Hahahahaha...
Leo hii mmeona mrudishe sera ya majambia mliyowasambaratisha Cuf? Mmenoa Mapakacha, sasa vifaa vya kijeshi viko wapi hapo nyie?
Visu na Manati? teh teh teh teh.....!! Mje na hapa nyumbani mi ninavyo vingi huwa nachinjia kuku, mbuzi nk.. kumbe ni vifaa vy kijeshi?
Duhhhhhhhh nchi hii...!!
BACK TANGANYIKA
Majanga, Chadema sera yao ni maandamano, vurugu na vurugu !!
Wana Ukumbi,
Baada ya mkuu wa jeshi la polisi nchini kuvipiga marufuku vyama vyote vya siasa kuhusu kuwa na makundi ya kujihami katika vyama hivyo, CHADEMA wamekaidi agizo hilo halali la polisi na wameendelea kuwatumia Red Brigedi katika chama chao!
Jambo ambalo CHADEMA hawakutarajia ni kuwa, polisi wana vyanzo vyingi vya taarifa, hivyo mmoja wa makamanda wa CHADEMA alifikisha taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa vifaa vya kivita ndani ya ofisi ya makao makuu na pia kuna mpango wa kusambaza vifaa hivyo kote nchini.
Zifuatazo ndio picha za vifaa hivyo na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kuandaa waasi ikitokea imeshindwa uchaguzi mkuu! Yale yanayotokea Kongo yataletwa Tanzania kama serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili.
![]()
Baada ya vijana wa CHADEMA kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi wakiwa na vifaa hivyo vya kijeshi.
![]()
Vifaa hivyo vikiwa vimekusanywa na jeshi la polisi ambavyo awali vilikuwa vimefichwa maeneo mbalimbali ndani ya ofisi ya CHADEMA na vingine vikiwa tayari kwa kusafirishwa kwenda mikoani.
![]()
Hapa pia tunaweza kujionea wenyewe jinsi CHADEMA walivyojipanga kuivuruga amani yetu kwani hakuna chama cha siasa kinachoweza kuwa na zana hatari za aina hii ofisini!
Hao vijana majina yao ni Alon Nzesa na Bakar Magodi ni makada wa uvcc, leo wamekuwa ni wanachadema?
Hahaha yani ccm mnapiga picha wenyewe, mnapost wenyewe, kisha mnajipa ukamanda wenyewe, na sasa nyinyi ndio wachangiaji wakuu wa uzi huu.
Poleni, dawa ya moto ni moto, subiri nasi tuingie chimbo
kufanya siasa tanzania yataka moyo. nimeamini hakuna kama cdm kamwe. yaani polis muda wote kupambana na vyama vya upinzani na kubambikizia kesi viongoz wa upinzani.
Uzalendo upi?huhuu wa kukamata vyama vya upinzani na mabuti wakati hata Mimi mwenyewe ninayo tena nilinunua kwenye mitumba,uzalendo huhuu wa kuwakamata vyama vya upinzani na visu wakati hata mke wangu anavyo tena ana vitumia kukatia nyanya na vitunguu jikoni,uzalendo huhuu wa kukamata vyama pinzani na manati wakati hata mtoto wangu anayo na ana yatumia kuwindia ndege porini,uzalendo huhu wakukamata bendera na uniform za vyama vya upinzani wakati uniform zinavaliwa kila pembe za nchi na bendera zinapepea nchi nzima au kuna uzalendo mwingine?.
Sijaona vifaa vya kijeshi hapo, nilitarajia kukuta MG, LMG, RPG, mabomu ya kutega ardhini na ya kutupa, kifaru nk, ninachokiona hapo ni nguo za mitumba za mtaa wa kongo wanazovyaa wasanii huko marekani na buti za migodini...teteteh....kama hizo ndo taarifa za kiinterejensia tutashuhudia mengi mwaka huu
Kumbe hata wamasai wanatembea zana ya kivita, kweli policcm ni ziro mpaka manatiiiii
Hapa pia tunaweza kujionea wenyewe jinsi CHADEMA walivyojipanga kuivuruga amani yetu kwani hakuna chama cha siasa kinachoweza kuwa na zana hatari za aina hii ofisini!
Vifaa hatari kabisa.kisu na manati