuleta changes kwa mtanzania haswa huhitaji kujiunga Chadema bakia uliko lakini huburi changes na Chadema watafanya kweli .
 
kwa mtazamo wangu chadema mmefanya vizuri sana uchaguzi wa igunga
naomba niweke wazi kuwa chadema ilikuwa inapambana na vyama viwili bila kujua
ccm na cuf wamechanganya kura zao ndio huu ushindi kiduchu ukapatikana
chadema mpo kwenye wakati mzuri zaidi wa kunyakua madaraka 2015
cha kufanya ni kujiandaa kwa sababu tumeshaona mnakubalika kwa wingi kabisa
kila la heri chadema!
 
Great thinket yeyote atakubaliana na maneno ya mtoa mada,zile kura za CUF ndo zilitabiriwa ziwe za CHADEMA nami pia naona uelewa wa wananchi unakua sasa,2015 tutarajie makubwa Igunga ilikuwa ni Chadema against Serikali lakini yaliyaojiri sote tumeyaona.
Ukombozi uko karibu sana TZ. nawapongeza wanachaema wote, kazi nzuri
 
Ukisema ccm imeshinda basi unamaanisha ccm ni hero among the fools, maana ushindi finyu uliotumia gharama kubwa unaonesha chadema is a real hero kuwakosesha usingizi size yao(ccm) labda cuf.
Any way chadema kwasasa inapaswa kuendelea na harakati kufa na kupona maana masikini hachoki kutafuta(kuna umasikini wa aina nyingi) vijana na chipukizi wengi kizazi hiki ni wapenzi wao tatizo wengi hawana vitambulisho vya kupigia kura hawajaandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura hili nalo walitazame maana wapiga kura wao ni vijana, kisha ndio watafakari wataiendesha vipi nchi yetu baada ya kuichukua kutoka mikononi mwa hao warasimu idiot kings.
Kuhusu igunga ni hivi to be won or to win is not the matter the matter is to fight hard leaving the struggle with nothing in your hands is nonesense.
WAR FRONT KAMA KITOVU CHADEMA LETS GO!
 

Mkuu, umekosea ulikuwa unataka kusema CDM wajiandae kuendesha Fuso zao walizonuna kwa Mbowe!
 
Reactions: Omr
Kufikiria kuwa CHADEMA wanaweza kuongoza kupata kuongoza nchi ni alinacha. Igunga kipimo tosha.
S
kama Igunga ndio kipimo, suppose hayo ndo yangekuwa matokeo ya jumla ya 2015, hali ingekuwaje, ukweli ni kuwa Iginga ni alarm kali sana kwa CCM, haiwezekani mtu aje nyumbani kwako halafu wanao wote wanamfuata yeye halafu wewe unabaki na mkeo tu,hatari kubwa ati!
Akili za nepi changanya na zako
 
Chadema wamejipanga kam Nyerere alivyoanza
We mtoto, acha kabisa kuchafua jina la nyerere, Nyerere hakuwahi kuiba mke wa mtu, hakuhamasisha wavuta bangi kufanya fujo na team yake nzima ilikuwa inaheshimika sana kwenye hii jamii.
 

Nakubaliana na wewe. Kwa sasa CHADEMA wanatakiwa kujiimarisha katika ngazi ya matawi zaidi. Ofisi za chama zifunguliwe na uongozi uwepo kwa ajili ya kuingiza wanachama zaidi na kutoa elimu ya uraia. Jambo la muhimu zaidi sio jinsi ya kuingusha CCM bali ni jinsi gani itaongoza dola kwa mafanikio na uadilifu bila kuongozwa na mashinikizo ya mabeberu wa nje na ndani. Plz CHADEMA imarisheni chama vijijini na mijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…